ROHO ZITAWALAZO MAENEO
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
ROHO ZITAWALAZO MAENEO
Katika makala hii ya
tatu tutaangalia mafundisho yanayohusiana na kile wanachokiita "Roho za
Kimaeneo". Kulingana na mafundisho hayo, wanadai kuna roho chafu maalum
ambazo zinatawala jamii, vijiji, miji, jiji au hata nchi nzima. Hiyo ina maana kwamba,
roho hizo zinatawala katika eneo zima kulingana na jiografia ya eneo lenyewe;
na hivyo huitwa "Roho za Maeneo". Inaendelea kufundishwa zaidi kwamba
eti hizi roho za maeneo zanao uwezo na mamlaka ya kuwabana watu katika giza,
vifungo na dhambi kulingana na jiografia ya eneo lao. Kimsingi, zaidi ya hilo,
hawa wanaohamasisha mafundisho hayo, wanatuambia kwamba hizi roho za maeneo
zinao uwezo wa kushikilia jamii ndogo au miji kiasi kwamba Injili peke yake
haiwezi kufaa, kupata kuingia wala kupendwa au kuenea katika eneo hilo hadi
hapo hizi roho za kimaeneo zitakapotambulikana na kisha zikafungwa, zikazidiwa
nguvu pamoja na kukemewa kwa njia ya maombi. Wanafundisha kwamba watu hawawezi
kumjia Bwana, wakaokolewa na kukombolewa kutoka katika dhambi, giza, pamoja na
vifungo mbalimbali, kwa idadi kubwa mpaka kwanza hapo tutakapotambua na kisha
kuzifunga na kukemea nguvu za roho hizo za kimaeneo. Hivyo ndivyo wanavyosema
na kuwafundisha watu.
Hiki ndicho kidokezo
cha mafundisho yao kwa lugha rahisi kadiri iwezekanavyo, na nina hakika kwamba
utakubali kuwa ikiwa mafundisho haya ni ya kweli, basi ni ya umuhimu mkubwa.
Kuenea kwa Injili pamoja na kuokolewa kwa watu kunategemea ufahamu na matumizi
ya mafundisho haya, ikiwa mafundisho hayo ni ya kweli! Jambo hili haliwezi kuwa
swala la jinsi mtu aonavyo au tafsiri ya kibinafsi, kwa sababu litaathiri
ufahamu wetu kuhusiana na jinsi Injili ilivyo, pamoja na lile alilolifanya Yesu
pale Kalvari.
Kama ilivyo katika
zile makala nyingine zilizopita, napenda kwanza niangalie yale ambayo Maandiko
yanavyosema na kufundisha. Kwa hivyo, kwa muda huu, hatutaangalia Maandiko
ambayo watu wanadhani wamepata kuyaona mambo hayo yakifundishwa. Jambo hili ni
la msingi na lenye uzito mkubwa kiasi kwamba hatuwezi kuyaachia kwenye ubunifu
au hisia za kibinadamu tu. Tunachotafuta ni maandiko ambayo mambo haya
yanafundishwa dhahiri na kutajwa bayana.
Mambo haya
yanafundishwa wapi ndani ya Agano Jipya?
Kwa jibu la urahisi
na la ujumla kuhusiana na habari hiyo hapo juu ni - "Hakuna popote!"
Hatuyapati mahala popote katika Agano jipya, mafundisho haya yahusuyo kutambua
na kuzifunga roho za kieneo!
Yesu hakutumia au
kufundisha mbinu hii.
Hakuna mahali popote
tunaposoma kuwa Yesu aliibainisha roho iliyokuwa ikitawala eneo, kijiji au mji,
na kisha akaifunga na kuikemea kabla hajaanza kuhubiri na kufanya miujiza
mahali hapo.
Hakuna mahali popote
ambapo Yesu aliwafundisha mitume wake au mtu mwingine yeyote kwamba Neno la
Mungu linaweza kuwa na nguvu na mafanikio katika eneo fulani ikiwa kwanza
utaibainisha roho ya lile eneo na kuifunga na kuzishinda nguvu zake kwa njia ya
maombi. Kamwe hatusomi popote Yesu akiitumia au kuifundisha mbinu hii.
Mitume hawakutumia
au kufundisha mbinu hii.
Hakuna mahali popote
pale katika Injili au kwenye Matendo ya Mitume ambapo tunasoma habari za mitume
au mtu mwingine yoyote yule akitumia mbinu za jinsi hiyo katika kuineza Injili.
Mtume Paulo alitembelea miji mingi sana ambamo kulikuwa na zinaa ya kutisha,
mambo ya kimwili, uchawi pamoja na dhambi. Hakuna popote pale ambapo tunasoma
juu yake akizitambua kwanza roho hizo katika miji hiyo ili aone ni aina gani ya
roho za kimaeneo zinazotawala katika miji, wala hatusomi mahala popote pale na
kuona akiomba juu ya roho za aina hiyo ili kwamba kazi ya Injili ipate kustawi.
Hakuna mahali popote
pale ndani ya maandishi yao kwa makanisa au kwa watu binafsi, ambapo mitume
hawa wamepata kutaja tu mbinu za jinsi hiyo, licha ya kuzifundisha. Yapo
mahusia mbalimbali kwa ajili ya kuomba katika Agano Jipya. Lakini hakuna mahali
popote pale ambapo mitume wanaelekeza kuwa roho za kimaeneo zina uwezo juu ya
watu katika baadhi ya maeneo na kwamba watu hawana budi kuomba dhidi ya roho
hizo na kuzivunja nguvu zake, ili kwamba Injili ipate kustawi na ili wanawake
na wanaume wapate kuokolewa.
Hayapo mafundisho ya
jinsi hiyo ndani ya Agano Jipya. Kwa msingi huu pekee, tunaweza, kwa usalama
kabisa, kuyakataa mafundisho ya jinsi hii.
Lakini sasa, mtindo
wa jinsi hii haufudishwi kwenye Agano la Kale wala hatuna hata mfano mmoja
katika Agano la Kale, unaoelezea juu ya mtu yeyote anayezitambua roho za
kimaeneo na kufunga nguvu zake kabla kazi ya Bwana haijakamilishwa ipasavyo.
Kwa kweli, waandishi hao wa kisasa wanarejea katika maandishi fulani fulani ya
Agano la Kale, na tutakwenda kuangalia maandishi hayo baadaye, lakini hata
hivyo, hakuna hata andiko moja linalounga mkono mtindo huo na mbinu zao
zinazoenezwa na waandishi hao.
Jukumu la Uongo
Wanawezaje walimu
hawa wa siku hizi kusema, "Lazima uzitumie mbinu hizi ili kuhakikisha
mafanikio ya uInjilisti katika ulimwengu", wakati ambapo maandiko
hayatushauri kufanya hivyo? Wanaweka jukumu juu ya watu we Mungu wakati ambapo
maandiko hayaweki jukumu la jinsi hiyo. Kwa maneno mengine, wao huongezea
maneno yao juu ya Neno la Mungu - na wakizitumia mamlaka zao juu ya watu wa
Mungu, mamlaka ambazo hazitokani na Mungu. Hili ni jambo la hatari sana. Ni
jambo moja kusema kuwa, kwa sababu maandiko hayawazuii kuzitumia mbinu hizo,
kwa hivyo wao wanajisikia uhuru kuzitumia. (Hata hivyo, hoja hii si ya msingi,
kwa sababu mafundisho yao yanagusa kweli za msingi za Injili na ufanisi katika
kuenezwa kwake, hivyo wanapaswa kuonyesha kwa uhakika mambo hayo yanafundishwa
wapi katika maandiko, kabla hawajafundisha na kuzitumia kanuni hizo). Lakini
kwa kweli wanafundisha kanuni zao za lazima kwa ajili ya kueneza Injili. Huo ni
udanganyifu na unaweza kuwapelekea watu wa Mungu, kutumbukia katika
kuchanganyikiwa, vifungo pamoja na hatari iwapo watapokea na kuyafuata
mafundisho ya jinsi hii.
Ikiwa mbinu hizi za
kuzitambua na kuzifunga roho za kimaeneo ni za lazima kwa ajili ya kuleta
mafanikio ya uenezaji wa Injili, kwa nini basi Yesu pamoja na mitume wake
hawakufundisha wala kutufunulia mambo hayo? Tunaelezwa na hawa walimu wa kisasa
kwamba maombezi dhidi ya mamlaka na uweza juu ya maeneo ya kijiografia,
yanahitajika sana kabla Injili haijapenya katika maeneo hayo. Je, mitume
walikuwa ni wajinga juu ya mbinu hizo? Au labda walishindwa kutufunulia kile
kilicho cha lazima kwa ajili ya uenezi wa Injili, na kwa ajili ya wokovu wa
nafsi za watu? Je kanisa litakuwa limeondolewa ukweli huu wa lazima kwa muda wa
miaka 2000? Hapana! Kanisa halijanyimwa ukweli huu wa lazima, na bado Injili
imeendelea kuenea muda wote huo kwa karne zote hizo, kama Yesu alivyosema
Injili haina budi kuenea, hata bila kanisa kufundisha au kuzitumia mbinu hizo
ambazo hawa walimu wa kisasa wamezibuni. Kutokea muda wa Matendo ya Mitume hadi
kufikia siku hii ya leo, kumekuwepo na uamsho, maelfu ya watu wamerejea kwa
Bwana kwa idadi kubwa, nao wameokolewa kutokana na dhambi, giza na vifungo vya
shetani pasipo hata kujulikana kwa mbinu hizo, kufundishwa wala kuzitumia!
Kutamani “matokeo”
kupita kiasi.
Lakini moja ya
kusudio lao kuu hawa wahubiri na walimu wa kisasa ni kuona “matokeo”. Mmoja wa
viongozi wa kanisa ambaye anaamini katika kutumia kanuni hizo amesikika akisema
kuwa iwapo kanisa lake halitaongezeka kutoka washirika 1000 hadi kufikia
washiriki 2000 ndani ya miaka miwili, basi hapo itakuwa ni kutokana na
kushindwa kwao katika kujaribu kwa makini kufanya hivyo. Kwa maneno mengine,
iwapo tutazitumia mbinu halisi basi tutegemee kanisani washirika kuongezeka
mara mbili zaidi ndani ya miaka miwili! Watu hawa wanalifanya kanisa kuwa kana
kwamba ni aina fulani ya biashara ambapo tunapaswa kuzitafuta kanuni bora zaidi
ili kutoa matokeo na kufikia malengo. Hata makanisa mengi kwa sasa yameanza
kutoa “maelezo ya umisheni” pamoja na malengo yao kwa ajili ya mafanikio yao.
Mtindo wa aina hii kwa kazi ya Mungu, umeazimwa moja kwa moja kutoka kwa
ulimwengu wa kibiashara. Hii yote inamdhalilisha Yesu Kristo ambaye ndiye
kichwa cha kanisa lake ambaye ndiye aliyetuonyesha kwa neno lake jinsi
itupasavyo kujishughulisha wenyewe. Mmoja wao amesema kwa uwazi kabisa kwamba
wanavutiwa zaidi na yale “yanayofanya kazi” ( yaani, yanayoleta mafanikio au
matokeo ) kuliko "yale yaliyo ya kweli". Kwa hiyo basi, tayari
wameanza kujenga msingi wa udanganyifu wao. Katika kujiondoa kwao kutoka katika
miongozo iliyo sahihi ya Neno la Mungu, wao wamekuwa wakijiweka wazi kwa
udanganyifu wa shetani; kadiri wanavyoendelea na kuzitumia mbinu na kanuni
zinazoweza kuwaletea matokeo ya haraka na yenye kuvutia.
Yesu anaomba kwa
Baba akisema “Neno lako ni kweli”, Yohana17:17. Sasa kama watu wa Mungu, sote
tunatamani na kuomba kwamba Injili iweze kufikia na kuokoa nafsi za watu wengi
watuzungukao na ulimwenguni kote. Lakini watu wa Mungu, maombi yetu, kazi zetu,
pamoja na mafundisho yetu lazima yawe kulingana na neno la Mungu, ambako ndiyo
kweli. Hamu yetu ya “kuona matokeo” isituongoze kuelekea kwenye kuikataa au
kujitenga na Neno la Mungu kama lilivyofunuliwa katika maandiko; au kuanzisha
mbinu zetu wenyewe au mtindo wa fikra kwa ajili tu ya kujipatia kile
kinachoonekana kuwa ni “matokeo” ya haraka. Mengi ya mafundisho hayo ya kisasa
yanasukumwa na mawazo ya “mafanikio” yakikusudia kutafuta kitu fulani
“kinachofanya kazi” na hiyo ni “Mafanikio”. Hawa walimu wa kisasa wanaendelea
kubuni mawazo mapya pamoja na mitindo ya kufundisha. Hakuna hata mmoja
anayeweza kujihoji mwenyewe kuwa inakuwaje kila baada ya miaka michache
kunahitajika “mitindo” mipya, katika mtazamo wa Kitheolojia - hii ni upepo mpya
wa imani! Wala hakuna hata mmoja anayeweza kuuliza, kulitokea nini na ule upepo
wa imani uliopita? Au kutambua kwamba kanisa halihitaji mtindo mpya katika
mafundisho yake ya Imani isipokuwa ni marejeo kwa yale ambayo tayari
yamefunuliwa vizuri katika maandiko. Ikiwa tutakuwa waaminifu, tutapaswa kuungama
kwamba, mafundisho hayo mengi ambayo yanaendeshwa na wazo la mafanikio ni
matokeo yanayotujia moja kwa moja kutoka kwenye mila za kibiashara za Marekani
(U.S.A); mahala ambako kila kitu kinategemea malengo, matokeo pamoja na
mafanikio. Na Wakristo zaidi sana huko Marekani wameazima akili hizo au
wamechukua mtazamo na silka kutoka kwa ulimwengu na wameuingiza kanisani,
umewapelekea kwenye ubunifu wa mafundisho na matendo ya kutatanisha.( Bila
shaka, mimi sisemi kwamba, wazo la roho za kimaeneo linakuja kutoka kwenye
desturi za kibiashara, lakini huu msukumo kwa ajili ya mafanikio - ambao
umewapelekea Wakristo hawa kutumbukia katika ubunifu na udanganyifu).
Mwandishi na mwalimu
ambaye ni mmoja wa waenezaji wakuu wa mafundisho haya anaelezea juu ya jambo
ambalo nimeligusia hapo juu, kuhusiana na kukosekana kwa maandiko yanayounga
mkono mafundisho haya. Katika utangulizi wa kitabu chake alichokiandika yeye
mwenyewe kiitwacho “Territorial Spirits” (“Roho za Kimaeneo”; Sovereign World
Ltd. 1991 C.P.Wagner), amesema kuwa, amewahi kutazama kwenye vitabu 100 huko
kwenye seminari ya theolojia ambavyo vimezungumzia kuhusiana na somo la malaika
na mapepo, ili aweze kugundua mafundisho yahusuyo roho za kimaeneo. Anaendelea
kueleza kuwa, siku za leo ipo haja kubwa sana ya kufanya utafiti kwa ajili ya
somo hilo. Lakini kwa nini tufanye utafiti? Je utafiti wa kwenye Biblia
hautoshi? Je hatuna Biblia? Neno la Mungu halitoshi kutuelekeza kuhusiana na
jambo kama hili la msingi? Kwa dhahiri kabisa sivyo hivyo, kwa kuwa yeye hawaaliki
watu wafanye utafiti katika Biblia. Ijapokuwa kwa hakika anajaribu kutafuta
ushahidi kwa ajili ya mafundisho hayo kwenye maandiko, kama tutakavyoweza kuona
hapo baadaye, yeye anaenda sehemu nyingine ili kuona iwapo anaweza kupata
uthibitisho kwa ajili ya ubunifu huu wa kigeni. Lakini anatuambia kwamba ni
vitabu vitano tu kati ya 100 vilivyotaja kuhusiana na somo hilo la roho za
kimaeneo, na kati ya hivyo vitabu vitano, ni vitatu tu ambavyo angalau vinasema
chochote kinachoweza kusaidia. Lakini hakuna chochote kati ya vitabu hivyo
ambacho kilistahili kujumuishwa katika kitabu chake. Hii haishangazi kwa vile
mafundisho hayo hayamo pia katika Biblia - na mpaka sasa hakuna hata mmoja
ambaye amebuni au kuyatumia kwa jinsi hiyo, kwa kadri nifahamuvyo. Kwa hiyo,
katika kitabu chake hicho anajumuisha michango kutoka hasa kwa waandishi wa
siku za leo ambao wanaoeneza mawazo ya jinsi hiyo. Wagner alikuwa anafanya
utafiti juu ya kanuni za ukuaji wa kanisa na maombi, alipowafikia viongozi wa
kanisa fulani ambao walikuwa wakifanya aina hii ya maombezi dhidi ya roho za
kimaeneo. Hapo, ilimpelekea kuingia ndani zaidi ya mafunzo yake juu ya somo
hili. Kama tulivyokwisha kuona katika makala nyingine iliyopita, watu hao
wanapofanya utafiti wao hawaanzi kwa kusoma Biblia, isipokuwa wao huanza kwa
kutegemea uzoefu wao wenyewe na “mafunuo ya kiroho” wanayoyapokea. Ndipo
hutafuta maandiko ambayo huyalazimisha au kuyafanya yaunge mkono “mafunuo”
waliyopokea. Nasi tutatazama maandiko hayo hapo baadaye. Lakini napaswa kusema
kuwa, hata hao viongozi wa makanisa - ambao waliiamini imani hiyo ya kigeni,
hawakubaliani wao kwa wao kuhusiana na mafundisho haya, na namna ambayo
yanapaswa kutumiwa. Kwa vile hayaungwi mkono na maandiko ya Neno la Mungu, basi
haishangazi kuona kwamba mmoja wa waenezaji wa mawazo haya ameamua kusema
kwamba kwa kuwa Mungu ni mwenye enzi, basi anafunua mbinu mpya na bora kwa
ajili ya uInjilisti wa ulimwengu mzima. Wanachomaanisha ni kwamba Mungu
anaufunua kwao ufunuo huu usiopatikana katika Biblia, na hivyo wanajihesabia
wenyewe mamlaka ya kitume! Yote hii inaonyesha jinsi wanavyoiacha imani, kwa
vile wanayainua mafununuo yao na uzoefu wao juu ya neno la Mungu.
<<<<<ITAENDELEA>>>
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: