HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
MWINJILIST: LAURENT ELIAS MPOMA
LENGO YA
SOMO:
Kuhakikisha
ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi
yanafunguliwa
➡Leo tuangalie jambo moja tu kufungua mafanikio yako
yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba
ya utumwa
Kumbukumbu
6:12
✅Angalia vizuri sana haya maneno Nchi
ya misri, nyumba ya utumwa
➡Angalia haya mambo vizuri kwa kutazama mambo yafuatayo
1 Kufuatana
na 2nyk 7:14 nchi maana yake ni ardhi yenye mipaka halali ya kuumiliki. Biblia
ya kiingereza maneno ya mwisho inasema kuiponya nchi yako (I will heal their
land)
➡Taifa ni tofauti na nchi linahusisha mkusanyiko ya
watu hasa linapozungumza maswala la uongozi waliokubaliana, lina mlolongo wake
utegemea nchi na nchi na katiba waliyo nayo.
➡Ukitoka kwenye taifa utakuta kabila, kabila utakuta
jamaa, ndani ya taifa kuna lugha.
➡Nchi imegawanywa tofautitofauti na mipaka yake.
➡Kiblia Taifa linaweza kuwepo lakini lisiwepo kwenye
nchi yake. Wana wa Israeli walikuwa Taifa lakini si kwenye nchi yao
2
Ukilinganisha mstari huu wa 2nyk 7:14 na ile Kumb 6:12 utaona ya kuwa hali ya
kiroho ya ardhi inaweza ikageuza eneo kuwa nyumba ya utumwa
Kumb 6:12
➡Nchi maana yake=2nyk 7:14 nchi hiyo inaitwa Misri
Nchi ya
Misri nyumba ya utumwa kwa hiyo ardhi imefanyika nyumba ya utumwa au ardhi ina
uwezo wa kufanya eneo likawa nyumba ya utumwa
3 Utumwa wa
wana wa Israeli ulikuwa ni wa kiroho lakini ulijitokeza katika maisha yao ya
kila siku
Sababu 3
zinakazokusaidia kueleza jambo ili
MOJA
Shida
haikuwa kazi waliyokuwa wanafanya lakini ni hali/mazingira ya kiroho ambayo
walikuwa wanafanya hiyo kazi
Kut 1:11-14
➡Kazi walizokuwa wanafanya Misri walizifanya pia
Kaanan. Walifanyishwa kazi ngumu
➡Sasa si kila kazi ngumu ni kazi ya utumwa. Walishughulika
na chokaa, matofali na kujenga miji na mashamba
➡Swala si aina ya kazi ndo iliwafanya kuwa watumwa bali
mazingira ya kiroho
➡Walipokuwa wanamlilia MUNGU hawakumlilia sababu ya
kazi walizokuwa wanafanya bali sababu ya utumwa Kut 2:23
➡Utumwa si kazi ni hali ya kiroho/mazingira ya kiroho
yanayotengeneza aina fulani yamaisha ambayo:-
✅Ubana fikra za watu,
✅Ubana maamuzi yao,
✅Uweka mipaka kwenye maisha yao na
kwenenda kwao
➡Si watu wengi sana wanaweza kujua wako kwenye hali ya
utumwa sababu ya kazi wanayofanya maana kazi hiyo hiyo mwingine anaomba kufanya
PILI
Walishindwa
kujitoa
➡Kama ingekuwa ni swala la kazi kwanini wasiache?
➡Kila siku walalamika kazi ngumu kazi ngumu kwanini
usiandike barua ya kuacha? Utafute iliyo nyepesi?
➡Unapokuwa mtumwa kwenye mazingira ya nyumba ni tofauti
nay ale ya gerezani
➡Yule aliyekwenye nyumba inamchukua mda mrefu sana
kujua kama ni mtumwa
Kama MUNGU
asingewatangazia kwamba wako utumwani wasingejua.
➡Walipokuwa wanalia MUNGU awaondolee uchungu wa ule
utumwa MUNGU akaondoa utumwa maana huo ndio uliosababisha uchungu ndani yao
TATU
MUNGU
aliwatoa kwa nguvu
Kumb 7:8
➡Swala alikuwa kazi bali ni ile hali ya mazingira ya
kiroho iliyowafunga kwenye utumwa
4 Waishio
ndani ya nyumba wanatambuliwa kiroho kwa kuangalia jina la mmliki wa nyumba
hiyo
Esta 8:1-2
Soma ile
Esta 7:10
➡Amani hayupo, nyumba yake kapewa Esta
➡Katika ulimwengu wa roho nyumba zinatazamwa tofauti na
tunavyotazama, angalia na Modekai naye akapewa pete ya Amani na Esta akamweka
Modekai juu ya mlango wake amani
Kumb 6:12
➡Nchi ya Misri nyumba ya utumwa weka misri haijalishi
uko nchi gani kama wewe ni Mmisri uko duniani unatambulikana kama mtu wanyumba
ya misri au nchi ya misri kuna alama inayokutambulisha
Nyumba ya
Israeli na nchi ya Israeli, wana kitambulisho katika ulimwengu wa roho
kinachofanana
➡Amani alikufa na aliyepewa mamlaka juu ya nyumba yake
alipewa Esta haijalishi walikaa kikao cha kuchagua msimamizi
Modekai
alipewa mamlaka kwenye lango la nyumba ya amani, haijalishi hawako nyumbani
wakati huo lakini wako na alama waliuwawa wote
➡Ukiwa na alama kwa ajili ya uangamifu utapata shida sana.
Kama nyumba ya baba yako inamilikiwa na adui utapata shida sana
Math 12:29
➡Nani anayemiliki nyumba na uzao wako?
➡Uwezi kuwafungua waliofungwa kabla ya kushughulika na
Yule aliye juu yao
5 MUNGU
aliwatoa wana wa Israeli toka kwenye nyumba ya utumwa kupitia kwenye mlango wa
nyumba ya utumwa
Kut 12:13-23
➡Alitumia kitu gani?… Jibu ni DAMU YA AGANO
➡Hakuwapitishia dirishani bali mlangoni lakini ilikuwa
lazima DAMU YA AGANO itumike kuwatoa
➡Nchi ya Misri kipindi kile yote ilikuwa chini ya
mazingira ya utumwa iliitwa nyumba ya utumwa na MUNGU alikwenda kuwafuta uzao
wa Ibrahimu, Isaka na Yacoko sababu ya kiapo alichowaapia kwamba kuwatoa wana
wa Israeli utumwani (walikuwa na alama) hakwenda kumfungulia kila mtu atoke
➡Mafanikio yao na kukua kwao kulikuwa kumefichwa na
kukamatwa na mazingira ya ardhi ya Misri na walikuwa hawajui
➡Angalia ardhi ya nyumbani kwenu ama mahali ulipo kama
ina mtawala anayetumia ardhi hiyo kama nyumba ya utumwa kuwa na uhakika utapata
shida sana kutoka
➡Mfano nyumba ina vijana wana akili sana wana uwezo wa
kufanya biashara, ana uwezo wa kufundisha na kufanya kazi lakini wako nyumbani
na wale wajirani hawana hata shule lakini wako kazini.
➡Wakati mwingine unafikiri ni sawasawa sababu yuko
kwako au nyumbani ujajua kuwa ardhi imegeuza nyumba yako kuwa nyumba ya utumwa
➡Kama baba yako alisimama na MUNGU mahali akaweka agano
usifiriki shetani atakuachia kirahisirahisi katika mambo yako ama kuamua kwako.
➡Utashangaa kwako tu mambo hayaendi lakini kwa wengine
yanaenda…hii yote ni yale mazingira ya kiroho yakibadilishwa na mambo yote
yanabadilika
➡Ujawahi kuona mtu anahama kutoka kwenye nyumba ya
kupanga kwenda kwenye nyumba yake gafla mambo yake yanasimama kiroho hata kiuchumi?
➡MUNGU aliwapitishia wana wa Israeli langoni ili kujua
kuwa walikuwa kwenye nyumba.
➡Wengi wamefungwa:-
✅Kufikiri kwao
✅Kutokupata msaada mahalipopote pale
✅Wasipate kazi
✅Wakae tu nyumbani
✅Kitu cha imani wakifikiri wako
kiroho. Hawafanyi kazi na ni watumishi wanatakuishi maisha fulani ya kiutumishi
hivi, hawafanyi biashara wala kazi yoyote, wengine wameacha masomo yao
➡YESU anasema nyumbani mwa BABA yake, na pia anasema
kanisa ni nyumba yake kwa hiyo, alama ya kiroho ya kanisa inategemea jina la
kanisa.
➡Kama unasali kanisani hujui jina la mchungaji wako
basi ujue alama yako ya kiunganiko chini ya mchungaji imepotea
➡Ardhi ni kama kompyuta kubwa ukikanyaga ardhi
inafahamu na kama haikufaamu upeleke taarifa kwenye system yake kujua
background yako na ndiyo maana ukikataliwa mjini hata mashambani utakataliwa na
ukibarikiwa mjini na mashambani umebarikiwa
MAOMBI
<NGUVU YA MUNGU KWANZA>
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
ENDELEA SIKU YA PILI
KUSUDI LA
SOMO:
Kuhakikisha
ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi
yanafunguliwa
Kumb 6:12,
2Nyk 7:14
✅Pitia somo la jana ili kujua
tulipotioka nay ale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako
yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba
ya utumwa
✅Kumbuka jambo la msingi utumwa wa
wana wa Isareli haukuwa sababu ya kazi walizokuwa wanafanya bali ni kwa ajili
ya hali ya kiroho ya mazingira ya kazi walizokuwa wanafanya
✅Walimlilia MUNGU juu ya uchungu
moyoni mwao wakati wanafanya kazi wala si kwa sababu ya kazi kuwa ngumu
➡Leo tuangalie NAMNA YA KUJIONDOA KWENYE MADHARA YA
LANGO YA ARDHI YA NYUMBA UNAYOISHI INAPOMILIKIWA KIROHO YA NGUVU ZA SHETANI
➡Ni jambo pana na jipya kwa watu wengi neema ya MUNGU
na iwe juu yako kuweza kuona na kufahamu jambo hili maana kujua na kufunguliwa
katika jambo hili utafunguliwa katika mambo mengi sana
Esta 8:1-2,
13-14
Mwz 22:17
Math 12:29
Kut 12:12-23
Tuangalie
vipengele vichache vya jambo hili ili iwe rahisi kuelewa
1 Ardhi na
nyumba iliyojengwa juu yake vina uhusiano wa kiroho
➡Unasema unajuaje…..?
➡Kufuatana na Kumb 6:12 MUNGU amelinganisha nchi na
nyumba kwa hiyo ardhi ile ambayo ina mipaka halali inauhusuano wa kiroho na
nyumba inayojengwa
2 Mlango wa
nyumba una uhusiano na mlango wa ardhi
➡Kwanini? sababu kama ardhi ina uhusiano wa kiroho na
nyumba basi na milango yao ina mahusiano
3 Ukigusa
mlango wa ardhi kiroho unagusa pia mlango wa nyumba kiroho
Matendo
16:26
➡Tetemeko lile halikuwa la kawaida lile la kuangusha
nyumba bali lilikuwa lile la kushughulika na ardhi ambayo juu yake gereza
lilikuwa lipo
➡Sababu walikuwa wapo gerezani kwa jinsi ya mwili
isingekuwa rahisi wao kutoka maana hawakufungwa kimwili bali kesi yao mpaka
kufungwa kwao ilikuwa kiroho
➡Ndiyo maana MUNGU alileta tetemeko akatikisa misingi
ya gereza na Biblia inasema milango ya gereza ikafunguka haisemi ikavunjwa na
vifungo walivyokuwa wamefungwa vikaachia
➡Yule askari alipoona milango iko wazi alitaka kujiua
maana alijua wametoroka lakini walimwambia asijiue akawakaribisha kwake
akawanawisha miguu na kuwatayarishia chakula na baada ya hapo walirudi gerezani
➡Kulipokucha asubuhi wale makadhi waliowafunga walitoa
order ya wakina Paulo kuachiliwa.
➡Nini nataka uone hapa gereza halikuvunjwa wala kuwa na
nyufa hata moja kutoka kwenye lile tetemeko
MUNGU hakuwa
na shida na gereza la nje bali alikuwa na shida na gereza la kiroho ambalo kwa
jinsi ya nje watu wanaona kama vile kuta tu na linaweza kuwa sehemu yoyote ile
➡MUNGU alikuwa anashughulika na ardhi ili kushughulika na nyumba iliyo juu ya ardhi
akafungua milango ya ardhi ili kufungua milango ya gereza iliyoko juu yake
➡Kama nyumba yako ni ya utumwa imezungukwa na mazingira
ya utumwa usiangaike kuombea nyumba bila kuombea ardhi ya nyumba hiyo maana
mlango wa ardhi una uhusiano na mlango wa nyumba yako
➡Vita ya ardhi si vita ya kumshirikisha kila mtu maana
ina mapamabano yake mabaya kama ujajipanga
➡Kama huna NENO la kutosha ndani yako MUNGU akikusemesha
uwezi kusikia maana kusikia huja kwa NENO la KRISTO maana waweza kushughulika
na ardhi MUNGU akikwambia shughulikia mlango la ardhi
➡Wakina paulo walienda kuhubiri wakatengeneza mahali pa
kusali bila kucheck na kushughulikia nani anamiliki lango la ardhi/nani ni
mmiliki wa lile eneo
➡Waulize watu wa nyumba ya amani maana kiroho nyumba
yake ilikabidhiwa Esta na Modekai sasa haijalishi kikao cha milathi kimeamua
nini maana wamiliki ndio wanaoamua na kutoa ruhusa hali ya kiroho na hali ya
maisha ya nyumba hiyo inaendaje
➡Unaanzisha kanisa/fellowship mahali badala ya
kuangalia na kucheck nani ameshikiria lango la roho nyingine inayopingana na
kitu unachofanya na ambaye ameshikiria lango la ardhi ambalo pia ndilo
limeshirikia lango la nyumba ya sehemu hyo na msingi wa kiroho unayotumia
kusali sasa kama vifungo hivi vimefungwa kwenye ardhi na vikaja kuonenakana
mpaka kwa nje usipojua namna ya kuvifungua kwenye ardhi uwezi kufunguka
➡Angalia habari ya kina paulo kama waliendele na maombi
kikundi cha cha ibada kikavurugika wakafungwa jera hata baada ya kutolewa
gerezani walifukuzwa kutoka nje ya mji sababu walianzisha huduma mjini bila
kusimamia malango ya ardhi ya mji
Matendo
16:39-40
➡Walipotoka gerezani walienda kwa Lidya na kukutana na
ndugu/wapendwa tu na wale wapendwa waliwafariji tu hawakuwa wa msaada nao
wakaenda zao
➡Ndiyo maana chunga sana watu wanaokushabikia huduma
wakati hawajui vita unayopitia, chunga sana watu wanakusumizia front line
wakati hawajua kupigana sababu ukifungwa gerezani watakufariji na kukupa pole
na kusema tunakuombea na wakati hawajui hata wanachoomba
➡Mji ule ulikuwa na wapendwa lakini hawakuweza
kuwasaidia kina Paulo sababu inategemea ni nani aliyeshirikia lango la ardhi
kiroho la mji ule.
➡Maana walioshirikilia kama hawaitaki huduma kuwa na
uhakika itafungwa na watu kuamia kwenye huduma ama kanisa jingine hata kama
wapendwa wapo na usije fikiri watakusaidia watakufariji tu
➡Vikundi vingi sana vya maombi watu hawajui ni kwanini
gafla vimechanua na gafla vimekufa sababu ni moja tu ulianzisha kikundi cha
maombi bila kushughulikia lango la ardhi ambalo Modekai ndiye aliyeshikiria
lango hilo na kama uko kinyume naye kuwa na uhakika kikundi hicho kitafungwa
kabisa
➡Ndiyo maana unaweza kukuta makanisa mengine yanapata
shida eneo hilo lakini nyumba nyingine hazipati hiyo shida ama kanisa moja
linapata shida na jingine walaa sasa ni mambo mawili au moja lina operate kwa
viwango vya juu sana au siyo tishio
➡Ndiyo maana watu wengi wanapata shida kwenye nyumba
zao Biblia inaita nyumba za kitumwa na wako kwao.
➡Umewahi kufikiri kwa mfano hicho kiwanja ulichonunua
ni nani anamiliki lango la hicho kiwanja katika ulimwengu wa roho?
➡Nani amepewa kumiliki ardhi uliyojenga? Wengine
alipewa marehemu sasa ukichanganya jambo hili kiroho kuwa na uhakika kama
usipojua namna ya kutengeneza kisiwa cha ardhi ya kwako utapata shida sana
kuvuka na vita yake si nyepesi
4⃣Kama vile
nyumba ilivyo na mlango zaidi ya mmoja vile vile na ardhi ina milango zaidi ya mmoja inayoweza
kutumika kumfunga mtu
Isay 26:1-2
➡Nchi ili kurikaribisha taifa, taifa lazima lipite
kwenye lango.
➡Anapozungumzia lango kwenye nchi anazungumzia lango la
kwenye ardhi linaloruhusu watu kupitia, kuingia na kutoka
Matendo
16:26-27, 24
➡….milango… Biblia haituambaii milango ilikuwa mingapi mlinzi
alipoamka alikuta milango yote imefunguliwa na funguo anazo yeye.
5⃣Kila lango
la kiroho katika ardhi au nyumba lina walinzi wa kiroho
Matendo
12:6,10
➡Kuliwa na walinzi kwa ajili ya petro na kulikuwa na
walinzi kwa ajili ya mlango/nyumba
➡Kuna mapepo unapewa wewe ukitoka nyumbani unakuwa nayo
na kuna yale yamepewa kulinda ardhi ya nyumba yako hayatoki.
➡Alipofika kwa wapendwa waliokuwa wanaomba aligonga
mlango (maana yake wakikupa kibali na kukufungulia ingia) malaika alazimishi
wapendwa kufungua, wakati huku pengine malaika alimpitisha na milango kufunguka
yenyewe. Swala ni kwanini hawakumfungulia? maana yuke dada hakufungua mlango
baadaye walikuja wakamfungulia
➡Ardhi lile lilikuwa na malango 4, walipita lindo la
kwanza na la pili hata mlango wa chuma na wa kuingilia mjini na mpaka kwa wale
wapendwa waliokuwa wanamwombea kuna watu amabo wamefungulia lakini wako
gerezani.
➡Fikiri Petro kama malaika alipomtokea angemwambi avae
nguo na viatu kisha akapotea maana yake nini yuko huru keshavaa nguo na viatu
lakini yuko gerezani kafungwa hana uhuru tena
➡Ndiyo maana tuna watu wengi sana tunawaombea na
inapofika kwenye kufunguliwa kwako tunafunga mlango tunatamani kuwaomba kwenye
chumba cha maombi lakini kuwafungulia hatufanyi hivyo.
➡Wengi tunawaombea halafu tukikutana nao tunakumbuka na
kuona lile tatizo bado kwako hata kama wamebadilika kwa hiyo tunajikuta bado
hatujawafungulia gafla wanarudi gerezani
6⃣Omba kwa
imani na kwa juhudi hadi aliyefungwa apite milango yote iliyomkwamisha
Matendo 12:5
Waamuzi 5:8
➡Kati ya eneo la uwanja la mapambano la MUNGU ni
langoni
➡Petro ililazimika avuke geti 4, mbili ndani ya gereza,
moja ndani ya mji na nyingine kwa waliokuwa wanamwombea hivyo MUNGU akikupa
eneo la kuwavusha watu na kukupa namna ya kuomba omba mpaka uwavushe geti zote
➡Wakati mwingine unapohitaji msaada wa vita unahitaji
watu ambao wanajua kupigana uhitaji msaada wa pole hata kama ni pole bali
hawata nyamaza mpaka umetoka
➡MUNGU atakupa mamlaka ya kukanyaga na kukika malangoni
na kuachilia DAMU YA YESU hapo maana hii ni ahadi ya MUNGU kwa Ibrahimu
<NGUVU YA
MUNGU KWANZA>
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
ENDELEA SIKU YA TATU
SOMO: HALI
YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO
LENGO YA
SOMO:
Kuhakikisha
ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi
yanafunguliwa
Kumb 6:12,
2Nyk 7:14
SUMMARY YA
SIKU 2
>>Pitia somo la siku ya kwanza na siku ya pili ili kujua
tulipotoka maana kuna yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako
yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba
ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara
ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani
kwa siku ya pili
>>Somo hili halifundishwi kama ile kawaida ila kila siku
MUNGU anampa kitu kipya ili yule atakayesikiliza kwa siku hiyo atapata jibu
lake
==>Si watu wengi pia wanalipokea kwa haraka sana mioyoni
mwao somo hili na kwa sababu hiyo ROHO MTAKATIFU anarirudia na kurirudia ili
lizidi kujengeka ndani yetu
➡Leo tuangalie KUFUNGULIWA TOKA KWENYE KIAPO
KILICHOIFUNGA NAFSI YAKO NA HALI YA KIROHO YA ARDHI
➡Na katika kulitazama jambo tuangalie mambo kadhaa
ambayo MUNGU ameachilia ndani ya kichwa cha Mtumishi ili yamkini yatufikishe
mahali pa kuweza kuingia kwenye maombi na wale ambao kuna viapo vimewafunga
wapate kufunguliwa
1⃣Njia
mojawapo inayounganisha mafanikio yako kimaisha na hali ya kiroho ya ardhi ni
maagano
Mwz 9:13
2Nyk 7:14
➡Anazungumzia juu ya kuiponya nchi yao na kumbuka nchi
ni ardhi lenye umiliki halali na ina mipaka kabisa. Biblia ya kiengereza
imewaka wazi kabisa inazungumzia juu ya ardhi
➡Sasa tazama kitu ambacho MUNGU alifanya wakati Nuhu
ametoka kwenye safina wako watu wachache waliojulikana kama wapo na wanyama na
ndege, ukisoma ile sura ya 8 na 9 na alipozungumza nao kwa habari za agano
➡..Anasema ni ishara ya agano kati yangu na nchi na
hasemi ni ishara ya agano kati yangu na wewe bali ni ishara ya agano kati yangu
na ardhi
2⃣Ishara ya
agano hilo juu ya ardhi husika kazi yake ni hizi zifuatazo:
MOJA (i)
Kazi kubwa
mojawapo ni kukumbusha kuwepo kwa agano
Mwz 9:13-16
Tazama
maneno haya….nami nitalikumbuka agano langu lililoko kati yangu na ninyi…..
➡Kukumbusha kwa watu wote waliohusika na maagano,
kiswahili kinakosa lugha iliyo nyepesi sana juu ya neno agano maana tukisema ni
mapatano halitoshi au mapatano ya kimkataba linasogea kidogo maana agano ni
pana kidogo
➡Jambo ambalo watu wengi hawafahamu Agano haliwezi kuwa
Agano isipokuwa kuna kitu cha kiroho kati yake, kunaweza kuwa na mapatano
lakini hakuna kitu cha kiroho kati yake
MBILI (ii)
Kukumbusha
kuwepo kwa kiapo kwa sababu ishara ni alama ya uhaminifu kwenye kiapo husika
Yosh
2:11-13-19
➡Rahabu alipokuwa amegundua ukombozi wake umekaribia,
kivipi ni kwa imani kama Waebrania isemavyo, kwa hiyo hakuangamia pamoja na
waovu wengine sababu aliwakaribisha wale wa pelelezi kwa furaha, kwa shukrani
na kwa imani
➡Swali la msingi kwanini MUNGU asiwapitishe pembeni ya
mji wa Yeriko kwa safari yao ya kwenda Kaanani? Maana mji ule uliangamizwa wote
na watu wakao humo isipokuwa Rahabu na familia yake na hata wakati wanaondoka
Joshua aliachilia laana ili asiwepo mtu wa kujenga hapo
➡Fahamu ili kilichomfanya MUNGU aende Yeriko ni Rahabu
peke yake hakuna kitu kingine chochote kilimpeleka kule maana Rahabu alikuwa na
destiny, alikuwa na kitu katika maisha yake na shetani alifikiri akiachilia
uasherati ndani yake na kumfunga katika ardhi ya mji wa yeriko hakuna atakaye
mkumbuka. Ukitizama utaona tokea pale MUNGU alimwamisha na kumwingiza katika
familia ya wayahudi yeye pamoja na familia yake na kumjengea maisha yake ya
baadaye
➡Mji waYeriko ulifungwa wote kwa jinsi ya kiroho si ya
mwili na ndiyo maana ilifunguliwa kwa jinsi ya kiroho. Gharama zote za
kuuzunguka mji ule siku zote 7 kama angeulizwa angejibu ni Rahabu ndiyo maana
walinyamazishwa
➡Kuna kitu MUNGU anaweka katika maisha yako na shetani
anajaribu kukuzamisha kabisa, haijalishi mahali ulipo, haijalishi shetani
amekufunguka kwa namna gani kama ni katika uasherati ama wizi au shida ili
kusudi ile ndoto MUNGU aliyoweka ndani yako isije kuchipua SIKIA NENO LA BWANA
MUNGU ATAKUFUATILIA NDANI YA YERIKO NA ATAKUTOA NA SI TU KUKUTOA YERIKO NA
ATAKUTOA KATIKA UASHERATI atakuweka katikati ya watu amabo kila mtu atashangaa
umetokea wapi na hawataacha kusema IMANI yake imemtoa pale na kumfikisha hapa
na kusema yuko MUNGU ambaye anaweza kushughulika na ukahaba
➡Ilichukua jeshi lote la Israeli kumtoa mtu mmoja
“Ndiyo maana
saa nyingine ninaposimama kwenye madhabahu huwa sijaribiwi kufikiri na wingi wa
watu nafikiria kuangalia mtu mmooja ambaye MUNGU amemkusudia”
➡Rahabu aliwaapisha kwa kusema ninawaapisha kwa BWANA,
maana yake ninawafunga kwa MUNGU wenu alafu akasema wampe alama ya uhaminifu,
wakasema tusije tukaingia hatia ya kiapo ulichotuapisha…funga kamba hii, wale
wapelelezi walikuwa wanatembea na kamba nyekundu ni kamba waliyokuwa wanatembea
nayo ili ijulikane ni watu wa agano.
TATU (iii)
Kukumbusha
masharti yaliyoambatanishwa na kiapo
➡Hakuna kiapo kisichokuwa na masharti ili kuonyesha
hakuna agano lisilokuwa na masharti na ni masharti ya kisheria na kihalali ile
roho iliyowaunganisha kwenye agano kazi yake ni kufuatilia masharti
➡Ndiyo maana alipowaapisha kwa BWANA walimpa masharti:
✅Uruhusiwi kusema
✅Hakikisha ndugu zako unaowataka waje
aje
✅Hawaruhusiwi kutoka nje
3⃣Kiapo cha
agano kinabeba wahusika
wakufuatiliwa
Yosh 2:12-13
➡Rahabu wakati anazungumza na wale wapelezi hata
kuingia kwenye kiapo ndugu zake hawakuwepo lakini aliingiza jina la baba, mama
yake na ndugu zake na listi ya vitu walivyokuwa navyo kwa hiyo kila
kilichitajwa hakikurusiwa kuwa nje ya nyumba
➡Kuna watu ndani yamioyo yao MUNGU amewabebesha
familia, wengine kampuni, wengine kanisa unamwona yuko peke yale lakini hayuko
peke yake ndani yake amebeba majina ya watu na vitu vyao na kila mahali
anawakumbuka kwamba anao.
➡Kumbuka habari ya yule tajiri aliwabeba ndugu zake
aliokuwa anawabeba kwenye pesa na alijua watapita na kuja njia hii hii wale
ndugu watano akataka wapelekewe taarifa mapema
➡Joshua alipewa watu wa kusafiri nao na watu wote wale
urithi wao ulikuwa kwa Joshua
➡Watu wa namna hiyo katika ulimwengu wa roho wana alama
zao ambazo zinafuatailiwa kila wakati na unapoingizwa kwenye kiapo haijalishi
kwamba umekubali ama hujakubali swala ni kwamba aliyekuingiza kwenye kiapo ana
sauti gani juu yako..kupitia kwenye kizazi, uhalali wa kukaa mahali pamoja
➡Kama mwenye nyumba ameapa kwa mungu wake juu ya ardhi
ya hapo kwake ambayo na wewe unakaa maana yake amekuingiza kwenye kiapo
➡Ndiyo maana vipao vya maagano vinasumbua sana maana
vinafunga watu hata kama hawajui kama wamefungwa
4⃣Kiapo
kinafungamanisha nafsi ya mtu na alichojiapiza
Hes 30:2
(Mahusiano ya kiroho kati ya baba na binti yake)-Daka hiyo ilikuwa aja ya
Mtumishi akafundishwa na MUNGU
➡Kwa hiyo kiapo ni kifungo na kiapo kinafunga nafsi na
kitu ambacho mtu ajiapiza nacho
➡Rahabu alipowaambia niapie kwa BWANA alikuwa anafunga
nafsi za wale wapelelezi kwa kitu watakacho kisema, walijua kabisa huyu
anazungumza kitu cha kiagano
Math 5:33-36
➡YESU alizuia viapo mahali ambapo havitakiwi kuwepo,
kuna vitu alivitaja kwa maskudi kabisa:-
✅Usiape kwa kichwa chako
✅Usiape kwa mji wa Yerusalem
✅Usiape kwa mbingu na
✅Usiape kwa mji
✅Usiape kwa ardhi
➡YESU kwa lugha nyingine alikuwa anatufundisha kuwa
waangalifu katika kuapa maana kuapa ni kuifunga nafsi yako na ardhi na roho
iliyoko mahali pale inabana hayo maneno uliyotamka mahali hapo
5⃣Ishara ya
agano inafanya wahusika wafuatiliwe katika ulimwengu wa roho kujua ikiwa masharti ya
kiapo yanazingatiwa
➡Ukisoma habari za MUNGU na agano lake la ibeahimu,
isaka na yakobo utakuta anasema …kile kiapo nilichowaapia baba zako…MUNGU
anamwambia mussa sijakufuata kwa ajili yako ila jina lako kwenye kiapo, nifuatilie
toka ukiwa tumboni, nicheck utavyoishi na kula saa ikifika nijifunue kwako,
nataka kucheck kama unafuata masharti
➡Wewe unaweza kusahau juu ya masharti ya kiapo lakini
MUNGU hawezi kusahau
➡Miungu inaingia mikataba katika ardhi kwamba
ikufanikishe ama isikufanikishe katika ardhi kwa nini sababu kwenye ardhi ndiko
kulikowekwa siri ya mafanikio ya hapa duniani.
➡Ulimwengu mwingine wowote hauna udongo kasoro ardhini
na mbegu zote za kiroho ziliwekwa ardhini kwa sabu Sura ya kwanza inasema kila
kilichoumbwa kilikuwa ni neno na neno ni mbegu na sura ya pili kila
kilichochipuka kilichipuka kutoka kwenye udongo kwa hiyo lile neno lilikuwa
mbegu lilivyotamkwa MUNGU akaliweka kwenye udongo kwa hiyo udongo una mbegu za
kiroho
➡Siri ya mavuzo yako iko kwenye ardhi, siri ya hali ya
hewa iko kwenye ardhi na hii ni ishara ya agano MUNGU aliyoweka na Nuhu kwamba
katika vitu alivyowekeana naye na ardhi ipo na kama ipo kuwa na uhakika na
mbingu yake ipo maana utegemea na kufanya kazi pamoja
6⃣Badala ya
kukimbilia kuvunja agano
badilisha na tangua kwanza kiapo ili kuliondoka jina lako na nafsi yako kwenye
kifungo
Hes
30:2,10-15
➡Usipotangua kiapo yote yaliyosemwa kwenye kiapo
yatatokea
➡Rahabu aliwaapisha kwa BWANA hakulijua agano likoje
lakini alijiingiza kwa njia ya kiapo na kuvunja lile agano ilikuwa kutengua
kile kiapo kwamba watu wale/ndugu zake wasikae ndani ya ile nyumba/ ndani ya
lile agano.
➡Sasa kiapo kile hakitawafunga hata kama agano lipo
➡Shida watu wengi sana wanakimbilia kuvunja agano
wasilolijua limefungwaje na limefungiwa wapi na vitu gani vimehusika kwenye
agano.
➡Usijaribu kumkwamua mwingine wakati wewe umekwama toka
wewe kwanza
➡Joshua aliwaambia watu chagueni hivi leo ila mimi na
nyumba yangu tutamtumikia MUNGU wakasema nasi tutamtumia huyo MUNGU akawaambia
kwanza ondoeni alama za miungu yenu kwanza
➡Ukifunga nafsi kwa kiapo usipotangua kila ulichokisema
kitatokea na kinaweza kukusumbua miaka na miaka. Unatangua kwa kutumia DAMU YA
YESU maana ni DAMU ya AGANO na ni DAMU BORA kuliko damu zozote zile
7⃣Miguu yako
ni lango rahisi la kutumia kuifunga nafsi yako na ardhi katika kiapo cha kiroho
Zab 56:6
Zab 57:6
➡Shetani anatumia nyayo kushika nafsi yako kwa hiyo
anaotea nyayo zako. Shetani amekuwekea nyavu kwenye miguu lakini usikii nyavu
unasikia moyoni mwako kukata tama, kila ukiganyaga usogei mpaka umeacha
kutembea
➡Sasa unaweza kujua kwanini Rahabu alipokuwa anataka
kutolewa kule ilibidi wazunguke kwa miguu siku zote zile, sababu miguu ya watu
wa MUNGU inaweza kuachilia nguvu za MUNGU inapokanyaga mahali
➡Walipokuwa wanazunguka walikuwa wanatafuta misingi ya
ile kuta zile hazikuwa kuta zimejengwa kawaida bali zilikuwa kuta za kiroho,
sababu ile ardhi ilikuwa na misingi ya kiroho 7 na ule wa 7 ulifungwa mara 7.
Kile kitu na kila mahali kulianguka chini kasoro nyumba ya rahabu misingi
mingine yote ilibomoka
➡Kuokoka kwako na kupona kwako si sababu ya matendo
yako bali ALAMA YA DAMU YA YESU moyoni mwako
<NGUVU
YA MUNGU KWANZA>
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: