ZIJUE SIRI KUBWA ZA SHETANI

KUTAZAMA VIDEO YAKE BONYEZA
HAPA CHINI▼▼


PICHA ZAKE ZOTE AKIWA MTUPU BONYEZA
HAPA CHINI▼▼


 INSI KUZIMU ILIVYO
Kuzimu ni nini?
Kuzimu ni mahali ambapo ni makao ya shetani na Joka kuu pamoja na malaika zake na mapepo na majini. Kuzimu ipo chini ya ardhi ya 900. Kuzimu kuna miji kama hapa ulimwenguni palivyo ila tofauti yake kuzimu pamejengwa kwa mpangilio, kuna magorofa ambayo hapa duniani hamna, kuna viwanda vya magari, nguo, vyakula, silaha na vinginevyo vingi.


BENKI YA KUZIMU (JLM BANK)
Benki hii kirefu chake ni Joka Kuu, Lusifa, Maxwell benki. Ndiyo benki ambayo ilikuwa inawapa watu pesa huku ulimwenguni pamoja na freemason ila nimeichoma na mtaona baadhi ya nchi zilizokuwa zikipata pesa kutoka kwenye benki hii, mtaona uchumi ukishuka, au mabenki yakififia na pia matajiri waliokuwa katika mtandao wa freemason wataporomoka. Ni wakati sasa ya watu wanaomtegemea MUNGU kutajirika na kumiliki. MUNGU anachukia sana na kazi hii ataifanya yeye mtakapoyaona hayo msishangae. Benki hii ina wanachama wengi sana waliopo duniani, wakiwemo manabii, wachungaji, wainjilisti, mitume, waalimu, wachezaji mpira maarufu, wasanii maarufu, idadi kubwa wanachukua pesa huko na ni watenda kazi wa shetani  (Black Money). Wana pesa ambazo ukiwakagua kimahesabu utaona ni pesa zisizojulikana zimetoka wapi asili yake.

MAVAZI YA KUZIMU

A)    WANAWAKE
1.         Mavazi haya ya kuzimu ambayo wanawake wanayovaa hapa ulimwenguni pasipokujua na wengine wakijua kabisa ni ya shetani ambayo yanabuniwa na Yezebeli ili kila anayevaa tayari amemfungia mwanamke baraka zake na pia kuyateka maisha yake na kumfungia asiende mbinguni, sababu katika mwili wake yeye anakuwa ni kahaba kiroho mpaka kimwili haijalishi kimwili yeye hatendi mambo ya ukahaba, ila kutokana na hilo vazi alilolivaa basi tayari anakuwa amevaa ukahaba na mapepo huishi juu yake bila kikwazo chochote.

2.           Mavazi haya asili yake ni kuzimu na mengine yamebadilishwa kwa kuandikwa kinyume mfano MAX wa kuzimu ikaandikwa WAX, huyu MAX yeye ndiye aliyekuwa namba tatu katika ufalme wa shetani na unapovaa kitu kilichoandikwa kwa jina lake tayari na wewe unamsujudu mzimu wa MAX na kuporwa baraka za maisha yako. Sasa wakawapiga watu upofu wakavipa vitu majina WAX- (MAX), pia NIDA nayo asili yake ni kuzimu.

3.         Yapo mavazi ya mwanamke ya kuonyesha tumbo wazi.


4.         Nguo za kuonyesha matiti na kuonyesha mgongo.

5.         Chupi za kike zenye zip na zenye mifuko ya kuwekea pesa.

6.         Chupi zilizochorwa moyo au zimeandikwa katika nguo za ndani za kike mfano; girlfriend, boyfriend, na maneno mengi tu ya ajabu, karibu, furahi, nakupenda mpenzi.

7.         Nguo za transparent.

8.         Stocking zote unapovaa unakuwa unavaa miguu ya majini.

9.         Vimini, katika ulimwengu wa roho wewe ni kahaba maarufu.

10.       Nguo zote zenye magamba au picha mfano wa nyoka, mamba, na nyingine zenye madoa doakama ya chui.

11.       Viatu vyote virefu- unapovivaa tayari unakuwa unaitwa twiga wa kuzimu na madhara yake maisha yako yanaibiwa ni kwa kupitia mlango huo.
12.         Pochi za mikononi pamoja na mabegi yote yenye scales au magamba au viatu mfano kamamagamba, ukiona tu utajua unapovitumia unakuwa umebeba nyoka na roho za shetani zinakumiliki. Inakuwa ni pamoja na mikanda yeyote yenye mfano wa picha za magamba.

13.       Nguo zenye mipasuko mbele, mfano katika skirt unapoivaa ina maana umewafungulia mapepo wa uzinzi waingie katika mwili wako na kwa njia hiyo ni lazima wataingia tu sababu wanao mlango.

14.       Eyeliner-  unapopaka katika jicho lako unakuwa unajiwekea alama na wewe ni mfuasi wa shetani, pia napenda uelewe kuwa na shetani na yeye huwa anajipaka eyeliner (wanja) katika jicho lake la kulia ila yeye hulizungushia mchoro wa duara, na unapojipaka wanja basi unakuwa wewe ni mali yake yamkini hata haujui na unampenda MUNGU.

15.       Kukata nyusi- unapokata hizo nywele unakuwa unayakata maisha yako na ndio sababu maisha ni magumu kwa wanawake wengi hiyo ni sababu moja wapo.

16.         Kuvaa shanga za kiunoni- kila unapovaa shanga katika kiuno chako unakuwa umejifungia majini, hata ukijifungia cheni ya gold au silver, uelewe tayari unayo majini katika mwili wako na madhara yake wanandoa wanakuwa wazinzi, faraka, ndoto za zinaa, mikosi na balaa, vitu hivyo havifai katika jina la YESU. Unapovivaa unakuwa unaliharibu hekalu la MUNGU kwa kufunga ndoa na mapepo katika kiuno chako, au kwa lugha nyingine hizo shanga ni pete za majini na unapovaa unajifungisha ndoa na wao katika ulimwengu wa roho.

17.       Nguo za kubana na kuonyesha maumbile yako yalivyo, jinsi ulivyoumbwa mfano hili siyo jambo jipya. Embu tembea katika maeneo mbali mbali utaona wanawake wamevaa suruali zinazoonyesha figure zao, sasa ujiulize wanamuonyesha nani? Jibu, wanawaletea wanaume maroho ya ushawishi ya uzinzi hivyo wanapovaa mavazi hayo tayari wao ni makahaba. Mavazi haya yameletwa ulimwenguni ili uzinzi ustawi na kuwateka wanaume katika majaribu, ili amri za MUNGU zivunjwe na kila anayevaa hivyo uelewe kwanza ni machukizo mbele za MUNGU na pia unatumikishwa katika upande wa shetani eidha kwa kujua au kutokujua. Sasa ufunguke, uyasitiri maungo yako au mwili, ili upone roho yako.

18.       Kuvaa mavazi ya kiume.

19.         Kuvaa hereni kubwa kuliko sikio- unakuwa unavaa hereni ya mama wa makahaba. Hereni salama ni ile ambayo ni ndogo ambayo inakuwa sawa na kasehemu cha kuwekea tundu la sikio, hizo kubwa kama bangili hizo ni za mama wa makahaba.

20.       Kila rangi unayoipaka katika kucha yako uelewe ni dhambi na unayafunika maisha yako usije ukafanikiwa, na pia yanaibiwa na yanapelekwa kuzimu unapewa wewe ya mapepo ambayo ni shida tupu, hata kupaka hyena kujichora mwili, matatoo yote ni dhambi. Unapojichora tattoo, unajiwekea alama wewe ni freemason, ni wa kuzimu siku zote.

21.         Kila product yenye neno ultra, iwe katika kitu chochote, kinatoka kuzimu kuja kuiba vitu vya wanadamu na kuwaharibu.

22.         Unapoweka rollers kichwani, unakuwa umejiwekea funza wa kuzimu katika akili zako. Na akili zako na ufahamu kuibiwa na hao funza wa kuzimu na matokeo yake mtu unakuwa haujielewi elewi na akili zinadumaa.

23.       Kutairiwa wanawake hiyo ni dhambi MUNGU hajamruhusu mwanamke atairiwe. Mwanamke anapotairiwa kile kiungo kilichokatwa kinapelekwa kuzimu na kumuibia mwanamke uthamani wa uke wake na uzao wake na kuharibu ndoa na kufanya mwanamke achanike wakati wa kuzaa na kijiwekea alama wewe ni wa mapepo.

24.         Pedicure- unaposugua miguu salooni unakuwa unayaondoa maisha yako na unamkufuru MUNGU yeye aliyekuumba na kukuwekea utayari wako katika miguu.







B)    WANAUME
•          Mavazi ya wanaume ambayo asili yake ni kutoka kuzimu katika viwanda vya kuzimu yapo mengi sana ila nitaelezea kwa kiasi fulani ili mpate picha na mpone.

•          Mavazi yote yenye nembo za ajabu, mfano T-shirt inapicha ya mti wa bangi au sigara.

•          Nguo yenye picha ufunguo- ina maana ule ufunguo umeivaa hiyo nguo ufunguo huo umekufungia usiende mbinguni na ufanikiwe kumkufuru mwenyezi MUNGU, na hata katika cheni, ukikuta kamaufunguo uelewe ni hatari tupu, hata cheni yenye msalaba ina maana uelewe unapovaa unakuwa wewe umelaaniwa na maisha yako yanasulubiwa katika ulimwengu wa roho. Pia uelewe hakuna msalaba mtakatifu kabisa hata ule aliouliwa nao YESU siyo msalaba mtakatifu ni msalaba wa laana na ndio sababu damu yake ilipomwagika pale msalabani ikatuondolea laana, sasa shetani akabuni njia nyingine na kuwapiga upofu watu waone msalaba ni kitu kizuri na kumbe siyo. Unajihukumu mwenyewe, hata kuzikwa na msalaba ni makosa.

•          Nikuulize swali unapozikwa je unaenda kuhukumiwa na wewe? Au je msalaba ni alama ya mkristo? Jibu siyo. Watumishi wanawapotosha watu kwa kumuamini shetani na kumfanya YESU akose watu wa kwenda mbinguni. Jiulize swali kina Ibrahim, Isaka na Yakobo katika makaburi yaoipo misalaba? Jibu hakuna. Na kamasisi tu uzao wa Ibrahim, kwa nini tusiige mfano wa Baba yetu Ibrahim? Na zaidi je YESU yeye alizikwa na msalaba? Jibu hapana, je YESU si ndiye kweli na alionyesha njia ili tuifuate. Sasa swali, kama alionyesha njia, tuanze katika maisha yake je uliletwa msalaba? Jibu hapana. Sasa hii misalaba madhara yake unapokufa ukawekewa katika kaburi inakufanya wewe uliyekufa usulubishwe katika ulimwengu wa roho, na wote waliozikwa na misalaba wanateseka katika ulimwengu wa roho na shetani anamnyanyulia MUNGU  si unaona msalaba wanataka wenyewe niwasulubishe na MUNGU ni MUNGU wa haki analiangalia neno lake, kataa kuzikwa na msalaba iga YESU alivyozikwa, iga mazishi ya Ibrahim, Isaka na Yakobo, pamoja na mitume na manabii wa MUNGU wa kweli waliopita ambao kwa heshima MUNGU amewaita wazee 24. Kataa huo uchafu watu wanapotezwa, amenituma YESU niwaeleze ukweli utakaye sikia utapona, utakaye kaza shingo damu yake haitamlilia MUNGU katika mikono yake.

•          Boxer- hizi ni chupi za nyani wa kuzimu unapozivaa  unaibiwa na mapepo uthamani wa nguvu zako za kiume na pia unaolewa na majini katika ulimwengu wa roho unakuwa wewe ni shoga. Na mlango ni hii boxer.

•          Nguo zote zenye zipu kifuani tu, unapokuwa na nguo ya aina hiyo kila unapofungua zip unakuwa unayachana maisha yako katika moyo wako na unapofungua zipu hiyo unakuwa unayafungua usifanikiwe.


•          Mikanda yenye bastola au bunduki- unakuwa umevaa jini bedui katika maisha yako na makata hivyo wanayaharibu. Mikanda yote yenye sura za watu katika bacol au nembo yeyote ile uelewe umeivaa kuzimu na kuzimu inajiunganisha na wewe kupitia katika kitovu chako kwa njia ya bacol ya mkanda.

•            Kusuka rasta- unakuwa umevaa pepo kichaa na mara nyingi huja kutokea katika mwili mtu anakuwa kichaa, na pia unakuwa na mambo ya freemason pasipokujua na wengine wanajua.

•          Kuvaa suruali mlegezo- hiyo ni dalili wewe ni shoga katika ulimwengu wa roho na unapovaa hivyo unayaita majini yaliyokuoa katika ulimwengu wa roho yeye yazini na wewe.

•          Kofia zote ambazo vijana wanasema ni za kileo zote zinatoka kuzimu na kijana anapovaa akili yake huibiwa ndoto zake zote hubakia boksi, na ndio sababu idadi kubwa ya wanaovaa hizo kofia fuatilia utakuta ni wavuta bangi, walaji wa cocaine, wahuni, wameharibika ni sababu ya hizo kofia zenye majina ya ajabu na ya wanamziki na watu ambao tayari ni wanachama wa freemason..

•          Nguo za kubana kupitiliza mfano T-shirt, suruali, inakubana unayaonyesha maungo yako jinsi yalivyo.
•          Kusuka nywele- unaposuka tayari uelewe wewe tayari  ni mke wa jini fulani kuzimu, na unaye mume unayemtumikia katika ulimwengu wa roho japo wanadamu hapa duniani wanakuwa ni wanaume tu ila ni boksi.

•          Mashati yenye mipasuko katika sehemu za mifuko, mashati haya watu hawapendi kuyachomekea sababu yana mipasuko, sina haja ya kuelezea sana, yapokama Kaunda suti. Nguo yeyote ya mwanaume yenye mipasuko sehemu za kiunoni hizo zote ni za kuzimu, unapoivaa uchumi wako unapasuka na maisha yako yanakuwa ni ya shida shida tu.

•            Nguo zenye sura ya nyoka, mamba, chui, madoa doa, viatu venye magamba au ukiviona vina sura ya magamba haijalishi ya aina gani havifai, ni viatu vya kuzimu.

•            Viatu vilivyochorwa tick (Ö) au X ina maana hiyo tick unakubali jina lako liandikwe katika ufalme wa shetani na X ina maana maisha yako yanatiwa X yote.

•            Kila kitu chenye jina MAX uelewe asili yake ni kuzimu na kina madhara. 

•            Viatu vyenye majina ya ajabu na vingi havielezeki hata sitaweza kuviacha kuandika even kwa 30 days, omba ROHO MTAKATIFU akufunulie wakati unahitaji viatu omba atakuongoza na roho ikigoma tu wacha, hiyo ni dalili.

•            Kofia zote za duara zisizo na chepeo halafu zina kamba au kinaninginia unapozivaa, unakuwa umeweka kwato ya jini katika maisha yako na nyingine ni kofia za duara ile zimetobolewa mashimo mengi zote hizo ni makwato ya majini na shetani amewaletea wanadamu ili wawe wajinga na wasimjue MUNGU wa kweli siku zote za maisha yao, sasa uamuzi unao wewe utavaa makwato ya majini au utayatupa.

•            Mwanaume anapovaa bangili (ringi) hapo unakuwa umejiingiza na kufunga ndoa na shetani, ila utakapoivua tu tayari umevunja ndoa na shetani, ringi hizi watu wengi wanafungulia vinywaji au kutumia kama silaha wakati wa kupigana na zaidi mwanaume hautakiwi kuvaa bangili katika mkono kabisa, unapovaa unafunga ndoa na shetani, na pia hata wengine wanafunga nyuzi katika mikono, hapo tayari umefunga ndoa na shetani na wewe ni mtu wa shetani, sasa amua, ila wengi wanajua kabisa ni masharti waliyopewa kuzimu inawezekana ni raia, mfalme, au mtu wa karibu, utashangaa siku zote ipo katika mkono, watu wanafikiri ni urembo, hapana hilo ni agano la shetani.

•          Kutoboa masikio au sikio- iwe ni mtu yeyote yule wapo hata wachungaji wanatoboa masikio na kuvaa hereni- hao wote katika ulimwengu wa roho ni mashoga wala YESU hana ushirikiano nao. YESU hana mashoga. Jiulize hawa wanatokea wapi? Ni mashoga wanaoeneza injili ya yesu wa uongo na kuwapeleka watu kuzimu.

•          Shetani aliwateka wengi hata waliookoka katika maeneo mbali mbali ila YESU amenituma niwaeleze ukweli sababu anaona mnavyoteseka na hampati majibu na akaniambia Hebron haya mateso yasingewapata wanadamu ila yamewapata sababu niliowaita wamemgeukia shetani na ndio anakuwa baba yao hivyo wanafanya kazi ya baba yao ambao ni lusifa hata wanangu wanateseka na kuangamia ila nimefurahi sasa sababu upo wewe Hebron, nimekupata wewe uliyenikubali kunitumikia na kuyatenda yale ambayo mimi na BABA yangu mbinguni na ROHO MTAKATIFU ndio tunayoyataka, na pia Hebron nataka uelewe kabla ya wewe kuumbwa MUNGU alishakuandaa na akajua ikifika muda wake atakusimamisha na anajua utaifanya kazi yake sababu anajua yeye aliyokuumba hivyo usiogope lolote. MUNGU alikuficha siku zote kama vile alivofichwa Musa akatunzwa na Farao hakuuwawa, hivyo ndivyo ilivyo kwako na utaifanya kazi yangu vizuri sana na kuzimu haitakuweza milele. Sasa nimefurahi sababu kila akusikilizaye na kubadilika na kutii unayowaeleza atapona sababu ndani yako MUNGU ameweka majibu ya viumbe vyote na kila kitu. Maneno haya kila nikumbukapo nasikia machozi yananitoka kwa ajili ya watumishi walivyomsaliti YESU hata na kugeuka freemason, wachawi, waongo, wanyang’anyi ila usiogope ninajua kinachokuja na watu mtamfurahia YESU WA NAZARETI.

•            Haya magauni ya harusi ya kuzimu- kila gauni la harusi lenye kuburuza mkia- ina maana ule mkia unaoburuzwa ni mkia wa lusifa. Lusifa anao mkia ila nilimkata mkia wake. Unapofunga ndoa na gauni la jinsi hiyo ndoa yako unampa lusifa. Na unapovaa gauni la harusi unaonyesha mabega na manyonyo unakuwa unavaa gauni la pepo kuzimu la kufungia harusi zao na wewe unajiunganisha hivyo hivyo na mama wa makahaba. Ukiangalia leo hii watu ndio wanasema ndio fashion. Hii siyo fashion mimi nasema yote ili nisije nikaulizwa na YESU siku ile ya mwisho sikuwaeleza ukweli ili mpone na usijisumbue hata kama jina lake YESU linatajwa haiunganishi hiyo ndoa sababu la hilo vazi mimi pia nilikuwa sijui, ila sasa uelewe ili upone. Wanawake mkatae sasa msiwekewe tena mikia ya shetani ukauburuza.

•          Kujipaka rangi ya kucha. Kila rangi inayo maana yake, rangi zote ulimwengu maana za kucha asili yake ni kuzimu. Ukipaka hizo rangi unaharibu maisha yako pasipo wewe kujua na hizo rangi zimechanganywa na rangi za ngozi za watu waliokufa baada ya kuchunwa ngozi zao na mashetani wakala nyama zao. Sasa unapozipaka unakaribisha majini katika maisha yako na uthamani wa mikono unaibiwa, hata pesa hazikai wala kazi zako hazibarikiwi sababu MUNGU hana mahali pa kupitishia baraka katika mikono yako sababu shetani ameshaweka vitu vyake katika mikono yako.

•            Kucha za bandia- hizo ni kucha za majini walizozikata  kuzimu kama vile na wewe unavyokataga zako, unapozivaa kucha za bandia unakuwa unawapa majini  uthamani wa kucha zako ambapo katika kucha zako zipo Baraka wanaziiba zako unabakia na zao na unakuwa tayari umeingia urafiki na majini pasipo kujua japo wengine wanajua na wanayapenda majini.

•            Nguo zote ambazo za wanawake zinakuwa na mipasuko zote hizo asili yake unakuwa unajitengenezea mkia wa lusifa na lusifa kuitumia njia hiyo kukupata.

•            Nguo ambazo ni short ni fupi zinazoonyesha mapaja na hupendwa sana kuvaliwa na masecretary katika ofisi mbali mbali, sasa hilo vazi kila unapolivaa ina maana unamkubali shetani kabisa ila sasa uelewe haifai.

•            Kuvaa pini katika ulimi, unapotoboa ulimi tayari unampa mama wa makahaba ulimi wako na vitu vyako kisha unabakia na ulimi wake na anakamata fahamu zako na kisha kwa kutumia ulimi huo uliovalisha pini anautumia kunyonya viungo vya siri vya kiume na mwanaume atakayefanyiwa hivyo anakuwa viungo vyake vimemezwa na Yezebeli katika ulimwengu wa roho kupitia mwili wa mwanadamu. Kazi kubwa ni kumeza viungo vya kiume kwa njia ya kuvinyonya na pia hata ukinyonywa ulimi au kiungo chochote na mtu aliyetoboa ulimi, uelewe anatumika kumeza vitu vya watu na ndani yake yupo Yezebeli na ndiyo sababu ametoboa ulimi. Ilikumjua mtu mwenye Yezebeli au Yezebeli anaishi ndani yake angalia ulimi ametoboa na katika ulimwengu wa roho na yeye anakuwa ni mtoto wa Yezebeli na Yezebeli anauhalali sababu anayo alama yake katika ulimi.

•            Alama nyingine ya Yezebeli ni inayokufanya kuunganika katika kitovu cha mtu na Yezebeli utaona mtu anatoboa kitovu au anatoboa pembeni ya kitovu, hii ina maana  amejiunganisha kupitia kitovu, huyo mwanadamu atakuwa anatabia za kipepo, hata kutembea uchi, mlevi, hafai kuolewa au kuwa mke bora, sababu atakuwa ni kahaba.

•          Na wengine wanatoboa (wanawake) wanakitoboa KISIMI wanakivalisha pini, yaani ukiona hivyo uelewe kile kiungo cha kike alicho nacho huyo binti siyo cha bindadamu ni cha pepo, kama alivyo mama wa makahaba na yeye amejitoboa na anavaa pin kubwa ya dhahabu ambayo ina urefu wa 30 cm na unene wa 2 cm. Mmh, haya mambo yanatisha kiasi hata mimi nimeandika huku nilikataa nisione alivyo ila YESU amenitia nguvu ili niwaeleze mjiepushe msifikiri ni vizuri hayo sasa yaelewe, okoka uvitupe hivyo vitu.

•          Na alama nyingine ya mtu mwenye Yezebeli anavaa pini katika macho, bangili miguuni hasa bangili moja katika mguu mmoja na kujichora katika mapaja au kuchora moyo na alama ya mshale au kuandika majina ya watu katika mapaja au tumboni, mgongoni au popote katika mwili.








  MALAPA MEKUNDU
•          Malapa yote yenye rangi ya nyekundu siyo salama sababu unapoyavaa unaibiwa maisha yako na shetani. Na katika haya malapa shetani aliweka pepo kivutio na ndio sababu utaona idadi kubwa ya watu wana malapa mekundu, haya yapo hapa ulimwenguni kwa ajili ya kuharibu maisha ya mwanadamu. Unapoyavaa maisha yako yanakuwa ni magumu sababu yale yako uliyopewa na MUNGU yanaibiwa utayari wako katika miguu na kukufanya wewe kubakia na maisha hatari ndio sababu ya hiyo red.

 PIPI KIFUA, PIPI KIJITI
•          Kila unapokula pipi kifua uelewe unakuwa unakula makamasi ya majini na unakula TB, unakula ukimwi na magonjwa ya kifua pamoja na pumu.
•          Pipi kijiti- kila unapokula pipi kijiti ina maana ile pipi ndio dunia na kile kijiti kilichoichoma hiyo pipi ni wewe unaichoma dunia katika maisha yako usifanikiwe, na maana nyingine ni wewe unajiharibu maisha yako.

VIFAA VYA UJENZI (Baadhi)
•            Mabati- yapo mabati yanayotoka katika nchi za America na South Africa ni tofauti na mabati yaliyozoeleka miaka mingi katika nchi mbali mbali. Unapoyatumia katika nyumba yako tayari paa lako umelifunika na shetani na ni vigumu YESU hata Malaika kuja katika nyumba za watoto wa MUNGU sababu ni haya mabati, tayari kuna kitu cha shetani.

•            Vipo vitasa vya milango vyenye rangi yeyote ya brown, unapotumia vile vitasa katika nyumba yako vinatumika sasa ndio mlango wa majini kuja kwako na kuingia bila tatizo na kuiba vitu vya watu kwa njia ya kipepo, na hata ukifunga na ufunguo wana kuja na kuvifungua na kuingia kimwili kabisa katika nyumba

•            Rangi- zipo rangi zinaanza na herufi S na nyingine herufi C unapopaka ragi hizi katika nyumba yako unakuwa umepaka makamasi ya majini katika nyumba yako, makufuru, balaa mikosi na kukufanya Baraka za MUNGU zisije katika nyumba yako na hata Malaika kuja kwako, hii ni sababu ni uchafu na watu hawajui, asili yake ni kuzimu, hazikomboleki wala hazitakasiki. YESU anawasaidia watu wote ili wapone. Unapoipaka katika nyumba, unapaka chuma ulete na ni mlango wa majini kuja kwako sababu upo na vitu vyao



>>>>>Ila shetani alibuni viwanda ili aharibu maisha ya watu,

YESU WA NAZARETI anawapenda sana mrejeeni yeye, wakati wake umefika wa kurudi, usidanganyike tena, katika makanisa mkifundishwa kinyume na biblia hao ni maajenti wa shetani ili kufaulisha kazi zake za kuua roho za wana wa MUNGU.


MADAHARA YA KUVAA WIGI (WEAVE).
1.      Kwanza kabisa uelewe katika kichwa chako unakuwa umevaa nywele za siri za majini na pia umevaa pepo.
2.      Madhara yake unakuwa umeuzuia utukufu wa MUNGU ushuke katika kichwa chako sababu tayari upo utukufu wa shetani katika kichwa chako yamkini unavaa pasipo kujua au kwa kujua.
3.      Akili yako na maono yako yanaibiwa na shetani na kisha shetani anakuwekea ya kwake pasipo wewe kujua.
4.      Mawigi yanakufanya usiweze kusimama katika wokovu.
5.      Mawigi haya yanaletwa ulimwenguni ili kuwazuia wanawake wasiende mbinguni sababu shetani anajua kabisa katika mioyo ya wanawake wengi wanampenda YESUkama vile kipindi ambacho YESU alikuwepo ilionekana wanawake ndio waliokuwa wengi na hata sasa ukiangalia idadi kubwa ya wanawake ndio wengi waliookoka kuliko wanaume.

 6. Ndani yako mizimu inaishi.
7.      Mapepo yanakuwa na uhalali wa kuishi ndani yako na wachawi hukuloga kwa urahisi na kukuibia vitu vyako.
8.      Unakuwa unayo alama ya mama wa makahaba (Yezebel) sababu unavaa vitu vyake.
NOTE: vitu vyote venye asili ya kuzimu ni vitu vya shetani hivyo havikomboleki wala havitakasiki, wala havibarikiki kwa jina la YESU WA NAZARETI sababu hauwezi ukazibariki kazi za shetani kwa jina la YESU, bali kazi za shetani huharibiwa kwa jina la YESU WA NAZARETI.
9.      Humfanya mwanamke kuwa na tabia za uzinzi, asiweze kutulia katika ndoa na huwaletea ndoto za uzinzi, na kuwaibia wanawake baraka zao walizoumbwa nazo na mwenyezi MUNGU.
10.  Kila anayevaa nywele hizi katika ulimwengu wa roho yeye ni mke wa jini pasipo kujijua na wengine hujijua, haijalishi umeokoka au haujaokoka, ukweli ndio huo.
11.  Katika ulimwengu wa roho jina lako unaitwa kahaba, na mfano rahisi tu angalia watu wenye tabia za ukahaba katika ulimwengu wote leo hii kwa upande wa watu weusi. Hata katika street wale wanaofanya uzinzi kujiuza mwili tazama katika kichwa utaona mawigi.
12.  Mwanawake anapokufa akazikwa na wigi tayari anajifungia asinyakuliwe katika unyakuo sababu anacho cha kuzimu na MUNGU anaangalia haki amenituma niseme ukweli ili watu wapone, sababu shetani alishaona kuwa watu waliookoka hatawapata sasa akabuni njia hii ya mawigi, nikuulize swali labda umeokoka unampenda YESU na unaishi maisha matakatifu lakini katika kichwa chako umevaa mapepo je utukufu wa MUNGU utashuka katika maisha yako? Jibu hakuna na je MUNGU atakubarikije wakati unavaa kofia ya shetani?
13.  Na majini haya ambayo yanayotoa nywele za siri ambazo ndizo wigi, majini haya nguo za ndani wale wa kiume wanavaa boxer na majini ya kike yanavaa BIKINI. Ukubwa wa size ya kiuno ni kama mita 4 kiuno.
14.  Ufahamu unashikiliwa na shetani na anayeongoza maisha yako na hapo ndipo unapotea na kuacha njia za MUNGU pasipo kupenda hii ni sababu moja wapo ni hizi zinazovaliwa zinatoka katika viungo vya siri ya majini.





KWA NAFASI ZA KAZI POPOTE TANZANIA, BONYEZA
HAPA CHINI▼▼

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
[3.00 MB]VIDEO YA ALIKIBA AKIBANDUANA NA JOKATE, BONYEZA
HAPA CHINI▼▼



2 comments:

  1. IFAHAMU MIZIMU NA MAJINI NA UNDANI WAKE KATIKA KUOMBA LOLOTE MALI,UTAJIRI, UPONYAJI N.K......

    DOKTA MDIRO whatsp/call +255 742162843

    ANGALIZO HUSIJARIBU JAMBO ULIZA KWA MAELEKEZO

    Omba lolotee kwa njiaa ya mizimu mungu atatenda asema DOKTA MDIRO,

    Kuna watu wakisikia neno mzimu wanatimkaa mbio lakini wakisikia neno mtakatifu wanabarikiwa na wakati ni kitu kilekile kasoro jina tu.

    Daktari wa kiafrika anaitwa mganga wa kienyeji na wa kigeni ni Mtaalamu au mwanasayansi.

    Ibada takatifu zinaitwa Kusali na za lienyeji zinaitwa matambiko amka wacha kulala.

    watakatifu wa kiafrika wanaitwa mizimu, Mzimu nii binadamu yeyote yule aloachaa mwili na ANAISHIII na mungu karibu, kwaiyo sisi sote nii mizimu watarajiwa, unapomfananisha Mzimu na shetaani nikukataa ukuu wa afrikaa, wazungu Mzimu uloishiii vizuri dunian wanauita mtakatifu sisi mizimu iloishi vizuri na VIBAYA duniani tunaayaita mashetani.

    Ndiomaana ktk orodha ya watakatifu karibu wote wazungu, waafrika wa kuwahesabu, @highlight

    WAZUNGU KWENDA MAKABURINI WANAITA HIJJA , SISI KWENDA MAKABURINI TUNAITA MATANDIKO, HATA MZIMU WA NYERERE UMECHUKUWA MUDA KWELI KUFANYWA MTAKATIFU KWASABABU HAKUWA MZUGU.
    🤫DOKTA MDIRO ANASEMA MIZIMU INAFAIDA KUBWA KTK MAISHA YA MUWAFRIKA, KUIKATAA NI KUKUBALI BALAAA NA KUKUBALI NI CHAZO CHA BARAKA.
    NA MAISHA MEMA APA DUNIANI,
    😒 Mikosi, manyanyaso balaa, na gundu ulizonazo haziwezi kuondoka mpk ukutane na mizimu yenu .
    Dokta MDIRO ANAKUAMBIA MIZIMU YA BIBI YAKO NA BABU YAKO INAA MAJIBU YA MATATIZO YAKO.

    ReplyDelete
  2. UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    (Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)

    MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    Everyone

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    ReplyDelete