UJUMBE: VIFUNGO VYA MWILINI
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Utangulizi:
Mungu anawapenda sana wanadamu na
Biblia inasema wazi kuhusu hili katika kitabu cha Maombolezo 3:31; Ni raha yake
kuona hatuna matatizo na tunaishi kwa amani. Mungu hakumuumba mwanadamu ateseke
bali alimuumba afanikiwe akiwa duniani na kuishi kwa furaha.
Wakati huohuo, shetani kwa asili
hapendi mtu aliyeumbwa na Mungu afanikiwe na ndio maana katika Luka 3:16
inasema, “…ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane…” (Matendo 10:38;
2Wathesalonike 2:18-19) kwa maandiko hayo tunaweza kujua kuwa shetani anaweza
kufunga, kuzuia, kupinga na kushindana na mtu. Kwa asili shetani ni mshindani
na furaha yake ni kuwatesa wanadamu ambao wanapendwa na Mungu. Yeye hufanya
hivi ili kuumiza moyo wa Mungu kupitia wanadamu walioumbwa na Mungu.
SHETANI ANAWEZA KUMFUNGA MTU:
Kama tulivyoona kuwa shetani anapenda
kuwatesa wanadamu na ili kutimiza lengo lake njia mojawapo anayotumia ni
kuwafunga watu. Na tunapotaja vifungo, tunakuwa tunazungumzia vifungo vya aina
kuu tatu, yaani, Vifungo vya mwilini, Vifungo vya rohoni na vifungo vya nafsini
kwasababu mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba iitwayo mwili. Katika hatua hii
ya kwanza tunaanza kuangalia kwa undani kuhusu vifungo vya mwilini:-
Mwili ni nini?
Hatuwezi kujua namna mwili unavyoweza
kufungwa bila kujua asili ya mwili wa binadamu. Tuanze kwa kuangalia andiko
hili Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi ya ardhi…”
kumbe asili ya mwili wa mwanadamu ni mavumbi au udongo. Na ndio maana katika
Isaya 64:8 Biblia inasema, “… sisi tu udongo nawe ni mfinyanzi wetu…” nabii
Isaya ambaye aliwahi kumuona Mungu lakini alijua ukweli huu kuwa mwili ni
mavumbi (Ayubu 7:21, 34:15). Kumbe pamoja na kuwa umevaa vizuri au umeupamba
mwili vizuri lakini asili yake ni udongo na katika ulimwengu wa roho huonekana
kuwa ni udongo kabisa. Kwa ufupi mwili wa mwanadamu ni udongo na mtu anapokufa
mwili huirudia nchi (Mhubiri 12:7) yaani mavumbi.
Ndio maana hata watu wanapooana ni
miili ndio ambayo inakuwa imeoana na si roho kwasababu mbinguni hakuna kuoa
wala kuoana kule ni katika roho. Kwa kujua kuwa mwili ni udongo basi namna
ambayo unaweza kuutendea udongo wa kawaida ndivyo vilevile waweza kuutendea
mwili wa binadamu. Udongo wa ardhini waweza kuoteshwa mimea na kuchimbwa,
vilevile na mwili wa binadamu waweza kufanyiwa hivyo.
TOFAUTI KATI YA MWILI NA UDONGO WA
KAWAIDA:
Kuna mambo mawili makuu
yanayosababisha mwili wa binadamu uwe tofauti na udongo wa kawaida.
1. Mwili uliwahi kushikwa na mikono
ya Mungu maana hakuna kitu kilichowahi kushikwa na Mungu na kikabaki kama
kilivyo.
2. Ndani ya mwili wa mwanadamu kuna
roho ambayo huuisha mwili na kuupa uhai. Kwasababu hizo mwili wa mwanadamu
hutofautina na udongo wa kawaida.
MWILI WA MWANADAMU UNAWEZA KUPANDIWA
VITU:
Biblia iko wazi kuwa Mungu wa
mbinguni anaweza kupanda, (Mwanzo 2:8); kumbe Mungu ambaye ni roho (Yohana
4:24) anaweza kupanda katika ardhi kabisa vivyo hivyo shetani naye ni roho naye
ana uwezo wa kupanda katika mwili ambao kwa asili ni udongo. Hapa ndipo lile
andiko la “KILA PANDO AMBALO BABA WA MBINGUNI HAKULIPANDA LITANG’OLEWA”
linapoleta maana; Mapando ambayo hayajapandwa na Baba wa mbinguni ni lazima
yatakuwa yamepandwa na shetani. Ndio maana ya mfano wa Yesu katika Mathayo
13:25 “lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya
ngano, akaenda zake.” Huyo ambaye Yesu anamwita adui ni shetani mwenyewe. Kumbe
unapolala au kujisahau shetani huja na kupanda magugu, hili jambo linatendeka
katika ulimwengu wa roho. Ni muhimu kujua siri hii kwamba kama vile udongo
unavyopandwa vivyohivyo shetani naye anao uwezo wa kupanda juu ya mwili wa
mwanadamu.
Unaweza kumsikia mtu analalamika kuwa
mwili unachoma lakini kumbe katika ulimwengu wa roho mtu huyo amechomwa mkuki
au kisu. Kufikia hapa sasa twaweza kujua kwanini Mungu alikataza kupanda mbegu
mbili za tofauti katika shamba moja (Mambo ya Walawi 19:19). Mungu alisema hivi
akitufundisha kuwa mahali ambapo Mungu amepanda shetani hatakiwi kupanda mahali
pale. Mtu anaweza kuhisi vitu vinatembea mwilini kumbe amepandiwa wanyama
wanaotembea katika mwili wake.
PEPO ANAWEZA KUJIGEUZA NA KUWA
CHOCHOTE:
Tulijifunza kuhusu sheria mbili za
rohoni, hapo tuliona uwezo wa pepo wachafu kujigeuza na kuwa kitu kingine yaani
kuvaa sura mbali mbali ili kutimiza kazi zao. Jambo hili twaweza kuliona katika
(1Wafalme 22:19-23) huyu pepo kwa asili hakuwa wa uongo lakini aliweza akaenda
na akawa pepo wa uongo. Yule pepo akaingia katika vinywa vya manabii wa Mfalme
Ahabu na kuwafanya wamtabirie uongo. Kwa maana hiyo tunaona uwezekano wa pepo
mchafu kujigeuza na kuwa kitu chochote ili kutimiza lengo alilokusudia.
Sasa twaweza jua kuwa mapando
tuliyokuwa tunayazungumzia ni pepo wachafu ambao hujigeuza na kuwa kile kitu na
hivi ndivyo vinavyoitwa “Vifungo vya mwilini”. Wakati mwingine pepo anaweza
kujigeuza na kuwa kinywa cha mtu, kama pepo wa katika (1wafalme 22:19-23)
alivyofanya. Hivyo; unaweza kumuona mtu anatukana matusi ya ajabu bila hata
aibu, kumbe pepo kajigeuza na kuwa kinywa chake. Pepo anaweza kuwa uso wa
simba, unamkuta baba mwenye nyumba mkali kwa watoto na mkewe kumbe ni uso wa
simba. Kwahiyo; pepo wanaweza kujigeuza maumbo mbalimbali kama nyani, simba,
paka hata bundi ili mradi kuharibu hatma ya mtu. Mnamkuta dada aolewi kumbe uso
wake umefunikwa kwa sura ya simba, kila mwanaume anayetaka kumchumbia haoni
sura nzuri bali anaona simba. Na ndio maana kuna baadhi ya wadada watumia muda
mwingi kujipodoa lakini bado hawapendezi kwa kuwa uso sio wa kwake.
KUNG’OA KILA KILICHOPANDWA KATIKA
MWILI WAKO:
Imeandikwa kila pando asilolipanda
Baba wa mbinguni litang’olewa, hivyo Mungu ametupa mamlaka ya kung’oa kila
pando la kishetani yaliyopandwa katika mwili. Miili yetu ni Hekalu la Roho
Mtakatifu hivyo shetani hatakiwi kugusa sehemu yoyote ya mwili wako.
Tumia mamlaka yako kung’oa kila pando
ambalo shetani amepanda katika maisha yako mapando ya magonjwa, homa
zisizoisha, ukimwi, mwasho wa mwili na matatizo mbalimbali. Jina la Yesu lina
mamlaka yote dhidi ya kazi zote za shetani katika maisha yako.
Sehemu ya Pili.
Utangulizi:
Shetani hajabadilika na silaha zake
ni zilezile; na jambo kubwa linaloshangaza watu ni kwamba silaha za shetani ni
zilezile lakini bado zinatenda kazi kwenye maisha ya watu. Moja ya kifungo
kinachosumbua watu ni kifungo cha tabia.
Mara nyingi kupata urafiki au
uhusiano ni rahisi lakini ili uweze kuendelea kuwa karibu na watu hao unatakiwa
uwe na tabia nzuri. Hivyo shetani anaweza kukuacha usonge mbele na kazi ya
Mungu lakini akakuzuia kupitia vifungo vya tabia. Kwasababu hii Roho Mtakatifu
ametaka leo tujifunze kuhusu vifungo vya tabia:
KIPAWA NA TABIA YA MTU:
Kuna vitu kadhaa vya kuangalia kama
mtu wa Mungu unayehitaji kufanikiwa, cha kwanza ni kipawa na pili ni tabia ya
mtu.
Mithali 18:16 “zawadi ya mtu humpatia
nafasi, humleta mbele ya watu wakuu; ” hili neno zawadi kwenye Biblia ya
kingereza linaitwa “GIFT” au kwa Kiswahili kipawa. Sasa basi kipawa cha mtu
chaweza kumfikisha mbele za watu wakubwa na kujulikana. Mfano mtu anaweza kuwa
na kipawa cha uwimbaji lakini anakaa kijijini na umaskini, ila kile kipawa
chake kikionekana kinaweza kumleta mtu huyo mjini hii ndio maana ya sehemu ya
kwanza ya andiko hilo. Kwasababu hiyo kila mtu aliyepo duniani amepewa kipawa
na Mungu ambacho kwa hicho anaweza kufika kwenye hatua ya juu zaidi.
Sasa basi kipawa cha mtu humleta mtu
kwenye mafanikio yake, tatizo linakuja pale mtu anapokuwa na kipawa lakini
tabia yake si nzuri. Hivyo tabia ndio ambayo inakubakiza katika sehemu uliyopo.
Mtu anaweza kuwa na macho ya rohoni au upako lakini kama tabia yake ni mbaya
hakuna mtu atakayetamani kuwa karibu naye. Ili Mungu akutumie kwa kiwango cha
juu ni muhimu kuanza kwa kubadili tabia yako.
TABIA ZA KIMUNGU NA TABIA ZA ASILI:
Biblia imeainisha tabia za aina
mbili, yaani tabia ya Kimungu na tabia ya kiasili au ya mwilini. Katika
1Wakoritho 2:14 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa
Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana
kwa jinsi ya rohoni.” 1Wakorintho 3:1 kuna tabia za rohoni na tabia za mwilini.
Hivyo anachosema Mtume Paulo ni kwamba unapoongea na watu inabidi ujue ama mtu
huyo ana tabia za rohoni au za mwilini. Mfano mtu anaweza kuwa mwimbaji mzuri
lakini ana tabia ya uongo; Mtu mwingine anaweza kuwa na kipawa kitakachomfanya
apate mchumba; lakini kama tabia yake ni mbaya ama uongo, au umbeya au uzinzi
inaweza kumfanya kuachwa na mchumba wake sio kwasababu hapendwi bali kwasababu
ya tabia. Tabia ya Kimungu ni tabia njema na nzuri lakini tabia ya kibinadamu
ni tabia mbaya aliyonayo mtu.
Shetani akitaka kuharibu kipawa cha
mtu anaanzia kwenye tabia yake; kwa maana hiyo tabia ya kibanadamu au ya
mwilini ndio hiyohiyo Biblia inaiita tabia ya kishetani. Ukisoma katika Yakobo
3:15 “Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya
kibinadamu, na Shetani.” Unaona kumbe tabia mbaya ya kinadamu ndio hiyo inaitwa
tabia ya kishetani. Mhubiri 10:1 “Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza
marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.” Hili ni
neno la hekima la Mfalme Suleimani kusema mainzi wanaweza kuharibu marhamu
nzuri; ikimaanisha unaweza kupata mpenyo katika maisha lakini tabia mbaya
inaweza kukupeleka mbali kabisa na upenyo wako.
Ndio maana waweza kumkuta mtu ni
mwombaji au anatenda miujiza lakini tabia yake ikawa mbaya kwasababu ya asili.
Jambo hili ndlo linalosabisha watu wengine kusema “kama ulokole ndio huu sitaki
kuokoka” kumbe mtu huyo aliwahi kumuona mtu ambaye ameokoka na ananena au
anaombea watu lakini ni mwongo au mzinzi. Katika Biblia, Samson alikuwa
mnadhiri wa Mungu na alikuwa amepakwa mafuta tangu tumboni mwa mamaye. Japokuwa
alikuwa mpakwa mafuta lakini alikuwa na tabia mbaya ya kutaka wasichana wa
kifilisti ambao Mungu alikataza tangu mwanzo. Hii ni sawa na mtu kung’ang’ania
kufungwa nira na mtu asiyeamini. Kwa njia hii Samson akakutana na Delila ambaye
lengo lake halikuwa upendo bali ni kumharibia kipawa chake kwa kuijua siri
yake. Vivyohivyo shetani amewaangamiza watu wa Mungu wengi kwa kuwafanya waoe
au kuolewa na watu wasiomjua Kristo na matokeo yake kile kipawa cha Kimungu
kilichokuwa ndani yao kinashindwa kuonekana tena.
KUBADILI TABIA:
Tabia mbaya ya mtu huondoka kwa
kuamua mwenyewe, hata kama mchungaji akuombee mara zote kama tabia yako ni
mbaya kwa asili inakulazimu kuamua kuibadili mwenyewe. Ni kweli tabia yako
inaweza kuwa imeshakupotezea kibali kwa watu au imeshakupotezea upenyo katika
maisha lakini ukiamua kuanza upya na BWANA na kuacha zile tabia mbaya Mungu
wetu ni wa nafasi ya pili. Mungu wetu anatoa nafasi ya pili biblia inasema,
“usifarahi ee adui yangu niangukapo mimi nitasimama tena”
Leo naongea na watu ambao walikuwa
waombaji leo hawaombi tena, walimuhofu Mungu lakini leo hawana hofu, walikuwa watakatifu
lakini leo ni waovu wakubwa Mungu anayo nafasi ya pili kwaajili yako. Amua
kutubu na kuacha dhambi na tabia hiyo mbaya; Mungu atakuwezesha tena kama
alivyomwezesha Samson kuwaangamiza wafilisti wote. Hivyo uamuzi wa kwanza ni
kuamua mwenyewe kuacha tabia hiyo.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
IFAHAMU MIZIMU NA MAJINI NA UNDANI WAKE KATIKA KUOMBA LOLOTE MALI,UTAJIRI, UPONYAJI N.K......
ReplyDeleteDOKTA MDIRO whatsp/call +255 742162843
ANGALIZO HUSIJARIBU JAMBO ULIZA KWA MAELEKEZO
Omba lolotee kwa njiaa ya mizimu mungu atatenda asema DOKTA MDIRO,
Kuna watu wakisikia neno mzimu wanatimkaa mbio lakini wakisikia neno mtakatifu wanabarikiwa na wakati ni kitu kilekile kasoro jina tu.
Daktari wa kiafrika anaitwa mganga wa kienyeji na wa kigeni ni Mtaalamu au mwanasayansi.
Ibada takatifu zinaitwa Kusali na za lienyeji zinaitwa matambiko amka wacha kulala.
watakatifu wa kiafrika wanaitwa mizimu, Mzimu nii binadamu yeyote yule aloachaa mwili na ANAISHIII na mungu karibu, kwaiyo sisi sote nii mizimu watarajiwa, unapomfananisha Mzimu na shetaani nikukataa ukuu wa afrikaa, wazungu Mzimu uloishiii vizuri dunian wanauita mtakatifu sisi mizimu iloishi vizuri na VIBAYA duniani tunaayaita mashetani.
Ndiomaana ktk orodha ya watakatifu karibu wote wazungu, waafrika wa kuwahesabu, @highlight
WAZUNGU KWENDA MAKABURINI WANAITA HIJJA , SISI KWENDA MAKABURINI TUNAITA MATANDIKO, HATA MZIMU WA NYERERE UMECHUKUWA MUDA KWELI KUFANYWA MTAKATIFU KWASABABU HAKUWA MZUGU.
🤫DOKTA MDIRO ANASEMA MIZIMU INAFAIDA KUBWA KTK MAISHA YA MUWAFRIKA, KUIKATAA NI KUKUBALI BALAAA NA KUKUBALI NI CHAZO CHA BARAKA.
NA MAISHA MEMA APA DUNIANI,
😒 Mikosi, manyanyaso balaa, na gundu ulizonazo haziwezi kuondoka mpk ukutane na mizimu yenu .
Dokta MDIRO ANAKUAMBIA MIZIMU YA BIBI YAKO NA BABU YAKO INAA MAJIBU YA MATATIZO YAKO.