ROHO ZITAWALAZO MAENEO .SEHEMU YA PILI
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Hebu sasa tuyatazame
kwa karibu yale yanayofundishwa na waandishi hawa wa kisasa kuhusu vita vya kiroho.
Mafundisho yao juu
ya Vita vya Kiroho.
Wanaigawa vita ya
kiroho katika ngazi tatu. Kwanza, kuna kile wakiitacho mapambano ya “ngazi ya
chini”, ambayo wanamaanisha kutumia mamlaka ambayo Mungu amelipatia kanisa lake
kuwatoa mapepo toka kwa mtu mmoja mmoja. Hii imetolewa mfano wake vizuri katika
Injili na Matendo ya Mitume na hivyo siyo jambo lenye kuleta hoja kwetu. Aina
ya pili inaitwa mapambano ya “ngazi ya kishirikina” ambavyo wanamaanisha kuwa
ni kukabiliana na kuzifunga roho za uchawi, dini ya kishetani, ibada za sanamu,
na kadhalika, mambo ambayo kwa kawaida yanaleta athari zake ovu kupitia kwa mtu
fulani binafsi. Ngazi ya “juu” ya mapambano ya kiroho inaitwa mapambano ya
“kimkakati” au ya “kwenye anga za juu” ambapo maombezi yanahitajika ili kuzitambua
na kuzifunga roho mbaya za ngazi za juu, au mamlaka na nguvu, ambazo zinatawala
katika maeneo makubwa ya kijografia.
Hizi ngazi mbili za
mwisho ni mambo ya kukisia na ubunifu wa hawa waandishi wa kisasa, kama
tutakavyoweza kuona. Ile ngazi ya pili haina umaarufu mkubwa na inaingiliana
kwa kiasi fulani na ile ya tatu. Kwa hiyo nitazungumza kidogo juu ya ngazi hii
ya pili, tutakapoangalia vifungu vinavyohusiana nayo. Lakini ni ngazi ile ya
tatu ambayo mafundisho yao yanakazia, kwa hiyo kwa upana zaidi tutakuwa
tunatazama ngazi ya mwisho, kwa vile ndiyo hasa inayowakilisha udanganyifu na
hatari kubwa.
Ni namna gani roho
hizi mbaya zinatambulikana na watu kukabiliana nazo? Sawa, kwa wale ambao
wanaamini kuwa wameitwa ili kuhusika na aina hii ya vita, wanatumia muda wao
mwingi katika maombi kutafuta kutambua kwa njia za karama za kiroho na
"upambanuzi", jina au aina ya roho (moja au zaidi ya moja)
iliyoshikilia eneo fulani - inaweza ikawa ni roho ya kiburi, uchoyo, tamaa
mbaya au uchafu, ndipo tena wanakabiliana nayo katika vita vya maombi na
kuzifunga nguvu zake - hii inaweza ikachukua siku kadhaa au wiki kadhaa. Ili
kutambua ni roho gani inatawala juu ya mji, wanafundisha pia haja ya kile
wanachokiita kuwa ni "kutengeneza ramani za kiroho", kazi ambayo inahusisha
uchunguzi wa historia ya mji – hali ya mji huo kidini, kijamii na kikabila, na
historia ya nyuma, hali kadhalika kuhusu matendo maovu yaliyofanywa katika mji
huo, au kufanywa na mji huo, au yaliyofanywa dhidi ya mji huo - kurudi nyuma
miaka zaidi ya mia au kama si elfu na zaidi! Inafundishwa kwamba tendo hili
litatusaidia sana kuzitambua ni roho chafu za jinsi gani zinazoshikilia mji kwa
nguvu sana ili kwamba tuweze kuomba kwa ufanisi dhidi yake na kisha kuzifunga
nguvu zake! Nilishughulikia juu ya hoja hii ya kiushirikina katika ile makala
yangu ya kwanza.
Baadhi ya hawa
wahubiri wa kisasa wanasema kwamba hawataweza kuhubiri Injili katika eneo
lolote lile hadi kwanza wawe wametambua roho mbaya zinazotawala na wakazifunga
nguvu zake. Lakini sasa Yesu hakutumia mtindo huu katika mji wowote aliouendea.
Hatusomi chochote kuhusiana na mtume Petro au Paulo akishiriki katika aina hii
ya "vita vya kiroho" kabla hajautembelea mji wowote ule; au kuhubiri
Injili hapo. Hatusomi chochote kile kuhusiana na mtume Paulo kuzifunga roho za
uzinzi, uchoyo au tamaa mbaya kule kwenye miji ya Efeso au Korintho kabla
hajaanza kazi yenye nguvu hapo. Wala hatusomi popote kwamba katika nyaraka zao
kuwa mitume hao waliwasihi watakatifu kuomba dhidi ya roho za kimaeneo, kama
hawa waandishi na wahubiri wa kisasa wanavyotutaka sisi tufanye!
Makosa Mawili ya
Kimsingi
Fundisho hilo siyo
tu kwamba ni nyongeza kwa Maandiko, bali kwa kweli linaielezea vibaya na
kuidhoofisha kazi yote ya Kristo pale Kalvari na jinsi Injili ilivyo. Na
tutaanza kwa kuyatazama makosa mawili ya kimsingi ambayo mafundisho hayo
yanawatumbukiza watu ndani yake.
Kwanza, fundisho
hili linakanusha au kupunguza ushindi mkamilifu ambao Yesu aliutimiza pale
msalabani. Mafundisho yenyewe hauyakiri kikweli ushindi halisi ambao Kristo
ameupata dhidi ya nguvu zote katika ulimwengu wa roho, kwa niaba ya kanisa
lake, kadhalika na kwa ajili ya wanadamu, wala hawa walimu hawaheshimu kikweli
na kujali mamlaka zote na haki ambazo Mungu anazo za kuwaelekezea watu wake na
kujenga kanisa lake.
Kabla ya pale
Kalvari, Yesu mwenyewe alikuwa akitembea huko na huko akihubiri habari njema ya
ufalme wa Mungu. Hali kadhalika aliwatuma mitume pamoja na wanafunzi kuhubiri
Injili ya ufalme wa Mungu na kuwatoa watu mapepo na kuwaponya wagonjwa. Akiwa
amepokea msamaha na ushindi juu ya majeshi ya uovu pale msalabani, Kristo aliita,
akatuma na akawatumia mitume vile vile na watu wengine katika kulijenga kanisa
lake. Tunajua kuwa watu wengi waliokolewa kupitia mahubiri ya mtume Petro.
Filipo alitumwa na Mungu kuwageuza wengi watokane na dhambi na uchawi. Matendo
8. Na katika ile Matendo 11:19-21, tunasoma kuwa, “… mkono wa Bwana ukawa
pamoja nao, wao … waliohubiri Yesu ni Bwana kwa mataifa na watu wengi
wakaongezeka upande wa Bwana”. Mtume Paulo aliitwa na Mungu, Matendo 26:13-18;
katika ile Matendo 13:2 mtume Paulo alitumwa na Mungu. Watu hawa wote
walihubiri neno la Mungu kwa watu wengine, wakikiri kile ambacho Kristo
amekifanya pale Kalvari na watu wengi walimgeukia Bwana. Mitume waliwakomboa
waume kwa wake pia kutokana na roho za uovu na waliyakemea mapepo yaliyokuwa
yakitenda kazi ndani ya mtu mmoja mmoja. Matendo 13:8-11; 16:18; 19:12. Hayo
yote yalitokea pasipo hata kupata mafundisho yahusuyo na pasipo matumizi ya
mtindo huu wa kisasa ambao unaitwa "mapambano ya kimkakati"
Hebu niseme hapa
kwamba inapaswa iwe wazi kwetu, kwamba sio mahubiri yoyote na kila mahubiri
huwa na ufanisi. Mtume Paulo alikuwa makini katika kumhubiri Kristo, lakini
yeye alijikabidhi mwenyewe kwa ndugu zake pamoja na kwa kanisa, naye alikuwa
tayari kurejea nyumbani kwake katika mji wa Tarso, Matendo 9:26-31. Baadaye
tunamkuta kama mmoja wa manabii na walimu huko Antiokia, Matendo 13:1. Paulo
hakuhubiri tu mahali popote pale kulingana na mipango yake na ubunifu wake,
bali akiwa na ushirika na Mungu na akimtii Roho na kanisa, Paulo aliitwa na
Mungu kuihubiri Injili, Matendo 13:1, na alielekezwa na Roho maeneo ya kwenda
na maeneo ya kutokwenda, Matendo 16:6 – 10. Hivyo mtume Paulo anasema katika
Warumi 10:14 - 15. “…basi wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikiaje pasipo
mhubiri? Tena wahubirije wasipopelekwa?” Mtume Paulo pamoja na wenzake walikuwa
makini sana kuhusiana na wito huu wa kimungu - 1 Kor. 9:16,17 na alikuwa makini
zaidi pia kuwa angeweza kufanya kazi vizuri tu kulingana na wito wake, 2 Kor.
10:13-18.
Ikiwa tutaenda mbali
na wito wa Kimungu na karama; ikiwa tutaenda mbali na muda wa Kimungu katika
maisha yetu; ikiwa tutaenda mbali na Neno la Mungu - basi tusitegemee kupata
matunda ambayo Mungu anayategemea kutoka kwetu. Tunapaswa kuwa watumishi wa
Mungu, hii ina maana kwamba tunatakiwa kufanya yale tu anayoyasema na
kujikabidhi kwenye maelekezo yake na muda wake katika maisha yetu. Hatutakiwi
pia kwenda mbali zaidi ya karama na wito wetu. Hii inaweza kuwa pengine ndiyo
sababu wengine wanaenda pasipo kupelekwa? Inaweza kuwa ndiyo sababu kwamba wanapata
mafanikio kidogo au hawaoni mafanikio kabisa kutokana na mahubiri yao. Juhudi
ya jinsi hii ya wahubiri wasio na subira wanatafuta sasa kutunga au kubuni
mtindo fulani au mbinu ambazo zitaifanya kazi yao iweze kufanya kazi vizuri na
kuleta “mafanikio”! Inaweza ikawa ndiyo sababu wanaenda mbali zaidi ya yale
ambayo yanafundishwa na Maandiko ili kwamba wapate haya? Ninafikiri kuwa mambo
hayo pia yanachangia katika jambo hili lote la UInjilisti wenye mafanikio
pamoja na kushughulikia “mbinu mpya”. Hii yote haimaanishi kuwa ikiwa tumetumwa
na Mungu, basi siku zote tutaona ‘matokeo makubwa’, bali ikiwa tuna shauku ya
kumtumikia Mungu na kumzalia matunda na kiukweli kupeleka Neno lake kwa watu,
basi tutaenenda kwa kufuata Neno lake na Roho wake.
Kama tusomavyo
Injili na Matendo ya Mitume, tunaona kwamba watu wa Mungu walihubiri na
kushuhudia juu ya kifo chake na ufufuo katika utii wa amri zake na maongozi
yake au kwa kadiri fursa zilipojitokeza. Ijapokuwa walifahamu kuwa Kristo
ameangamiza mamlaka na uwezo, haina maana yoyote, kama tusomavyo katika habari
zao, kwa watu wa Mungu kuchukua UInjilisti "katika mikono yao
wenyewe" na kujaribu kuifanya kazi ya Mungu kwa ajili yake. Mitume
hawakufanya mambo kwa kukisia pale walipokuwa wakilitumia neno la Bwana au walipotumia
uwezo na mamlaka ambazo aliwapatia. Walimtii Mungu na Mungu aliwarejesha wengi
kwake na akadhihirisha nguvu zake kuu. Na Mungu aliupata utukufu! Hayo yote
yalitendeka pasipo hata kuzitambua au kuzifunga roho za kimaeneo! Hawakujaribu
kuongezea chochote kile juu ya yale ambayo Mungu alisema na kuyafanya ili
kuufanya uInjilisti uwe wenye mafanikio zaidi! Lakini hawa walimu wa kisasa
pamoja na wahubiri wanathubutu kuonyesha kwa mafundisho yao, kwamba yale ambayo
Kristo aliyafanya pale msalabani hayakutosha. Ndiyo, wanatangaza kwamba Kristo
alipata ushindi pale msalabani, lakini inaonekana kana kwamba hakuzivunja
mamlaka na enzi vya kutosha kwa ajili yao, kwa sababu wahubiri hawa wanaamini
kuwa roho chafu bado zina haki kisheria kuwashikilia watu katika giza na
kifungo na kuwa Injili haiwezi kupenya katika eneo linalotawaliwa na roho hizo.
Wanafundisha kuwa mtu anahitajika kwanza kufanya “vita vya kiroho” ana kwa ana
na mamlaka hizo pamoja na nguvu hizo kwa maombi, hadi kuzishinda nguvu zake
kupitia maombi kwanza, kabla Mungu hajazirejesha roho za watu kwake! Mawazo ya
aina hii kwa hakika ni ya jamii ya kiushirika tu na yenye milki ya ulozi zaidi
kuliko kuwa na mawazo ya kimaandiko. Mtazamo huu juu ya aina hii ya roho ya
kimaeneo pamoja na uwezo wao pamoja na aina hii ya kuzingatia katika maombi
dhidi ya roho ya uovu, hayapatikani katika maandiko ya neno la Mungu. Mtazamo
huu unaweza kumtukuza ibilisi kwa namna itakayowanyima watu wa Mungu ufahamu wa
kweli na nguvu ya Kristo ndani ya watakatifu wake na kupitia kanisa lake.
Inawafanya watu wamfikirie shetani zaidi badala ya kuweka mawazo yao kwa
Kristo, na kwa jinsi hiyo wanampatia shetani uwezo zaidi na utukufu na
kuwanyang'anya watakatifu ile imani yao ya kweli katika Mungu. Maandiko
yanasema kwamba, “Ijapokuwa hatujayaona mambo yote yakitiishwa chini ya nyayo
zake, lakini tunamwona Kristo.” Amina! Lakini sasa, badala yake walimu hawa wa
kisasa wanatutaka sisi tuyaone mapepo! Ni mafundisho madhaifu na manyonge kama
vile yenyewe yalivyo si ya kibiblia. Na hao walioyahamasisha mafundisho hayo
ndio huwa wa kwanza kukubali katika vitabu vyao kwamba watu wameharibiwa
walipokuwa wanajaribu kutumia mbinu hizo. Mafundisho hayo ni kashfa dhidi ya
mamlaka ya Mungu na shambulizi dhidi ya ushindi kamili wa Kristo alioupata pale
Kalvari, ambao ndio unaomruhusu kulijenga kanisa lake kulingana uradhi wa
mapenzi yake mwenyewe. Katika uweza ambao Mungu aliutumia katika kumfufua
Kristo kutoka katika wafu. (Efe 1: 19-23)!
Ndiyo tunatambua
kile kinachofundishwa na maandiko, kwamba mfalme wa uweza wa anga ni ile roho
itendayo kazi sasa katika wana wa uasi; Efe 2:2. Shetani huzungukazunguka kama
simba angurumaye akiwafunga wengi kuyatenda mapenzi yake na hafanyi lolote
isipokuwa ni kuua, kunyang'anya na kuharibu. Yeye hudanganya na kuwafunga wengi
katika vifungo. Mambo hayo pamoja na mengineyo yanafundishwa ndani ya maandiko,
na wala hiyo sio hoja yetu tena hapa. Nami sisemi hapa kwamba hatuwezi kuomba
kwa Mungu, kuhusiana na mambo ya aina hii; wakati ambapo tunajua hali na watu ambao
wanahitaji neema ya Mungu, rehema pamoja na wokovu wake. Lakini linapokuja
jambo la uenezi wa Injili na jinsi inavyoenezwa na kubadilisha maisha ya watu,
ndipo tunaweza kusema kuwa mafundisho hayo ya kisasa yameenda nje ya maandiko,
na yametumbukia katika kasoro na udanganyifu - yanawafanya watu wawe shabaha ya
roho za udanganyifu. Wanakubali kuwa Kristo amepata ushindi pale kalvari dhidi
ya shetani, lakini bado wanaamini kwamba wanatakiwa pia wapate ushindi zaidi
juu ya roho zinazotawala ju ya maeneo yote yanayokaliwa na watu.
Ni nini kinaipatia
roho hizo za kimaeneo haki ya kisheria kukamata mamlaka za aina hii juu ya
watu, kiasi kwamba hata iifanye Injili isiwe yenye mafanikio katikati yao? Haya
ati wanasema ni zile dhambi zilizopita za jumuia hiyo au mkoa na ile laana
iliyowekwa juu yake kwa sababu ya dhambi hizo! Napenda niwaambie ukweli,
wanachokifanya hawa walimu wa kisasa ni kuzijaza akili za watu wa Mungu mambo
yasiyo ya kiInjili yenye ushirikina mtupu na yenye kasoro nyingi. Kristo
amezichukua dhambi za ulimwengu mzima na amelipia gharama kubwa isiyohesabika
ili kufanya hayo. Kristo ni mwenye mamlaka zote za juu - ni Mkuu. Shetani
anaweza tu akaenda pale ambapo Mungu amemruhusu kwenda. Sawa, maandiko yanakiri
kuwa ipo haja ya maombi, kuhubiri, uInjilisti, kazi pamoja na ukombozi wa mtu
mmoja mmoja kutokana na mapepo; lakini kadiri ya haja ya kuihubiri Injili
inavyohusika, bado maandiko hayakiri kwamba kuna haja ya toleo lingine zaidi ya
lile alilolinunua tayari Kristo pale msalabani kwa ajili ya ulimwengu wala
maandiko hayakiri kwamba "dhambi zile za kihistoria" zilizopita za
maeneo ndizo zinaipatia roho za kimaeneo haki ya kisheria kuzuia Injili; wala
pia maandiko hayakiri kuwa ipo haja ya watakatifu kujiingiza moja kwa moja
katika makubaliano ya kiroho na hizo roho za kimaeneo kana kwamba roho hizo
zinahitajika kufungwa kabla ya Injili kufanyika na kuenezwa kwa mafanikio
yanayopaswa ( tafadhali angalia makala yangu ya kwanza ambamo jambo hili
limeelezwa kwa undani zaidi ).
Wakati mtume Paulo
alipokuwa Athene, hawakupatikana watu wengi waliomgeukia Mungu lakini pamoja na
hali hiyo, si Paulo mwenyewe wala si maandiko ya Neno la Mungu yanapohesabu
hali hiyo ya watu kutoipokea Injili kuwa ilisababishwa na nguvu kuu na mamlaka
au haki ya roho za uovu kupinga Injili au kazi ya Mungu. Mtume Paulo hakuianza
kuzishughulikia roho za kimaeneo katika maombi kwa sababu ya kuonyesha
"upungufu wa mafanikio" katika huduma yake. Mtume Paulo alikuwa na
ufahamu mkubwa zaidi na mafunuo kuliko hawa walimu wa kisasa, lakini yeye
hakukimbilia kwenye "mbinu za kiwango cha kimkakati" ili kuzishinda
"roho ya kuabudu sanamu" ambazo zilidhaniwa "kutawala"
katika mji wa Athene, katika jitihada yake ya kuushinda upungufu huu wa
mwitikio katikati ya watu. Unaona, hawa walimu wa kisasa wao wanasema kwamba,
watu kwa kweli hawapo huru kuitikia Injili hadi hapo tutakapokuwa tumezifunga
roho za kimaeneo! Mmoja wa waandishi, kwa kweli anapendekeza kuwa roho za
kimaeneo zinazotawala kule Athene, zilikuwa zenye uwezo mkubwa kiasi kwamba zilimfanya
mtume Paulo kuzishindwa na eti hiyo ndiyo sababu alipata mafanikio kidogo sana
huko! Lakini sio Paulo wala maandiko ya neno la Mungu yanayohitimisha jambo
hilo kuhusu aina hii ya "upungufu wa mafanikio". Badala yake, mtume
Paulo yeye anaendelea mbele na safari yake kwa mapenzi yake Mungu na mpaka
anapoingia katika mji wa Korintho, hatuoni popote pale panapomuonyesha
akijishughulisha na kazi ya kuzifunga roho za kimaeneo, na bado watu wengi sana
walimgeukia Bwana. Maandiko hayaelezei sababu hasa inayofanya watu wengi zaidi
wamgeukie Bwana katika eneo moja kuliko jingine, lakini yanatupa vidokezo na
kutuelekeza kwenye kanuni fulani fulani, ambazo tutaziangalia hivi punde.
Lakini jambo moja lenye uwazi ni kwamba
maandiko hawayahesabii "mafaniko" au "kupungua kwa
mafanikio" kwamba imetokana na mtu mmoja ambaye ameweza kuzishinda roho za
kimaeneo zinazotawala au la.
Ninadhani kuwa kama
hawa walimu wa kisasa wangekuwepo kule nyakati zile za Paulo alipotembelea
Athene, wangeweza kushauri kuwa Paulo aweze kuhudhuria masomo katika moja ya
seminari ya Kithiolojia ili aweze kujifunza kwanza "kanuni za kukua kwa
kanisa". Pengine wangeweza kumwelezea pia kuwa mtindo wake anaoutumia
katika UInjilisti bila shaka "haufanyi kazi" vizuri na hivyo anapaswa
kuzisomea "mbinu mpya za mafanikio" ya uenezaji wa Injili, ambazo
ndizo zimethibitishwa kuleta mafanikio! Wangeweza kumwambia kuwa yote
aliyoyafanya amekosea kwa sababu tatizo halikuwa ni Wathene binafsi isipokuwa
ni ile roho ya kieneo ya kuabudu sanamu ndiyo iliyokuwa inawazuia watu kule
wasiweze kuiitikia Injili. Mtume Paulo angelazimika kufundishwa vita vya kiroho
iwapo angependa kuona mafanikio katika kuieneza Injili! Angepaswa kujifunza
kuhusu kutambua majina ya roho chafu za kimaeneo na namna ya kuzikabili katika
kuzifunga kwa maombi! Asingetazamia kupata mafanikio hadi kwanza afahamu jinsi
ya kuyafanya mambo haya! Lakini sasa hebu fikiria jinsi Paulo alivyoweza
kuwashughulikia walimu wa uongo walionyemelea makanisa ya Galatia; sifikirii
kwamba angeweza kuvutiwa kwa vyovyote vile, badala yake angeweza kuwakemea kwa
nguvu kwa ajili ya kuichafua Injili ya Kristo.
Hii ndiyo sababu
inayonifanya niseme kwamba, mafundisho hayo wanayotuletea ni kashfa dhidi ya
mamlaka na busara za Mungu, ambaye huwaita na kuwatuma watu kwenda kuhubiri
Injili kulingana na amri na mafundisho ambayo ameyaweka kwa ajili yetu. Hawa
waandishi wa kisasa wanaweka busara yake Mungu na mamlaka za utawala wake
katika maswali. Wangeweza kuiita huduma ya Paulo kwa ajili ya watu wa Athene ni
jambo “lililoshindwa". Wako makini kutafuta mafanikio kiasi kwamba
wanadiriki kuisukumilia mbali amri ya Kristo – ya kwenda ulimwenguni kote
kuihubiri Injili - sasa kinyume chake wao wanazunguka huku na huko wakianzisha
amri zao wenyewe, na hivyo wanajiweka kinyume na busara za mamlaka ya Mungu na
utawala wake juu ya mambo haya.
Hata kama Mungu
alibariki au kama aliwaruhusu waweze kujaribiwa, hata kama kulikuwa na mwitikio
mkubwa wa watu au kidogo - bado mitume wa mwanzoni kabisa, wao pamoja na kanisa
waliendelea kumwangalia Mungu; wakijikabidhi kwake, wakimwamini yeye na
kumtukuza yeye! Hivyo ndivyo walivyofanya! Na kama hapakuwepo na mwitikio sana,
hawakumtilia shaka Mungu na kuanza kukimbia huko na kuko kujifunza na kubuni
"kanuni mpya za ukuaji wa kanisa"! Wao walikuwa wakiomba na
wakihubiri na walikuwa imara katika imani na upendo; kama vile tusomavyo katika
kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini wao pia hawakujishughulisha katika aina ya
maombi yanayohusika na kuzishambulia roho za kimaeneo kama ambavyo inavyohamasishwa
na waandishi hawa wapya.
Ijapokuwa wanakiri
juu ya ushindi wa Kristo pale Kalvari, lakini mafundisho yao hayo yanaufanya
wokovu wa roho za watu uonekane kuwa unategemea matokeo ya aina fulani ya
mapambano ya ana kwa ana kati ya majeshi ya kiroho ikiwepo roho chafu kwa
upande mmoja, ikipambana na karama za Roho na maombezi ya Wakristo kwa upande
mwingine; vita hiyo inayoelezwa humo ni ubunifu wa akili zao wenyewe tu (
ambayo wanaiazima kutoka kwenye milki za ulozi. Vitabu vya ubunifu - kama vile
kitabu cha Frank Perret ) na vinajaribu kuongezea kitu kingine juu ya ushindi
ambao Kristo aliupata pale Kalvari (msalabani). Katika maandishi yao, wakati
mwingine inatolewa mfano wa nguvu za upinzani zilizo sawa sawa zikipigana dhidi
ya roho. Wanaonyesha kuwa iwapo hutazishinda roho za kimaeneo zilizo za
kienyeji na za kimaeneo zinazomiliki eneo fulani, basi kazi ya Injili na wokovu
wa nafsi haiwezi kufanikiwa ipasavyo. Katika kutimiza hamu yao ya kupata
"mitindo ya mafanikio", wahubiri hawa pamoja na waandishi wao
hawajikabidhi katika Neno la Mungu na maelekezo yake ambayo Yesu ameyakamilisha
pale msalabani - wanafanya hayo yote kwa ajili tu ya kutafuta matokeo. Nasema
tena kwamba mawazo hayo ni ya kuanzishwa toka duniani, hayamtukuzi Mungu,
badala yake yanatukuza mafundisho yasiyothibitishwa ambayo husababisha
machafuko na kukata tamaa, na zaidi ya yote yanamtukuza shetani.
Mafundisho
yasiyothibitishwa ambayo husababisha kuchanganyikiwa na kukata tamaa.
Lakini hebu niseme
hapa kuwa shauri lao halijathibitishwa! Bila shaka haionyeshi kwamba wanaweza
kwa kweli kuonyesha kuwa jamii imebadilishwa kutokana na mafundisho hayo yao.
Zaidi ya hayo yote, wengi wa mashabiki wa mafundisho hayo wanaishi Marekani (USA).
Je huko kwao yameleta mabadiliko gani? Mchungaji mmoja wa kanisa moja kubwa
kule New York aliwahi kuandika kitabu kuhusu kazi za kanisa lake na jinsi Mungu
alivyopambana na mafundisho haya ya kisasa - na jinsi hata yeye alivyoumizwa
katika moyo wake kuona jinsi ambavyo dhana hii isiyo ya kibiblia inavyoweza
kushikilia akili za watu wa Mungu na inaendelezwa kufundishwa nchi nzima.
Lakini analiweka swali lile lile na linalofanana - kuelezea ni kwa nini basi,
iwapo mafundisho hayo ni ya ukweli, mbona hayabadilishi miji ya Amerika -
tunaambiwa na watu wengine kuwa California ya kusini ni mji unaowakilisha kituo
cha vivutio vya matamanio katika ulimwengu. Yako wapi basi mabadiliko hayo
makubwa katika miji ya Marekani iwapo mafundisho hayo ni ya ukweli? Lakini mtu
mwingine anaweza kuuliza hivyo hivyo kuhusu miji mingine mingi pamoja na nchi.
Mafundisho hayo hayo yamekuwa yakiendeshwa Uingereza karibu miaka 15 sasa kwa
kadiri ninavyofahamu, lakini sasa, yako wapi - basi mabadiliko hayo makubwa
yaliyoahidiwa na mafundisho hayo? Ninafikiri kuwa watu wengi wangekubali
kwamba, sio jamii tu yenye hali mbaya, isipokuwa kanisa leo limo katika hali
mbaya zaidi; kwa kusema kwa ujumla, liko katika hali mbaya kuliko ilivyokuwa
miaka 20 iliyopita. Tendo mojawapo lililosababisha machafuko, matengano,
maumivu ya mioyo, kuchanika kwa makanisa, kadhalika na kugawanyika kwa
makanisa, je huko ndiko kuzaa kwa wingi kwa imani hiyo mpya!
Mashabiki wa
mafundisho hayo wametengeneza mkanda wa video, ili kuwashawishi watu waone
namna ambavyo vita hivyo vya kiroho vinavyoleta mafanikio. Baadhi ya watu
wengine ambao wamechunguza yale yanayodaiwa na mikanda hiyo ya video, kwa
kuzuru hadi kwenye maeneo hayo waliyo chukulia mkanda huo pamoja na kupata
habari sahihi za maeneo hayo, wanatuambia kuwa mambo mengi, yaliyodaiwa ndani
ya mikanda hiyo yametiwa chumvi - na mara nyingi ni habari za uongo. Wale
wanaoamini katika imani au mafundisho hayo, kwa uasili wa kutosha wanaamini
kwamba "inafanya kazi" na wanajaribu kuonyesha watu kuwa ni kutokana
na mtindo wao mpya wa kuomba dhidi ya roho za kimaeneo, ndiyo iliyoleta
mafanikio makuu pale Injili ilipobanwa katika jumuiya fulani fulani. Lakini
hatuoni kuungwa mkono na maandiko ya Neno la Mungu katika maeneo hayo; na wala
haiwezi ikaonyeshwa kuwa hilo limekuwa ndiyo "ufunguo" au
"jawabu" la ufanisi wa uInjilisti kwa namna ya kimatendo, mbali ya
malalamiko ya hadithi zao.
Kwa kweli kitabu
kimeandikwa ambacho nimekitaja hapo punde tu, kwa usahihi kabisa ni kwa sababu
kumekuwepo na machafuko pamoja na maumivu ya moyo yaliyosababishwa na
mafundisho hayo. Mwandishi wa kitabu hicho yeye mwenyewe pia anaamini katika
vita vya kiroho dhidi ya roho, lakini anatueleza kuhusiana na kukata tamaa
pamoja na hofu iliyowanyemelea wakristo waliokuwa na matazamio ya hali ya juu
ya mafanikio kutokana na mafundisho hayo. Lakini hatimaye waligundua kuwa
haikufanya kazi yoyote; ile kama walivyotarajia na hata ikawasababishia
majanga! Hali hiyo imewasababishia kujisikia ni watu wawezao kunaswa na shida,
hofu na machafuko! Ingawaje anajaribu kuonyesha kuwa mambo yaliwaharibikia kwa
sababu ya ongezeko na ujinga wa watu wenyewe wa kutokujua kanuni za aina hii ya
mapambano; mbali ya hayo yote kitabu hicho pia kinakazia ukweli kwamba, upepo
huu mpya wa imani sio huo ambao mashabiki wake wamelalamikia kuwa ndio, na wala
hautoi matokeo kwa namna ambayo hawa waandishi wapya wangetupelekea sisi
tuamini hivyo.
Katika kitabu chake
cha "Roho za Kimaeneo", (kurasa za 17, 18), Wagner anakiri kuwa
katika hali nyingi mtindo huu hautoi matokeo yanayokusudiwa. Anatoa sababu gani
hapo? Haya, anatueleza kuwa shetani “anapinga mwenendo wa mambo". Je, hii
ina maana kwamba huyo shetani ana uwezo mkubwa kiasi kwamba watu hawawezi
kuokolewa? Hapo haelezei kwa ufasaha. Lakini anatuelezea kuhusu uwezo, na werevu
alionao na kwamba shetani anawapinga watakatifu, kupitia roho zenye kiwango cha
ngazi tofauti; ili watu wasitambue mapenzi ya Mungu ipasavyo! Na kwamba kwa
kadiri kiwango cha roho za kimaeneo kinavyozidi kuwa juu zaidi ndivyo nguvu
zaidi zinahitajika ili kuzishinda! Hali kadhalika anatuambia kuwa Wakristo
wengi hawajajiimarisha ili kukabiliana na aina hii ya roho za viwango vya juu.
Kwa hivyo basi inaonyesha shetani anaweza kuzuia watu kuyatambua mapenzi ya
Mungu katika mapambano haya; na hata kama watatambua aina ya roho zinazopaswa
kushughulikiwa bado watu wengi hawana msimamo wa kiroho ili kuyashinda. Jambo
hili humpatia mtu utukufu na humpatia pia uwezo mwingi shetani. Kwa hiyo
hitimisho tunalolipata hapo ni kwamba wokovu wa roho za watu unategemea aina
fulani ya watu walio jaliwa kuwa na uwezo wa kutambua mambo katika
"ulimwengu wa kiroho". Pasipo uwezo wa "kutambua" jina na
tabia ya roho za kimaeneo na pasipo uwezo wa kiroho wa mtu binafsi pamoja na
msimamo wa mtu binafsi kuyashinda hayo katika maombi - hakutakuwepo na ufanisi
wa UInjilisti! Hakika, kama utasadiki porojo hizo zisizo na msimamo wa
Kibiblia, basi wewe unaweza kuamini lolote lile! Ili kuonyesha jinsi mafundisho
haya yanavyokaribia kuingia kwenye ulozi, hebu uniruhusu ninukuu yale anayoyasema
mwishoni mwa ushauri wake hapo juu; anasema kuwa, ".... tunapogundua kuwa
sisi ni muhimu katika kuzifunga (roho za kimaeneo) ..... tutafanya vema
kutafiti uwezekano wa chanzo chake katika ulimwengu wa kiroho". Kutafuta
chanzo, na sio katika maandiko, isipokuwa katika ulimwengu wa kiroho! Je
wanatutaka sisi tuwe waaguzi, wachawi au waangaliao mambo ya roho? Pasipo
kuelewa, hivyo ndivyo inavyotendeka katikati yao. Wao hawaenendi kiroho, haupo
utambuzi wa kiroho na kweli, hii sio maombi ya kiroho. Hivi sio vita vya kiroho
- huu ni udanganyifu. Wanafanya mawasiliano ya kiuharamu na yenye hatari na
ulimwengu wa maroho na hivyo hudanganyika (ninaposema ulimwengu wa kiroho
ninamaanisha kuwa wanafanya mawasiliano na maroho maovu, au kujiweka katika
hali inayoweza kuwashawishi na kudanganywa na maroho maovu). Tutaangalia zaidi
kidogo hilo hapo baadaye kidogo. Lakini sasa hapa tunaona kwamba ili kuweza
kusimulia kushindwa kwa mafundisho yao pamoja na maumivu ya moyo
yaliyosababisha - wanatafuta kiurahisi tu kubuni makosa zaidi.
Niruhusu nitaje hapa
yale ambayo nimewahi kuyasema mahala penginepo yaani, tunajua kwamba Bwana
analijenga kanisa lake na anayaheshimu mahubiri ya neno lake na hakika hujali
anapoona watu wake hujinyenyekeza wenyewe katika maombi na kuutafuta uso wake
kwa mioyo yao yote. Inawezekana kuwa Mungu anafanya kazi katikati ya watu ambao
baadhi yao viongozi wao huamini katika mafundisho haya na kuyashikilia, lakini
kazi yake ya neema haiwezi kuhalalisha mafundisho hayo yote ambayo yameshikiliwa
na watu ambao wanaweza wakawa ndio wanaoongoza kazi mahala fulani. Tunajua
hivyo kutokana na historia, pia tunaweza kuziona kanuni hizo sisi wenyewe ndani
ya maandiko pia. Lakini napenda niseme tena kuwa kule kuona Mungu akitembea
katikati ya watu katika uweza wa kuokoa, haihalalishi kila mafundisho
yaliyoshikiliwa na hao wanaokuwa katika uongozi wa sehemu fulani, na wapo mbali
sana katika kuonyesha kuwa mtindo wao huo mpya kwa kweli unafanya
"kazi" au kwamba mtindo huo ndio unaohusika katika kuwaleta watu wengi
katika ufalme wa Mungu.
Katika mambo ya
matukio ya kiroho ya nyuma na katika kujua kwa nini mambo hutokea au kutotokea,
mara nyingi maandiko hayatoi jibu la maswali yetu au kufunua kila kitu. Na
kutokana na hoja hiyo, Mungu anatuonya katika Kumbukumbu la Torati 29:29 kwamba
"mambo ya siri ni ya Bwana Mungu wetu, lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu
sisi na watoto wetu milele". Hatutakiwi kupenyeza tu katika mambo ambayo
Mungu hajatufunulia kwa neno lake. Ni busara zake Mungu, kwamba ameyaweka mambo
fulani mbali na ufahamu wetu. Lakini tunatakiwa kuyazingatia kikamilifu mambo
ambayo ametufunulia tayari. Hayo yatakuwa ni yenye kutuletea faida kwetu -
katika kukuza ufahamu wa Mungu na kuimarisha imani yetu. Lakini katika jitihada
zao za kupata matokeo wakati wote na katika sehemu zote, hawa wahubiri na
walimu wa kisasa wanapenyeza kwenye mambo yasiyoonekana - ambamo wanajigamba
juu ya maono yao, mafunzo yao, na uzoefu wao wa mambo ya juu - ambayo ni mazao
ya akili zao za kimwili tu na wala hayailetei jamii mabadiliko katika maisha
yao. Kama tunavyoambiwa katika Kolosai 2:18 na wala hawashikilii kichwa cha
kanisa, Yesu Kristo. Ijapokuwa Mtume Paulo anaongelea maalum kuhusu wale
wanaotafuta kuwarejesha watakatifu kwenye mila za kiyahudi, ile sura nzima Kolosai
2:6-19 inashauri sana juu yetu, kuhusiana na mambo haya ya mafundisho mapya.
Ulinganifu wa
kimaandiko - kanisa katika kuomba.
Nyakati za matendo
ya mitume kanisa lilijiheshimu na kuomba kwa jinsi ya tofauti kabisa
ukilinganisha na hawa walimu wa kisasa wanavyoamuru. Kulipotokea mateso kule
Yerusalemu, kanisa halikukabiliana na roho chafu katika maombi yao.
Kanisa halikukiri
juu ya roho za kimaeneo kwamba ndizo zinazowashikilia wanaume na wanawake hata
wasiupokee ufalme wa Mungu. Wao waliomba kwa Mungu na kukiri juu ya mamlaka
zake na uungu wake. Kulikuwepo na upinzani mkali wakati huo ( kuliko hata
ilivyo sasa naweza kusema ) juu ya kuihubiri Injili; naye ni nani anayeweza
kupinga kwamba shetani anachochea ugumu wa mioyo ya hao wasiotaka kuamini ili wapinge
kazi ya Mungu? Lakini sasa hebu sikiliza jinsi kanisa lilivyoomba katika
Matendo 4: 24-30, kwanza walitangaza busara kuu na uweza, wa Mungu juu ya yote
mengine, wakipokea maelekezo na hamasa kutoka katika maandiko ya neno la Mungu!
Ndipo wakatangaza:
". . . Basi
sasa ee Bwana, yaangalie matisho yao, ukawajaalie watumwa wako kunena neno lako
kwa ujasiri wote, ukinyoosha mkono wako kuponya, ishara na maajabu zikafanyike
kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu".
Hebu tazama hapo
watumishi hao wametishwa, lakini maombi yao yameelekezwa kwa Mungu, wala
hawayaelekezi dhidi ya aina yoyote ile ya roho za kimaeneo zinazotawala
Yerusalemu, wanayohisia juu ya mamlaka za Mungu na za ushindi wake juu ya mambo
yanayowapata, na wanaomba sio kwa ajili ya kukabililiana na roho za kimaeneo
ili kwamba ziweze kufungwa, lakini wao wanaomba ili kwamba waweze kulisema neno
lake kwa ujasiri na kwamba Bwana aweze kutenda kazi kwa nguvu katikati yao.
Lakini hata hivyo wanakiri juu ya mamlaka za utawala wa Mungu na ushindi wake
kupitia Kristo. Hayo hayawaelekezi kufuata mambo ya kuhisihisi - wao hawachukui
kutoka kwa Mungu ule uweza wake mkuu na kutafuta kumtumikia kwa ajili ya
kutimiza matakwa yao na mipango yao kwa ajili ya ukuaji wa kanisa. Isipokuwa
wanabakia wakiwa wamejikabidhi kwa Mungu na katika busara zake wakikiri kuwa
wao ni watumishi wake tu. Hilo ndilo kanisa ambalo linamwinua Yesu juu zaidi
kuliko chochote kile. Na ijapokuwa wanadamu na mapepo wanaweza kupanga, wao
wanaendelea kubakia wakiwa wamekaza macho yao kumwelekea Kristo- na kile
alichokikamilisha kupitia kifo chake na ufufuo wake - yote mawili katika fikara
zao na maombi yao. Hawatafuti kuongezea chochote kile juu ya ushindi kamili
pale Kalvari, au kunyang'anya uwezo wake na maana yake kwa kuhesabia uwezo huo
juu ya "roho za kimaeneo" ambao hawanao! Maombi yao yanakazia macho
kwa Kristo na mamlaka zake na wanamtukuza yeye, sio shetani au roho za
kimaeneo.
( Kuhusiana na
maombi na kanisa, vile vile na kuhubiri Injili kama njia ya Mungu ya kuokoa hao
waaminio, tafadhali soma sehemu ya pili ya makala ya kwanza ya "Kutubu kwa
ajili ya Dhambi za Taifa")
Na ni kweli tunaona
kwamba wanayo sababu nzuri inayowafanya wafikiri na kuomba namna hiyo. Katika
Wakolosai 2:15, tunasoma kuhusu kifo cha Kristo pale Kalvari kwamba; "...
akisha kuzivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri
akazishangilia katika msalaba huo". Na kwa hiyo Mungu alikuwa na uwezo wa
"kutukomboa kutokana na nguvu za giza na kutuingiza katika ufalme wa mwana
wake mpendwa".
Na katika Waebrania
2:14 tunaambiwa kuwa, "Yesu Kristo alishiriki damu na mwili vivyo
hivyo;.ili kwamba kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti
yaani Ibilisi".
Na mtume Yohana
anakubaliana na hilo pale anaposema katika Yoh 3:8 "... kwa kusudi hili
mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziharibu kazi za shetani"
Ukuu wa kimungu
alilonao Kristo na mamlaka zake juu ya mambo yote umetangazwa katika Wakolosai
1:16. " kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na
vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana, ikiwa ni vitu vya enzi
au usultani au enzi au mamlaka, vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili
yake."
Haupo wito wowote
kwa kanisa tena ili kuzidi kuharibu "mamlaka na uweza" kwa kuzifunga
na kukemea roho za kimaeneo kana kwamba zenyewe zinayo haki ya kisheria juu ya
nafsi. Yesu Kristo alizichukua dhambi za ulimwengu mzima na kwa hiyo yeye ni
mwokozi wa wanadamu wote (1Tim 4:10) hata kama wanaamini na kupokea wakovu huo
au hapana. Yeye amenunua msamaha na wokovu kwa ajili ya wanadamu kwa damu yake
mwenyewe na kwa hiyo imeandikwa kwamba, "Mungu alikuwa ndani ya Kristo
....... asiwahesabie makosa yao...". Kwa wale ambao wangeweza kuamini Injili
na wakapatanishwa na Mungu, Mungu asingeweza tena kuyashikilia dhidi yao mambo
yao maovu ya dhambi zilizopita (2 Kor 5:19) isipokuwa yeye huwaachia na
kuwasamehe bure - pasipo malipo yoyote. Wale ambao wanaukataa na kuupinga
wokovu wa bure wa Mungu na ambao wanaendelea kuzishikilia dhambi zao,
watahesabiwa kuwa wanapaswa kuhukumu.
Lakini sasa haya
mafundisho yao ya kisasa kwa kweli yanaifanya damu na dhabihu ya Bwana wetu
Yesu Kristo pale msalabani ionekane kuwa haina maana. Mafundisho hayo yanamkataa
yeye aliye wa kweli na mwenye mamlaka alizozinunua na kuzipata kama mwokozi wa
wanadamu wote kupitia kumwagwa kwa damu yake. Kristo amekwishachukua msamaha wa
wale wote watakaoamini. Lakini mafundisho haya ya kisasa yanatangua kazi ya
msalaba kwa kuzihesabia roho za kimaeneo haki ya kisheria katika kuwaweka watu
nje ya ufalme wa Mungu, kwa sababu ya kile wanachokiita wao kuwa ni “dhambi
zisizoungamwa na kusamehewa za eneo la kijografia katika mkoa au jumuia.” Wao
wanafundisha kuwa roho za uovu bado zina uwezo juu ya eneo lolote lile, ambalo
mambo yaliyopita ya kijamii au mengineyo ya uovu uliotendeka. Imani za aina hii
zinashikiliwa na kizazi kipya cha roho za wanadamu wa leo; na hapo ndipo imani
ya aina hii inakotokea, kuliko kutokea katika Biblia. Wanasema kuwa maovu
yaliyopita yanahitajika yapate "ondoleo" (toleo) lake, kwa wakristo
kuungama na kuzitubia dhambi hizo, na kutumia damu ya Yesu, kabla roho za
kimaeneo hazijaweza kufungwa! Kwa hiyo wanalundika kosa moja juu ya kosa
jingine. Jambo hili limetazamwa ipasavyo ndani ya makala yangu ya kwanza.
Ikiwa tutafuata
mafundisho hayo yao, tutagundua kwamba kila mtu katika ulimwengu huu sasa
hawezi kusamehewa mara moja, wala kuokolewa na kukombolewa kutokana na nguvu za
shetani kwa sababu ya msalaba. Hapana; ni kweli kwamba haiwi mara moja kwa
haraka. Lakini Kristo akiwa amenunua wokovu huu wa bure na mkamilifu kutokana
na dhambi, kuhukumiwa na uwezo wa shetani. Biblia inatangaza kwa nguvu sasa
kuwa, "Injili ya Kristo ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila
aaminiye." Rumi 1:16. Hivyo ndivyo maandiko yanavyofundisha; na kwa sababu
ya wokovu hutujia pasipo haja ya kuzitambua na kuzifunga hizo zinazoitwa roho
za kimaeneo - isipokuwa kama unataka kubatilisha matokeo ya damu ya Yesu pamoja
na ushindi wake dhidi ya mamlaka na uwezo.
Hata hivyo ili
kuonyesha kuwa sitii chumvi ule umaana wa jambo hili pale ninaposema kuwa
mafundisho haya yanawakilisha mashambulizi juu ya Injili ya Yesu, hebu tutazame
kwa makini yale ambayo kiongozi maarufu wa thiolojia hii mpya (George Ottis jr)
anavyotangaza. Katika kutoa mhadhara wake kwa kusanyiko la YWAM huko Tacoma,
Washingtone mnamo mwaka 1981, yeye pamoja na mambo mengine alisema kwamba:
"...Kristo
hajatukomboa kwa kutupatia uzima wake kama fidia kwa ajili ya dhambi zetu, ili
kwamba apate kutuachilia. Ikiwa tutazikubali asili au (chanzo) ambacho Kristo
kikweli amenunua......wokovu wetu kwa damu yake ........ naye alimlipa Baba.
Hivyo mtindo huu kabla ya yote unamwonyesha Mungu ambaye ni Baba kana kwamba
yeye ni mwenye kulipiza mambo na ni mwenye kiu ya damu na kwa ujumla asiye
patana na msamaha utolewao na Biblia."
“Msamaha....... ni
kiburudisho cha madai ya haki.......itakuwa ni vigumu kwa Mungu kuwa nayo kama
mtunzi wa nyimbo anavyoiweka, "alilipa deni langu na akanisamehe dhambi
zangu zote"
“Manukato ya toleo
la Kristo yaliendelea katika utii wake kwa sheria za kimwili kwa niaba ya
mwenye dhambi. Kristo katika maisha yake alitii sheria za mwili kwa ajili yetu
na hayo ndiyo kwa uhalisi ni manukato ya toleo.”
Ijapo kuwa mwandishi
huyo haelezei kwa uwazi sana kutokana na mpangilio huu, lakini bado hajayakana
mawazo kama hayo, na wengine wanaamini kwamba yale aliyo yaandika tangu hapo
pia yamejaa mawazo yenye kukaririwa. ( Kuyatambua mambo ya hapo juu, pamoja na
taarifa nyinginezo juu ya mwandishi huyo aitwaye Ottis na mafundisho yake, hali
kadhalika na mkanda wa video nilioutaja hapa kwenye makala hii angalia
www.Bibleguide.com. Makala inayoitwa “George Ottis na mafundisho yake ya
udanganyifu yaliyotayarishwa na Profesa J.S Malan – yote katika lugha ya
Kiingereza.) Shirika lile ambalo linaongozwa na Ottis ndilo lililo husika na
utayarishaji wa mkanda huo wa uongo wa video. Kwa sasa wameutayarisha mkanda wa
pili wa video - ambao niliutaja mwanzoni - ambao unakusudia kuonyesha kwamba
jumuia fulani fulani zimebadilishwa kupitia mafundisho haya ya roho za
kimaeneo. Ottis pia anaheshimika kama mwanzilishi wa mawazo ya "ramani ya
kiroho" ambayo nayo tutalitazama tutakapokuwa tukifikiria Ezekiel sura ya
4. Kama nilivyokwisha kusema, msingi wa kweli kuhusiana na maisha ya dhambi ya
mwanadamu na hitaji lake la toba, pamoja na tabia na kusudi la kifo cha Yesu
pale msalabani - inaonekana ilikuwa ni jambo lenye kutia giza (lisilo eleweka)
kama si kupingwa kwa moja kwa moja na mafundisho haya ya kisasa! Ninatumaini
kwamba unaweza ukajionea mwenyewe kutokana na maelezo ya hapo juu, kuwa
hayawakilishi mambo mawili yote kwa pamoja, yaani ni mashambulizi juu yake na
kuukana wokovu ambao Kristo amenunua kwa mapenzi ya damu yake. Ni kuyakana
maisha ya dhambi ya mwanadamu ambayo ndiyo yanayomtenganisha na Mungu na pia ni
kukana hitaji na tabia juu ya wokovu wetu wa ajabu kutokana na dhambi pamoja na
milki yake.
Ni Injili Nyingine!
Hili sasa
linatupeleka kwenye msingi wa pili wa makosa ya mafundisho haya, ambayo pengine
ni ya hatari zaidi kuliko jambo lingine lolote lile kwa namna inavyodhalilisha
na kushambulia moyo halisi wa Injili. Mafundisho hayo yanaonyesha kiini cha
matatizo kisiwe ni dhambi, ugumu na kutokuamini kwa moyo wangu, bali uonekane kwamba
ni majeshi ya uovu ya kiroho ndiyo yanayonizuia mimi kushindwa kumkubali Mungu.
Wanasema kwa ujumla sio mimi mwenyewe wala sio hali ya moyo wangu ambayo ndiyo
tatizo, isipokuwa ni roho chafu ndizo zinazonizuia nisimjue Mungu na kufungika
katika giza. Chini ya mafundisho hayo, wenye dhambi sasa wamekuwa ni (wajinga)
nao wamewekwa kuwa ni shabaha ya roho za uovu na kwamba inaelezwa kuwa, sio
hali ya mioyo yao ambayo ndiyo tatizo, isipokuwa ni hizo roho za kimaeneo
ambazo ndizo zinazowazuia wenye dhambi kushindwa kuitikia! Wazidi kudai kuwa
kwa sasa haiwi tena ni dhambi za mtu binafsi kuwa ndiyo tatizo, isipokuwa sasa
tatizo ni dhambi za jumuia, au miji, ambazo ndizo zinazohusika na roho hizi za
kitaifa! Kwa sababu wao huyaamini mambo hayo, pia kuyafundisha kuwa njia kuu ya
kuleta wokovu kwa watu sio kuihubiri Injili, isipokuwa ni kwanza kuzifunga roho
za kimaeneo! Mahubiri ya Injili yanachukua nafasi ya pili na bado yanaweza tu
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi pale tu ambapo roho za uovu zitakuwa zimefungwa
kwanza! Kwa hakika mafundisho ya jinsi hii yanawakilisha Injili nyingine - ni
mashambulio kwenye ile sababu ya kimsingi na halisi juu ya kwa nini Yesu
alikufa msalabani! Ni kukana mafundisho ya Yesu mwenyewe kuhusiana na mtu,
kuhusiana na dhambi, kuhusiana na shetani, na kuhusiana na hukumu.
Mwandishi mmoja
anatuambia kuhusu kiongozi mmoja maarufu wa kanisa huko Amerika ya kusini
ambaye kwa kawaida huomba yeye mwenyewe kwa muda wa wiki moja kabla hajaanza
kampeni zake. Anafanya hivyo ili aweze kuzitambua na kuzifunga mamlaka ya nguvu
za giza juu ya mji huo ambao amekuja kuuhudumu. Mpaka “anapojisikia” kuwa
amelipata lengo lake, ndipo anapoanza kuhutubia katika mikutano ya hadhara
akiwaelezea watu kuwa “sasa” wako huru kumjia Kristo! Watu hawa wanajiinua wenyewe
pamoja na mafundisho yao, wanajiinua juu zaidi ya Kristo pamoja na mitume ambao
hawakuwahi kufanya madai ya jinsi hiyo kwa watu waliowajia. Kristo pamoja na
mitume walikuja wakihubiri habari njema na wakiwasihi waume kwa wanawake
watubu! Kwa maneno mengine, watu hao wanafundisha kuwa tatizo halisi sio ugumu
wa moyo wangu mwenyewe wala sio dhambi, isipokuwa ni hizi roho za kimaeneo
ambazo zinatakiwa kutambuliwa na kufungwa! Sio kupinga kwa moyo wangu kuwa
ndilo tatizo, isipokuwa kupinga kuwa roho za kimaeneo ndicho kinachoniweka nje
ya ufalme wa Mungu. Wanataka tuelewe kuwa ni roho za kimaeneo sasa ndizo zenye
kuhusika na kiburi, tamaa mbaya na ugumu wa moyo wangu - kadhalika na
kutokuamini kwangu?- na sio mimi mwenyewe. Mara tu mtu akizifunga roho za kimaeneo
katika jamii basi, wenye dhambi wanakuwa wamewekwa "huru" kumjua
Kristo! Mwinjilisti mwingine hawezi kuhubiri katika mji mpaka pale
watakapojisikia kuwa wamezishinda katika maombi hizi roho za kimaeneo ambazo
zinaushikilia mji huo kwa nguvu zao, na mmoja wa viongozi maarufu wa kanisa
ambaye amehamasisha makosa hayo anatangaza kuwa: "ninafahamu vizuri pasipo
shaka yoyote ndani yake, kuwa mahubiri makubwa hayawezi kuzisababisha roho za
watu kuokoka na kanisa kukua ... Hapana, isipokuwa ni pale utakapozishusha
chini ( kuziangusha ) nguvu za giza zililzokuwa zinawazuia watu kumwishia Mungu
katika maisha yao; hiyo ndiyo itakayosababisha kanisa kukua". (Makala ya
Larry Lea katika kitabu cha "Roho za Kimaeneo." – Territorial
Spirits” - Kilichoandikwa na Wagner, ukurasa wa 91 kilichokubaliwa na “Karisma
na Maisha ya Kikristo” 1989, Strang Communication Company.)
Je watu hawa
hawadhihaki kwa kumpinga Kristo mwenyewe? Mwandishi wa hapo juu anasema kuwa
ana uhakika mkamilifu kwamba - hata mahubiri makubwa, hayawezi kuokoa roho za
watu au kulijenga kanisa! Lakini tazama mwana wa Mungu aliwaambia wanafunzi
wake, "Nendeni katika ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Yeye aaminiye na kubatizwa ataokoka". Mk 16: 15,16. Mtume Paulo naye anaurudia
usemi huo huo, "siionei haya Injili ya Kristo kwa sababu ni uweza wa Mungu
uletao wokovu kwa kila aaminiye.” Rumi 1:16. Pia katika 1Kor.1:17,18,21 kwa
kuwa Kristo hakunituma ili kubatiza isipokuwa kuihubiri Injili ... kwa sababu
neno la msalaba .... ni nguvu ya Mungu iletayo wokovu .... Mungu alipenda
kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa". Maandiko
mengineyo mengi yangeweza kunukuliwa ili kuthibitisha tangazo lake Mungu
litolewalo kwa ajili ya wokovu wa hao waliopotea na kulijenga kanisa lake,
lakini sasa hawa waandishi wa kisasa wanapinga moja kwa moja ukweli huu kwa
hiyo imani yao. Kristo hakuwaagiza wanafunzi wake, “kwenda kuzitambua na
kuzifunga roho za kimaeneo ambazo zinawazuia watu washindwe kuokoka!”
Ijapokuwa waandishi
hawa wanaamini kuwa kuhubiri Injili ni njia ya kuokoa roho za watu, bado wao
huanza kwa kuzifunga roho za kimaeneo kana kwamba hilo ndiyo tendo la mwanzo na
lenye msingi katika kanisa. Na kule kuihubiri Injili sasa hushika nafasi ya
pili katika mipango yao - na bado Injili hiyo inategemea kikamilifu mtindo huo
wao wa kuomba dhidi ya roho za kimaeneo. Hili ni tatizo kubwa la kasoro na ni
sawa na kusema kuwa, "Sawa, ni kupitia Yesu kristo mtu anaweza kuokolewa,
lakini unahitaji kutahiriwa kwanza". Ukumbuke kuwa katika makanisa ya
Galatia waliamini mambo mengi yaliyo mazuri na yenye haki kuhusu Kristo, na
msamaha pamoja na wokovu ambao tunapata kwa yeye. Lakini wao waliongezea
mafundisho yasiyo ya kiinjili, ambayo yalidhalilisha na kutishia uwepo wa imani
yote! Mtume Paulo amesema "wamelogwa" kwa mafundisho ya aina hiyo. Na
ijapokuwa wahubiri hawa wa kisasa ambao wanafundisha mapambano dhidi ya roho za
kimaeneo, wanaweza pia wakaamini mambo mema na yenye haki vile vile, bila
kujali kiasi gani wamejiingiza katika kujishughulisha na kazi
"halisi" ya Mungu, hawajali kuwa mafundisho hayo yahusuyo roho za
kimaeneo ni uchawi wenye hila ndani yake! Inayodhalilisha imani ya Injili.
Mafundisho haya
hayaji kutoka kwa Yesu wala kutoka kwa mitume, au tusemeje sasa? Je Yesu
alishindwa kuzitambua na kuzifunga roho zilizokuwa zinatawala Kapenaumu?
Korazin na Bethsaida? Huko kulikuwa na mwitikio mdogo sana kufuatia mafundisho
yake ijapokuwa amefanya kazi kwa nguvu kwao. Mat 11:20-24. Je tunaweza kulaumu
upungufu wa mwitikio wa watu hawa katika miji hiyo kuwa unatokana na roho za
kimaeneo, au kutokana na kushindwa kuyatambua majina ya roho hizo za kimaeneo?
Au je, roho hizo za kimaeneo zilikuwa na mamlaka ya "kuzuia" huduma
ya Yesu kwa sababu alikuwa bado hajafa pale msalabani (Kalvari)? Hapana! Hakuna
lolote kati ya mawazo hayo ambalo lina ukweli wowote. Yesu alisema kwamba,
ikiwa kazi alizozifanya katika miji hiyo zingefanyika huko Tarso na Sidon,
wangekwisha kutubu siku nyingi iliyopita na hata Sodoma ingesalia hadi leo.
Yesu anawakaripia watu wa miji hiyo ya Israel kwa sababu ya kukataa kwao
kutubu. Anawakaripia kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kulingana na yote
aliyoyasema na kuyafanya bado hawakuweza kuzioacha dhambi zao. Walikataa
kumwamini na kumruhusu Yesu ayabadili maisha yao. Hiyo ilikuwa ni ugumu wa
mioyo yao wenyewe na kutokuamini ndiyo iliyosababisha upungufu wa mwitikio, na
ilikuwa ni kutokana na hilo ndio maana Yesu alitangaza hukumu kali juu yao.
Walipaswa kujilaumu wao wenyewe na sio shetani wala sio roho za kimaeneo! Ikiwa
tutafuata maelezo basi haya ndiyo mafundisho halisi ya maandiko ya neno la
Mungu. Katika matendo ya mitume hatumsomi mtume Paulo akijifungia ndani
mwenyewe kwa siku nyingi ili kujishughulisha na mapambano ya moja kwa moja na
roho chafu, kabla hajahubiri katika mji - kana kwamba hiyo ilikuwa mbinu ya
lazima! Hapana. Tunajua kuwa yeye alikuwa ni mtu wa maombi, lakini alipowasili
katika miji na jiji, kwa kawaida anasema habari zake kwamba alikuwa akienda
moja kwa moja kwenye masinagogi, au sehemu za masoko kumhubiri Yesu Kristo kwa
watu. Na pale wayahudi walipoupinga ukweli wa Injili, Mtume Paulo analaumu juu
ya mioyo yao. Mtd 13: 45,46.
Mtume Paulo
alipokuwa huko Athene na alipoona mji mzima umekabidhiwa kwa masanamu kwa mara
nyingine yeye hakujiingiza katika "ulimwengu wa kiroho" ili kuzifunga
roho za ibada za masanamu. Hapana, bali yeye alienda katika masinagogi na
sehemu za sokoni kumhubiri Kristo na ufufuo! Mtd 17:16-19. Sio wengi
waliookolewa kule Athene. Na baada ya kuondoka hapo alielekea kwenye mji wa
Korintho. Baadaye alipokuwa akiwaandikia Wakorintho, aliwaambia kuwa, alifika
kwao baada ya kuondoka kule Athene akidhamiria asikijue kitu kingine chochote isipokuwa
"Yesu Kristo aliyerubiwa", 1Kor.2:2. Pengine kudhamiria huku kwake
kuliweza kuimarishwa ndani yake alipoona uhafifu wa busara ya kibinadamu ambayo
iliwashika watu wengi wa Athene, ambayo ndiyo iliyowafanya washindwe kuupokea
ukweli wa Mungu. Hata kama hiyo ni kweli au hapana, Paulo mwenyewe analifafanua
kwa ajili yetu, kwa nini iko hivyo kwamba watu hawapokei kweli ya injili.
"Kwa kuwa
Wayahudi wanahitaji kuona ishara, Wayunani wanatafuta hekima, lakini
tunamhubiri Kristo aliye sulubiwa, ambaye kwa wayahudi ni kikwazo na kwa
Wayunani ni upuuzi."
Anaendelea kueleza
kuwa sio watu wengi wenye hekima na wenye nguvu walioitwa; 1Kor.1:22-29.
Anafafanua hivyo kwa makini kuwa ni hekima za kibinadamu au tungeweza kusema ni
kiburi ndicho kinachowazuia watu kuupokea ukweli wa Mungu - na sio roho za
kimaeneo! Inashangaza kuona Biblia yenyewe inavyofafanua vizuri mambo yake.
Wayahudi wanatafuta kuona aina fulani za ishara au miujiza na Wayunani
wanatukuza hekima zao wenyewe - watu wenye vitabia vya jinsi hiyo hawako tayari
kulipokea neno la Mungu kwa moyo wa unyenyekevu bali hujiinua wao wenyewe
kinyume na kweli ya Mungu.
Katika mwangaza wa
ukweli huu, sasa tunaweza kuona ni kwa nini watu wengi hawakuweza kuitikia kule
Athene. Katika ule mstari wa 18 mtume Paulo anatangaza, "kwa kuwa mahubiri
ya msalaba kwa wao waangamiao ni upumbavu bali kwetu sisi tuokolewao ni uweza
wa Mungu." Katika ile 2Kor 4:3,4 anapanua wazo hili kidogo; anasema Injili
imefichwa kwao waliopotea, na anaendelea kuelezea "ambamo ndani yao mungu
wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini isiwazukie nuru ya Injili ya
utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
Katika sura hiyo
anasimulia kwamba shetani anao uwanja wa matendo yake maovu kwa sababu ya
kutokuamini au ugumu wa mioyo ya watu; ni ule ugumu wa mioyo ya watu wenyewe
ambayo humpatia shetani fursa ya kuwadanganya na kuwafanya wawe mateka wa
dhambi. Hapa mtume Paulo anaelezea hali ya kiroho ya hao wanaoipinga Injili;
sura hii haiwakilishi mbinu kwa ajili ya "vita za kiroho". Mtume Paulo
hatuambii hapa kwamba tunapaswa kumfunga mungu wa ulimwengu huu kupitia maombi
ya maombezi ili kwamba hao watu (wajinga?) waweze "kuwekwa huru" ili
waweze kuamini Injili. Ijapo kuwa katika kukubaliana na hilo, maneno ya Yesu
mwenyewe alipokuwa akiongelea kuhusu "saa yake" ambayo inamaanisha
kifo chake pale msalabani. Katika Yoh 12:31 anasema: "Sasa hukumu ya
ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje"
Ukweli huu unarudiwa
tena pale Yesu anapoongea kuhusu kuja kwa Roho Mtakatifu. Yesu anasema kwamba,
Roho Mtakatifu atawahukumu wanadamu kwa hukumu kwa sababu "...yule mkuu wa
ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa", Yoh16:11. Bwana Yesu anaungana moja
kwa moja na hukumu ya mfalme wa ulimwengu huu ambayo alikuwa anaenda kuitimiza
pale Kalvari, pamoja na hukumu ya ulimwengu, ambayo ni hukumu ya ulimwengu huu
ina maana kwamba ni ya watu waishio ndani yake. Akizichukua dhambi za ulimwengu
pale msalabani Yesu angekinyang'anya kifo ule uwezo wake uliokuwa nao,
("uchungu wa mauti ni dhambi" 1Kor.15:56; Tim.1:10). Na atambatilisha
yeye aliyekuwa na uwezo wa mauti, yaani huyo shetani, Heb. 2:14. Kila
amwaminiye Yesu Kristo - kwake huyo mauti pamoja na shetani wamekwishapoteza
haki yao na mamlaka juu yao. Kwa sababu mwanakondoo wa Mungu amezichukua dhambi
zao - dhambi zao zote - na hivyo akanyang'anya toka kwa mauti na shetani ile
haki yote waliyokuwa nayo juu yao. Zaidi ya hayo, kwa kuwa Kristo alikufa kwa
ajili ya wanadamu wote, anayo haki juu ya wote na kwa hiyo anawaagiza watu wote
mahala pote kutubu (Mtd 17:30, tupo kule Athene Tena!). Tanga mwanzo mwa huduma
yake na katika kuhubiri Injili, Kristo alikuwa akiwasihi watu kutubu, na mitume
waliendeleza ujumbe huo huo Mk 1: 14-15; Mtd 2:38. Je, hawa waandishi wa kisasa
wanasema kwamba wanaume na wanawake hawawezi kutubu mpaka kwanza roho zile za
kienyeji katika taifa ziwe zimefungwa? Je hiyo ndiyo sababu iliyowafanya watu
wa Kapenaum washindwe kutubu kwa sababu Kristo ameshindwa kuzifunga roho hizo
juu ya Kapenaumu? Mafundisho haya hayaleti maana yoyote ile katika Agano Jipya!
Yesu Kristo alizivunja mamlaka na uwezo pale msalabani kwa sababu alibakia
pasipo dhambi, na bado akazibeba dhambi za ulimwengu wote na ufufuo wake ni
muhuri kamili wa wokovu wetu, 1Kor.15:12–22. Akiwa amemnyang'anya shetani ule
uwezo wake, Kristo sasa anaweza kupanua kwa neema ya Mungu ule uwezo wa uzima
wake yeye mwenyewe akawapa hao wamwaminio. Akiwa amewasafisha kutokana na
dhambi. Yesu pia anavunja ile milki ya dhambi katika maisha yetu kwa uwezo wa
ufufuo wa uzima wake ndani yetu.
"Sasa hukumu ya
ulimwengu huu ipo" kwa sababu shetani pamoja na uwezo wake wamehukumiwa na
amezitangua pale msalabani. Kwa maneno mengine, huwezi kumlaumu shetani -
hakuna popote inapohesabu hivyo! Sawa ni hakika kuwa shetani anawaweka watu katika
giza, dhambi na vifungo - hiyo ina maana wale watu ambao hawaamini. Na yeye
huja kunyang'anya, kuiba na kuharibu maisha ya watu. Lakini sasa, kwa sababu ya
Kalvari huwezi tena kusema kuwa, njia ya kumwendea Yesu imefungwa kwa watu
mpaka kwanza zile roho za kimaeneo zizuiazo ziwe zimefungwa! Jambo kama hili
linabatilisha tu yale yote ambayo Kristo alilkuja kuyafilia. Hapana, wajibu
unaangukia juu yako wewe na mimi kuiamini injili. Kama hatuamini Injili, basi
kwa vyovyote vile tutakuwa tunampatia shetani pamoja na dhambi ile fursa na
uwanja wa kufanya kazi ndani ya maisha yetu. Na katika hali yoyote ile bado
shetani ni jeshi la uovu lenye nguvu katika ulimwengu, sawa sawa kama vile
maandiko yanavyotangaza. Lakini maandiko yanatangaza kwa sauti na kwa ufasaha
kwamba Yesu Kristo amezishinda dhambi, shetani pamoja na mauti, na akiwataka
waume kwa wanawake watoroke wakawe huru kutokana na toleo la wokovu katika yeye
ambalo linawakilishwa kupitia Injili.
Kwa sababu ya mambo
haya pia, Yesu alisema kuwa na hii ndiyo kazi ya Mungu, ".... kwamba
umwamini yeye aliyetumwa", Yoh 6:29. Na kwa sababu gani roho mtakatifu
atawahukumu wanadamu kwa dhambi? Yesu anasema kuwa ni kwa sababu, hawamwamini
yeye. Yoh 6:9.
Na hii ndiyo dhambi
ambayo wanaume na wanawake watahukumiwa kwayo. Dhambi zinginezo Yesu anaweza
kutuweka huru kwa sababu kutokana na kile alicho kikamilisha pale Kalvari.
Lakini njia pekee ya kuupokea wokovu huu ni kwa kumwamini yeye; na kama
hatutamwamini yeye, basi tutakuwa tumepotea. Mtume Paulo anahitimisha kwa jinsi
ya ajabu kwa ajili yetu pale katika Efeso 2:8. "kwa kuwa mliokolewa kwa
neema katika imani na hii sio kwa uwezo wenu, bali ni kwa karama ya
Mungu". Na hawa Waefeso walikuwa ni watu wa aina gani? Haya, Mtume Paulo
anatujulisha katika ule mstari wa 1-3 wa sura hii - kuwa walikuwa wafu kwa
sababu ya makosa ya dhambi zao; waliishi kwa kuzifuata kawaida ya ulimwengu huu
na mfalme wa uweza wa aga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi!
Na wakawa kama wengine walivyo, watoto wa hasira. Kwa hiyo hapa tunawaona watu
ambao wanatenda dhambi kisha wanajiridhia wenyewe, chini ya usimamizi wa
shetani na vishawishi vyake kwa sababu ya kutokutii kwao; na kwa hiyo wapo
chini ya hukumu ya Mungu. Na tunaambiwa wazi kwamba hiyo ndiyo hali ya wale
wote ambao hawataki kuamini. Lakini mambo yalibadilikaje kwa hawa Waefeso? Haya
mtu yule aitwaye Paulo, alitumiwa pia huko kwa Wamataifa ili apate
"kuwafungua macho yao" na kuwarejesha kutoka katika nguvu za giza na
kuwaingiza katika nuru; na kutoka katika nguvu za shetani waingie katika nguvu
za Mungu, ili kwamba wapate kupokea msamaha wa dhambi, Mtd 26:18. Hii ilikuwa
ni sehemu ya huduma ambayo Mungu ambaye aliyashinda mamlaka na uwezo kupitia
Kristo pale Kalvari - alimpatia Paul. Mtume Paulo hakuhitaji kujitahidi au
kupigana katika kupata huduma na mamlaka kwa kuzifunga roho za kimaeneo!
Hapana, Paulo alikuwa kati ya Wayahudi kwa muda mrefu wa miezi mitatu kwanza
kule Athene halafu akawa kwa wamataifa kwa muda wa miaka miwili, akiwa
anazungumza, anajadiliana, akichunguza na kuhubiri - na watu wengi walimgeukia
Bwana! Na hawa waefeso walipataje kuokolewa? Haya mtume Paulo anatuelezea
katika ile sura ya kwanza mstari wa 13. Walimtegemea Kristo baada ya kusikia
lile neno la kweli, injili ya wokovu wao! Ilikuwa ni kupitia Mtume Paulo
aliyeihubiri Injili ya Kristo kwao na wao wakaiamini Injili, hilo ndilo
lilliowasababishia kumgeukia Mungu wakiondokana na nguvu za shetani! Mungu
asifiwe!
Kristo alipoenda
kwenye nchi yake mwenyewe, Mk 6:1-6, hakuweza kufanya kazi zenye nguvu kwenye
eneo hilo mbali ya uponyaji alioufanya kwa watu wachache. Je hii ni kwa sababu
roho ya kieneo hiyo ilikuwa ni nguvu sana? Hapana! Biblia inatupatia sababu -
inasema Yesu alishangazwa na kutokuamini kwao. Hakushangazwa na nguvu za baadhi
ya roho za kimaeneo, isipokuwa yeye alishangazwa na ugumu wa mioyo yao na
kutokuamini kwa watu hapo. Mty 13:58 anatuambia kwamba, " ... wala
hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao". Ni ile imani
katika Kristo ndiyo iletayo wokovu na sio kule kuzifunga roho ya kitaifa; na
imani inakuja kwa kusikia neno la Mungu - Rumi 10:17! Hivyo Yesu Kristo
anatueleza katika Yohana 3:18,19:
“Amwaminiye yeye
hahukumiwi, bali yeye asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini
jina la Bwana pekee ya Mungu. Na hii ndiyo hukumu, ya kuwa nuru imekuja
ulimwenguni na watu wakapenda giza kuliko nuru, kwa maana matendo yao yalikuwa
maovu.”
Sawasawa na
mafundisho ya Yesu, watu wale ambao wanakataa wasimjie na kumwamini, wanafanya
hivyo si kwa sababu wanazuiwa na roho za kimaeneo, bali kwa sababu walipenda
matendo maovu yao. Mafundisho haya ya kisasa kwa ujumla yanasababisha
kuchanganyikiwa na inaleta dhihaka kwa mafundisho ya biblia. Yanafanya maroho
ya kimaeneo yaonekana ndiyo yanayohusika na uovu wa watu pamoja na kutokuamini.
Wanataka tuelewe kuwa, iwapo tutafanikiwa kuzifunga hizi roho za kimaeneo ndipo
watu watakuwa huru kuitikia Injili. Na hivyo makanisa yetu yataongezeka kwa
kiwango kikubwa ambacho hujawahi kukiona kabla. Hii kimsingi inachafua
mafundisho ya Kristo na ya Mitume. Hawa walimu wa kisasa wanasema kuwa ikiwa
mji umeshikiliwa na matabia ya uchoyo, kiburi, ulevi na au tamaa mbaya basi
hiyo ni roho ya kieneo ya uchoyo, kiburi, ulevi au tamaa mbaya ambayo inatawala
juu ya mji huo na hiyo inahitajika kufungwa katika maombezi ya maombi. Hakuna
lolote kama hilo ndani ya biblia. Eti nini? Kukemea roho za kimaeneo au tamaa
mbaya na kisha watu wa mji huo wataachiliwa huru kutokana na dhambi hizo? Eti
nini? Kwamba tatizo halisi sio mioyo ya watu bali ni uwezo wa roho za kimaeneo?
Haya si mafundisho ya kibiblia. Biblia inatambua tatizo halisi kuwa ni moyo wa
mwanadamu mwenyewe - au ndani ya moyo wa mwanadamu mwenyewe ndiko liliko
tatizo. Tatizo sio kuwa tunatawaliwa na roho za kimaeneo za nje yetu - hapana -
bali tatizo halisi ni dhambi iliyomo ndani ya moyo wangu mwenyewe na kule
kujipenda. Tatizo halisi ni ugumu wa moyo wangu mimi mwenyewe. Hawa walimu wa
kisasa wanafikiri kuwa iwapo utafunga "roho ya ulevi" katika eneo au
jumuia ndipo nguvu ya kupendelea ulevi itavunjwa katika jumuia na kuwawezesha
watu wote kuwa huru kutokana na ulevi. Huwezi kuifukuzilia mbali roho ya
"ulevi" kutoka kwenye eneo kana kwamba hiyo ndiyo inayowashikilia
watu katika dhambi hiyo! Watu hawa wanafikiri nini? Wanajaribu kulihamisha lengo
la Injili lisieleweke kwa jamii; na lengo la Mungu kwa ulimwengu mzima pale
wanapopotosha ukweli wa Injili. Wanajaribu kung'oa mwelekeo wa Mungu kwa
wanadamu, kwa kuichepusha ile kweli. Lakini sasa unaweza ukaihubiri Injili kwa
watu wote na ikiwa kwa neema ya Mungu watu binafsi wataitikia na kuokoka. Ndipo
bila shaka utaweza kuona kupungua kukubwa kama sio kutoweka kabisa kwa ubaya wa
aina fulani kama matokeo ya watu wakigeuka kutoka katika dhambi wakimgeukia
Mungu! Mtd 19:19, 23-27. Huko Efeso watu wengi walichoma moto vitabu vyao vya
uchawi na kuabudu sanamu ya Diana yalitoweka kimchezo tu - lakini hiyo ilitokea
kama matokeo ya watu wengi kugeuka kutoka katika dhambi zao kupitia mahubiri ya
mtume Paulo (mstari wa 26)! Katika Biblia nzima neno la Mungu huja moja kwa
moja kwenye mioyo ya watu wa kuliona tatizo halisi pamoja na kupinga limelala
hapo, yaani ndani ya mioyo ya watu. Tunaweza kutaja Yeremia 4:1-4 na
Lk.13:34,35, pamoja ni mifano miwili kati ya mingi iliyomo katika Biblia.
Ijapokukwa watu wa
Mungu walipaswa kumuombea, lakini hakuna chochote kile cha kuzifunga roho za
kijiografia kana kwamba hizo zinawakilisha jeshi linalowaweka watu katika
vifungo na kuwakataza wasimpokee Mungu.
Hii tena ni msingi
mwingine wa kasoro za mafundisho haya ya kisasa - ni hatari izidiyo. Tatizo la
wema na ubaya linaonekana kama ni jitihada kati ya mambo mawili ya ulimwengu
mzima au nguvu za roho zinazopingana; na hazionekani kama zinahusika na chaguo
ambalo mtu anaweza kulifanya kama yale yaliyoumbwa kwa mfano wa Mungu!
Inaonekana kana kwamba wenye dhambi wenyewe sio tatizo halisi na hawafikiriwi
kuwa wao wanabeba sehemu muhimu katika kuokoka kwao. Hapo inaonesha kwamba
mapambano hayamo ndani yao au kwa ajili ya mioyo yao, bali ni sehemu fulani
huko "angani". Haionyeshi pia kuwa ni dhambi zangu binafsi na kule
kutokuamini kwangu, hilo ndilo tatizo, bali inaonekana kama ninashikwa juu
kwenye mashindano ya majeshi ya kiroho. Na mimi nipo pale katikati, karibu sawa
na mlengwa mjinga. Ninahitaji tu nguvu za roho zilizo kubwa zaidi ili kuzidisha
nguvu za roho ndogo ndogo kunifanya niwe huru! Ni huzuni ya jinsi gani hiyo;
kuchanganya mafundisho kwa udanganyifu kwa jinsi gani huko? Injili ya Kristo ni
uweza wa Mungu kwa kila aaminiye. Wokovu wa roho za watu hautegemei kule kuzishinda
roho za kimaeneo! Lakini hawa walimu wa kisasa, sasa wamebuni Injili mpya ya
ukombozi kupitia vita vya kiroho!
Kama nilivyokwisha
kusema katika zile makala zangu mbili, na bado nazidi kukazia tena kuwa
mafundisho hayo ni ya kimwili yanakazania kwenye mambo ya nje na siyo mambo ya
kweli ya ndani. Wanamfananisha shetani kama anayetaka kuichukua nchi
anayofikiri kuwa kama yake. Na wao wamesema kuwa hiyo ndiyo nchi ya
kijiografia! Shetani ni mungu wa dunia hii maadam hii ndiyo mazingira ya kazi
yake. Lakini kwa vyovyote vile viwavyo, iwe ni roho za kimalaika, mamlaka za
uweza uwao wowote, bado maandiko yanaiweka wazi kwamba uwanja ambao ibilisi
anapenda kuumiliki ni mioyo yetu, akili na nafsi zetu! Mapepo hawahamii kwenye
“vumbi” kavu, bali wao wanapenda kupata makazi ndani ya binadamu Mty 12:43-45.
Hawapati pumziko kwenye maeneo makavu, isipokuwa wanapenda kuishi ndani ya
watu. Na hii ndiyo "nchi" ambayo Yesu aliifilia na akamwaga damu yake
ili kutafuta nafasi ya kukaa yeye pamoja na Baba! Yoh 14:18-23. Tunatakiwa tuwe
makazi ya Mungu kwa Roho, Efe 2: 22. Kwa kupitia kuiamini Injili ya Kristo sisi
tumesamehewa na tumeingizwa ndani ya Ufalme wa Mungu kwa uzao mpya! Bali
Shetani anataka kutufanya sisi tuwe ni makazi ya roho zake, sio kupitia nguvu
za ziada za roho ya kitaifa, isipokuwa kwa kututaka sisi tuamini uongo wake
ambao anaupendekeza kwetu kwa kutujaribu ili tusimwamini Mungu na kisha
tujipendeze wenyewe. Huo ndio uwanja wa mapambano. Na katika huo uwanja wa
mapambano mioyo yetu pamoja na dhamira zetu, Mungu alionyesha pendo lake
mwenyewe kwetu sisi kwa kumtuma mwanae pekee afe kwa ajili yetu na kututaka
tugeuke mbali na matendo maovu na tuupokee wokovu wake wa bure. Hiki ni kipawa
cha Mungu!
Lakini madanganyo ya
mafundisho hayo yanazidi kutumbukia ndani zaidi. Baada ya kuwa wameamini kuwa
wamekwisha kuzifunga roho za kimaeneo zitawalazo juu ya mji, wengine wao wanawachagua
"walinzi wa milangoni." Eti hao ni watu ambao wanapaswa kuomba ili
kuzuia roho za uovu zisiweze kuingia katika miji - hatimaye, watu hao
watasimama pia kwa mbinu fulani ndani na karibu na mji - kwenye barabara kuu
ndani na nje ya mji na kuendelea! Kwa kufanya hivyo, wanazihesabia roho za
mikoa yaani wanazipatia uwezo wa kutawala jumuia yote kana kwamba watu hawana
chaguo lao katika mambo - na kwa kiasi kwamba Injili ya Kristo haiwezi
kuwafikia kwa ufasaha na kuwaokoa! Hivyo siyo Injili ya Kristo - wanacheza
michezo ya ulozi pasipo kutambua! Kwa hivyo, wao kwa vyovyote wanaamini kwamba
ikiwa utaweza kuzifunga roho hizo, basi roho ya Mungu itatawala juu ya mkoa,
basi hapo sasa watu wapo huru kuitikia Injili na kisha Wakristo wanaweza
kuanzisha utawala wa Mungu katika taratibu za jamii ya kienyeji - kwenye mifumo
mbali mbali ya serikali na jamii katika mji! Hii inaonekana kama uanzishaji wa
ufalme wa Mungu hapa dunianli na "kurejesha" nchi kutoka katika
mikono ya shetani. Hawa waombezi wapya wanachokifanya hapo wanapigana ili
kupata ardhi, vumbi na dunia ambayo ndiyo wanayoisemea kuwa inapaswa kurejeshwa
kutoka katika mikono ya shetani. Baadhi ya hao waandishi wanayo mafundisho
mengine yanaweka kwa urahisi yanaeleza kwamba, kwa sababu ya dhambi zake katika
bustani ya Adeni - Adamu alipoteza milki ya mipaka ya nchi kwa shetani kwa
kufanya hivyo, wanazipatia haki roho za mikoa yaani wanazipatia uwezo kutawala
sio tu nchi bali pamoja na watu wanaoishi katika nchi hiyo. Wanasema kuwa Yesu
alikufa pale msalabani ili kurejesha milki juu ya vumbi hili na dunia - pamoja
na mipaka ya kijiografia. Lakini tunaelezwa zaidi na hawa waandishi wa kisasa
kwamba, pale msalabani hapakuharibu mamlaka zote pamoja na uweza wake. Hapana,
tunatakiwa kutumia uwezo ambao Bwana ametupatia sasa, ili kuzifunga roho hizi
chafu zitawalazo juu ya mkoa na kisha watu wa mkoa ule watakuwa huru kuupokea
utawala wa Mungu! Hiyo ni injili yao ya kimwili. Kulingana na mafundisho hayo,
pambano la msingi sio kwa ajili ya nafsi za watu (wauume kwa wake) isipokuwa ni
mavumbi – yaani, sehemu ya kiografia! Na mara tu tunapokuwa tumezifunga roho
hizo zinazotawala juu ya kipande hicho cha vumbi na ardhi, kwa watu wanaotembea
au kuishi juu ya kipande hicho cha vumbi au ardhi, watakuwa huru kuipokea Injili
na kuingia katika ufalme wa Mungu. Mafundisho haya ya kimwili yote yanawafunika
macho watu wasiijue kweli ya maandiko, ihusuyo asili ya dhambi, wokovu na
ufalme wa Mungu.
Hebu niseme hapa,
kwamba, ninafikiri sote tunajua kwamba eneo fulani fulani au jumuia inaweza
ikaingiwa na tabia fulani ya dhambi maalumu inayoonekana kumiliki eneo hilo. Na
kwa vyovyote vile, mtu yeyote anayezaliwa katika mazingira ya aina hii, anaweza
akashawishika. Na desturi hii ya dhambi katika jumuia, na desturi hii ya dhambi
bila mashaka yoyote yale, inakuzwa na Ibilisi na anaweza kuwatumia kuchanganya
upinzani wa Injili ndani ya wale wasioamini, Mtd.19:23-28. Lakini hali hii
ndivyo haswa iliovyokuwa katika jumuia nyingi na miji ambayo mtume Paulo
alitembmelea. Kulikuwepo na zinaa inayoendelea katika miji mingi. Dini za Ulozi
na Uchawi zilishikilia jumuia fulani fulani. Kulikuwepo na uchoyo, kiburi, na
uchafu. Koritho ilikuwa ni sehemu iliyozoelea mambo ya aina hiyo. Lakini sasa
kupambana na roho za kimaeneo ili kuwaweka huru watu kutokana na tabia zao za
uzinzi, mambo ya kimwili au uchawi, jambo hili hamna msingi wowote ule wa
Kibiblia.
Kwa hakika, mtume
Paulo anachagua maneno kwa makini pale anapoyaulizia makanisa ya kule Galatia -
"Ni nani aliyewaloga? Mafundisho hayo yanafanana kama ulozi na kadiri mtu
anavyoendelea kujifunza mafundisho haya ya kisasa ndivyo mtu anavyoona kwa
urahisi kuwa yanafanana na kile ambacho mtu anaweza akafikiria kuwa ni
mafundisho na mtindo wa ulozi au wa Uaguzi. Kadiri mafundisho haya yanavyozidi
kuenea ulimwenguni kote, bila shaka yanaweza kutengeneza vijitabia vyake kutoka
nchi fulani hadi nyingine kadiri watu walivyo na shauku ya mambo mapya; na
katika njia tofauti. Kwa mfano; yapo magazeti ambayo yanawahamasisha na
kuwasihi wakristo wote kuomba dhidi ya roho za kimaeneo juu ya baadhi ya miji
na jiji fulani; magazeti hayo yanajishughulisha sana katika kutafutia aina
fulani ya dhambi nyingi hasa Uchawi, ambao umefanywa katika nchi. Na kisha
huyatangaza matokeo waliyoyapata ili kwamba wakristo waweze kuomba maalumu
dhidi ya roho hizi za kimaeneo, ambazo zinafikiriwa kuhusika na matatizo ya
dhambi hizi zote. Hata pia wanawasihi wakristo watembelee maeneo fulani fulani
ya kijiografia katika jiji huku wakikemea roho chafu. Lakini vitabu
vinavyoongoza ambavyo vimeandikwa kuhusu somo hili kwa ujumla haviwahamasishi
wakristo kuingia katika "vita vya kiroho" dhidi ya roho za kimaeneo.
Kinyume chake, wanaonya juu ya hayo na watuambia kuwa ni wakristo wale waliokomaa,
"na wenye karama rasmi" na wale walioitwa ndio wanaopaswa kuingia
katika mapambano hayo. Ijapokuwa bado wanasema kwamba vita hivyo ni vya lazima
kwa ajili ya kuleta mafanikio ya uenezaji wa Injili. Zaidi ya hayo bado
wanakubali kuwa jambo hili ni kujitumbukiza katika matatizo ya bure na yenye
kuogofya na ni mapambano ya hatari yenye kuwapatia wengi misiba. Hayo yote ni
sawa na kubatizwa katika mambo ya ushirikina na udanganyifu.
Vita vya Kiroho - ni
Matendo yenye Hatari?
Lakini sasa kwa nini
"vita hivyo" viwe ni mambo "yenye hatari", kuogofya na
kukuletea matatizo? Haya, wanasema kwamba wakristo “wa kawaida” huwa hawana
mamlaka na nguvu zilizo katika kiwango cha "madaraka ya juu" ya roho
za kimaeneo. Na wanazidi kutuambia kuwa kumewahi kutokea na itaendelea kuleta
msiba katika "vita" hivyo! Waandishi hawa wanatuambia juu ya
wachungaji ambao wameanguka katika dhambi “kwa sababu” ya kujiingiza kaika
“mbinu ya kiwango cha mapambano ya kiroho” (strategic - level spiritual
walfare)! Waandishi hawa wanatuelezea kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa,
magonjwa, mambo ya kimwili, watu wanajifanyia uvunjifu juu ya Imani zao na hata
juu ya kifo - kwa sababu ya kujihusisha kwao katika aina hii ya vita! (Ikiwa ni
kweli kuwa matatizo hayo yamewazukia kwa sababu ya watu wenyewe kujihusisha
katika aina hii ya mapambano, basi litakuwa ni swali lingine lenye kuhojiana).
Kumekuwepo na michanganyiko mingi pamoja na maumivu ya moyo kutokana na
mafundisho haya kiasi kwamba kiongozi wa aina fulani ya huduma huko Amerika
ameandika kitabu kuhusiana na jambo hili kiitwacho (Needless Casualties of
War"; “Misiba isiyo ya Lazima katika Vita”, kilichoandikwa na John Paulo
Jackson, Kingsway Publications. Copyright John Paul Jackson 1999). Yeye pia
anapendelea mapambano dhidi ya maroho, lakini katika kitabu chake anaeleza
jambo fulani zuri na anaonya kuhusu kutokuwa na kiasi, ambako analaumu kuwa
ndiko kunako husika na majanga ya kutisha katika maisha ya wakristo. Lakini
sasa kule kuamini kwao juu ya imani ya kufunga roho za kimaeneo, kinawafanya waandishi
hawa wote wawe vipofu juu ya ukweli uliofunuliwa katika maandiko, nao huuacha
ukweli huo kirahisi tu na hawaonyeshi kuhusika kihalisi kwa yale
yanayofundishwa na Biblia ili wahalalishe makosa yao. Wanaeneza mafundisho
yenye kasoro, na watu wengi wanayafuata mafundisho hayo na mara zote hutumbukia
katika matatizo ya kutisha. Kwa hiyo waandishi hawa wanabuni kasoro ili waweze
kuzielezea ni kwa nini misiba hiyo! Kwa hiyo, hata mwandishi niliyemtaja hapo
juu, anaelezea kwamba "kwa kawaida" wakristo huwa ndani ya Kristo
Yesu, Kolosai 3: 3, lakini kama tutajihusisha katika aina yoyote ile ya
mapambano ya kiroho, basi hapo tutakuwa tumejiweka wazi kama shabaha kwa nguvu
za mapepo na tunaweza kudhuriwa na kuharibiwa na mapepo yale!
Anasema kwamba hata
kule kuomba tu kwa Mungu kuhusiana na nguvu za mapepo ni mtindo wa mapambano ya
kiroho! Inafanana kama mbwa mwitu kuweka kichwa chake nje ya tundu lake la
usalama, hiyo inamfanya aonekane ni chambo cha mnyang'anyi anayezurura! Hii ni
aina fulani ya udanganyifu ambao unaenezwa na hawa waandishi. Hayo ni
mashambulizi juu ya mafunuo ya mandiko kuhusiana usalama wetu na wokovu katika
Kristo! Eti mimi? “Kwa kawaida” tupo ndani ya Kristo, isipokuwa
tunapojishughulisha na mapambano ya kiroho “hatuwi tena ndani ya Kristo” au
“hatuwi kabisa ndani ya Kristo”, isipokuwa tunakuwa tu “sehemu ndani yake?” Eti
mimi? Na kwamba eti tunaweza tukawa ni “shabaha” ya roho chafu anayeweza
kusababisha uvunjifu wa ndoa, maradhi na kifo ikiwa tutakuwa si waangalifu?!
Hii si kitu kingine isipokuwa ni ubatizo katika mambo ya ushirikina na
mafundisho ya ulozi. Agano jipya linafundisha kinyume cha hayo yote; yaani
inafundisha kuwa ni kwa njia ya kuenenda katika silaha zote za Mungu tu na
kupigana vita vizuri vya imani, hapo tunakaa kwa Usalama kutokana na michezo
yenye maumivu ya shetani - hivi ni vita vya kweli vya kiroho na vinapaswa
kuhusika na mwenendo wetu kiroho - na wala sio katika kupambana dhidi ya roho
za uovu katika maombi kama tutakavyoona baadaye katika Efs.6:10 –18.
Maandiko hayafundishi
wala kuhamasisha udanganyifu huu; wala hawawezi kuingiza aina hii ya woga ndani
ya moyo yetu. Tunaambiwa kuwa "yeye aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye
aliye ulimwenguni" na kwamba “hakuna kitu kinachoweza kututenga na upendo
wa Mungu uliomo katika Kristo Yesu." Na hii Inajumlisha mamlaka zote na
uwezo! Tumeketi pamoja katika Kristo Yesu mbinguni na Uhai wetu umefichwa
katika Kristo ndani yake Mungu" - mambo mengi ni yenye kutia moyo na ahadi
zake Mungu akituthibitishia Usalama na baraka zaidi ya kingine chochote kile
pale tunapotunza neno lake na kumwamini yeye. Hatusomi chochote kihusucho
kushambuliwa na maroho machafu au maisha yetu kuharibiwa kwa sababu tu,
tunaomba kama maandiko yanavyo tushauri kuomba. Biblia haikiri aina yoyote ile
ya misiba kati ya wale wanaoomba. Au je! Unaweza kupata mausia yoyote ya maombi
katika Biblia yanatuonya juu ya uwezekano wowote ule wa misiba. Au Biblia
inaelezaea kukumbukia wapi ili kuonyesha kikundi maalum na teule cha Kikristo,
ambacho wao pekee waliitwa kwenye vita maalum kwa sababu tu kwamba mapambano
hayo ni yenye hatari sana kwa wakristo wa kawaida kuyashiriki?! Hivyo ndivyo
wao wanavyofundisha, lakini hii pasipo ugumu wowote ni kuwatumbukiza watu ndani
ya nyumba ya matope ya ushirikina na makosa.
Mausia yote ya
kuomba katika Agano jipya, ni kwa waamini wote na hakuna hata mausia yanayohusu
maonyo kwamba inawezekana ikawa ni "hatari" kuomba, na kwamba aina
fulani ya maombi inapaswa kushirikisha aina fulani tu ya waamini wenye wito
maalum!
Lakini hii karama
maalum ni kitu gani ambacho hawa waombezi wanamaanisha kuwa nazo kulingana na
mafundisho hayo? Tunaelezwa kuwa wanapaswa kuwa ni wakristo walio komaa na
haswa wawe na karama ya kutambua majina na tabia ya roho za kimaeneo na uwezo
wa kusikia toka kwa Mungu, ambaye huwasiliana nao ili kujua ni aina gani ya
roho inaweza na inahitajika kufungwa. Karama hizi zinafikiriwa kuwa ni za
lazima katika vita vya kiroho. Kwa hiyo waombezi hao wanaweza kutumia masiku na
mawiki katika maombi wakiwa na shabaha ya kutambua jina au aina ya roho za
kimaeneo zinazotawala juu ya jiji na wanasubiri toka kwa Mungu ili kuwaonyesha
ni aina gani ya roho inayostahili kukabiliwa katika maombi yao. Wengine wao
wanashuhudia kuwa wanajisikia kuwa wanaingia katika milki nyingine ambako wanakabiliana
na roho chafu. Wakati mwingine eti wanaweza kuziona hizi roho chafu labda kama
katika maono, au dhahiri. Yanaweza kujitokeza kama kiumbe cha kutisha, nasi
tunaambiwa kuwa "mivutano" inaweza wakati mwingine ikawa kwa nguvu.
Mchungaji mmoja alivutana ili kutia changamoto roho ya kieneo kuhusu mitaa
mingapi katika mji inapaswa kuachiliwa. (Inaonekana kuwa mitaa hiyo ambayo huyo
roho mchafu aliiachilia kwa washujaa wa maombi, basi watu katika eneo hilo
wangeweza kuitikia Injili, lakini kwa bahati mbaya mitaa ambayo roho mchafu
hakuiachilia kwa washujaa wa maombi, watu waliopo pale hawakuweza kuokoka! Au
tufikirije?!). Baada ya kufungwa kwa roho za kimaeneo (kama wanavyofikiri),
mhubiri huyo anaita mikutano ya Injili akiwaambia watu, eti sasa wamewekwa huru
waitikie Injili!
Hatari za Mafundisho
ya Kisasa - mafundisho yenye makosa, yanayowaongoza watu katika uzoefu
udanganyao.
Wanasema kuwa aina
hii ya "mapambano ya kiroho" ni muhimu kwa ajili ya mafanikio ya
Injili. Pasipo shaka yoyote huo ni udanganyifu. Lakini tena wanatuambia kuwa
kutakuwa na "majeruhi" miongoni mwa Wakristo, kwa sababu Wakristo
wengi "hawana silaha zifaazo" kwa ajili ya aina hii ya mapambano au
hawajafahamu "jinsi ya kupigana" aina hii ya vita! Lakini wazo la
kuwa mtu anajishughulisha na vita vya kweli vya kiroho inaweza kumletea matokeo
ya roho chafu kukushambulia na kuharibu maisha ya familia yake ni mafundisho
yasiyo na maana na yasiyo ya Kibiblia. Hii ni zaidi ya aina fulani ya
mafundisho ya ulozi ambayo yanaweza tu kuwaletea watu hofu katika mioyo yao.
Hata kama chanzo cha majanga ambayo tunaelewa yanawaangukia wakristo, yanaweza
kuwa ni kutokana na kujihusisha kwao na aina hii ya vita vya kiroho ambavyo sio
vya Kibiblia, hii ni hoja ya kuijadili kama nilivyokwisha sema. Na sasa
ningependa kufanya mambo mawili ya muhimu.
Kwanza, kwa vyovyote
vile aina zote za matatizo hutokea katika maisha yetu ikiwa tutakuwa hatuishi
kulingana na neno la Mungu. Katika Efeso 4:11-14, Mtume Paulo anaongea kuhusu
huduma zitolewazo na Mungu kwa kanisa ili kwamba wote tupate kupokea kukua
katika Kristo. Tunapaswa kukua na kuwa wenye nguvu katika ufahamu wa Kristo na
tusibaki kama watoto wadogo au kama watu wa mwilini ambao huchukuliwa na kila
aina ya upepo wa imani wakitazamia "jambo jipya" linalofuata - ili
kutushitusha sisi na hivyo kutufanya shabaha ya hila na udanganyifu wa
wanadamu.
Kumewahi kutokea
uzao mwingi wenye hatari ya "upepo wa imani" au makosa yenye hatari
kwa kadiri ya miaka mingi sasa. Makosa haya yawezekana yanaanzia au yanapata
msaada wenye nguvu kutoka kwa waamini wa Amerika. Mafundisho hayo hayana msingi
wowote wa neno la Mungu isipokuwa ni matokeo ya kufikiri kwa watu wenyewe na
mafunuo ya pekee. Hali kadhalika na uzoefu wao binafsi ambao hauna ulinganifu
wa kweli wa kimaandiko. Imani hizo zinahamasishwa na baadhi ya majina yanayo
julikana vema, wengi wao ni viongozi wa mashirika yenye nafasi nzuri ya fedha
nyingi ambazo ndizo zinazo wasaidia sana kusambaza ujumbe wao. Mengine hupeperushwa
na upepo huu wa imani, pasipo hata kufikiria yale ambayo Biblia inasema au
kufundisha. Na mradi wanakataa kuongozwa na neno la Mungu, haishangazi kwa hiyo
kuona kwamba matendo yao pia huwa ni ya kimwili, Rumi 1:21-24. Ikiwa
tutajiondoa kutoka kwenye neno la Mungu ndipo tutakuwa tunajiondoa pia kutoka
katika maisha matakatifu yaliyo takasika. Yesu alisema, “watakase kwa kweli.”
Yoh 17:17. Maisha ya watu hayajajengwa juu ya mwamba wa Yesu Kristo; juu ya
mwamba wa kulitii neno la Mungu. Kwa hiyo si jambo kubwa la kushangaza kuona
watu wengi wakipitia katika maisha ya taabu - katika nyakati hizi kunaonekana
kuenea kwingi kwa watu kuondoka kutoka katika neno la Mungu ambavyo inaleta
matokeo katika hali ya maisha kuwa ni ya kimwili na yasiyo imara kwa wakristo,
ikiwafanya watu kuanguka katika aina fulani ya dhambi na shida na kuchomana wao
kwa wao na kupitia kwenye huzuni nyingi. Katika mtiririko wa habari hii ni
rahisi kwa waandishi hawa kusema kuwa watu wanapambana na matatizo katika
maisha yao “kwa sababu” ya kujihusisha kwao katika aina hii ya vita vya kiroho,
kwa sababu wapo wengi wenye matatizo tayari, lakini chanzo halisi cha matatizo
yao kwa hakika yaweza ikawa ipo sehemu fulani.
Watu hawa hawaingii
katika mapambano ya kiroho kabisa, bali wanaingia kwenye ulimwengu wa maroho
unaotofautiana kabisa - pale wanapokuwa katika kudanganywa na kutokana na hilo
huwajia “Injili nyingine”, “Yesu mwingine” na “roho mwingine”. Wanazitengeneza
nguvu za "maroho ya kibinadamu" na kufanyika kuwa ni shabaha ya
maroho yadanganyayo, ambayo ndiyo yanayowashawishi kuona kuwa wanajishughulisha
na vita vya kiroho na kwamba watu wengi wanaendelea kudanganywa kunyang'anywa
ufahamu wa kweli wa Mungu ambao umo ndani ya Kristo. Ndiyo naweza kuhisia
kwamba mtu yeyote anayeifuata elimu ya mtindo huu na kuamini huku katika uzoefu
unaofanana, lazima watajitumbukiza katika matatizo makubwa. Wanalivunja neno la
Mungu, na wanalivunja ndani ya milki isiyo halali.
Inaweza ikatusaidia
tukitazama katika 2Kor.11:1-15 ili kutusaidia kuelewa jinsi gani mambo haya
yanavyoweza kuwa. (Tafadhali angalia katika makala ya kwanza ambamo hali ya
kanisa la wakorintho pamoja na misingi ya udanganyifu wao ilivyoangaliwa).
Katika kanisa la Korintho wengi wa watu wa Mungu huko walikuwa wanaenenda
kimwili. Walipenda kupata "uwezo na utukufu". Na hiyo hali ya kimwili
pamoja na hayo matamanio ya kimwili ya kupata uwezo na vyeo ili wasababishia
kupotelea mbali na mafundisho ya Kristo. Kung'ang'ania kudumu katika mwenendo na tabia hizo
kuliwaletea kuonekana wazi na kuwafanya wawe ni kafara ya udanganyifu wa
shetani - ni udanganyifu wa kutisha! Tunaambiwa kuwa shetani mwenyewe hujigeuza
katika sura ya "malaika wa nuru", ule mstari wa 14. Ninaamini kwamba
baadhi ya uzoefu wa watu hawa unapaswa ueleweke katika habari hii. Katika
mstari wa 13 anaongea kuhusu "mitume wa uongo, wafanyakazi wenye hila,
wakijibadilisha wenyewe kuwa mitume wa Kristo”. Katika mstari ule wa 4
anatueleza kwamba hata watu wa Mungu wanaweza kuongozwa na udanganyifu huu
katika kumpokea Kristo "mwingine", roho "mwingine" na
Injili "nyingine". Hatujaelezwa, kuwa mambo yanaweza kuwaje, lakini
yanaweza kutokea iwapo mtu analiacha neno la Mungu, hilo limewekwa wazi sana
kwetu. Na iwapo hilo liliweza kuwatokea wale ambao mtume Paulo mwenyewe
aliwashuhudia na kuokoka ambao pia walikuwa katika hesabu ya kuongozwa na
kuangaliwa kwa karibu na mafundisho yake; hivyo tusifikiri kuwa mambo haya basi
hayawezekaniki nyakati za leo! Na hiyo ndiyo sababu inayoelekea kuandikwa kwa
makala hii, kwa sababu mafundisho hata ya kisasa yanatuletea hila za shetani
ili kuzichafua fikira za watakatifu kutokana na unyofu uliomo katika kristo -
msitari wa 3. Katika Yeremia 5:30,31, tunakuta kufanana kunako shangaza juu ya
yale anayoyasema mtume Paulo kwenye 2 Kor.11:13-20. Manabii wa uongo
wakiwadanganya watu wa Mungu, viongozi wao wakiwatawala kwa nguvu, na bado watu
wa Mungu wakiyapenda hayo yote! Mungu anaisema juu manabii kwenye Yeremia
14:14, "ndipo Bwana akaniambia, hao manabii wanatabiri uongo kwa jina
langu mimi, mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru , wala sikusema nao; wanawapeni
unabii wa maono ya uongo na uaguzi na neno la ubatili na hadaa ya mioyo
yao". Mambo kama haya yamewai kutokea na hata leo yanatokea pia.
Ijapokuwa
yanawezekana kuwa mambo katika habari hii ambayo si rahisi kueleweka,
inaonyesha wazi kuwa mtu yeyote asiye na haki anaweza akawasiliana na ulimwengu
wa maroho, lakini umaarufu wake kwa watu wa Mungu ni kuwachafua iwapo angepata
nafasi ya kufanya hivyo. Nimenukuu habari hapo juu ili kuonyesha kuwa watu
wanaweza kuwasililana kimakosa na maroho, hata wakristo wanaweza kufanya hivyo.
Ijapokuwa bila shaka sio habari yote hiyo ambayo inaweza kuwahusu waandishi
hawa wa kisasa, bado kwa namna fulani, ninafikiri wameiharifu mipaka halali
kama ilivyoonyeshwa katika 2 Kor.11:1-15.
Nilikuwa nasoma
kitabu kimoja ambacho kimezungukia kasoro zote nilizo zitazama katika makala
hizi tatu. Nilipokuwa nikisoma, niliamini kuwa mwandishi huyo amehalifu na ametumbukia
katika udanganyifu. Kisha nikasoma kuwa mwandishi wa kitabu hicho yeye mwenyewe
alikuwa analifahamu hilo. Yeye ni mwenye historia ya nyuma ya Kimarekani ya
asili, naye anashuhudia kuwa, akiwa kama mkristo, bado mambo ya siri zake za
hapo kale (au pengine tungeweza kusema kwamba unajimu au uchawi) ule uwezo wake
wa kinajimu alioupata kutokana na desturi au mila za kihindi, ungeweza
kujitokeza tena ndani yake na angeweza kufanya mambo yenye fumbo za kiunajimu
(akiendesha ndani ya ulimwengu wa roho) ambao kwa uaminifu kabisa anakiri wazi
kuwa hiyo haikuwa karama ya Roho Mtakatifu. (Ninaamini kuwa mambo kama hayo
yanaweza kutokea na yanatokea siku za leo). Lakini ndipo anaendelea kusema kuwa
alimwomba Bwana ili aondoshe na kuangamiza kabisa uwezo huo aliokuwa nao hapo
kale. Hilo ni jambo jema. Lakini tena anaendelea kusema kwamba Roho Mtakatifu
alishuka chini na kufikia kwenye ujuzi huo wa zamani na akawasafisha ili
kuwatumia kwa ukamilifu zaidi! Hilo sio jambo jema! Na kadiri mtu anavyosoma
kitabu, mtu huyo anaona kuwa huo ni ushuhuda wa uwezo wake wa mambo yake ya
"kiunajimu" ya hapo kale yakimpeleka kwenye udanganyifu wa mambo ya
uzoefu wa maroho ya kigeni ambayo hayatokani na Mungu. Wamebuni mafundisho
mapya na uzoefu ambao wao wanauita "Baraza la Bwana" ambapo unaitwa
mbele ya uwepo wa Bwana kwa ajili ya aina fulani ya mazungumzo. Sio uchaguzi
wako. Mwandishi wa kitabu hicho wakati fualni alijisikia “ameitwa” kwenye uwepo
wa Mungu pamoja na mtu mwingine, ambako Bwana aliwauliza iwapo Mungu sasa anaweza
kuihukumu dunia hii. Na eti kwa sababu ya maombezi yao, ulimwengu uliachiliwa
kutokana na hukumu ya dunia nzima kwa wakati ule, hii ni kulingana na watu hawa
wawili wote kwa pamoja walivyoona na kuskia katika maono yao! Katika aliamini
kuwa yeye mmoja na rafiki zake wanane walikuwa wakiitwa kwenye baraza la Bwana,
lakini sasa yeye alishangaa kuona kuwa imekuwaje watu wote tisa waweze kusikia
kitu kile kile na kuyaona maono yale yale (yanayofanana) kwa wakati mmoja. Hata
hivyo alijisikia kuwa anapaswa “kutii na” wakaondoka pamoja, naye anasimulia
jinsi ambavyo wote walivyoona kitu kile kile "katika roho" na kusikia
kitu kile kile - sauti na maono ambayo wote kwa pamoja walipata kuyajua! Huo
ndio upuuzi wa makutaniko ya mizimu, unajimu na ulozi! Hakuna hata moja kati ya
hayo inayotokana na Mungu. Halifanani na chochote katika maandiko ya neno la
Mungu. Wamefanya makosa ya nje hatari sana na wamedanganywa vibaya na hali hiyo
italeta madhara mabaya. Kwa hakika huu ni “moto wa kigeni”! Yeye anasimulia
maono hayo kwa kirefu katika kitabu chake lakini bado ni ya tabia ya kigeni na
wala hayaleti sura yoyote ile ya kibiblia au hayana misingi yoyote ile ya
Kimungu ndani yake. Ni kutokana na wanaume na wanawake wa jinsi hii ndio wanao
leta mafundisho ya aina hii. Kama ilivyo kuwa kule Korintho nyakati za Mtume
Paulo, ndivyo inavyotokea nyakati za leo pia. Watu wamejazwa maono yao wenyewe,
wakimleta roho mwingine, Yesu mwingine, Injili nyingine. Wao wanaamini, kwa
kadiri mnavyojua kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa wakimtumikia Mungu, lakini kwa
ujumla kwa huzuni kubwa wamekosea.
Mambo haya yote
huwaletea huzuni watu wengi wa leo kadiri wanavyo ona udanganyifu wa aina hii
na kuchanganyikiwa kunako sababisha maumivu ya moyo, pamoja na matengano
ikiwasababisha watu wa Mungu kukosea na kuwaondoa kutoka katika kweli na
kuwaingiza kwenye vifungo Inaonyesha kuwa nyakati hizi shetani anajitahidi
kufanya kila awezalo kudanganya ikibidi hata wateule. Je, anatumia njia gani
kujaribu kufanikisha jambo hili? Kwa mujibu wa Yesu Kristo. Wakristo wa uongo
(hii inamaana kuwa, ni wale wenye upako wa uongo) na watatokea manabii wa uongo
nao watatoa ishara kubwa na maajabu. Ishara, maajabu manabii wa uongo na upako
wa uongo ni vitu ambavyo shetani atatafuta kudanganya ikiwezekana hata wateule Mt.
24:24. Ikiwa mtu yeyote anaweza kutoa aina yoyote ya ishara na maajabu, au
wanajifanya wenyewe kuwa ni mitume wenye nguvu au manabii, hapo ndipo wengi wa
watu wa Mungu huonekana kuwa tayari kupokea mafundisho yoyote yale
yanayoambatana nao! Hizo ndizo nyakati tunazoishi.
Kwa hiyo, ikiwa watu
wanapata matatizo katika maisha yao, sababu kuu ni kwamba wamechagua kuishi
pasipo imani na kutokuwa na utii wa neno la Mungu. Na nyakati za leo ni yote
mawili hufanyika; yaani mafundisho ya uongo na uzoefu wa uongo ndiyo
yanayowapeleka watu wa Mungu kuwa mbali na kweli na kuishi kwa ile kweli; sio
kule kujiingiza katika mapambano ya maandiko kiroho ambako ndiko kunako
sababisha matatizo, isipokuwa ni mafundisho yaliyokosewa ya aina hii ya vita
vya kiroho, hiyo ndiyo chanzo cha mchanganyiko mkubwa, udanganyifu pamoja na
matatizo.
Fungu la Maandiko
Wanayoyatumia
Sasa tutaangalia
aina ya aya ambazo waandishi hawa hupenda kuzilinganisha ili wapate
kuyahalalisha makosa yao. Moja kati ya zile kuu inapatikana katika Efeso 6 na
tutaanza kwanza kuitazama sura hii, pamoja na kufikiria kwa kifupi juu ya vita
vya kiroho ni nini hasa, kabla hatujaendelea kuangalia katika sura nyinginezo.
EFESO 6:10-20
Hii penginepo ni
sura ya msingi mkuu na ambayo mara nyingi hunukuriwa vibaya, ambayo hutumiwa
kuunga mkono mafundisho yao kuhusu roho zitawalazo katika nchi. Mara nyingi
hutumiwa na hawa waandishi wa kisasa ili kuainisha mapambano ya kiroho kuwa
yanahusika na kuomba dhidi ya, na kuzifunga mamlaka na uweza ambayo inahusisha
na roho zile za kiinchi, hii ni kulingana na tafsiri yao. Kama tunavyoangalia
katika sura hiyo tuliyoitaja hapa, tunaona kuwa sura nzima haihusiki na
chochote juu ya mambo kama hayo (niliishughulikia kwa makini sura hii pia pale
nilipokuwa nafikiria ju ya maombi katika Agano Jipya kwenye makala yangu ya
kwanza). Katika mstari wa 10 na wa 11, mtume Paulo anatusihi tuwe hodari katika
Bwana tukizivaa silaha zote za Mungu ili tupate kuzipinga hila za shetani. Kwa
nini tunahitaji silaha za Mungu? Ni kwa sababu adui yetu ni wa kiroho na
kushindana kwetu ni kwa kiroho. Ule mstari wa 12 unatuambia kwamba kushindana
kwetu, au vita vyetu sisi, sio juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho", (katika hali hiyo hatuhitaji kufafanua majeshi hayo
yote ya kiroho, isipokuwa ni bora kuendelea kufuata hoja za mtume Paulo hapa).
Kwa sababu ya hilo, tunahitajika kukamilika kiroho. Peke yetu wenyewe tu,
hatuwezi kuushinda upinzani huu wa kiroho na hila! Sasa, baada ya kuliweka hili
wazi katika ule mstari wa 12 mtume Paulo anatusihi kufanya nini hapo? Je, yeye
anasema kwamba, “kwa kuwa upinzani wetu ni wa kiroho, jichukulieni wenyewe
silaha za Mungu ili kwamba unaweza kuomba dhidi ya mamlaka hizi na uweza na
kuzifunga kwa jina la Bwana"? Je, hivyo ndivyo mtume Paulo anavyozielewa
vita vya kiroho? Je, hii ndiyo njia ya kupata ushindi? Hapana! Hivyo siyo hoja
yake kabisa!
Anatuambia katika
ule mstari wa 13 kwamba tutwae silaha zote za Mungu, ili tupate kuweza
kushindana siku ya uovu na tukisha yatimiza yote kusimama! Mtume Paulo
anazungumza kuhusu silaha ambazo zitatuwezesha kuyashinda majaribu na
vishawishi mbali mbali ambavyo majeshi ya kiroho ya uovu yanaweza kutuingizia,
na hatimaye tuweze kushinda. Anazungumza kuhusu mwenendo wetu kiroho katika
Bwana. Hivyo mtume Paulo anatutia moyo kwamba "tupate kusimama", hiyo
ina maana kumpinga shetani na kuyashinda vishawishi vyake katika maisha yetu ya
kila siku. Ili kuyafanya hayo tunapaswa kuipata kweli ya Mungu, na kuvaa dirii
ya haki (mstari wa 14). Kweli ya Mungu itashughulikia uongo wa shetani na pia
itatuadilisha na kututia moyo. Kusimama katika haki tuipatayo katika Kristo
kutaitunza mioyo yetu ikiwa imesafishwa na kulindwa. Ushuhuda wa Kristo unapaswa
mara zote uwe hai ndani yetu ili kwamba tuwe tumejiandaa kuwashirikisha watu
wengine Injili hii (mstari wa 15). Kisha katika ule mstari wa 16 mtume Paulo
anatusihi, "zaidi ya yote, tuitwae ngao ya imani ambayo kwa hiyo
itatuwezesha kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu”. Anachokiongelea
hapa ni kujishughulisha na kukataa malaumu yote, uongo na mashauri ya shetani
ambao anatutupia ili kutufanya tumtilie mashaka Mungu pamoja na upendo wake
kwetu, ili kutufanya tujisikie wenye kuhukumiwa, tusio na maana; na pweke ili
kutufanya tujisikie wasikitivu au tunao jihurumia. Tunapaswa kuyashughulikia
hayo yote kwa kuiweka imani yetu na matumaini yetu kwa Mungu na katika yale
aliyokwisha yasema. Wote huwa tunashawishiwa na kujaribiwa kama ilivyo katika
mstari huu; sote tunajua yanafananaje mambo hayo. Lakini sasa hayo ndiyo
mapambano yetu kiroho na tunapaswa kuchukua ngao ya imani na wala tusijiachie
wenyewe kudhurika kwa uongo wa shetani na mashauri yake. Ni kweli kuwa katika
hali hii wengi wetu huanguka. Hatusimami kama mtume Paulo anavyo tusihi, na
hivo tunaupoteza ujasiri wetu, furaha na amani yetu katika Bwana. Tunaishia
katika kujisikia kuhukumiwa na tusio na maana, tukishangaa iwapo ni kweli Mungu
anatupenda na kutujali. Katika hali ya jinsi hii, kwa kweli hatuwezi kukua
katika Bwana na bado kuna upungufu wa matunda juu ya Mungu. Sura hii inapiga
moja kwa moja nyumbani katikati ya mwenendo wetu na vita vyetu kiroho.
Ukweli ambao mtume
Paulo anauelezea hapa ni wa lazima kwa ajili ya mwenendo wetu kiroho na
kimapambano. Ni wa maana na ni dhahiri. Wanakaa katika moyo wa maisha ya kiroho
na ya ushindi. Hivyo ndivyo inavyohusika na vita vya kiroho. Sio kuanza
kuikunja "mikono ya kiroho" na kupiga kelele na kumkemea shetani na
maroho ya nchi. Pasipo maswali yoyote, ni vyepesi zaidi na inaashiria kimwili
zaidi mtu kuomba dhidi ya roho mbaya katika maombi ya mikutano, kuliko ilivyo
katika maisha ya kila siku katika imani, upendo na utii kwa Mungu kusimama
katika silaha za Mungu; hi ya mwishoni inawakilisha vita vya kiroho kulingana
na maandiko, lile la kwanza halina lolote!
Mtume Paulo
anaendelea katika kutusihi tuchukue chepeo ya wokovu - ambayo itatunza na
kulinda akili zetu katika kristo - na upanga wa roho, ambao ni neno la Mungu.
Tukiwa tumevaa silaha zote za Mungu, Paulo anatusihi sasa kuomba (mstari wa
18). Haya, je sasa tunatakiwa kuomba dhidi ya mamlaka na uweza na kuzifunga?
Sasa, kwa kuwa tumepata silaha za Mungu, tunapaswa kusimama dhidi ya roho
zitawalazo maeneo na kufunga uweza wake? Hapana. Sio hivyo, kulingana na mtume
Paulo. Lakini Je, hivyo si ndivyo silaha inavyotakiwa kuwa? Kutujaza nguvu
katika maombi kuzifunga roho mbaya? Hapana; sio hivyo, kulingana na mtume
Paulo. Mtume Paulo hataji kuomba dhidi ya maroho na kuzifunga. Anazungumza
kuhusu “kuomba kwa sala zote, na maombi kila wakati katika roho, mkikesha kwa
jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote na kwa ajili yangu
mimi.....”
Kwa hiyo kuenenda
kiroho, na kuzishinda kwa mafanikio hila za shetani katika vita hivi vya kiroho
katika maisha yetu ya kila siku, kunatuwezesha kuomba kwa ufasaha kwa ajili ya
watakatifu. Kwa uwazi kabisa maombi ni sehemu muhimu ya mwenendo wetu kiroho
mbele za Mungu, lakini tunawezaje kuomba kwa ufasaha pale tunapolitilia shaka
pendo la Mungu na matunzo yake kwa ajili yetu, pale tunapojisikia kuhukumiwa
watu tusio na maana, au tusiopendwa, pale tunapokuwa na uchungu, kutokusamehe
na ugumu mioyoni mwetu; pale tunapokuwa katika kutokuamini! Kwa hiyo tunaweza
kuona kuwa, mtume Paulo anatupatia amri sahihi katika sura hii - uhusiano wetu
na Mungu, pamoja na mwenendo wetu mbele zake lazima uwe safi kabla hatujaweza
kuwa wenye mafanikio kiroho katika maeneo mengine. Kwa hiyo vita vya kiroho
vinahusika na kupinga vishawishi vya shetani na uongo wake katika mwenendo wetu
wa siku kwa siku na Bwana - tukivaa silaha zote za Mungu. Hilo ndilo
linatuwezesha kuomba kama itupasavyo kwa ajili ya watakatifu.
Sura hii yote ya
mtume Paulo haiwakilishi mbinu fulani fulani au maagizo ya kuyashambulia na
kufunga maroho mabaya kupitia maombi! Kwa urahisi tu anasema kwamba, kwa sababu
adui yetu ni wa kiroho, kwa hiyo silaha zetu zinapaswa kuwa za kiroho, katika
mapigano yanayotuhusu ili kupinga vishawishi, uongo na mashauri ya kutokuamini
ambayo shetani atayapanda ndani ya mioyo yetu na maisha yetu. Kwa kweli, mbali
ya mapepo kufukuzwa nje ya mtu mmoja mmoja, haupo mfano hata mmoja katika
maandiko unao mwonyesha mtakatifu yeyote moja kwa moja akishambuliana na
kuzifunga mamlaka zozote zile, uweza au roho zitawalazo maeneo, katika maombi.
Maombi yote katika Biblia yanaelekezwa kwa Mungu.
Katika maombi watu
wa Mungu wanakiri na kutukuza Uungu wa matoleo yake na wanatoa haja zao
kulingana na mafunuo ya neema ya tabia ya uungu wake. Na maombi yao mengi ni
kwa ajili ya watu wa Mungu. Kama inavyoonyeshwa na mtume Paulo katika sura hii.
Vita vya Kiroho
Kulingana na Maandiko - kwa kifupi.
Hatutakwenda
kuangalia kwa undani juu ya somo hili katika makala hii, lakini ningependa
kutoa muhtasari wa ukweli huu wa lazima; huku tukifikiria juu ya Efeso sura ya
6.
Hebu tuanze mwanzoni
kabisa; katika bustani ya Adeni mambo yote yalikuwa mema, lakini baadaye nyoka
alikuja katika bustani. Je, hiyo ilikuwa ni kuvamiwa kwa nchi ya Mungu na
mapepo? Je, haya yalikuwa ni mashambulizi ya ghafla na upenyezaji usiotakiwa
ili kuharibu kusudi la Mungu? Kibinadamu, tunaweza kufikiri, kuwa ni jambo la
kuhuzunisha kuona shetani kupewa nafasi katika bustani, wakati kila kitu
kilikuwa salama na pengine tunashawishiwa kufikiri kuwa Adamu na Hawa wangeweza
kufanya maendeleo iwapo kama isingekuwa huo upenyezaji wa shetani. Tunaweza
kufikiri ingeweza kuwa ni vema kuitisha mkutano wa maombi na kuanza kumfunga na
kumkemea shetani au kumtaka Mungu atumie uwezo wake kumfukuza shetani. Lakini
pengine tunaweza kupata ufahamu mzuri zaidi na undani wake juu ya tukio hilo
kwa kuyatazama maandiko mengine.
Kama tutaangalia
katika kitabu cha kumbukumbu ya torati sura 8:2,3, Ayubu 1:6-12 na Mathayo 4:1,
kwa uangalifu na moja baada ya nyingine, tunaona kuwa Mungu aliruhusu watu wake
pamoja na mwanae pekee ili aweze kujaribiwa na kushawishiwa kwa kupitia
mazingira na kwa mashauri ya shetani. Kusudi la Mungu ni kuona kuwa hakuna mtu
hata mmoja awezaye kuumizwa, kuharibiwa au kuanguka katika dhambi bali waweze
kupitia katika mazingira hayo yanayowajaribu na kuwapima. Na ilikuwa ni
mazingira hayo ambayo ndiyo yangewataka kufanya uchaguzi! Kupitia mambo yote
mawili lile linalohusu namna walivyofikiri na lile lihusulo jinsi walivyoweza
kufanya. Na ilikuwa ni kupitia uchaguzi huu sahihi, kwa kuchagua kumwamini na
kumtii Mungu ndiko kutakako wafanya wakue kiroho katika maumbile na katika
kumfahamu Mungu. Majaribu na shida za jinsi hiyo kwa kweli ndizo zilizokuwa ni
njia yao ya kukua katika neema na kumfahamu Mungu. Mungu hakuhitaji watu wake
waanguke au watende dhambi. Hiyo ni kinyume cha tabia yake! Yeye alipenda
kuwaleta katika ufahamu na sura yake yeye mwenyewe, kwa wao kuukataa uovu na
kuchagua mema. Mistari inayofuatia inabeba ukweli huu tunao uangalia hapa Rumi
5:3-5; Heb.5:8,9,13,14; Yak.1:2-4; 1Pet.1:6-8.
Kusudi la Mungu la
kumturuhusu shetani amjaribu Adamu na Hawa ilikuwa ni kuwawezesha kukua katika
neema na haki ya Mungu wao, na katika upendo wao kwa yeye. Na walipokabiliana
na mashauri ya shetani jibu la Adamu na Hawa halikuwa ni kuitisha mkutano wa
maombi ili kumfukuza shetani nje ya Adeni; isipokuwa ni kuvaa silaha zote za
Mungu na kuupinga uongo wa shetani na sio kuyaruhusu mashauri ya shetani yapate
sehemu katika mioyo na akili zao! Hili la mwishoni linawakilisha vita vya
kiroho; lakini lile lililo tangulia halihusiki na lolote. Kama wangaliweza
kulifanya hilo la mwishoni, ndipo shetani
angewaachia Yakobo 4:7. Shetani alipomjia Hawa angepaswa kutumia upanga
wa roho dhidi yake shetani kwa sababu alilijua neno la Mungu kwamba watakufa
iwapo watakula mti wa ufahamu wa mema na mabaya. Lakini yeye hakuuchukua upanga
wa kiroho dhidi ya uwongo wa shetani; hakuchukua ngao ya imani dhidi ya
mashauri yake yanayoendelea. Mungu alikuwa ni mwema sana kwa Adamu na Hawa kwa
kuwaumbia kila kitu kwa ajili yao naye kuwaumbia kwa mfano wake mwenyewe ili
kwamba waweze kuwa na ushirika pamoja naye.
Yule nyoka
alipomjia, Hawa angeweza kutumia upanga wa kiroho dhidi yake, kwa vile alilijua
neno la Mungu kwamba wangekufa iwapo wangekula tunda lile. Lakini Hawa
hakuushika upanga wa Roho wala ngao ya imani juu ya maongo ya Shetani. Alisahau
ule wema wa Mungu kwao akiona tunda lile alilolitaka ili kujipendeza. Hivyo
shetani anawadanganya na kuwaongoza kuelekea kwenye kiburi. Na hasipo dirii ya
haki na chepeo ya wokovu kwa kule kumruhusu mawazo mabaya kuhusu Mungu yaweze
kupandwa ndani ya moyo wake na akili zake. Mawazo mabaya ya kutokuamini ambayo
shetani aliyapanda ndani ya moyo wake, ilimfanya Mungu aonekane kama ni mtu
asiyetujali na kutupenda, kana kwamba anayekataza mambo mazuri yasitupate,
kwamba aonekane ni mtu asiyetutakia mema ila mabaya. Mungu alikwisha waambia
wasile mti ule kwa ajili ya manufaa yao wao wenyewe na wokovu wao. Yeye
alipenda wawe kama yeye alivyo, lakini shetani aliwashauri kuwa Mungu alikuwa
anawazuia kula tunda la mti ule, kwa sababu hakupenda mambo mema yawajie.
Hakupenda wao wawe kama yeye alivyo! Ni kweli shetani ni baba wa uongo! Anaweza
tu kuzungumza uongo, na kusudi lake ni kutokumheshimu Mungu na tabia yake ndani
ya mioyo na akili za watu, ili kwamba watu hao wasiweze kuweka imani zao na
matumaini yao kwa Mungu. Kwa hakika pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu,
naye asiyeamini amemfanya Mungu kuwa ni muongo, 1Yoh.5:10. Pasipo imani
hatuwezi kuufaidi wokovu wa Mungu pamoja na neema yake ambao tumepewa kupitia
Kristo. Jambo hili kwa hakika shetani analijua na hapo ndipo anapopazingatia na
kuelekeza shughuli zake, ambayo ni kutufanya sisi tumtilie shaka Mungu!
Shetani huja kupanda
hoja na mawazo yasiyo na faida ndani ya mioyo ya watu, ikiwa pamoja na watu wa
Mungu. Kwa kutumia mashaauri yake yanayoendelea, yeye hutafuta kuziinua hoja
zake hizo kinyume na ufahamu wa Mungu; na kuangamiza ile sura na ufahamu wa
Mungu. Mashauri yake hayo yakudanganya yanaendelea kushikilia akili za watu
wale wanaoyakubali. Ni "mambo ya juu" yanayopinga maarifa na utukufu
wa Mungu, 2 Kor.4:4-5. Katika sura hii, ndani ya waraka wa Wakorinto wa pili,
Mtume Paulo anaelezea ukweli unaofanana na ule ulioko katika Efeso 6, yaani,
vita vyetu sio vya kimwili, lakini silaha zetu zina nguvu kupitia Mungu, na
kuziangusha "kila ngome" za aina hii, hoja za udanganyifu ndani ya
akili za watu, ambazo zinapinga ukweli na ufahamu wa Mungu. Sura hii
haiwakilishi mbinu ya kuzifunga roho zitawalazo katika maeneo ambazo ziko
mahala fulani huko angani, bali inakusudia kuonyesha silaha za ki-Mungu ambazo
tunazo pale tunaposhughulika na hoja za udanganyifu za shetani! Ufumbuzi kwa
Hawa, haikuwa ni kujaribu kumfunga shetani, isipokuwa ni kupinga na kukataa
uwongo wake na ndipo angeweza kumkimbia, Yak. 4:7.
Majaribu ya jinsi
hii yanaruhusiwa na Mungu. Kristo alipokuwa anabatizwa, mara moja akaongozwa na
Roho Mtakatifu kwenda nyikani kujaribiwa na shetani, Mt. 4:1. Hayo yalikuwa ni
maongozi ya ki-Mungu. Wala haikuwa ni kujipenyeza kwa mapepo! Hiyo ilikuwa ni
msingi wa makusudi alioudhamiria Mungu; haikuwa ni ajali ya bahati mbaya ili
kuiharibu kazi ya Mungu. Ilikuwa ni kupitia majaribu haya halisi, ndiyo
yanayotufanya tuwe imara katika Mungu na kukua kiroho. Tunasoma katika Injili
ya Luka kuwa Yesu alienda nyikani akiwa amejaa Roho. Na baadaye alirudi akiwa
na nguvu za Roho (Luka 4:1-14), na hilo ndilo kusudi la Mungu kwetu. Lakini
sasa Mungu anatutazamia tumchague, kumpenda na kumwamini yeye! Ikiwa hatuwezi, ndipo majaribu yanafunua
udhaifu, kujipendeza kwetu au matendo maovu katika mioyo yetu, Kumb.8:2,3. Sura
hii yenye msingi katika kumbukumbu ya Torati inatuonyesha kwamba Mungu
anayaruhusu majaribu ili kutufanya tuweze kujifunza kumtumaini yeye kuliko kitu
kingine chochote kile. Hata mbele ya mahitaji mengi na masumbufu; neno lake
ndilo lipaswalo kuwa la maana zaidi kwetu kuliko baraka zozote za muda zilizo
nje. Upendo wetu na imani unapaswa uendelezwe na kutumbukia ndani zaidi nyakati
kama hizo - na hivyo haitatusababishia sisi kukua katika maumbile kiroho tu -
bali pia itamtukuza Mungu!
Hebu angalia jinsi
Yesu anavyomshughulikia shetani pale nyikani. Yesu hakumpigia makelele shetani
na kumfunga kwa kujaribu kumfuata yeye! Kwa hakika, yeye ameongozwa katika
nyika ili aweze kujaribiwa na shetani. Na shetani mara zote huja na aina hiyo
hiyo ya mashauri: “Mungu wako yuko wapi? Je, wewe ni mwana wake hasa? Una njaa
na ni muhitaji. Je ni kweli anakujali wewe? Kwa nini hufanyi kitu kingine
chochote kile sasa ili kutimiza hitaji lako? Fanya ili kujisaidia wewe
mwenyewe! Fanya ili kujipanga mwenyewe. Ikiwa utajifurahisha mwenyewe, tazama
utanufaikaje na jinsi gani ambavyo mambo yako yatakuwia rahisi!” Mambo kama
hayo ndiyo tabia ya mashauri yake. Lakini Yesu alijibuje? Alijibu kwa upanga wa
roho - kwa neno la Mungu. Naye ananukuru katika kumbukumbu la Torati 8:31
Israel wamekuwa wakitembea jangwani kwa miaka 40; na Yesu aliitumia siku moja
nyikani kwa ajili ya kila mwaka wa miaka hiyo, akiwa anajaribiwa, kama vile na
wao walivyojaribiwa. Lakini Yesu hakuhusika na "mahitaji" yake
mwenyewe, wala hakuweza kumpatia muda wowote ule shetani kwa kuyasikiliza
mashauri yake - Yesu yeye aliishi kwa neno la Mungu, akimheshimu na kumwabudu
Mungu zaidi kuliko lolote lile lingine! Yesu alimpinga shetani na shetani
akamwachia kwa muda.
Lakini Israel
alishindwa kule jangwani. Wao hawakuishi kulingana na neno la Mungu pale
walipokabiliana na shida na mahitaji. Hawakuchukua upanga wa imani bali
waliruhusu shetani ajaze mioyo yao na akili zao kwa mashauri ya uongo kumhusu
Mungu. Na hivyo mashauri hayo yakajenga ngome katika fikara zao nao wakampinga
Mungu na kukufuru tabia yake. Asili ya vita vya kiroho vya shetani ni
kuwaelekeza watu waingie katika hali ya akili na moyo ambapo watakuwa
wakifikiri kama Israel walivyofikiri. Katika Kumb. 1:27, tunaambiwa kuwa kwa
kweli Israel waliamini kuwa Mungu alikuwa amewachukia na kwamba amewaleta
jangwani ili kuwaangamiza! Na hivyo ndivyo walivyoweza kufikiri hata baada ya
kuona yale maajabu ya Mungu aliyowafanyia huko Misri na katika jangwa! Huo ndio
udanganyifu wa dhambi na kutokuamini! Na hizo ndizo mbinu za shetani kutufunga
sisi tufikirie mambo mabaya kuhusu Mungu na kuutilia shaka wema wake juu yetu.
Ni kwa njia hiyo ndivyo shetani anavyo tafuta kutuleta au kutuweka nje ya neema
ya Mungu, wokovu na urithi ambao ametuwekea. Tunaweza kutenda dhambi, lakini
ikiwa tutajinyenyekeza wenyewe na kumtumainia Mungu kuutafuta msamaha wake,
ndipo atatusamehe kulingana na neno lake. Lakini ikiwa mtu atautilia shaka wema
wake na asili yake Mungu, mtu huzo atawezaje kupokea chochote toka kwa Mungu?
Tunaelewa kuwa Israel alipoteza kutokana na kutokuamini. Lakini hawakuweza
kumlaumu shetani kwa ajili ya hali ya mioyo yao. Mungu alikuwa anawategemea
wamwamini na kumtii yeye. Majaribu hayo yaliweza tu kufunua hali ya mioyo yao.
Ni kazi ya shetani
kuwapata watu ili waweze kuamini mambo haya, lakini sisi tunahusika kama wana
wa Mungu, ikiwa tutajiruhusu kushawishika katika kuamini mambo hayo! Hivyo
ndivyo moja ya sababu kuu za kwa nini Paulo anaandika yale anayofanya katika
Efeso 6.
Kama ilivyokuwa kwa
Hawa katika bustani, na ilivyo kwa Israeli kule jangwani, na ilivyo kuwa kwa
Yesu kule nyikani, ndivyo itakavyokuwa kwako wewe na mimi. Shetani hutujia ili
kupanda mashaka ndani ya mioyo yetu dhidi ya Mungu. Dhambi hii ya kutoamini
inavunja ushirika wetu na Mungu na inatuzuia kupokea mambo mema aliyo tuwekea
Mungu, inapofusha mioyo yetu isione kweli na inampa nafasi shetani kutufanya
mateka kwa aina zote au mwenendo mbaya. Hivyo tunapaswa kumpinga na kupigana
vita vizuri vya imani, ambavyo kwa hiyo tumetunzwa salama na kukua na ambavyo kwa
hiyo Mungu anaheshimika!
Mmoja wa
wahamasishaji wakuu wa mafundisho hayo ya kisasa anashauri kuwa Yesu alishiriki
katika "vita vya kiroho vya kiwango cha mbinu" (strategic - level
spiritual warfare) ambapo alijaribiwa nyikani. Anasema kuwa, eti hayo majaribu
aliyoyapata Yesu kule nyikani yanawakilisha kiwango cha juu cha mapambano ya
kiroho na shetani, ambayo wachache wetu tu au hakuna hata mmoja awezaye
kuyapata. Kwa vyovyote vile jambo kama hilo ni uwongo mtupu! Sote huwa
tunapitia katika majaribu yanayofanana vile vile kama hayo, ndani ya maisha
yetu! Shetani hatokezi kwetu kama aina fulani ya dudu baya lenye mapembe
kutushurutisha kufanya makosa. Ingekuwa ni wazi! Tungeweza kuona kupitia mbinu
hizo na kushituka! Shetani yeye hutumia hila. Huja katikati ya majaribu na
shida; na kujaribu kupanda lile linaloonekana kama la "maana" au
"mashauri yenye kusihi" na mawazo katika "akili" zetu.
Lakini mashauri yote hayo yanalo lengo moja tu na yanatuongoza kuelekea katika
aina moja ya hali ya akili - kutufanya tumtilie mashaka Mungu na tutende kwa
kujitegemea! “Yuko wapi sasa Mungu wako? Je, ni kweli anakujali? Kwa nini basi
huchagui njia nyepesi?” Haya ndiyo aina ya mawazo ambayo shetani anaweza
kuyapandikiza ndani ya akili zetu. Nasi tunaweza kuona kutokana na mistari
iliyotajwa hapo juu, kwamba iwapo tutakuwa tunaonyesha haja ya kutaka
kutosheleza miili yetu au sisi wenyewe, kuliko kumpenda na kumtii Mungu, ndipo
majaribu ya shetani yatatujia. Kwa vyovyote vile shetani hawezi kutujia na
kutusimamisha juu ya jengo, wala hataweza kuja na "kutupatia"
ulimwengu iwapo tutamwabudu yeye. Mazingira haya maalum kwa hakika ni ya
kipekee kabisa kulinganisha na majaribu ya Yesu. Lakini lile ambalo sio la
kipekee ni kwamba shetani anatujia na aina ile ile ya majaribu kwetu kila
mmoja. Ikiwa shetani hatafanikwa kutupata tumtilie mashaka Mungu, ndipo
anajaribu kutupata tutumbukie mbali zaidi katika yale tunayoyaamini ili kwamba
tuweze kuwa na kiburi na tuishie katika kumjaribu Mungu - ambayo ndiyo yale
ambayo shetani anajaribu kuyafanya kwa vyovyote vile, ili kumtia moyo Yesu
aweze kurukia juu ya hekalu, au shetani atajaribu kutia moyo au kuweka katika
akili zetu chanzo cha tendo fulani ambalo litatufurahisha, kufanya mambo yawe
rahisi kwa ajili yetu, kutupatia faida au litutukuze sisi. Hii ndiyo ilikuwa tabia
ya jaribu la mwisho la Yesu. Lakini maandiko yote yanatusihi kujikana wenyewe,
kumpinga shetani na tujikabidhi wenyewe kwa Mungu na kuyaweka matumaini yetu
kwake. Hivyo ndivyo alivyofanya Yesu, ambaye katika maeneo yote alijaribiwa
kama tunavyojaribiwa sisi, (Heb. 4:15), na hivyo ndivyo itupasavyo na sisi
kufanya. Hivyo ndivyo tunabyokua kiroho kiroho, na hivyo ndivyo tunavyoweza
kuingia katika urithi ambao Mungu ameutayarisha kwa ajili yetu katika Kristo.
Tabia halisi ya vita
vya kiroho kama ilivyo kuwa kwa Adamu na Hawa, kama ilivyo kuwa kwa Israel kule
jangwani, kama ilivyo kuwa kwa Yesu kule nyikani na kama ilivyo kwako wewe na
mimi, inatupasa kupinga na kukataa mashauri yote ya aina hii ili kusudi
yasipate nafasi katika mioyo yetu. Na tunapaswa kufanya hivyo hasa tuwapo
katikati ya majaribu, wakati wa shida na maumivu, tukiwa na juhudi katika imani
ya Mungu pamoja na wema wake ambayo inalikumbatia neno lake. Na katika hili
agano jipya sasa tumepewa nguvu ya kumpinga na kumshinda yule adui kwa roho na
ule uzima wa Kristo uliomo ndani yetu.
Nimewahi kuhudhuria
katika makanisa ambayo tumeweza kuomba dhidi ya shetani na kuzifunga roho
chafu. Wakati fulani mtu mwingine angeweza kuomba, angeweza kumfunga shetani na
kumtupa katika bahari au shimoni! Ninakiri ya kuwa niliweza kushangaa niliona
ni jinsi gani shetani alivyoweza kutoka huko alikotupiwa baada ya kuwa
tulikwisha "mfunga" katika mikutano ya maombi yetu! Nilijiuliza iwapo
yale tuliyokuwa tukiyafanya yalikuwa ni mambo ya kiroho au la, na iwapo ilikuwa
na ufanisi wa kweli mbali ya kutufanya sisi “tujisikie vizuri”. Na ilitufanya
sisi tujisikie vizuri na “wenye ushindi" kule kupandisha sauti zetu na
kupiga kelele na kuzifunga roho chafu - kwa vyovyote vile kulikuwa upande wa
washindi! Ninaamini kuwa shetani na roho chafu na kwamba wapo kazini kupinga
kazi ya Mungu ndani na kati ya watu, lakini kwa uaminifu kabisa siwezi kusema
kuwa kwa kelele katika mikutano ya maombi yetu ambayo inakazia juu ya shetani
na kuomba moja kwa moja dhidi yake, kuwa inaweza kuwa na ufanisi wowote ule wa
kweli. Hapa sisemi kuwa haitupasi kuomba juu ya mazingira ambayo yanaonyesha
kuwa shetani anaingilia, au haitupasi kupiga kelele katika maombi. Sisemi
hivyo. Napenda tu kuwatia moiyo watu wa Bwana katika maombi, lakini iwapo tutaangalia
katika maandiko kwa uaminifu, hatuwezi kupata kuiona aina hii ya uombaji kuwa
ndio njia ya kumshinda adui.
Niliwahi kujihusisha
na aina hii ya maombi hapo zamani, na bado sijabadili kuamini kwangu juu ya
Mungu au shetani, lakini ninatakiwa kukabiliana na yale ambayo kwa kweli
maandiko yanaonyesha na kufundisha, kuhusiana na kuomba pamoja na vita vya
kiroho. Vile vile nilipaswa kukabiliana na ukweli kwamba, mbali ya kutufanya
tujisikie wazuri, hatukuweza kwa hakika kuelewa au kusikia ushahidi wowote
kwamba kumfunga shetani kwetu au roho chafu kuliweza kuleta ufanisi wowote ule.
Katika hayo yote kuhusika kwangu ni kwamba tunajaribiwa na Ibilisi mwenyewe
kutuingiza katika kiburi. Mbinu moja wapo ya shetani, pale aliposhindwa kumpata
Yesu ili ajifurahishe mwenyewe na kuyabadili mawe yawe mkate, ilikuwa ni
kumshawishi Yesu zaidi ya njia nyingine. Kwa kuwa Yesu alikuwa akiishi kwa neno
la Mungu, shetani angejaribu kutumia hilo ili kumpeleka Yesu katika kiburi.
Shetani alimpandisha Yesu juu ya hekalu, akanukuu maandiko kutoka katika kitabu
cha Zaburi kuhusu malaika wakimwangalia Yesu ili kwamba asiweze kudhurika. Na
tena akasema ikiwa yeye ni mwana wa Mungu basi ajidhihirishe kwa kuruka kutoka
juu ya hekalu! Yesu hakufanya hivyo, akanukuu maandiko "usimjaribu bwana
Mungu wako", Kumb. 6:16. Katika majaribu hayo tunaona kwamba shetani
ananukuu maandiko lakini anafanya hivyo ili tu aweze kumpata Yesu ili
afanyemambo kipekee pasipo Mungu. Yesu hakuhitaji kufanya mbinu maalum kwa
ajili ya shetani ili kuhakikisha kuwa yeye ni mwana wa Mungu.Yesu anaishi tu
katika kumtukuza na kumpendeza Baba yake!
Lakini hivyo ndivyo
ambavyo shetani atajaribu kututendea kutujaza akili zetu na mambo ya hakika
yaliyo na ukweli fulani wa kimaanddiko, lakini yote hayo ni ili kutufanya
tuende mbali zaidi na yale ambayo Mungu ametuamuru ili atusababishie maumivu au
hasara kwa namna fulani. Hivyo watu wanaweza kufikiri, "sawa, sisi ni wana
wa Mungu naye ametupatia uwezo kumshinda shetani! Basi hebu tuombe dhidi yake
na kuzifunga nguvu zake!" Lakini mtazamo wa aina hii sio wa kibiblia. Ni
majivuno. Na inaenda mbali zaidi ya yale ambayo Mungu ametuagiza kuliko
kumshinda shetani, inalenga uangalifu wetu tuutupie kwa shetani na hivyo
kutufanya tumtukuze yeye na kumhesabia yeye kuwa ni maarufu na mwenye uwezo
kuliko ile aliyonayo kwa hakika au inayompasa! Hii kwa kweli inapora utukufu wa
Mungu na uweza wake katikati yetu! Bwana Yesu alisema kuwa - walipo wawili au
watatu wamekusanyika pamoja kwa jina langu; yeye atakuwa katikati yao. Hakusema
kuwa - pale wawili au watatu wamekusanyika pamoja kwa jina lake, shetani
atakuwa hapo na kwa hiyo kanisa litahitajika kuomba na kuzifunga na kukemea
roho chafu kutoka katika kusanyiko lao! Lakini ikiwa tutafanya aina hii ya
mambo nje ya aina fulani za desturi zetu tulizo nazo, hapo tutakuwa
tukidhirisha kutokuamini katika Mungu na katika neno lake na tutakuwa
tunamwabudu shetani kwa yale matendo ya ushirikina ambayo tunayaita ni vita vya
kiroho! Ninalifahamu kanisa fulani katika mji ninaoishi, ambako mchungaji wa
hapo aliwachukua watu ili kuombea jengo lote la kanisa - kuzifukuza roho chafu
ambazo alisema ndizo zilizokuwa zinaishi katika jingo lile na zinapinga kazi ya
Mungu sehemu hiyo! Jambo hili ni aina ya kutokuamini na ushirikina, tunaweza
kutumbukia humo kwa mafundisho haya ya kisasa!
Vita vya kiroho
inatuhusisha kusimama huku tukiwa tumeshika silaha ya imani katika Mungu pamoja
na neno lake kinyume na uongo wote, mashutumu na majaribu ya shetani. Hiyo
ndiyo inayoelezwa katika Efeso 6 yote. Haihusiki na kuvaa aina fulani ya silaha
za kiroho ili kwamba tuweze kupigana mieleka moja kwa moja na aina fulani ya
roho chafu au ya kieneo, tukipiga kelele na kukemea katika maombi. Kuhusiana na
kupiga kelele na kukasirika kwa ajili ya shetani, ambayo imeenea sana kwa
baadhi ya watu siku hizi, yapo maandiko fulani ambayo yanatuelekeza vizuri.
Tumekwisha kuona tayari jinsi Yesu alivyoweza kumkabili shetani kule Nyikani.
Hakuweza kupata joto na kukasirika kuhusiana na Ibiilisi, ampigie makelele kana
kwamba hapaswi kuwepo pale. Pengine tunaona kushangazwa jinsi ambavyo Mungu
alivyomwelezea yule shetani kule katika sura ya kwanza na ya pili ya kitabu cha
Ayubu. Mungu anamruhusu Shetani aseme maneno yake na anaruhusu mabishano yake
na matendo yake - lakini tu ni kulingana na kusudi lake mwenyewe. Mungu yu
salama na mwenye uhakika katika haki yake ya umilele. Yeye anatawala katika
haki, na kila mmoja kule mwishoni atahukumia kwa haki ya Mungu. Yeye pia ni
mwenye mamlaka juu ya mambo ya wanadamu na yeye anayemruhusu shetani kuwajaribu
watakatifu wake. Mungu hachanganyikiwi kuhusu shetani - hukumu yake ya mwisho
ni yenye uhakika. Shetani anatupwa katika ziwa la moto. Mpaka hapo, shetani
anachofanya ni kuzunguka huku na kule kama Simba angurumaye, naye anatafuta
kunyang'anya, kuua na kuangamiza. Bado anawadanganya watu na kupinga kazi ya
Mungu. Kwa wale wanao mwamini Krsito, nguvu za shetani zimevunjwa naye hana
uwezo dhidi yao, ingawaje kama tulivyokwisha kuona. Mungu anamruhusu shetani
hatua fulani, lakini yote hiyo ni kwa ajili ya kuwajaribu watu wake ili kwamba
imani yao ipate kuwa kama dhahabu! Lakini katika mfano wa hapo juu si Kristo
hapa duniani wala Mungu kule mbinguni aliyechemka kwa kumkaripia shetani.
Amepewa nafasi na fursa kulingana na hekima yake Mungu mwenyewe na mamlaka
zake, lakini kazi za shetani pia hukemewa na kuvunjwa pale anapoingilia kazi ya
Mungu ya kuokoa roho kama tulivyokwisha kuona katika Matendo ya Mitume. Sasa ni
Yuda anayeandika katika Agano Jipya anatupatia neno la kutuonya kuhusiana na
jambo hili. Yuda 1:8-10. Hapa anatuambia kuwa hata malaika mkuu Mikaeli hakutoa
mashutumu ya kukemea dhid ya shetani. Sisemi hapa kuwa shetani anayo nafasi
maalumu na uwezo ambao yatupasa sisi kuogopa. Hapana! Hapana kabisa! Aliye
ndani yetu ni mkuu kuliko yeye aliye nje ulimwenguni.
Lakini ninapenda
tuone maandiko yanavyotufunulia kuhusiana na jambo hili na yanavyofundisha.
Lengo langu katika kusema haya yote ni kuona kuwa, hatumpatii shetani nafasi
kubwa na uwezo katika kufikiri kwetu na ndani ya maombi yetu kwa kumhesabia
umaarufu ambao hastahili kuwa nao; au kwa kwenda mbali na maandiko kwa kujaribu
kupigana naye na kumkemea au kupambana na roho zitawalazo maeneo (roho za
kimaeneo) kama zinavyoitwa! Yuda hapa anaongelea kuhusu watu wanaoongea uovu
juu ya mambo wasiyo yajua au wasiyoyaelewa. Na hivyo ndivyo sawa sawa na hawa
waandishi wa kisasa na walimu wa kisasa wanavyofanya. Bila shaka roho chafu ni
ushetani. Lakini sasa hawa waandishi wa kisasa wanaongea mambo kuhusu hao
pasipo kuelewa wanasema nini hasa! Wanatutaka tukazie macho yetu kwa shetani na
roho chafu, tukiwapatia uwezo na mamlaka juu ya miji ambayo kwa kulingana na
maandiko hawanavyo! Kisha wanatutaka tujihusishe katika mapambano binafsi ya
kirogho pamoja na maroho hayo na kukemea dhidi yao katika maombi! Mambo hayo
yote yanaenda mbali zaidi na maandiko na pia yanaenda mbali zaidi na yale yote
ambayo Mungu ametuagiza.
Sipendi nikupatie
kanuni ya jinsi ya kuomba au kutokuomba katika mazingira maalum ambayo
utakabiliana nayo mbali ya kuelekeza maandiko halisi na ukweli wa kiroho ambao
unapaswa kutulinda katika kuomba kwetu. Pia sisemi kwamba hatuwezi kupiga
kelele au kuomba kwa sauti kuu inapohatijika tunapofanya maombezi – inategemea
na aina ya maombi. Ninaloandika ninaliandika juu ya kujaribiwa kwetu tupige
kelele kwa hasira dhidi ya Shetani kupita kiasi na bila kujali mafundisho ya
Biblia na mfano wa Yesu Kristo. Tunaweza kuhakikishiwa kuwa Kristo
aliziangamiza kazi zote za shetani juu ya msalaba na kuharibu mamlaka na uweza
pale msalabani. Hii inaweza kutufariji tunapoomba kwa Mungu kuhusu mazingira
ambayo tunaamini kuwa shetani anapinga kazi ya Mungu, lakini pasipo
kujishughulisha na mambo hayo yao yasiyo ya kibiblia ambayo yanahamasishwa na
waandishi hawa wa kisasa!
Nimewahi kuwasikia,
watu wakisema miaka mingi sasa, "namchukia shetani" hasa kama mtu
ametenda dhambi vibaya au ameumia vibaya. Haya, haikusaidia chochote kumchukia
shetani kwa ujumla haitoshi na wala sio hoja yenyewe. Hoja hapa ni kwamba iwapo
mtu atajikana mwenyewe na kumpenda pamoja na kumtii Mungu. Ile kinachoweza
kutusaidia zaidi katika maisha yetu kiroho ni iwapo tunazichukia dhambi na
kuipenda haki (Heb 1:9), ikiwa tunamwamini na kumtii Mungu. Tunapaswa kumpinga
shetani kwa moyo wetu wote na wala tusikubaliane na mashauri yake ya udanganyifu
au matoleo yake ya kujaribu watu. Hii ndiyo njia kuelekea kwenye furaha, amani,
na haki. Kutoka katika maandiko ningeweza kusema kuwa, ni jambo jema sana
kutokujihusisha mwenyewe na hisia zozote zile kuelekea kwa shetani. Yesu kule
nyikani hakupenyeza uso wake mbele kwa hasira yenye dharau na kuanza kumkemea
shetani, akirusha ngumi yake hewani! Je tunapaswa kufanya hivyo? Lakini tunaona
kuwa shetani hakuwa na uwezo wowowte juu yake, na Yesu alirudi toka nyikani
akiwa amejaa nguvu za Roho - baada ya kuwa amepinga vishawishi vya shetani.
Ikiwa unapenda kuchukia kitu chochte hapa duniani, basi uichukie dhambi na
katika hali ya kuwa hupendi kufanya lolote lile navyo. Na kama tunawaona
wengine wanatenda dhambi, basi hebu tumwombe Mungu ambaye ni tajiri wa rehema
na neema 1Yoh 5:16. Hebu tumfuate Yesu ambaye alipenda haki na akachukia maasi
(Ebr.1:9) ambaye alipinga na kukataa vishawishi vya shetani pasipo kukemea juu
yake kwa hasira, na ambaye kama kuhani mkuu huchukua majina yetu mara kwa mara
kifuani pake mbele za Mungu katika maombi! Kut 28:12, 29, Heb 7:25. Nasi
tuzifuate nyayo zake, Efs. 6:18.
Hebu sasa tutazame
sura nyinginezo za maandiko ambazo hutumiwa kuunga mkono mafundisho hayo mapya.
Daniel 10
Hii ni sura ya aina
yake ambavyo hutupatia kumbukumba za uwepo wa kimalaika ambao kuhusishwa na
nchi au ufalme. Hata hivyo katika sura hiyo hamna lolote linaloweza
kutufundisha au kutufanya tuamini kwamba watu wa Mungu wanaweza kujihusisha na
uombaji dhdi ya nguvu hizo.
Wayahudi
walichukuliwa mateka huko Babiloni na Daniel aliumizwa na katika kuhuzunika na
kumtafuta Mungu kwa niaba ya watu wake. Wayahudi hawakuchukuliwa mateka kwa
sababu ya nguvu za juu zaidi za shetani wala haikuwa nguvu za shetani ambazo
ndizo zilizokuwa zikiwashikilia matekani huko.
Waisraeli walitenda
dhambi ya mara nyingi kinyume na Mungu, na huo umateka waliowekwa ilikuwa ni
hukumu ya Mungu mwenyewe juu yao, lakini ni hukumu ambayo alikwisha waonya
mwanzoni. Na Daniel aliyatambua hayo yote. Hasa katika sura ile ya 9 tunamkuta
Daniel akiomba kwa Mungu akikiri kuwa umateka huo waliofanyiwa ni hukumu ya
Mungu kwa dhambi za Israel . Daniel anaungama dhambi za watu wake, ambazo ndizo
zilizosababisha hukumu hiyo, na anatafuta rehema za Mungu kwa ajili ya watu
wake. Katika ile sura ya 10 tunamkuta Daniel anahuzunika tena kwa muda wa wiki
tatu, ambapo baada ya hapo anatokewa na “malaika”; malaika huyu anamwelezea
kuhusiana na mapambano yaliyo tokea kati ya roho za kimalaika mstari ule wa
13,20. Malaika huyu ametumwa ili kujibu maombi ya Daniel lakini sasa alizuiwa
na "Mkuu wa Ufalme Uajemi". Lakini baadaye Mikaeli, mmoja wa malaika
wakuu, alikuja kumsaidia. Baadaye angeweza kurudi ili kupigana na mfalme wa
Uajemi na kisha mfalme wa Uyunani atakuja. Hapa inaonekana kwamba hayo ni
mapambano kati ya roho za kimalaika. Daniel alikuwa hapigani dhidi ya mfalme
uajemi au dhidi ya roho za kimataifa! Wala tu hakuwa na ufahamu wowote
kuhusiana na mapambano ya hao roho wa kimalaika pale alipokuwa akiomba na wala
haikuwa ni sehemu ya mbinu zake kuzifunga roho zozote zile zitawalazo maeneo
(roho za kimaeneo)! Hakuna hata mahala pamoja katika maombi yake anapopanga
kuzifunga roho chafu kana kwamba zenyewe ndizo zinazo husika na kule kutekwa
kwa waisraeli au kana kwamba shetani alikuwa na haki ya kisheria juu ya
waisraeli kwa sababu ya dhambi zao! Ilikuwa hafanani wala haina ukweli wowote.
Waisraeli walitenda dhambi kinyume na Mungu. Kule kutekwa kwao kulikuwa ni
matokeo ya dhambi zao na hiyo ndiyo ilikuwa ni hukumu ya Mungu juu yao. Jawabu
la hapo ilikuwa ni kuomba kwa Mungu kwa ajili ya rehema zake. Ilikuwa ni yeye
Mungu pekee ndiye angewarejesha watu wake baada ya miaka sabini katika nchi
yao. Kama alivyo ahidi Daniel 9:2, na hakuna mamlaka yoyote waka uweza ambao
ungeweza kuzuia hilo!
Sura hii kwa ujumla
inatuonyesha yale ambayo nilikuwa nikiyaeleza katika ile makala yangu ya kwanza
hali kadhalika na hii pia, kwa mfano watu wa Mungu wanapeleka maombi yao kwa
Mungu kwa niaba ya watu wake na kwa niaba ya kazi yake kati ya wanaume na wanawake.
Maombi ya Daniel yanakazia kwa Mungu pekee juu ya watu wake, juu ya rehema zake
na juu ya uvumilivu wake. Maombi yake yanakiri kwamba Mungu ni mtawala wa mambo
ya watu! Daniel anajihusisha katika kuomba kwa ajili ya watu wa Mungu! Sura
hiyo haitafundishi lolote lile kuhusiana na kuomba dhidi ya roho zitawalazo
maeneo (roho za kimaeneo) kwa sababu kwa ujumla hazina nafasi wala hazina
nafasi ndani ya maombi ya Daniel au katika maombi mengine yoyote yaliyomo ndani
ya Agano la kale. Kile ambacho tunakupata katika sura hiyo ambacho ni mtazamo
wa kipekee, ni kwamba kulikuwa na mapambano kati ya majeshi ya kimalaika
wenyewe kwa wenyewe, lakini haituonyeshi juu ya Daniel akiomba dhidi ya majeshi
hayo ya kimalaika. (Wengine wanaamini kwamba “malaika” yule aliyemjia Daniel
alikuwa Bwana Yesu mwenyewe.)
Tunapata tena
mtazamo mwingine mdogo katika milki ya kiroho wakati Elisha alipoomba kwa ajili
ya mtumishi wake mdogo, pale anapowaona maadui wakiwa wamewazunguka. Elisha
anamwambia mtumishi wake kuwa wapo wengi upande wetu kuliko walivyo upande wa
adui. Kisha anaomba ili Mungu apate kufungua macho ya mtumishi wake ili kwamba
apate kuona. 2Falm.6:16,17. Yule kijana ndipo anauona mlima umefurika farasi na
magari ya moto! Na jambo hili lilitukia wakati wa Agano la Kale! Na sasa
tunapofikiria juu ya sura hiyo ya Daniel. Tunapaswa kuamini kuwaKalvari
haijafanya jambo la tofauti katika milki ya kiroho pale tunapo soma sura kama
vile Efeso 1:17-23; 2:6, Yn. 2:15-21?! Lakini sasa hata katika Agano la Kale
lenyewe, watakatifu wa Mungu hawakujihusisha na mambo ya kuzifunga roho
zitawalazo maeneo, kwa sababu kulikuwa hakuna haja kwao kufanya hivyo! Walijua
kuwa Mungu ndiye mtawala na maombi yao yalielekezwa kwake nyakati za majaribu
na mapambano. Walikuwa wanajihusisha katika kuomba kwa ajili ya watu wa Mungu.
Matumaini yao, upendo na utii kumwelekea Mungu ilikuwa ni yale yanayomtukuza
yeye na yale yaliyowapatia usalama ao, mibaraka na ulinzi!
Kitabu cha Ufunuo
Waandishi hao
wanafanya makosa yale yale wanapoelekea katika Ufunuo 12. Wanafanya hivyo ili
kuthibitisha mawazo yao juu ya mbinu za kiwango cha vita vya kiroho. Kuna
mapambano kule mbinguni kati ya Mikael na malaika zake na shetani na malaika
zake, na shetani ametupwa inje, mstari wa 7 na 8. Lakini hapa napo kile ambacho
tayari tumekwisha kukionyesha ni mapambano kati ya jamii ya kimalaika, na ni
ishara ya aya ya aina ya kipekee ya mwana aliyenaswa huko juu mbinguni na
kutupwa chini ya mbingu ya shetani. Vyovyote vile viwavyo juu ya tafsiri zetu
za sura hiyo yote kwa ujumla. Hakuna lolote pale kwa njia ya mifano na
mafundisho ili kuunga mkono mawazo kuwa watakatifu wanapaswa kujihusisha katika
kuzifunga roho zitawalazo maeneo. Hayo hayakuwa ni maombi ya mashujaa ambao
walimshusha chini shetani toka mbinguni! Kwa kweli waandishi hawa wa kisasa
wanapenda kurejea katika kitabu cha Ufunuo kwa ujumla, kwa sababu humo nguvu za
uovu zinawakilishwa kwa mtindo wa ishara na picha. Wanasema kuwa uwakilishi huu
unakumbukikia mamlaka na uweza na kwa hiyo unathibitisha uwepo wa zile roho
zitawalazo maeneo. Lakini hakuna hata moja kati ya hayo yote kuwa ndiyo hoja
yenyewe! Tunaamini juu ya uwepo wa mamlaka na uweza, lakini hakuna popote pale
ambapo watakatifu walijihusisha na kuzitambua pamoja na kuyafunga majeshi hayo
ya uovu - hakuna hata katika kitabu cha Ufunuo.
Kinyume chake,
alipokuwa akihutubia katika makanisa ya Smirna na Pergamo, (Ufunuo 2:8-17),
Bwana anaongelea kuhusu wale walio katika Sinagogi la shetani, na mahala ambapo
shetani anakaa. Lakini Bwana hawasihi watu wake kuomba dhidi ya maroho
yatawalayo maeneo kana kwamba yenyewe yanayo uwezo wa zaidi kuzuia yale ambayo
Mungu alikuwa anataka kuyafanya. Kinyume chake tunaona hapa, kama ilivyo katika
sehemu nyingine za maandiko, kuwa Bwana anatumia au anamruhusu adui kuwa tihani
au kuwajaribu watu wake, hata katika kifo. Anajitukuza jina lake kwa kupitia
watu wake, kwa kuwaonyesha watu, mapepo na malaika kuwa uzima wake ndani ya
watu wake ni wenye ushindi katika mambo yote na kwamba watu wake wanampenda
Mungu wao zaidi kuliko chochote kile - hata zaidi ya uzima wenyewe. Lakini
anawahakikishia juu ya taji ya uzima na kwamba wasiogope lolote lile ambalo
shetani anawatupia. Mungu ni mtawala anaweza kuwaokoa watu kutokana na nguvu za
giza na za shetani, kama alivyofanya kule Efeso, naye anaweza kumruhusu shetani
kujaribu mabaya yake kwa watu wake Mungu kwa nje, ili kusudi kulitukuza jina
lake na kuwafanya watu kuwa kama dhahabu. Kati ya nyaraka kwa makanisa yote
saba hakuna hata sehemu moja inayoonyesha kuwa shetani kwa namna fulani anafanikiwa
katika hizo kazi za Mungu kwenye miji hiyo. Hapana, kuhusika kwa Bwana ilikuwa
ni kuhusu dhambi, hali ya kiroho na mafundisho ya uongo kati ya watu wake
mwenyewe tu, ambao ndio aliokuwa anawajibika nao na ambao alikuwa anawasihi
wafikie toba.
Yeremia 1:9,10
Hiyo ni sura
nyingine ambayo wanapendelea sana kuikumbukia wakiweka kama mfano wa
"mbinu za kiwango cha vita vya kiroho". Wanatueleza kuwa Yeremia
alipewa uwezo wa Mungu kuzifunga roho za kimaeneo, kwa vyovyote vile mistari
hiyo haina lolote lile la aina hiyo. Katika Amosi 3:7, tunaambiwa kwamba
"Bwana Mungu hatafanya lolote lile, bila kuwaunulia watumishi wake manabii
siri yake", na katika mstari wa 5 wa Yeremia sura ya kwanza, tunaambiwa
kuwa Mungu amemchagua Yeremia kama nabii. Kwa maneno mengine Mungu angeweza
kusema kwa kupitia nabii Yeremia, hukumu zile ambazo yeye Mungu atakwenda
kuhakikisha kuwa zinapokea kabla Mungu hajafanya hivyo. Ataweza kutangaza
baraza na amri zake kwa kinywa cha Yeremia. Nasi tunao mfano wa karibu katika
mstari unaofuatia ambazo Yeremia anaona mafunuo ambayo yanatabiri juu ya
hukumu, ambayo Mungu anakwenda kuileta juu ya Yerusalemu kutoka Kaskazini.
Hivyo ndiyo maana ya ule mstari wa kumi, mstari huu haurejei kwenye aina yoyote
ile ya kuzifunga roho zitawalazo maeneo kwa kupita Yeremia au aina yoyote ile
ya vita vya kiroho! Roho hizo za kitaifa zilikuwa hazianzishi mashambulizi juu
ya Yerusalemu na kwa hiyo kuleta upinzani wa kazi ya Mungu hapo! Hiyo ilikuwa
ni hukumu ya Mungu kwa watu wake. Hakuna sehemu yoyote ambapo Yeremia anatafuta
kuzifunga roho zitawalazo maeneo ambazo zinategemewa kuipinga mipango ya Mungu
wala hafundishi maombi kama hayo. Kitabu cha Yeremia kwa ujumla kinaonyesha
mambo ambayo nimekuwa nikiyasema kwa muda mrefu, kwamba Mungu anahuzunishwa na hali
ya moyo na dhambi za watu wake na hii ndiyo tatizo pekee la kweli ambalo
limekwisha kutambuliwa. Mbali na maonyo ya tangu mwanzo ya hukumu ya Mungu,
huduma ya kiroho ya Yeremia inamhusisha yeye katika kuwasihi watu wa Mungu
kutubu na maombolezo kwa niaba yao - Yer.4:1-6; 14:7-9. Hiyo ni mistari miwili
michache tu kati ya habari zinazolingana katika Yeremia!
Ezekiel 4:1-3
Katika sura hii,
Mungu anamwagiza Ezekiel kuchukua tofali na achore ramani ya Yerusalem juu
yake. Kisha ajenge ngome juu yake na kufanya boma juu yake. Sura hii
inatuonyesha jinsi Mungu anavyotangaza hukumu yake mwenyewe dhidi ya Yerusalem
kupitia maneno na matendo ya ishara ya nabii Ezekiel. Hata hivyo, hii ndiyo
sura ambayo hawa waandishi wa kisasa wanapenda kuitumia kukumbushia kama habari
ambayo inaunga mkono mafundisho yao kuhusu "uchoraji ramani ya
kiroho"! Yaani, anatuambia kuwa mistari hiyo inatuonyesha kuwa tunapaswa
kuchunguza na kugundua ni dhambi gani kuu, kukosa haki, na usitawi au uovu wa
jamii unaochukua nafasi katika mji huo, hata kurudi nyuma zaidi hata ya miaka
100, na katika maeneo gani ya mji huo mambo hayo yanachukua nafasi zaidi. Kwa
maneno mengine tunatakiwa kuchora aina ya "ramani" ya kiroho ya mji
wetu au jiji. Eti hiyo, wanasema, itatusaidia kutambua roho za aina mabli mbali
zitawalazo maeneo ambazo zinayo "haki ya kisheria na mamlaka" juu ya
jiji hilo kwa sababu ya dhambi hizo zilizopita. Wanadai kwamba hapo ndipo sasa
tunaweza kwa ufasaha na ufanisi tukaomba dhidi ya roho hizo mbaya pamoja na
kizifunga! Hii inafikiriwa kuwakilisha "ujengaji wa boma" ya kiroho
katika mji! Hii inaweza vile vile ikahusisha na mambo ya "maombi ya
matembezi" kuzunguka maeneo fulani ya mji. Hayo yote yanafikiriwa kuwa
yanaweza kuukomboa mji kutokana na haya maroho ya kimaeneo na ndipo
tutakapoweza kuhubiri sehemu hiyo kwa mafanikio! Je, huu sio roho ya
udanganyifu nyuma ya aina hii ya mafundisho ambayo yanaweza kupotosha maandiko
namna hii?! Ezekiel hakujishughulisha na aina yoyote ya mambo kama haya, ya
kushughulika na kuzitambua na kuzishambulia roho hizo za kimataifa ili aweze
kukomboa Yerusalemu! Ezekiel hakuhitaji kutafuta lolote lile lihusulo roho hizi
za kitaifa, na sababu moja kubwa ilikuwa ni kwamba roho hizo zitawalazo maeneo
(roho za kimaeneo) halikuwa ni tatizo kwake. Tatizo halikuhitaji uchunguzi
wowote! Lilikuwa ni wazi kama vile siku ilivyo wazi! Waisrael walikuwa
wametenda dhambi na kuasi dhidi ya Mungu mara nyingi na walihitaji watubu
kutoka ndani ya mioyo yao!
Ilikuwa ni Mungu
ambaye anasababisha kuzingirwa kwa watu wake, iwe kama hukumu juu yao kwa
sababu ya ugumu wa mioyo yao! Na Mungu analitangaza hilo kwa uwazi zaidi kwa
watu wake kupitia matendo ya Ishara ya nabii Ezekiel. Ezekiel alikuwa hazifungi
roho zitawalazo maeneo ili kwamba wasioamini kule Yerusalemu wangeweza kumrudia
Mungu! Yeye alikuwa akitangaza hukumu ya Mungu kwa watu wake mwenyewe, ambayo
ilikuwa haitoi mwanya wa kutoroka, iwapo watu wake watakuwa hawajamgeukia yeye
kwa mioyo yao yote! Mafundisho hayo yote yahusuyo "kuchora ramani za
kiroho" ni yenye kasoro na inaanzisha mashambulizi juu ya injili ya Bwana
Yesu Kristo. Mmoja wa waanzilishi wake wakubwa ni George Otis ambaye mafundisho
yake tuliyaangalia mapema katika makala zilizopita.
Tunachoweza kuona
hapa, tutakipata pia katika sura zote ambazo waandishi hawa wa kisasa
huzirejea. Yaani, kwa vile wameshindwa kutupatia hata mfano mmoja tu wa
mafundisho yao kutoka katika Biblia; wanajaribu kutumia habari yoyote ile
ambayo kwa namna yoyote ile inawarejesha kwenye tukio moja la mafundisho yao na
mara moja wanalichukulia maanani kuwa habari hiyo inaunga mkono mafundisho yao
yote juu ya "vita vya kiroho". Kwa hiyo, iwapo kuna mstari wowote
unaoturejesha kwenye "mamlaka na uweza" au mstari unaoturejesha"
kuzifunga" au mstari wowote unaoongelea kuhusu "kuzishusha
chini", basi mstari huu ndio wanaoutumia ili kuunga mkono mfumo wao mzima
wa mafundisho yahusuyo “vita vya kiroho”! Katika kufanya hivyo, wanachafua
maana halisi ya mistari ile wanayoitumia. Lakini sasa, tunapoiangalia mistari
hiyo wanayoirejea, ndipo tunaona kuwa mistari hiyo inaonyesha tu ukweli ambao
nimekuwa nikiuelezea katika makala hii. Yaani kwamba Mungu anahusika na hali ya
mioyo ya watu wake pamoja na dhambi, na kwamba ni kupitia maombezi ya
watakatifu wake kwa Mungu na kupitia tangazo la neno la Mungu kwa watu wake;
kwamba kazi ya Mungu katika kuokoa watu inapaswa kutimilizwa! Vitabu vya
Daniel, Ufunuo, na Yeremia wote wanaonyesha hili - hali kadhalika na sehemu
nyingine za Biblia.
Mahali palipoinuka
Mungu aliwaambia
Waisrael kuzibomoa kabisa mahali pa juu pa ibada za sanamu za mataifa mengine
pale watakapo fika ili kuimiliki nchi, (Kumb. 12:2). Lakini hawa waandishi wa
kisasa wanasema kuwa mahali pa juu panawakilisha maroho yatawalayo maeneo (roho
za kimaeneo) na wanatoa mifano namna ambavyo mataifa na makabila ya kipagani
waliamini kwamba miungu yao mbali mbali ilitawala juu ya maeneo maalum. Kwanza,
tunaweza kusoma kuwa, haileti tofauti yoyote iwapo mahali pa juu panakumbukia
kwa roho zitawalazo maeneo au la; kwa sababu hatuoni sehemu yoyote katika
kumbukumbu ya Torati ambayo Mungu anawasihi watu wake kujishughulisha na
"vita vya kiroho" na maroho ya aina hii; wala hatuna hata mfano mmoja
wa Waisrael wakifanya hivyo. Maana yake hapa ipo wazi kabisa kuwa. Kuabudu
sanamu wa mahali pa juu, inawakilisha dhambi dhidi ya Mungu wa asili ya msingi
mkuu. Mungu alizuia hilo kwenye amri zake ya kwanza. Na kwa hakika aliwahitaji
kuzivunja aina yote ya mahala pa masanamu. Tatizo la msingi halikuwa roho za
kimaeneo, bali kule kuwepo na kuabudu kwa mahala pa juu kuliwakilisha dhambi ya
waisrael na uasi, dhidi ya Mungu. Tatizo halisi ni katika mioyo ya watu na wala
siyo kule angani! Matengenezo yake yalikuwa ni neno la Mungu likiwajia waisrael
ili kuwaelekeza kwenye kutubu ambayo kwa vyovyote ingehusisha kuvunjwa kwa
maibada ya sanamu ya mahali pa juu na kurejea kwa Mungu kwa mioyo yao yote.
Kama nilivyokwisha kusema mahala pengine, pasipo kutubu, kwa vyovyote vile
kutampatia shetani uwanja na fursa ya kupotosha mioyo yao zaidi. Lakini sasa
jawabu hapa sio kumfunga shetani, isipokuwa ni toba halisi ya watu wa Mungu
ambao ndiyo inayomnyang'anya shetani ile fursa ya kufanya kazi katika maisha ya
watu! (Mwandishi wa vitabu mmoja anasema kwamba, waisrael wengi waliamini kuwa
"nchi ya Mungu" ilikuwa ni Kaanani, na kwamba hii ndiyo inayounga
mkono wazo la maroho fulani kutawala juu ya maeneo fulani ya kijiografia!
Lakini kama wewe unaijua Biblia na mistari kama hii; Zab. 24:1- "Nchi na
vyote viijazavyo ni mali ya Bwana", ndipo sasa nitaacha kwako kutoa maamuzi
yako kuhusu hoja hizi!) Sasa, kwa sababu 1 Kor.10:20, ninaamini kuwa watu wale
wanaojihusisha katika Ibada za sanamu wanayatumikia mapepo, na kwamba majeshi
ya mapepo yapo nyuma ya mambo kama hayo. Na ulimwengu wa Kirumi wa nyakati za
mtume Paulo kulikuwepo na kujaa kwa maibada ya jinsi hiyo. Lakini hata hivyo
hakuna mahala popote pale ambapo Paulo anawasihi watakatifu kuzitambua na kisha
kuzifunga "roho hizi za kitaifa". Lakini katika hamu yao kubwa ya
kuthibitisha kuwepo kwa maroho haya ya kitaifa, waandishi hawa wa kisasa mara
nyingi hurejea kwenye kuamini kwa mataifa ya kipagani na makabila yao katika
Agano la Kale na kati ya makabila ya siku hizi. Wanasema kuwa watu wapagani
hapo kale na nyakati hizi wanaamini kuwa roho mbaya zinatawala juu ya maeneo
maalum na kwamba, kwa hiyo tunapaswa kuchukulia maanani mambo haya na kwamba
huenda ukawepo ukweli fulani ndani yake. Ni huzuni kuona kuwa wao wanajaribu
kupata mkazo mkuu wa mawazo yao ya roho za kimaeneo, kutoka nje ya Biblia; na
ni kutoka katika imani za ushirikina za watu wale anaojihusisha na mambo ya
uchawi.
Sasa maandiko
yanasema wazi kuhusiana na kuwepo kwa mamlaka na uweza, lakini katika Agano
Jipya hapajatajwa lolote juu ya roho hizi zitawalazo maeneo. Hata hivyo, ikiwa
kuna vitu ambavyo wewe unaweza kuviita ni roho za kimaeneo au hapana hilo siyo
jambo ninalohusika nalo katika makala hii. Kuhusika kwangu kukuu, ni kwamba,
wapo watu ambao wanawaonya na kuwalazimisha watu wa Mungu ili kujaribu na
kutambua majina na tabia ya maroho haya mabaya na kisha kujaribu kujihusisha
kukabiliana nazo ana kwa ana na kupigana na maroho ya aina hii. Kufanya hivyo
ni kinyume na Biblia na kwa hiyo ni hatari kwa hao wanaoweza kukosea katika
hali hiyo! Na kufundisha watu kuwa mbinu za aina hii ni za muhimu kwa ajili ya
kuieneza injili ni udanganyifu na mashambulizi kwenye moyo wa Injili.
Hii inawakilisha
habari kuu na hoja ambayo wanaitumia kutoka katika Agano la Kale. Kwa hiyo sasa
tutakwenda kuangalia namna wanavyoitafsiri misitari katika Agano Jipya.
Mathayo 12:22-30
Sasa ijapokuwa
hayapo mafundisho yoyote yale katika sura hii yanayohusu kuzifunga roho
zitawalazo maeneo (roho za kimaeneo) ili kwamba kazi ya Mungu ipate kuendelea
katika maeneo fulani ya kijiografia, bado hawa walimu wa kisasa wanapenda
kurejea kwenye sura hiyo, kwa sababu sura hiyo inaongelea kuhusu "kumfunga
mtu mwenye nguvu" ule mstari wa 29. Ni wazi kutokana na sura hii, kuwa
yale ambayo Bwana anayaongelea ni kuwatoa mapepo kutoka kwa mtu binafsi. Hivyo
ndivyo ilivyo tokea katika ule mstari wa 22 na mafarisayo baadaye wakamshitaki
Yesu kwa kutoa mapepo kwa uweza wa shetani, pia hapa inajulikana kama
Beelzebuli, lakini yeye Yesu anawathibitishia kuwa hiyo inafanyika kwa kidole
cha Mungu kinachomwezesha kuwatoa mapepo. Na ni kutokana na habari hii ndipo
anaongea kuhusu kumfunga kwanza mtu mwenye nguvu kabla hajaviteka vitu vyake.
Lakini sasa kadiri
tunavyoendelea kuisoma habari hiyo, Bwana anakazia ukweli wake kuwa, hata sio
mapepo ambayo ndiyo tatizo kuu, isipokuwa ni kule kutokutubu au ugumu wa moyo
wa watu wenyewe. Yesu hakuwa na shida hata kidogo katika kuwafukuza mapepo
yatoke kwa watu. Lakini yeye hawalazimishi watu kutubu! Lakini kutokuamini na
ugumu wa moyo ndicho kinacho sababisha yeye kushangaa na kutoa machozi, Luka
19:41. Na kaatika ile Luka 13:34,35, Yesu anawaelezea hamu yake ya kutaka
kuwakusanya pamoja naye. Lakini hawakutaka na hivyo wameachiwa nyumba yao
ukiwa! Anawaambia mafarisayo kuwa ilikuwa ni rahisi kwa waninawi kutubu
walipohubiriwa na Yona (kwa hakika hapa hakuweza kuzifunga roho za kimaeneo
kwanza!). Lakini sasa mkuu kuliko Yona alikuwepo hapa, yaani Yesu, na bado
wayahudi walikataa kutubu, mstari wa 41. Kati ya maswala haya yote, roho za
kimaeneo halikuwa ndiyo tatizo lao, lakini kila suala lilikuwa na matokeo yake
ya tofauti kwa sababu ya utofauti wa hali ya mioyo ya watu! Lakini tena Bwana
anaendelea kuelezea kuwa mara tu roho mchafu amtokapo mtu na anarudi tena na
kuiangalia nyumba yake, "Ikiwa tupu, imefagiliwa na kutunzwa vizuri",
ndipo huenda na kuwachukua wenzie pamoja naye na kuja kukaa katika nyumba hiyo
na hali ya mtu huyo sasa huwa ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzo. Kisha
Bwana anasema, "hivyo ndivyo itakavyokuwa katika kizazi hiki cha
uovu". Na kama tulivyo kwisha kuona katika sura zilizopita ya Mathayo,
Yesu anailaumu miji ambamo amekwisha fanya kazi kubwa - ambayo imehusisha pia
na kuwatoa mapepo kwa watu - kwa sababu mbali ya hayo yote waliyoyaona
hawakutubu. Yesu alifukuza roho chafu kutoka kwa watu lakini hawakuruhusu
maisha yao ya ndani kujazwa na kukaliwa na matunda yapasayo toba. Pengine hii
ingeweza kufanya mioyo yao iwe imeandaliwa (nyumba zao) kwa ajili ya Bwana!
Lakini badala yake mioyo yao isiyo na toba iliyaacha maisha yao ya ndani kuwa
"matupu" na kuandaliwa kuvamiwa hata na mapepo mengi zaidi! Maelekezo
tunayoyapata katika sura hii ni kwamba, watu wanaweza wakawa na hamu kubwa sana
ya kupokea "mibaraka" ambayo Mungu anaitoa bure, lakini wanaweza
kufanya hivyo pasipo hata kutaka kubadili maisha yao! Sura hii inatuonyesha uwezo
wa Bwana wa kutoa mapepo kutoka kwa watu, lakini hiyo pia haileti maana yoyote
iwapo watu hawatatubu kikweli! Lakini hakuna lolote lile ndani ya sura hiyo
linalo wakilisha mafundisho yahusuyo kuzifunga roho ambazo zinadhaniwa kutawala
miji.
Mathayo 16:15-20
Kadhalika sura hii
inanukuliwa kwa sababu inaonyesha mamlaka ambayo kanisa limepewa
"kuzifunga". Kuzifunga nini? Haya, kwa vyovyote vile hawa walimu wa
kisasa wanasema kuwa hii inahusisha pia kuzifunga roho za kimaeneo. Lakini
hakuna lolote lile katika sura hii linalotuambia namna hiyo. Hata hivyo, iwapo
tutaiangalia ile sura ya 18 mstari wa 15-20, hapo panatupatia habari ambayo
inatufanya tuyaelewe maelezo haya ya Yesu, na habari yenyewe hapa ni nidhamu ya
kanisa. Wafafanuzi wengine wanaihusisha sura hiyo na ile ya Yohana 20:23, pale
ambapo Yesu anawapa uwezo mitume kuzizuia au kuziachilia dhambi za watu
wengine. Ukiijumlisha na hiyo, watu wengi wanakiri kwamba kuna umakini mkubwa
wa tafsiri ya kigiriki katika Mathayo 16:19 ambayo inasema, "lolote mtakalolifunga
duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote mtakaloliachilia duniani
litakuwa limeliachiliwa mbinguni." Hii kwa vyovyote vile ingeweza kuleta
maana nzuri inaonyesha kuwa mamlaka ya kanisa imesimamia juu ya utambuzi wa
kiroho au ujuzi wa yale yanayokubaliana na utendaji kazi wa mapenzi ya Mungu na
haki yake hapa duniani, kuliko usimamizi wa uweza na mamlaka za kanisa kama
inavyoona yafaa. Kwa hiyo katika Mtd. 5, hukumu juu ya Anania na Safira
halikuwa tu ni suala la Mtume Petro kupitisha hasira yake, lakini kile
alichokisema na kukifanya ilikuwa ni dalili ya akili za Mungu mwenyewe katika
muda huo; alipo kuwa akifanya kazi kwa uhuru na bila kukoma kupitia kanisa la
Mungu - yeye ambaye amepewa zaidi mengi yatahitajika kwake.
Kwa hiyo katika Mt.
18:15-20 Yesu analiweka jambo la kufunga na kuachilia katika habari maalum ya
nidhamu ya kanisa. Iwapo Yesu angependa kutufundisha juu ya umuhimu wakufunga
na kuachilia uweza wa kiroho kwa ajili ya kueneza injili, angeweza kufanya
hivyo katika sura hizo - lakini sasa hakufanya hivyo!
Marko 5:1-19
Wanarejea katika
sura hii ili kuonyesha watu kuwa zipo roho zinazohusika katika mikoa
kijiografia. Wanaonyesha hilo katika ule mstari wa 10. Pale ambapo mapepo
yanamwomba Yesu asiwafukuzie mbali na nchi ile. Hivyo inafikiriwa kuwa roho
hiyo ni ya aina ya "roho zitawalazo maeneo", lakini tunapoangalia
katika jambo hilo hilo katika Lk.8:31, tunaona kwamba sababu iliyomfanya pepo
huyo amwombe Yesu; sio kwa sababu kuwa walikuwa wanahofia kuwa Yesu atawapeleka
katika nchi nyingine, bali ni kwa sababu walikuwa wanaogopa kuwa Yesu
angewapeleka kwenye gushimo! ( Tazama pia Rumi 10;7 na Ufunuo 20:3 ). Hata
hivyo, mwandishi mmoja mkubwa anaendelea kusema kuwa; eti baada ya wale nguruwe
kutumbukizwa katika kifo chao maroho hayo yaliyowakalia walenguruwe
yaliwaachilia na kutoka na yakaenda kuwashawishi watu katika mkoa ule wawe
kinyume na Yesu - ndio maana kwamba walimwomba Yesu awaachilie mstari ule wa
57. Lakini sasa, tunaona tena katika habari ya Luka tunasoma kuwa, Yesu Kristo
aliporudia katika mkoa ule, "watu hao walimpokea kwa furaha!” - Lk.8:40.
Je, maroho hayo yalikuwa yamesafiri au labda yamelala usingizi kwamba sasa watu
hao walimpokea Yesu kwa furaha?! Hapana!
Mtu huyu aliyeponywa aliwahubiria Yesu kwao! Ilikuwa ni mahubiri ya Kristo
ambayo ndiyo yaliyoandaa na kuifungua mioyo yao! Kwa hiyo tena tunaona kuwa
sura hiyo hiyo wanayoinukuu siyo tu haithibitishi mafundisho yao isipokuwa kwa
kweli inakazia yale ambayo yamesemwa katika makala hii!
Mhamasishaji
mmojawapo anayeongoza katika mafundisho hayo ya kisasa, anakiri wazi kuwa kuna
sura chache sana katika Agano Jipya ambayo inaweza kutupatia mifano hii ya
""maroho ya kimaeneo". Kwa kweli, sura hiyo hapo juu ndiyo pekee
anayoitegemea katika kutambua kuwa labda pengine ndiyo iwe kwamba ni mfano ulio
wazi! Lakini kama vile tulivyokwisha kuona, sasa sura hiyo sio mfano ulio wazi
kabisa wa mafundisho yake. Zaidi ya yote, hata kama wangeweza kutupatia mifano
ya Agano Jipya juu ya roho hizi za kimaeneo, bado hawajaanza kutuonyesha kwamba
maandiko hayo yanafundisha au kutusihi sisi tuombe dhidi yake na kuzifunga roho
hizo ili kwamba kazi ya Mungu upate kuendelea! Na ni jambo hili ndilo lipo
katikati ya moyo wa mafundisho yao! Na ni jambo hili ndilo tunalolijali kuwa
sio la kibiblia na lisilo na afya yoyote. Lakini kwa kuwa hawapati mifano
yoyote ile ndani ya Biblia hivyo wanatumia muda wao mwingi katika kujaribu kwa
kuthibitisha kuwa roho hizi za kimaeneo zipo!
Pengine hata
tungeweza kutaja hapa kuwa, waandishi hawa wa kisasa wanatumia sura hii
kushauri kuwa tunapaswa kutafuta majina ya maroho haya ya kimaeneo ili
kuweza" kuyafunga". Ijapokuwa katika sura hii na ndipo sura pekee
ambayo Yesu anauliza jina la mapepo hayo, lakini pia haionyeshi kuwa yeye
alipenda kuyajua majina yao ili apate kuyafukuza. Katika mashauri mengine yote
yaliyomo katika Agano Jipya - roho chafu zinatolewa nje pasipo Yesu au mitume
kuomba kujua majina ya mapepo hayo. Na kwa vyovyote haupo ushauri wa mbali
katika Biblia ambao tunahitaji au tunapaswa kuugundua majina ya "roho za
kimaeneo" kabla ya "kuzifunga roho hizo!"
Matendo ya Mitume 19
Hiyo ni sura
nyingine tena ambayo pengine ingeweza kuaminiwa kuwa inaweza kuonyesha kuwa
roho za kimaeneo zinaishi na zinapinga kazi ya Injili; ijapokuwa inakubaliwa
kuwa bado sura hiyo haiwezi kuthibitisha hilo! Tunaambiwa na waandishi hawa wa
kisasa kwamba roho hizo za kitaifa zilizokuwa nyuma ya uungu wa Diana wa Efeso,
zilileta upinzani katika kazi ya Mungu kupitia mashambulizi ambayo Demotria
mtengenezaji wa vyombo vya vyuma alianzisha. Lakini hakuna lolote kati ya hayo
linaloleta maana yoyote. Kupitia mahubiri na huduma aliyoifanya Paulo, miujiza
mingi ilikwisha tendeka na umati mkubwa wa watu tayari ulikwisha rejea kwa
Bwana, lakini hawa waandishi wa kisasa wanasema kuwa roho za kimaeneo zinazuia
hayo yasitokee! Hivyo unatakiwa kuzifunga kwanza kabla watu hawajaanza kugeuza
kwa Bwana kwa wingi! Tunachoweza kusema hapa basi ni kuwa haya maroho ya kieneo
yalikuwa yamechelewa kiasi, katika kuifanya kazi yao, na hata yale waliyoyafanya,
haya kusababisha lolote lile kufuatana na uzuiaji wa Injili - usiku mmoja wa
misukosuko ambao ni Demotria pekee na wafuasi wake walipata kukemewa! Ni kweli,
wanaposema kuwa sura hii haiwezi kuthibitisha lolote lihusulo kuwepo na kazi ya
roho za kimaeneo!
Ninafikiri katika
kukata tamaa kutafuta chochote cha kuunga mkono mafundisho yao, ndipo huja na
kila aina ya mawazo na ubunifu. Kwa mfano, katika Mtdo.19:20, inasema kuwa neno
la Mungu lilizidi na kuongezeka kwa wingi na "lilishinda". Na mwandishi
mmoja anadai kuwa kwa neno la Mungu kushinda, lazima lishinde “juu ya kitu
Fulani”, kwa hiyo kitu fulani ndicho kinachopinga kazi ya Mungu. Na "kitu
fulani" ni kitu gani? Haya eti ni “roho za kimaeneo” tunaambiwa hivyo!
Waandishi hawa wote wanajarbu "kukisia" namna Paulo "labda"
alivyojiunga na ndugu wengine kuomba dhidi ya roho za kimaeneo ambazo
zilitawala juu ya mji wa Efeso, ili kwamba kazi ya Mungu iweze kufanikiwa
katika mji ule! Lakini neno la Mungu halitaji hayo.
Kadhalika
mhamasishaji mmoja maarufu wa mafundisho hayo anakumbushia Luka 11:22, mahala
ambapo Yesu alitaja "kumshinda" mtu mwenye nguvu. Katika sura
inayolingana na hiyo pale katika Marko 3:27 inaonyeshwa kuwa badala ya lile
neno la "kumshinda", Yesu anaongelea kuhusu "kumfunga" mtu
mwenye nguvu, hiyo ni nguvu za mapepo. Mwandishi huyo wa vitabu anaendelea tena
kutuambia kuwa, maneno hayo ya "kumshinda" na "kumfunga"
(ambayo kwayo anamaanisha kuzifunga roho chafu) kwamba yako sawa sawa ili
kwamba kila unapoliona neno "kushinda" katika agano Jipya, basi hiyo
inaweza kuonyesha kuwa ni kuzifunga roho mbaya roho za kimaeneo! Tunaambiwa pia
kuwa Yesu alipokuwa anayaandikia makanisa saba ya Asia na akiwasihi
"kushinda", eti alikuwa anafanya hivyo akiwataka watakatifu kuzifunga
roho za kimaeneo kwa mafanikio makubwa! Lakini tunapoangalia katika kile Yesu
anachokiongelea kwa makanisa hayo, hakuna lolote lile kwa dhahiri linalounga
mkono mawazo hayo yao. Hoja za jinsi hii zinachafua neno la kweli, kwa vile
Yesu hapa anaongea kuhusu watakatifu wasimame na kushikilia imani, upendo na
utii mbele ya kukabiliana na kila aina ya matatizo na majaribu na vishawishi.
"Kushinda" inaonyesha katika mwenendo wetu kiroho na kukua mbele za
Mungu, na wala sio kupigana katika maombi dhidi ya roho hizo za kitaifa! Ninasema
tena na tena kuwa haya mafundisho ya kisasa yanafanikiwa tu kutunyang'anya ule
ukweli.
Kwa njia hiyo hiyo,
wao hunukuu Yakobo 4:7 ambako tumeambiwa kuwa tujikabidhi kwa Mungu na tumpinge
shetani. Wao wanatafsiri kule kumpinga shetani kuwa kama ni kujumlisha pamoja
na kushambulia na kuzifunga roho za kimaeneo jambo ambalo Yakobo hataji chochote
kile cha aina hiyo! Hapa Yakobo anaelezea kuhusu mwenendo wa maisha yetu kiroho
mbele zake Mungu.
Paulo anatusihi,
tusilichafue neno la Mungu wala tusilichukue kwa hila bali tuligawe neno la
kweli katika haki. 2Kor.2:17; 4:2; 2Tim 2:15. Mifano niliyotaja hapo juu
inashindwa kabisa kutekeleza hayo yote!
Matendo ya Mitume
13:4 - 12
Katika sura hii yule
Elina Mchawi anajaribu kumzuia liwali wa nchi ile aliyejulikana kwa jina la
Sergio Paulo ili asiweze kuamini. Mtume Paulo anamkemea Eliaa na kumletea upofu
juu yake. Hapa sasa tunao mfano wa mtume akitumia mamlaka alizopewa na Bwana
ili kushughulika na upinzani huu ulio dhihirika wa kimapepo. Ukiipinga kazi ya
Injili (kwa mfano unaofanana na huo katika Mtd. 16:16-18) sasa, baada ya kuwa
Paulo amekwisha mshughulikia Elima, yule liwali wa nchi ile akaamini, na hii
inapaswa kutuonyesha sisi kuwa pengine na roho hizi zitawalazo maeneo ndizo
zinazowashikilia watu wasiweze kuamini. Hata hivyo mwandishi ambaye ndiye
anayeijenga hoja hiyo, yeye mwenyewe anakiri kwamba, sura hii kwa kweli
haitupatii ushahidi wowote ule au uthibitisho kuonyesha kuwa roho hizi
zitwalazo maeneo ndizo zilizohusika na matatizo hayo. Kwa hiyo angalau
ameonyesha uaminifu kuhusu hilo. Lakini sasa, waandishi hawa wa kisasa wao
hawaelezei kwa nini wao wanayaita matukio hayo kuwa ni mifano ya "mbinu za
vita za kiroho" (Hii ni kuwa kinyume na roho hizi za kitaifa au roho
zitawalazo maeneo), pale ambapo kulingana na mafundisho yao wao wenyewe,
matukio haya yanahusika na kiwango cha chini au kiwango cha vita ya kiroho ya
kilozi - hii ni kwamba kushughulika na mtu binafsi na nguvu zao za kiulozi
katika lolote like liwalo, hakuna lolote lile ambalo linafundisha au kuonyesha
kwetu chochote kile kuhusiana na kuzitambua na kuzifunga roho za kimaeneo.
Hitimisho
Waandishi pamoja na
walimu hawa wa kisasa hutumia muda wao msingi wakijaribu kuonyesha kuwa kuna
hata mambo haya ya roho zitawalazo maeneo, na labda mbali ya ule mfano mmoja
uliomo katika kitabu cha Daniel katika Agano la Kale, hawawezi kuelezea jambo
hili zaidi – bila shaka hawawezi kupata kutoka katika Agano Jipya. Hii ndiyo
sababu wanarukia imani nyingi za kipagani za kiaguzi ili kusudi waweze kupata
ushahidi fulani juu ya elimu yao hiyo. Lakini kama nilivyokwisha kusema, na
hata kama wanaweza kuonyesha kuwa roho zitawalazo maeneo zipo, hawawezi kuanza
kuthibitisha mwelekeo wao na mafundisho yao juu ya maombi dhidi ya roho hizi
pamoja na kuzifunga. Wanashindwa kabisa kutupatia hata mfano mmoja kutoka
katika maandiko yote ya watakatifu wakiomba dhidi ya roho hizi za kitaifa au za
kimaeneo. Wanashindwa kabisa kuturejesha hata kwenye andiko mojawapo
linafundisha kwamba kwa namna fulani kazi ya Mungu imezuiwa katika miji fulani
au jiji fulani au nchi, kwa sababu ya roho hizi zitawalazo maeneo na kwamba
watakatifu wanahitajika kuomba dhidi yao kabla watu hawajaweza kuamini na
kuifanya kazi ya Injili kuendelea.
Mpendwa msomaji,
ufuate yale yote yanayofundishwa na maandiko ya neno la Mungu, lakini usilogwe
na mafundisho haya ya kisasa kukufanya uende zaidi ya yale yanayofundishwa na
Biblia na papo hapo hayaongezei kwenye Injili ya Kristo bali kwa kweli
yanaipinga Injili.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI
ReplyDelete(Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)
MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA
kwa maelezo kamili piga namba +255742162843
(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.
NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.
Everyone
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.