KANUNI ZA KUTEKA MIJI KWA AJILI YA BWANA,
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
UTANGULIZI
Ndugu mpendwa
napenda kukusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.Pia ninapenda
kukukaribisha katika kujifunza somo hili.Somo hili lina umuhimu mkubwa sana
katika nyakati/majira tuliyopo
sasa.Kama kichwa cha somo kinavyoonyesha,somo hili ni somo ambalo naamini
litakwenda kuleta mapinduzi ya kiroho katika jamii,familia na kanisa kwa
ujumla.Nakushauri ulisome somo hili kwa mtiririko ili uweze kupata maarifa
mapya na vitu vipya kutoka kwa Roho Mtakatifu.Lengo la kwanza la somo hili ni
kukuandaa kama mwanajeshi wa Bwana,kwa ajili ya kuteka miji iliyo chini ya
shetani na kuirejeza kwenye ufalme wa Mungu Baba.Sasa unaweza ukawa unajiuliza,swali
hili;kwamba kwa nini mimi ndio niteke miji hiyo?kwanini Mungu mwenyewe asifanye
kazi hiyo?Jibu ni kwamba Mungu huwa anafanya kazi pamoja nasi kwa ajili ya
kutupatia mema[Rumi.8:28],Na mema hayawezi kuja kama miji tunayoishi itaendelea
kuwa chini ya ufalme wa giza.Kwa nini tuteke miji wakati,aliyeumba miji yote ni
Mungu na wala sio shetani?
Dhambi ya Adamu
na Eva pale eden ilipelekea dunia yote kuwa chini ya shetani(yaani shetani
akawa ndio mungu wa dunia hii)[2kor.4:4] badala ya mwanadamu. Kwa hiyo asilimia
kubwa ya miji tunayoishi inamilikiwa na adui(shetani).Na ndio maana kazi ya
Mungu inapigwa vita kwa kiasi kikubwa.Sasa lengo la pili la somo hili ni
kukuwekea(impart knowledge) ufahamu utakaokusaidia kuirejeza miji hiyo mikononi
mwako,kama mwakilishi wa ufalme wa Mungu.Kutokana na miji mingi kuwa chini ya
shetani,matukio mengi ya kutisha yamekuwa yakitokea kila siku,mfano vifo vya
ajabu,ajali za barabarani,mauaji ya albino nk.
Sasa shetani
amekuwa akipofusha watu ili watu wasijue kuwa yeye(shetani) ndiye anayehusika
katika matukio hayo yasiyo na hata chembe ya huruma[Mungu ni mwenye huruma]
hawezi amuru maalbino wauae,ajali za watu kufa kama vile kuku kwa mkupuo.Ndugu
mpendwa shetani ni mjanja na biblia inasema kwenye kitabu cha ufunuo kuwa
anajua wakati uliobaki ni mchache..kwa hiyo anachofanya ni kuhakikisha anav
Ni muda mrefu sana nimekuwa
nikisikia matukio mengi ya kutisha na ya
ajabu yakitokea katika jamii tunazoishi; hasahasa matukio ya ajali za
barabarani, ukatili , watu kujinyonga na kunywa sumu nk.Na mara nyingi nimekuwa
nikisikia watu wengi wakisema yote hayo ni mapenzi ya Mungu(yaani Mungu ndio
amesababisha) na muda mwingine hata watumishi wa Mungu wengi wakati wa mazishi
nimewasikia na wewe umewasikia wakisema “Bwana ametoa na Bwana ametwaa;jina la
Bwana libarikiwe”
Kwa upande wangu nimekuwa nikipata
shida kidogo juu ya misemo hii ya
mazishi, na Je ni kweli Bwana ndiye anayetwaa hao watu wote? mfano mlevi,ajali
nk.Maana muda mwingine unakuta wala Mungu hahusiki hata kidogo katika matukio
hayo, bali aiza mtu amejisababishia mwenyewe au kuna mkono wa shetani
umehusika!.Si kwamba nasema Mungu hahusiki kwa asilimia zote,hapana!.Bali
ukikuta Mungu amehusika basi mtu huyo amekuwa mgumu sana na amekuwa akiharibu
kazi ya Mungu mfano,Herode[Matendo.12:22-23] au Mungu amependa kumpumzisha mtu
huyo kwasababu ya umri[1Fal.1:1,1nyak.29:28 .
Kumbuka kuwa si
mapenzi ya Mungu mtu afe katika
dhambi[Eze.18:23; 33:11], pia si mapenzi ya Mungu ufe kabla ya wakati
ambao yeye amekusudia uishi hapa duniani ambao ni miaka 120[Mwanzo.6:3] kama
ukiishi vizuri na Bwana hiki ni kiwango cha chini tu unaweza ukaishi zaidi ya
hapo mfano ibrahimu aliishi miaka 140,Ayubu 140.Sasa kama ndio hivyo kwa nini
uondoke kabla ya hapo.
Sio hivyo tu bali
kwa wewe mtumishi wa Mungu uwepo wako hapa duniani ni wa muhimu sana,Yesu
alimwomba Baba wa mbinguni ili asitutoe ulimwenguni [Yoh.17:15] , maana yake
kuna kazi unatakiwa ufanye,na endapo utaonekana huifanyi na wala humzalii Mungu
matunda basi ndio unakatwa[Math.3:11,7:19; Luka.13:6-9](sasa hii ni kwa ajili
ya wale tu ya waliokoka).ni kweli kufa ni faida kwa mtu aliyeokoka,hilo
nakubaliana nalo asilimia zote,lakini pia kuishi ni kristo na kwafaa sana
kubaki kwa ajili ya kristo na ili kuendelea kuziremba taji zetu za kule
mbinguni(kumbuka kuwa utalipwa kwa ajili ya kazi unayofanya hapa
Duniani,utavalishwa taji,kama ukienda huko na hakuna matunda yoyote uliyomzalia
Mungu basi usitarajie kitu.
Unajua
utakuwaje?Embu fikiria unahitimu kidato cha 4/6 au chuo alafu siku hiyo wenzako
wote wanapewa zawadi na kuvalishwa taji, alafu wewe peke yako tu ,ndio huna mtu
wa kukuvalisha taji wala kukupa zawadi,unafikiri utajisikiaje?lazima ujisikie
vibaya.Ndivyo itakavyokuwa unavyong’ang’ania kufa ukisema ni faida wakati hamna
chochote ulichokifanya hapa duniani kwa ajili ya Mungu[Luka.12:47-48].
Ujue hii
inakuhusu wewe ndugu uliyeokoka na lengo langu hapa ni kuona unabadilisha
mawazo uliyonayo na maombi ambayo umekuwa ukimwomba Mungu ili akuondoe
duniani.Kumbuka kuwa Mungu anakuhitaji ili uendelee kuwepo hapa duniani kwa
aijli ya kazi yake[Yoh.17:15].Wewe ukifa shetani anafurahia kwa sababu upinzani
unapungua.Hivyo badilisha hayo mawazo ya kutaka kuondoka(kufa) bali umwombe
Mungu akuongezee siku za kuishi angalau na wewe ujitengenezee taji yako kule
mbinguni[Ufunuo.2,3].
Sasa kwa watu ambao
hawajaokoka Mungu anasema anachukia kufa kwao katika dhambi,na kwasababu hiyo
basi inamanisha kuwa Mungu hahusiki katika vifo vingi vya watu wanaokufa kabla
ya wakati uliokusudiwa.Na ukijaribu kuchunguza kwa undani zaidi utakuta asilmia
kubwa ya ajali na vifo vinavyotokea nyakati za leo, wala Mungu hahusiki na kama
anahusika naweza nikasema kuwa ni kwa asilimia chache sana( 25%) tu tena hiki
ni kiwango kikubwa sana.Embu fikiria
vifo vya maalibino,watoto wachanga,vijana wadogo,Ajali za kila siku
barabarani na watu kujinyonga na kunywa sumu je haya yote utasema Mungu
anahusika?
Sasa usishtuke maana lengo la somo
hili sio kukuogopesha bali somo hili lengo lake kubwa ni kufuta mawazo
hasi(potofu) uliyojengewa na watu kuhusu masuala hayo na upate ufahamu
mpya(chanya) ili uweze kuchukua hatua ambazo Mungu anataka wewe uzichukue ili
angalau wewe uweze fikisha siku za Bwana.
NB:Kuna watu ambao
mmekuwa na mawazo potofu,eti kwamba ukifundisha mafundisho kama haya una
mtukuza shetani sana kwasababu yeye ndiye anatajwa mara nyingi.Nani
kakudanganya kuwa unapomtaja mtu kwa ubaya,kwa lengo la kufichua maovu yake,ni
kwamba unamsifia?.Siri ya vita vyote sikuzote ni kumsoma adui yako na kumsoma
adui yako haimaanishi unamtukuza.Ndugu kama na wew ulikuwa na mawazo kama haya
uyaondoe,maana hayatoki kwa Mungu bali kwa shetani ; kwa lengo la kukufanya
usizijue hila zake na ili aendelee kukutawala na kutawala mji unaoishi.
Kanuni ya kusoma
somo hili ni kwamba kabla haujaendelea na somo hili nakusihi ufanye maombi
kwanza umuombe Roho mtakatifu akupe kiu ya kujifunza somo hili na nguvu ya
kulitendea kazi [soma Mt.7:24-27; 13:18-23] maana somo hili lina upinzani
sana.mpaka nimeweza kuliandaa somo hili ni kwa neema ya Mungu tu na kama sio
neema hiyo basi sasa hivi usingekuwa na nakala hii.Hivyo anza kwa maombi,haribu
na uvunje kila roho zilizotumwa na mwovu ili kukuzuia usipate kitu katika somo
hili.Pia uwe na biblia yako karibu.Somo hili limegawanyika katika sehemu kuu
tano (5); sehemu ya kwanza ,ya pili ,ya tatu,nne,tano na hitimisho.
SEHEMU YA
KWANZA:KUJITAMBUA NA KUTAMBUA
Somo hili
limekuja wakati muafaka ambao wewe kama mtu wa Mungu unatakiwa ujitambue wewe
ni nani,unapambana nanani(adui)? ;na ni nini unatakiwa kufanya katika nyakati
hizi za mwisho.
Tunaposema
kujitambua inamaanisha kuwa wewe mtu wa Mungu unatakiwa kujitambua kuwa wewe ni
nani mbele za Mungu na nini unatakiwa kufanya.Na tunaposema kutambua maana yake
unapaswa kujua adui yako ni nani?,na ni majira gani uliyoko?
Na nianze kwa
kusema kwamba shida kubwa iliyoko katikati ya wana wa Mungu(waliookoka) ni
kutokujua majira waliyoko na hata kama wanajua wanashindwa kutambua ninini
wanachotakiwa kufanya kwenye majira hayo[Efeso.5:15-21].Wapendwa wengi nyakati
za leo wamejikita zaidi kwenye kuombea masuala ya kwao na ya madhehebu ya
kwao.Wamesahau kuwa nini Yesu aliwaagiza(The great commission)
[Mathayo.24:14]..Kumbuka kuwa Yesu alisema kwamba ; “Basi enendeni, mkawafanye
mataifa yote kuwa wanafunzi…na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru
ninyi..”[Mathayo.28:19-20].
Lakini wapendwa
wengi swala hili hawana mpango nalo ,badala yake wamegeuka na kuwa kama
wanasiasa ambao badala ya kuwatetea
wananchi waliowachagua,wananza kutetea vyama vyao;na ndivyo walivyo
watumishi na wapendwa wengi wa leo.badala ya kumtetea Yesu aliyewatuma wanaanza
kutetea madhehebu ya yao.Hii yote ni kutokujitambua na kutokutambua mapenzi ya
Bwana wao[Luka.12:47-48].
Biblia inasema
katika kitabu cha [Ufunuo.12:12b].“Ole wa nchi na bahari! kwa maana yule ibilisi ameshuka
kwenu mwenye ghadhabu nyingi ,akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”Biblia
inaweka wazi kuwa shetani yeye anajua majira aliyoko na anayatumia
vizuri…Kanisa la leo limesahau na hata kama halijasahau basi limeacha wajibu
wake na kazi ambayo Mungu alikusudia kanisa lifanye(The great
commission)[Mathayo.24:14].
Kila
kanisa(madhehebu) leo hii, limejiwekea vipao mbele vyake katika mambo
yao.Lakini masuala ya Mungu wameyaweka pembeni.Kanisa la leo halina muda wa
kutafuta mapenzi ya Mungu.Ukikuta mipango wanayopanga ni ya kwao binafsi na
hata ukikuta mahubiri wanayoyafundisha ni ya kusengenya kanisa
lingine,wakifikiri kuwa wanapatia kumbe wanakosea w.Kanisa la mitume halikuwa
na tabia hizi za leo.
Na kwa sababu
hiyo tunahitaji matenge wanasahau kuwa Yesu alisema; “……na kuwafundisha
kuyashika yote niliyowaamuru ninyi..”[Mathayo.28:19-20] ikiwemo
upedo[Yoh.13:34-35],kupenda jirani na Adui yako[Matthayo.5:43-48].Kanisa la leo
linahitaji matengenezo(reformation) mapya kama yale aliyoyafanya mtumishi wa
Mungu Martin Luther.Kanisa la leo halina umoja,halina upendo, halina unyenyekevu
,wala uvumilivu na kusamehana nk.Zaidi sana ubinafsi na kusengenyana ndio
kumejaa makanisani Kwakweli kanisa linapaswa kutubu na kurudi kwenye kusudi
ambalo Mungu alikusudia kanisa lifanye.
Sasa unaweza
ukaanza kufikiria kuwa ninalalama bure hapana! Ila nakufundisha kitu ambacho
kipo kwenye biblia.Wala sio
nimebuni.sasa tufuatane nikupitishe kwenye maandiko ili upate kujua nini ,Mungu
alikusudia kwa ajili ya kanisa;alafu linganisha na jinsi kanisa la leo
linavyoishi.Sasa tuanzie mwanzo kabisa wa nini ambacho Mungu alikuwa anakusudia
kwa ajili ya kanisa:-
Kitabu cha
[mwanzo.1:26-28] kinaonyesha mwanzo wa uumbaji wa Mungu wa kumuumba
mwanadamu.Mungu anasema ″Na tufanye mtu kwa mfano wetu ;na kwa sura yetu
;wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani ;na wanyama ;na nchi yote
pia;na kila chenye kutambaa kitambaacho
juu ya nchi……″
Lengo kubwa la Mungu kuumba Dunia ni kwa ajili ya
mwanadamu na ndio maana aliweka kila kitu cha kumsaidia na cha kumfaa mwanadamu
katika maisha yake ;kabla hajaumbwa aliwekewa hewa
–oksjeni;maji;miti;mifugo;mimea n.k.Vyote hivi ni kwa ajili ya mwanadamu.
Na baada ya
Bwana Mungu kumuumba mwanadamu alimkabidhi utawala na umiliki wa Dunia
hii.Alipewa kumiliki dunia na vyote vilivyomo ndani yake- [Mwanzo1:
27-28].“Mungu akawabarikia……na kuitiisha ;mkatawale……na kila kiumbe chenye uhai
kiendacho juu ya nchi ″.Neno ninalotaka ulione hapo kwenye mistari hiyo ni
“kutiisha na kutawala dunia”
Wakati huohuo
ndani ya Dunia pia alikuwemo shetan, kwa sababu tayari alishahasi kule mbinguni
na akatupwa Duniani.soma-[Isaya.14:12-15,Eze.28:11-19].
[Ufunuo. 12:10.]“………kwa
maana ametupwa chini mshitaki wa
ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wet,u mchana na usiku ″.
Mungu alipomuumba
mwanadamu alimpa nafasi moja ya heshima na kubwa sana –na nafasi hiyo ni ya
umiliki wa Dunia hii-Na kwa ujumla hakuna malaika yeyote aliyewahi kupewa
nafasi kama aliyopewa mwanadamu,hata shetani enzi za uhai wake (kule mbinguni)
hakuwahi kupata nafasi kama hiyo, japo aliitamani sana na ndio maana alifanya
uhasi akifikiri kuwa angepata sehemu ya kumiliki, na yeye awe kama Mungu.
Katika
ranking(ngazi) ya ufalme wa Mungu hapa duniani, mwanadamu alipewa nafasi ya
pili-yaani baada ya Mungu alifuata mwanadamu;alafu malaika na mwisho ni shetani
na mapepo yake .
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: