SHETANI NI NANI?
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
- Ni roho
iliyoasi, ambayo haina mwili, ingawa wakati mwingine anajivika umbo Fulani la
kitu kujionyesha kuwa siyo yeye, kumbe ndani ni yeye halisi.
Mwanzo 3:1-5
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wote wa mwitu aliowafanya BWANA
Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya
miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini
twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema,
Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika
hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti
huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Ayubu 1:6
Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za
BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. Ayubu 2:1 Tena kulikuwa na siku hao wana
wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati
yao, ili kujihudhurisha mbele za BWANA.
- Ni roho
iliyoasi na ina uwezo wa kuzunguka na kuingia popote kwa vile haina mwili
1 Petro 5:8
Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama samba angurumaye,
huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
- Ni adui
yetu na amejiandaa vema na vita Ufunuo 12:7-9
Shetani
maana yake ni mshindani, pia ni joka na ibilisi.
TABIA ZA
IBILISI/SHETANI
i. Yeye
hapumziki (1Petro 5:8)
ii. Yeye
halali
iii. Siyo
kama bundi anayesinzia (yeye hasinzii)
iv. Yeye
siyo mvivu
v. Wakati
wote amevaa silaha za vita na anazitumia vema kwa kadri ya mahitaji yake
vi. Hafanyi
kazi kimazoea
vii. Ni
mbunifu
viii.
Anawaza vita muda wote
ix.
Anajifunza jinsi ya kutumia silaha wakati wote
x. Hana
likizo ya uzazi wala ya kazi
xi. Ni fundi
mzuri wa kulipiza kisasi
xii. Ni kama
panya anayevizia kutoboa sanduku na akipata nafasi kidogo ya kuingia ataharibu
kila kitu
xiii. Ni
baba wa uongo (Yohana 8:44) Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tama za baba
yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala
hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo,
husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.
xiv. Ni
mdanganyifu mkubwa (Ufunuo 12:9) Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa
zamani, aitwaye ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata
nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
xv. Ni
mpambaji mzuri wa maneno yake (Mwanzo 3:1-5)
xvi. Hachoki
kutafuta habari mpya
xvii. Ni
mwivi (Yohana 10:10a) Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;
xviii. Yeye
ni mwuaji (Yohana 8:44)
JINSI YA
KUMSHINDA/KUPIGANA NA IBILISI/SHETANI
•
Kumtangazia shetani kuwa mtu aliye ndani ya Yesu Kristo ana nguvu kubwa kuliko
yeye (shetani)
• Ili uweze
kumshinda/kupigana na Ibilisi ni lazima uende kiroho kama yeye alivyo katika
roho iliyoasi. Ndani ya miili hii ya kibinadamu, tujawe Roho Mtakatifu, tuvikwe
ule utukufu wa Mungu na hatimaye tuwe tayari kupigana. Tunapaswa kwenda kinyume
na hizo tabia zake, na hapo itakuwa rahisi kumshinda. Luka 4:1-13, 1Yohana
2:13-14
• Yeye
hapumziki, sisi tusipumzike wala tusilale (1Wathesalonike 5:6-7)
• Yeye siyo
mvivu – Tunatakiwa tuwe hodari zaidi yake. Tusiwe wavivu wa sala, maombi,
kusoma Neno la Mungu. Kudumu katika sala, maombi na kusoma neno la mungu ndiyo
njia pekee ya kumshinda shetani.
• Tuvae
silaha za Kristo na tuzitumie kama inavyotakiwa. Waefeso 6:10-18
Kuwa na
silaha za kiroho ni muhimu sana katika maisha ya kiroho.
WAKRISTO WA
SASA
- Hatuna ile
kweli iliyo moyoni ya kuishi maisha ya wokovu, haki na ukweli.
- Hatutumii
ule upanga wa Roho Mtakatifu ambao ni Neno la Mungu kama Yesu alivyotumia na
kumshinda adui yake.
- Zaidi ya
yote hatudumu katika maombi, hata tukifanya ni kwa kiasi kidogo.
- Hatuna ule
utayari wa kupeleka Injili.
• Maisha ya
kiroho hayana likizo mpaka pale utakapokufa (2Timotheo 4:7) Nimevipiga vita
vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.
• Shetani ni
mwongo na mdanganyifu, sisi tuwe wakweli na waaminifu.
• Shetani ni
fundi wa kutengeneza urafiki kama alivyofanya kwa Eva. Hivyo tusimpe nafasi
katika maisha yetu kwa jinsi yo yote na wala tusiwe na urafiki naye. (Yakobo
4:7) Basi mtiini Mungu, Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
MUNGU
AWABARIKI SANA KWA KUJIFUNZA SOMO HILI NI JUKUMU LAKO KULIWEKA KATIKA MATENDO
ILI UWEZE KUISHI MAISHA YA USHINDI DHIDI YA SHETANI.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼

0 coment�rios: