ZIJUE HATUA 11 ZINAZOKAMILISHA TOBA HALISI.
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Bwana Yesu
asifiwe…
Siku ya
leo,ndani yangu ninawiwa nikueleze hatua kumi na moja muhimu utakazozitumia kukamilisha
toba yako. Hatua hizi hutumika mara kwa mara zikionesha mpangilio mzuri katika
toba.
Hivyo
basi,hatuna budi kuanza kujifunza ni nini haswa maana ya toba. Ili
tutakapoziangalia hatua hizo zikawe msaada mkubwa kwetu;
Toba ni neno
lenye asili ya lugha ya Kiebrania,lenye maana ya geuka.neno hili linapotumika
lina maana ya kugeuka kutoka katika dhambi na kumuelekea Mungu kwa njia ya
maungamo na kufuatiwa na matendo mema mara tu baada ya toba,kuonesha kwamba mtu
huyu,sasa amebadilika kupitia maungamo yake.
Tuangalie
mfano huu;
“ bali
kwanza niliwahubiri wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi yote ya
Uyahudi, na watu wa Mataifa, kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda
matendo yanayopatana na kutubu kwao.” Matendo 26:20
Paulo
anatuambia kwamba,alipowahubiria watu hao,kitendo kilichofuata;kilikuwa ni
toba,yaani watu hao walipaswa kutubu,kugeuka kutoka katika dhambi na wamwelekee
Mungu. Kisha wayatende matendo mema yenye kuambatana na kutubu kwao.
Kumbe toba
yenye maana ni ile yenye kugeuka kutoka dhambini. Lakini ikiwa unatubu kisha
uko vile vile,hakuna badiliko basi toba hiyo haitakuwa na maana kwako,kwa maana
haiwezekani ukatubia dhambi ya uzinzi huku ukiwa umepanga kwenda kuifanya kesho
yake.
▪Hivyo basi
toba ni tendo la imani la kurejesha roho iliyopotea katika dhambi imuelekee
MUNGU kwa njia ya kuungama dhambi zote kwa msaada wa Roho mtakatifu.
Neno
Kuungama dhambi maana yake ni kukiri makosa yako mbele za Mungu bila kujiami
wala kujitetea na kujutia dhambi zote ulizozifanya kisha kuweka adhimio kwamba
hutarudia tena.
Katika
maungamo yako,hutakiwi kujitetea au kujiami. Mfano wa mtu anayejitetea mbele za
Mungu kipindi anatubia dhambi zake,Ni kama vile anasema hivi;
“…Baba,Mungu
kwa kweli natubia dhambi hii ya wizi,lakini kwa kweli sasa ningefanyeje maana
ela zenyewe zilikuwa wazi wazi,kwanza mtu yoyote yule asingeweza kuzikwepa,sasa
Mungu unisamehe Bwana,maana ela zenyewe zilikuwa ni nyingi alafu zilikaa
kiasara asara mimi ndio maana nilizichukua,nisamehe Mungu wangu...!”
Mtu wa namna
hiyo,kwa kweli hajatubu chochote kile kwa sababu kwanza anajiami,na
kujitetea,pili hana mpangilio maalumu. Tuangalie mfano wa Danieli alipokuwa
akitubia dhambi za ndugu zake;
“Nikamwomba
BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha,
ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; tumefanya
dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha
maagizo yako na hukumu zako;”Danieli 9:4-5
Kumbuka;Toba
ya kweli ni lazima imuhusishe Roho mtakatifu. Kwa maana Yeye ndie amsaada wa
kweli,Yeye ndie akukumbushae dhambi zako zote ulizozitenda. Kwa maana ziko
dhambi nyingine huwezi kuzikumbuka kwa akili zako za kibinadamu,unamuhitaji
Roho wa Bwana akukumbushe na kukupa wepesi wakati wa toba yako.
KWA NINI
TUNATUBU?
Hivi
umeshawahi kujiuliza hivyo? Au kwa nini tunarudia rudia toba? Au je vile
tulivyotubu mara ya kwanza tulipoongozwa sala ya toba haikutosha?
Hayo ni
maswali ya muhimu sana kujiuliza. Zipo sababu mbali mbali zinazotufanya kutubu
kila siku,kila saa. Nimejaribu kukupatia sababu tatu za msingi zinazotufanya
kutubu mara kwa mara;
01. Tunatubu
kwa sababu miili tuliyonayo imebeba asili ya dhambi.
Ni ukweli
usiopingika kwamba asili ya miili yetu ni dhambi. Tazama,mwili hutamani
ukishindana na Roho,Roho nayo hushindana na mwili. Soma Wagalatia 5:17. Hivyo
utagundua kwamba mwili humejawa na mambo mengi ya kidunia,hutamani,hupenda ya
dunia. Kwa sababu hii ya mwili kuwa na asili ya dhambi,yatupasa kudumu katika
toba. Biblia inazidi kutupa mwanga katika hili,tunasoma tena;
“Tukisema
kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.Tukisema
kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo
mwetu.” 1 Yoh.1:8&10
02.
Tunatubia dhambi kwa sababu ya kurejesha ushirika kati yetu sisi na MUNGU wetu.
Kumbuka,dhambi
ilipoingia ulimwenguni, ilitengeneza kiambaza kilichomtenga mtu na Mungu wake.
Kiasi kwamba Mungu hakuwa na mawasiliano ya karibu kama jinsi ilivyokuwa,hivyo
ushirika kati ya Mungu na mwanadamu ukapotea. Isaya 59:2
Mtu
huyu,akapoteza mfanano na Mungu wake kwa sababu ya uwepo wa dhambi. Tazama vile
Yesu asemavyo katika Luka 19:10; kwamba Yeye alikuja kutafuta na kuokoa kile
kilichokuwa kimepotea ( yaani ushirika,ulipotea) Tunapotubu tunarejesha mfanano
wa mwanzo na kufanyika rafiki wa Mungu.
Kumbuka;Dhambi
yoyote ile inakutenga mbali na Mungu wako kwa maana hukumu ya dhambi zote ziko
sawa,ni katika ziwa la moto wa milele. Hivyo basi hakuna dhimbi ndogo wala
dhambi kubwa~dhambi ni dhambi,tubia sasa urejeshwe.
03.Tunatubu
mara kwa mara kwa sababu ya kujiandaa na safari yetu ya mbinguni kwa maana
hatujui siku wala saa.
HATUA KUMI
NA MOJA ZINAZOKAMILISHA TOBA YAKO.
Hatua
hizi,zapendeza kuzifuata katika toba yako,nazo ni
01. Mshukuru Bwana Mungu wako.
Kushukuru ni
hatua ya kwanza katika toba yako. Hakikisha unamshukuru Bwana Mungu kwa kupata
fursa ya toba,maana si wengi wapatao fursa hiyo.
Kwa sababu
wapo watu ambao walitamani wapate japo dakika 1 tu ya toba lakini hawakupata
nao hivi sasa ni marehemu,wengine vinywa vyao vimefungwa akili zimeruka wapo
vitandani hospitalini,sasa wewe ni nani basi hata upate muda kama huo wa toba!
Je si neema na rehema za BWANA? Ukitambua hilo,utamshukuru MUNGU kabla ya
kuanza toba yako. Zab.138:1-2
02.Lisifu
jina la Bwana Mungu wako.
Kumbuka
Mungu hushuka katika sifa zake. Hivyo kusifu kwapendeza sana kabla ya kuomba
chochote kile. Mungu alishuka kipindi cha ibada ya sifa na maombi ya akina
Paulo na Sila Soma Matendo 16:25-26.
Tumia neno
la Mungu katika kusifu kwako wakati unajiandaa kutubu,mfano waweza kutumia
“…kwa maana
yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa
rehema, naye hughairi mabaya.” Yoeli 2:13
03.Omba
msaada wa Roho mtakatifu.
Ni lazima
ujue kwamba wewe pasipo Roho mtakatifu hauwezi kabisa. Maombi yoyote yale
yanahitaji Roho mtakatifu ayaongoze,kadhalika hata maombi ya toba yanamuhitaji
Roho ayatawale na kuyaongoza. Sisi wenyewe hatujui kuomba ipasavyo,bali Roho
hutusaidia udhaifu wetu.
“ Kadhalika
Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo,
lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”Warumi 8:26 Soma
pia Yohana14:26
04. Samehe
wote waliokuudhi.
Huwezi
kusamehewa dhambi zako ikiwa wewe hujawasamehe wakosa wako. Kipimo cha msamaha
kwako ni kuwasamehe wakosa wako;
“Kwa maana
mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.Bali
msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”
Mathayo 6:14-15
Hivyo
basi,tangaza msamaha kwa wote waliokukosa. Waachilie watoke moyoni mwako na
wala usiwe na uchungu maana uchungu ni ukuta katika toba yako. Fanya hivyo kwa
kumaanisha kabisa,kabla hujaanza kuomba toba katika haja zako binafsi.
05. Eleza
dhambi zako zote,unazozikumbuka na usizozikumbuka.
Hakikisha
unaeleza dhambi zako zote,bila kuficha ficha. Zile unazozikumbuka omba
toba,hata zile usizozikumbuka mwambie Mungu “natubia hata dhambi ambazo
nimezitenda lakini sizikumbuki kwa sasa,Ee Roho mtakatifu unisaidie...”
Umjulishe Bwana dhambi zako zote,ili usamehewe. Mungu ukimficha,utakuwa
unajidanganya mwenyewe kwa maana Yeye anazijua zote;
“Nalikujulisha
dhambi yangu,Wala sikuuficha upotovu wangu.Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa
BWANA,Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.” Zab.32:5.
06.Jutia
dhambi zako zote.
Hiki ni kitendo
cha kusikitikia dhambi ulizozitenda. Kwamba kwa nini umefanya dhambi hizo?
Hakikisha majuto haya yatoke moyoni mwako,isiwe kwa mdomo tu.
“Kwa maana
nitaungama uovu wangu,Na kusikitika kwa dhambi zangu” Zab.38:18
Mfano;
Mtazame Petro alipotenda dhambi ya kumkana Bwana Yesu,alitubu kwa majonzi,huku
ndiko kujutia dhambi zako;
“Petro
akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana
mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.” Mathayo 26:75
07.Omba
msamaha,omba rehema mbele za Mungu.
Sasa hapa
ndipo kwenye kiini chenyewe cha toba yako. Omba msamaha kwa kumaanisha
kabisa,waweza kuanza kutumia maneno ya toba katika Zab. ya 51 yote.
“ Ee Mungu, unirehemu,Sawasawa na fadhili
zako.Kiasi cha wingi wa rehema zako,Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na
uovu wangu,Unitakase dhambi zangu.” Zab. 51:1-2
08.Ialike
damu ya YESU,ikaoshe dhambi zako.
Toba yoyote
ile ya kweli ni lazima ihusishe damu ya Yesu,kwa maana damu ndio itakasayo
dhambi. Damu ni ya muhimu sana katika toba;
“kwa maana
hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la
dhambi.” Mathayo 26:28
“ Katika
yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na
wingi wa neema yake.” Waefeso 1:7
09.
Hakikisha unapata amani ya msamaha kwa kila dhambi unayotubu.
Mfano;
unataka kutubia dhambi za aina tatu,chukulia ya kwanza ni dhambi ya wizi,dhambi
ya uzinzi,na dhambi ya kiburi. Sasa, unapoanza kutubia dhambi ya wizi,basi
hakikisha umeimaliza yote na kupata amani ya msamaha kwa dhambi hiyo ndiposa
uingie kutubia dhambi nyingine ya uzinzi nayo ni vivyo hivyo,kisha umalizie
dhambi ya kiburi.
Haitakiwi
kuruka ruka,kwamba umetubia kidogo tu mara umeingia kutubia nyinge tena gafla
ukaanza na nyingine, hapana sio hivyo!
10.Weka
adhimio kwamba hutarudia tena.
Ukimaliza
kutubu,na upo vizuri kwamba amani ya Kristo Yesu imepatikana basi usisahau
kuweka adhimio kwamba“sitarudia tena dhambi hii,Ee Roho mtakatifu unisaidie”
“ Afichaye
dhambi zake hatafanikiwa;Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata
rehema.“Mithali 28:13
11.Mshukuru
Mungu kwa kuamini yote uliyoomba umeyapokea.
Kumbuka,ukiomba
jambo lolote lile usisahau kumalizia na shukrani kwa Bwana Mungu ukiamini lile
uliloliomba limekuwa lako.
“Na yo yote
mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.” Mathayo 21:22
FAIDA ZA
TOBA YA KWELI.
01.Kuponywa
magonjwa.
Toba halisi
huleta uponyaji, kwa sababu magonjwa mengi husababishwa na uwepo wa dhambi.
Hivyo ikiwa dhambi itaondolewa basi afya urejea.
“Akusamehe
maovu yako yote,Akuponya magonjwa yako yote,”Zab. 103:3
02. Kuwa na
uhakika na uzima wa milele.
Mtu
aliyesamehewa dhambi huwa na uhakika na kuupata uzima wa milele kwa sababu sasa
amehuishwa tena,kwamba alikuwa amepotea sasa amepatikana.
03.Kupata
kibali.
Fikiri ukiwa
rafiki wa Mungu,je hutapata kibali? Au fikiria mtu aliyesamehewa dhambi
hatakubalika mbele za Mungu. Na akikubalika mbele za Mungu,basi ujue hata kwa
wanadamu hukubalika katika kibali kikuu.
“ Afichaye
dhambi zake hatafanikiwa;Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
Mithali 28:13.
Angalia; yule atakaye zificha dhambi zake
hatafanikiwa,kinyume chake ni sawa na kusema atakayeziungama dhambi zake
atafanikiwa.
MADHARA YA
KUTOTUBU.
Yapo madhara
mengi kwa mtu anayeishi maisha bila kutubu kwa Mungu wake. Haya yafuatayo ni
machache tu;
01.
Kutawaliwa na roho ya hasira,visasi na malipizi.
02.Kushindwa
kusamehe wengine.
03.Kutembea
katika laana.
04. Kokosa
tumaini la maisha ya uzima wa milele. N.K
Hivyo
basi,yatupasa kuishi maisha ya toba kila siku. Sisemi utengeneze makosa ili
utubu kila siku,hapana! Bali pale unapoingia katika maombi yako,anza na toba,na
wala usije kujihesabia haki.
Inawezekana
labda ulishawahi mara nyingi kutubu,lakini bado warudia dhambi ile ile kila
siku,na umeshindwa kuiacha,naomba niombe na wewe leo,nipigie sasa kwa namba
hii;+255763652896.
Mwinjilist :
Laurent Elias
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼

0 coment�rios: