VITA VYA KIROHO NA KUOMBA
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Paulo
anafundisha: ‘Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu
zake.Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.Kwa
maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho.’ (Waefeso 6:10-12).
Kwa hiyo,
ndugu, tufanyaje? Tuombe dhidi ya ‘falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili,
juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.’? Hapana! Hiyo siyo
shauri la Paulo! Kwa kweli. HAMNA mahali mmoja katika Biblia ambapo tunasoma
kwamba hata muumini mmoja katika maombi yake anaomba juu ya shetani, falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho. Hata Danieli hakuomba juu ya mapepo mabaya katika ulimwengu
wa roho. Aliomba kwa ajili ya kazi ya Mungu na watu wa Mungu tu! (Soma Danieli
10. Yule aliyeongea na Danieli alimjulisha kuhusu vita vya pekee juu ya mkuu wa
ufalme wa Uajemi na kuhusu msaada wa Mikaeli, lakini Danieli mwenyewe hakuwa
ameomba juu ya mambo haya wala hakutaja mambo haya katika maombi yake!)
Kwa kweli
Bwana Yesu alitoa pepo na watumishi wake wanaweza kufanya hivyo. Hiyo ni jambo
lingine kabisa! Lakini hamna mstari mmoja katika Biblia unaofundisha tuombe
dhidi ya ‘falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo
wabaya katika ulimwengu wa roho’ na hamna mfano mmoja wa muumini aliyefanya
hivyo. Sasa fundisho la mtume Paulo ni nini juu ya ‘kushindana kwetu’? Anasema:
‘KWA SABABU
HIYO twaeni SILAHA zote za Mungu…’ Kwa nini? Je, ili tupate kuomba dhidi ya
‘falme na mamlala? Hapana! Paulo anaendelea kueleza, ili ‘mpate kuweza
kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi SIMAMENI,
hali mmejifunga KWELI viunoni, na KUVAA DIRII YA HAKI kifuani,na KUFUNGIWA
MIGUU utayari tupatao kwa Injili ya amani;zaidi ya yote MKIITWAA NGAO YA IMANI,
ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.Tena
ipokeeni CHAPEO YA WOKOVU, na UPANGA WA ROHO ambao ni neno la Mungu.’
Mafundisho ya Paulo juu ya ‘vita vya kiroho’ inahusu mwenendo wetu wa kiroho,
yaani, jinsi ya kusimama katika haki na imani! Kama Yakobo pia anafundisha,
‘Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.’ (Yak.4:7). Pia na kama
Paulo anafundisha kwenye 2 Wakor.10:3-5, ‘Maana ingawa tunaenenda katika mwili,
hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali
zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome tukiangusha mawazo na kila kitu
kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira
ipate kumtii Kristo;’ Unaona? Vita vyo kiroho kwa msingi vinahusu ‘kuangusha’
mawazo ambayo shetani anataka kuchochea moyoni mwetu yajiinuayo juu ya elimu ya
Mungu! Kupinga hayo, Paulo anasema ‘silaha za vita vyetu zina uwezo katika
Mungu hata kuangusha ngome’. Silaha hizo zinazingatia, ‘ngao ya imani’ na
‘upanga wa Roho’.
Tukisimama
imara kwa imani katika Bwana ndipo tunaweza kuomba. Je, tuombe dhidi ya falme
na mamlaka nkd? Hapana! Paulo anafundisha kwa wazi, ‘kudumu katika kuwaombea
watakatifu wote…’. Basi, anafundisha tusimame imara katika Bwana ili tuweze
kuomba kwa ajili ya WATAKATIFU wote – yaani, kwa waumini wote katika Kristo –
na kwa ajili ya kazi ya Mungu.
Je, ni Paulo
tu anayetufundisha tuwaombeeni watakatifu wote? Hapana.
Yesu
aliomba, “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa
hao ni wako.” Kumbe! Mzigo wa Bwana Yesu katika maombi yake ulikuwa (na unaendelea
kuwa) kwa ajili ya watu wake, kwa ajili ya watakatifu! Alisema kwa wazi,
“siombei ulimwenguni”. Je, Bwana Yesu aliwaombea wengine? Ndiyo. “Wala si hao
tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao (Yoh.
17:9,20,21). Aliwaombea waumini na wao watakaoamini! Je, katika maombi yetu,
tunaongozwa na Neno la Mungu, na Roho Mtakatifu?
“Kadhalika…
Roho mwenyewe HUTUOMBEA kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.Na yeye aichunguzaye
mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa HUWAOMBEA WATAKATIFU kama apendavyo
Mungu.” (Warumi 8:26,27).
Kumbe! Roho
Mtakatifu alituongoza kuwaombea watakatifu, yaani, waumini, watu wa Mungu.
Na Yesu,
kama kuhani mkuu, anaendelea kutuombea kama imeandikwa,
“…tunaye
kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu…Naye,… kwa sababu
hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote
ili AWAOMBEE.” (Waebr.4:14; 7:25). Tena imeandikwa, “Kristo Yesu ndiye
aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa
kuume wa Mungu; tena ndiye ANAYETUOMBEA.” (Warumi 8:34).
Na sisi,
katika maombi yetu na katika ‘vita vya kiroho’, je, tunaelekezwa kuombe kwa
ajili ya nini au nani? Neno la Mungu husema kwa wazi, “kwa sala zote na maombi
mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika
KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE.”(Waefeso 6:18).
Tunapaswa
kuwaombea wataktifu wote katika Roho. Je, mtume Paulo aliomba kwa ajili ya
watakatifu? Ndiyo. “Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, SIKU
ZOTE TUKIWAOMBEA…Kwa sababu hiyo sisi nasi, … HATUACHI kufanya maombi na dua
KWA AJILI YENU, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na
ufahamu wa rohoni.” (Wakol.1:3, 9).
Ni wazi
tunaweza na tunapaswa kuomba kwa ajili ya mambo mengine, kwa mfano:
“Basi, kabla
ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa
ajili ya watu wote;kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka…” Kwa nini? Paulo
anatujulisha, “tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na
ustahivu.” (1 Tim.2:1,2).
Paulo
aliwaombea ndugu zake kwa jinsi ya mwili, yaani, Wayahudi, ili waokolewe,
“Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni
kwa ajili yao, ili waokolewe.” (Warumi 10:1). Ni wazi tunaweza kuwaombea
wengine ili waokolewe.
Ni vema
kuomba kwa ajili ya kazi ya Mungu na kwa ajili ya watumishi Wake,
“Hatimaye,
ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo
kwenu.” (2Wathes.3:1)
“Mkituombea
na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri
ya Kristo.” (Wakol.4:3)
Yesu
anawaombea waumini. Roho Mtakatifu anawaombea waumini. Paulo aliwaombea waumini
sikuzote. Na sisi tumeambiwa kuwaombea watakatifu kila wakati katika Roho. Kwa
ujumla, haya ni mafundisho hasa ya Agano Jipya na yanawakilisha mzigo wa maombi
ya watakatifu. Pamoja na hayo tunafundishwa kuomba kwa ajili ya kazi ya Mungu
na watumishi Wake pia ili wengine waokolewe.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: