Toba ni nini na ni muhimu kwa ajili ya wokovu
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Swali:
"Toba ni nini na ni muhimu kwa ajili ya wokovu?"
Jibu: Wengi
huelewa neno toba kuwa na maana ya "kugeuka kutoka dhambi" Hii si
tafsiri ya Biblia ya toba. Katika Biblia, neno toba lina maana ya "kubadili
mawazo ya mtu." Biblia pia inatuambia kwamba toba ya kweli itasababisha
mabadiliko ya vitendo (Luka 3:8-14; Matendo 3:19). Matendo 26:20 inasema,
"bali kwanza niliwahubiri wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi
yote ya Uyahudi, na watu wa Mataifa kwamba watubu na kumwelekea Mungu,
wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao." Ufafanuzi kamili wa
Biblia wa toba ni badiliko la nia akilini ambayo matokeo yake yamo katika
matendo yaliyobadilika.
Basi, kuna
uhusiano gani kati ya toba na wokovu? Kitabu cha Matendo kinaonekana kuzingatia
toba hasa inayo husu wokovu (Matendo 2:38; 3:19; 11:18; 17:30; 20:21; 26:20).
Kutubu, kuhusiana na wokovu, ni kubadili akili yako katika suala la Yesu
Kristo. Katika mahubiri ya Petro siku ya Pentekoste (Matendo 2), anamalizia na
wito kwa watu watubu (Matendo 2:38). Tubu kutokana na nini? Petro anawaita watu
walio mkataa Yesu (Matendo 2:36 ) wabadili mawazo yao kumhusu, kutambua kwamba
hakika Yeye ni "Bwana na Kristo" (Matendo 2:36 ). Petro anawaita watu
wabadili mawazo yao kutoka kumkataa Kristo kama Masihi na kuwa na imani kwake
kama Masihi na mwokozi wetu.
Toba na
imani inaweza kueleweka kama vile "pande mbili za sarafu moja."
Haiwezekani kuiweka imani yako katika Yesu Kristo kama mwokozi bila kwanza
kubadilisha mawazo yako kumhusu yeye na chenye amefanya. Hata kama ni toba ya
katao ya makusudi au toba ya kutojua au kutokua na haja, ni badiliko la akili.
Toba ya kibiblia, uhusiana na wokovu, ni kubadilisha mawazo yako kutoka kwa
kumkataa Kristo hadi kuwa na imani katika Kristo.
Ni muhimu
sana tuelewe kuwa toba si kazi sisi huifanya ili tupate wokovu. Hakuna mtu
anayeweza kutubu na kuja kwa Mungu, isipokuwa Mungu amvute huyo mtu kwake
(Yohana 6:44). Matendo 5:31 na 11:18 zinaonyesha kwamba toba ni kitu ambacho Mungu
anatoa - inawezekana tu kwa sababu ya neema yake. Hakuna mtu anaweza kutubu,
isipokuwa Mungu ampe toba. Wokovu wote, ikiwa ni pamoja na toba na imani, ni
matokeo ya Mungu kutuvuta kwake, kuyafungua macho yetu, na kubadilisha mioyo
yetu. Uvumilivu wa Mungu hutuongoza sisi kutubu (2 Petro 3:9), kama ilivyo wema
wake (Warumi 2:4).
Huku toba
ikiwa si kazi inayotuletea wokovu, toba kwa ajili ya wokovu huishia katika
matendo. Ni vigumu sana kubadili akili yako kikamilifu bila ya kusababisha
mabadiliko katika matendo. Katika Biblia, toba matokeo yake ni mabadiliko ya
tabia. Hiyo ndio sababu ni kwa nini Yohana Mbatizaji aliwaita watu "kuzaa
matunda yapasayo toba" (Mathayo 3:8). Mtu ambaye kwa kweli ametubu kutoka
kwa kumkataa Kristo hadi imani katika Kristo atatoa ushahidi wa maisha
yaliyobadilishwa (2 Wakorintho 5:17, Wagalatia 5:19-23; Yakobo 2:14-26). Toba,
ikieleweka vizuri, ni muhimu kwa wokovu. Toba ya kibiblia ni kubadilisha mawazo
yako kuhusu Yesu Kristo na kumgeukia Mungu katika imani kwa wokovu ( Matendo
3:19). Kugeuka kutoka dhambi sio fafanuzi sahihi ya toba, lakini ni mojawapo ya
matokeo ya kweli, toba iliyoweka misingi yake katika kuelekea kwa Bwana Yesu
Kristo.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼

0 coment�rios: