MAOMBI YA KUFUTA MAAGANO YOTE YA KISHETANI.
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Leo nataka
tuombe maombi ya kuvunja maagano.
Mwanzoni wa
wiki hii tukiwa katika maombi ya mkesha kanisani sauti ilinijia kusema vunja
maagano ya giza, ufafanuzi ulikuwa mkubwa na nikashangaa sana.
Kumbe kuna
maagano mabaya mengi ya adui ili kuhakikisha hatusongi mbele lakini ashukuriwe
BWANA YESU maana damu yake ya Pasaka inaweza kufuta maagano yote ya kipepo.
Kutoka 23:32
''Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.''
Agano ni
kitu kikubwa sana, Agana la kipepo ni mapatano ya kishetani, ni mikataba ya
kishetani na MUNGU hataki tuingie agano lolote na shetani wala mawakala wake.
Adui kwa
kulijua hilo kwamba hatumtaki na mipango yake yote basi kuna vitu huwa
vimefanyiwa maagano tayari kwa ajili yetu kitu ambacho tusipoomba kuna madhara
ya kiroho na hata ya kimwili.
-Kumbe kuna
maagano kwenye baadhi ya vyakula hivyo ni muhimu sana kuombea chakula.
-Kuna
vitanda vina maagano mabaya.
-Kuna maeneo
yamejaa maagano mabaya.
-Hata ardhi
yako adui anaweza kuifanyia maagano mabaya ili usifanikiwe.
-Mambo mengi
sana yamewekewa maagano na adui ndio maana tunatakiwa kuomba sana.
unaweza
kujiuliza swali dogo tu kama hili; kwanini wanawake wengi ndio huteswa sana na
mapepo?
Jibu ni vitu
wanavyotumia maana vingi vina maagano ya kipepo, vingi vina mapando ya shetani
mfano vipodozi, mapambo, nywele bandia n.k.
Adui
anapanda kitu kidogo tu lakini ukizubaa utajikuta mara unavalishwa pete na
mwanaume usiyemjua dotoni kumbe jini maana vitu vyako ndivyo vilivyofungua
mlango kwa jini huyo kuingia kwako, na akikuweza anaweza hata kukuzuilia
kufunga ndoa au kwenda kanisani au kusoma biblia huku ukitamani lakini
umeshindwa.
Adui anaweza
kupanda kitu kidogo tu na ukizubaa utajikuza unapenda miziki ya kidunia tu na
nyimbo za MUNGU utaona machukizo kumbe adui anakuendeza kipepo.
Adui ukimpa
nafasi kidogo tu, ukizubaa unaweza kujikuta kila siku unaota ndoto ukizini
kumbe shetani anaongeza maagano mengine zaidi ili hata kupata mtoto baadae iwe
tatizo.
Ndugu yangu,
maagano ya kipepo lazima yaondoke kwa jina la YESU KRISTO ndio utakuwa huru.
-Kuna watu
sura zao zimefanyiwa maagano ya kipepo ya kuchukiwa na kila mtu, unaweza
ukakosa mme au mke kwa sababu tu ya tatizo hilo la kishetani la maagano.
Maagano ni
mabaya sana.
-Kuna
maagano kwenye baadhi ya mavazi tunayonunua N.K, hivyo ni muhimu sana kutakasa
Tunavyonunua kwa jina la YESU.
Hata kuna
baadhi ya vitanda vina maagano mabaya, na MUNGU anapokataza uzinzi ni kwa lengo
la kukusaidia tu mwanadamu wewe na sio vinginevyo. maana uzinzi unaweza
ukaongeza tatizo zaidi badala ya dhambi tu basi na maagano ya giza juu yake.
Isaya 57:8
'' Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua
nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua
kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo
ulipokiona. ''
-Maagano mabaya
ni jambo baya sana ndugu. kama zamani uliwahi kuingia maagano ya kishetani basi
kimbilia kanisani ukaombewe maana maagano ni mkataba na ukiingia mkataba na
shetani mwishowe anaweza kukuangamiza tu na uzima wa milele ukaukosa.
Hosea 10:4
''Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo
hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba.''
-Maagano ya
kishetani ni mabaya sana na ni muhimu kujitenga nayo kwa kumkimbilia BWANA YESU
na nguvu zake.
Wachawi
wakati mwingine wanaweza kuifanyia maagano mabaya sauti yako na ndio maana
kinywa chako kila siku kinakutendesha dhambi.
-Sio kila
zawadi unapokea tu bila hata kuiombea.
-Sio kila
mialiko lazima uende. omba kwanza na msikilize ROHO.
Adui ana
mbinu nyingi lakini kama utakuwa mwombaji hakika utashinda.
Kuna maagano
mengine inahitajika nguvu kubwa sana ili kuyavunja na nguvu kubwa ni mbili tu,
Damu ya YESU KRISTO na jina la YESU KRISTO.
Najua
umejifunza kitu na utachukua hatua ya kuomba na kujiunga na kanisa la kiroho
ili uwe kwenye mzunguko wa maombi.
Kuna watu
huwa nawaambia wajiunge na kanisa na wanapofanya hivyo tu mateso yao ya kuteswa
na wachawi yanakoma. unajua ni kwanini? ni kwa sababu wanakuwa katika mzunguko
wa maombi, mfano mchungaji kama atafunga au ataomba kwa ajili ya huduma yake ni
lazima akujumuishe na wewe maana uko katika huduma hiyo, kama viongozi wa
wamama au viongozi wa vijana watakuwa wanaombea vijana wao au wamama au wababa
lazima na wewe utakuwa unaombewa hivyo ukiongeza na maombi yako mwenyewe na
kuhudhuria ibada hakika adui atakimbia hata kama hataki maana atakuwa anapata
kipigo kila saa, kama anadhani umelala wewe akisogea tu anapata kipigo maana
wakati huo mchungaji anaomba, wakati huo kundi la maombi linaomba.
Kujiunga na
kanisa na kuanza kuishi maisha mataktifu ya wokovu wa BWANA YESU ni jambo la
muhimu sana.
Maombi ya
kuvunja maagano ya kishetani.
BABA yangu
uliye mbinguni, jina lako litukuzwe milele, ninakushukuru BWANA kwa kunilinda
na kunipa afya njema.
Ninakushukuru
kwa kuwalinda ndugu zangu na familia yangu.
BWANA YESU,
mimi ni binadamu na yawezekana kabisa kuna sehemu nimekosea, BWANA naomba
unisamehe dhambi zangu zote, zile ninazokumbuka na zile ambazo sikumbuki. Neno
lako Katika Matendo 3:19 linasema ''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu
zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;'' . BWANA
ninatubu leo na naomba unisamehe MUNGU wangu. nipe kuishi maisha ya ushhindi
dhidi ya dhambi na nipe kumtii ROHO MTAKATIFU maana ndiye mwangalizi wa roho yangu.
nakushukuru JEHOVAH BWANA maana naamini umenisamehe MUNGU wa uzima.
BWANA neno
lako linasema katika Isaya 41:21 kwamba '' Haya, leteni maneno yenu, asema
BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.''. BWANA hoja yangu
yeye nguvu ni maagano ya kipepo yote ambayo ninaomba yafutike leo kwa damu ya
YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO. Maagano ya magonjwa na maagano ya ardhi
ninayokaa nayafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO maagano ya
mavazi na maagano ya maagano ya vyakula nayafuta kwa damu ya YESU na kwa jina
la YESU KRISTO, Kila aina ya agano la shetani maishani mwangu ninalifita leo
kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO. Kila agano la giza, haijalishi
nililifanya mimi au wazazi wangu ninafuta agano hilo kwa damu ya YESU na kwa
jina la YESU KRISTO. Kila agano la kishetani kwenye ardhi yangu au nyumba yangu
ninalifuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO. kila agano la giza
kwenye kitanda nilichowahi kulalia au kwenye mashuka niliyowahi kujifunika
ninafuta maagano hayo kwa jina la YESU KRISTO. Kila agano la giza kutoka kwa
wote niliowahi kufanya nao mapenzi kimwili au ndotoni ninafuta maagano hayo kwa
damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO. Kila agano ambalo yawezekana silijui
au nalijua ambalo nila giza ninalifuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU
KRISTO.
Kila agano
la giza kuanzia leo limefutika kwa jina la YESU KRISTO, kuanzia sasa niko huru
mbali na maagano ya kishetani, kuanzia sasa mimi ni mishindi kwa jina la YESU
KRISTO. Nakushukuru BABA wa mbinguni maana umenishindia, nakushukuru BWANA YESU
maana damu imenena mema kwangu kuanzia sasa maana maagano mabaya yote
yamefutika kwa jina la YESU.
Katika jina
la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi. Amen Amen AMEN KWA yesu.
Ndugu Yangu,
Usikubali Kumkana YESU Na Hakikisha Unajikana Ili Umpendeze MUNGU.
Usitende
Dhambi Maana Kutenda Dhambi Ni Kumkana BWANA YESU.
Ukidumu
katika mema bila kumkana YESU utafanya vyema.
Yeye BWANA
YESU anasema '' Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala
hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. -Yohana 10:28 ''
Kwa sasa
naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa
mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni
anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana.
mwinjilist: Laurent elias mpoma
+255714890889
nguvuyamungu@gmail.com
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: