MAMBO MATATU(3) YANAYOAMBATANA NA TOBA YAKO YA KWELI.
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
MAMBO
MATATU(3) YANAYOAMBATANA NA TOBA YAKO YA KWELI.
BWANA YESU
alikuja kwa ajili ya wanadamu watubu na kurudi katika miliki ya MUNGU kwa ajili
ya uzima wa milele.
Luka 5:32 ''
Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu. ''
-Kutubu ni
kugeuka kutoka kwenye dhambi na kuingia kwenye utakatifu.
-Kutubu ni
kuomba msamaha kwa MUNGU na baada ya kuomba msamaha unaacha dhambi zote ikiwemo
na ile iliyosababisha ukaomba msamaha.
-Kutubu ni
mabadiliko katika mtazamo, kutoka mtazamo mbaya na kuingia katika mtazamo
mzuri.
-Kutubu ni
kutafuta kumpendeza MUNGU.
-Kutubu ni
kujitenga na dhambi zote huku ukiambatana na KRISTO YESU.
-Kutubu ni
muhimu sana.
Luka 15:7 ''
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi
mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja
ya kutubu. ''
Mimi Peter
Nilipookoka jambo la kwanza nilianza kuharibu vitu vyangu ambayo havimpendezi
MUNGU, Ufahamu wangu kumbe kabla ya kuokoka haukujua mambo mambo mazuri.
nilikusanya CD zangu zote na kukuta sina hata CD au DVD moja ya nyimbo za
injili wala mahubiri, DVD zangu zote zilikuwa ni miziki tu ya kidunia na filamu
tena filamu mbaya mbaya, nilizichukua na kuanza kuvunja, rafiki yangu mmoja
aliniona na kunishangaa na kuniambia nimpe yeye lakini nilikataa na kuzivunja
zote na kuna vitabu vya mambo mabaya nilivichoma moto. Video zote za ngono na
picha kwenye simu yangu nilifuta maana nilidhamilia haswaaaaa kumpendeza MUNGU.
Toba ya
kweli ndugu zangu huambatana na mabadiliko yatakayodumu siku zote za maisha
yako.
2 Petro 3:9
'' BWANA hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia,
bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie
toba.''
MAMBO 3
YANAYOAMBATANA NA TOBA YA KWELI.
1. TOBA YA
KWELI HUAMBATANA NA KUBADILIKA NIA..
Warumi 12:2
'' Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia
zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya MUNGU yaliyo mema, ya kumpendeza, na
ukamilifu. ''
-Baada ya
kutubu dhambi lazima ubadilishe nia yako kutoka nia ya dhambi na kuingia katika
nia ya utakatifu. kuna mtu kila siku hufanya uzinzi na kila siku hutubu, hiyo
sio toba ya kweli maana nia yake haijabadilika. Nia ikibadilika hutaruhusu tena
dhambi ambazo zilikutesa kabla hujatubu. kama nia yako imekuwa nia safi hakika
huwezi hata kukaa katika bar ambayo kila siku ulikuwa unashinda pale kabla
hujatubu kwa BWANA YESU. Kama nia yako isipobadilika hakika kila siku utakuwa
unajikwaa katika lilelile unalolitubia na hapo unakuwa hujatubu toba ambayo
inampendeza MUNGU.
Mathayo
15:19 ''Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi,
ushuhuda wa uongo, na matukano; ''
-Ukibadilika
nia kutoka nia kuwaza uzinzi na uasherati hakika utafanikiwa kuingia katika
toba ya kweli. kama mabaya hayo bado yako moyoni mwako hakika utajikuta tu
unayatenda tena maana bado wewe ni mtumwa wa dhambi hizo.
-Ukitubia
dhambi fulani hakikisha unabadilika nia ya kufuata dhambi hiyo tena.
Waebrania
8:10b '' Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao
nitaziandika; Nami nitakuwa MUNGU kwao, Nao watakuwa watu wangu. ''
-Katika nia
yako MUNGU huweka sheria yake yaani huweka kila jambo ambalo unatakiwa uliendee
au uliishi baada ya hapo. Sheria hiyo MUNGU huitoa kupitia watumishi wake na
neno lake Biblia takatifu . baada ya kutubu unatakiwa usitende dhambi tena hiyo
ndio sheria ya MUNGU kwako.
2. TOBA YA
KWELI HUAMBATANA NA KUBADILIKA MTAZAMO.
Yohana 15:4
'' Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke
yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.''.
-BWANA YESU
hapo anaposema kwamba tukae ndani yake maana yake tusiondoke ndani yake
kimtazamo na kimatendo.
-Huwezi
kusema umetubu halafu mtazamo wako ukabaki kwamba hakuna haja ya kwenda
kanisani wala kujifunza Neno la MUNGU. Ndugu ukifanya hivyo hutafika popote
utajikwaa tu na kuirudia dhambi ambayo ilikufanya utubu. toba ya kweli ni
pamoja na kubadilika mtazamo kutoka mitazamo mibaya na kuingia katika mtazamo
mzuri ambao ni kukaa ndani ya YESU.
Kukaa ndani
ya YESU ni;
-Kukaa katika
Fundisho lake.
-Kukaa
katika Wokovu wake.
-Kukaa
katika Neno la MUNGU na maombi.
-Kukaa
katika mapenzi yake.
-Kukaa
katika utakatifu.
-Kukaa
katika upenndo wa wake.
-Kukaa
katika Imani pasipo kuondoka wala kuhama.
1 Kor
15:33-34 '' Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. Tumieni
akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu.
Ninanena hayo niwafedheheshe.''
-Kama bado
mtazamo wako uko katika kujumuika na marafiki zako watenda dhambi katika eneo
lile lile lililokuwa linasababisha kutenda dhambi basi utajikuta tu unaanguka
tena na tena katika dhambi.
-Kama
mtazamo wako ni kwamba unatubu kisha unajitenga na kanisa hakika hutafika
popote bali utaanguka tu dhambini.
Toba halisi
ni pamoja na kubadilika mtazamo. kuna watu mtazamo wao ni kwamba kwenda disko
kujirusha na kucheza ni jambo jema wakati mtazamo huo ni wa shetani maana ukiwa
katika maeneo hayo utajikuta una ''onja ila usilewe'' kumbe ni usanii tu wa
shetani. disko utajikuta unatamani watu wasiokuhusu maana upo katika uwepo wa
shetani. Mtazamo kama huo lazima ubadilike ndipo toba yako itakaa maana adui
hatapeleka mashitaki yeyote kuhusu wewe.
3. TOBA YA
KWELI HUAMBATANA NA KUFANYA MABADILIKO KATIKA JINSI YA KUISHI.
2
Thesalonike 1:9-10 '' Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi
kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia MUNGU mkaziacha sanamu,
ili kumtumikia MUNGU aliye hai, wa kweli; na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni,
ambaye alimfufua katika wafu, naye ni YESU, mwenye kutuokoa na ghadhabu
itakayokuja. ''.
-Huu ni
mfano wa yule aliyebadilika baada ya toba na kuacha na maisha ya kuabudu sana
au kusujudia. Kama alikuwa na sanamu nyumbani mwake ambayo kila siku alikuwa
anaibussu na kuisujudia baada ya toba ya kweli anachoma moto sanamu hizo, hayo
ndio matokeo halisi ya toba ya kweli.
-Kama
ulikuwa mganga wa kienyenyi baada ya toba unabadilika na kuchoma moto zana zote
za uganga na kuanza kuishi maisha mapya matakatifu mbele za MUNGU BABA, Hiyo
ndio toba ya kweli.
-Kama
ulikuwa unaroga watu au kuwatapeli, baada ya kumpokea YESU na kutubu unaamua
kuharibu zana zote za uchawi ulizokuwa nazo, hayo ndio matokeo ya toba ya
kweli.
-Haiwezekani
mfano kijana mzinzi anaamua kumpokea YESU na kutubu kisha kuacha uzinzi lakini nyumbani
kwake ana pakti 3 za kondomu na kila siku huvaa moja kwa kijifurahisha na pia
ana kitabu cha picha za x na katika laptop yake amejaza filamu za ngono. mtu wa
hivyo kama anajishughulisha na vitu hivyo vitamnajisi tu na kujikuta akirudi
tena dhambi.
Mathayo 3:8
'' Basi zaeni matunda yapasayo toba;''
-Ndugu, ni
matunda gani au ni mambo gani yanazaliwa baada ya wewe kutubu? je unazaliwa
utakatifu wa kudumu au utakatifu wa muda tu?
Ndugu
nakushauri zaa matunda/matendo mazuri baada ya kutubu.
KAMA UNATAKA
KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO UKAJIUNGE NA KUANZA
KUISHI MAISHA MATAKITI.
''BABA
katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi, lakini leo
nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote, nisamehe dhambi
ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu
cha hukumu na uliandike jina langu katika kitabu cha uzima. Neno lako katika
Warumi sura ya 10 Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa sababu,
ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata
kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu '' . BWANA YESU mimi
nimekuamini leo na hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika nimeokoka.
Kuanzia leo Naufunga ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo mema
na matakatifu. BWANA nipe ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda dhambi na
anasa zote za dunia. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye
haki zote. ninafuta laana zote na kila roho ya shetani inayonifuatilia
naiharibu kwa jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia
sura ya kwanza mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa. Yote
haya kwa imani nimepokea na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU kunitumia.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea Amen.
Kama umetubu
toba ya kweli hakika wewe kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa.
Kwa sasa
naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine. ulishindwa
kumpokea BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa kumpokea ni leo wala sio
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe,
hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU
akubariki sana .
Ni mimi
ndugu yako Laurent elias mpoma
+255763652896
nguvuyamungu@gmail.com
MUNGU
akubariki sana uliyesoma somo hili.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼

0 coment�rios: