SIRI YA OMBI LINALOJIBIWA
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
SIRI YA OMBI LINALOJIBIWA
Anatoli
Levitini, mwandishi na mwanahistoria wa Kirusi, alitumia miaka yake mingi
katika Gulag ya Siberia, ambako dua zilizotolewa kwa Mungu zilionekana kana
kwamba zimeganda ardhini. Lakini alirudi akiwa mzima kiroho. "Mwujiza mkuu
kuliko yote ni maombi," aliandika. "Yanipasa tu kumgeukia Mungu
kimawazo na mara moja naisikia nguvu inayoingia ndani yangu kutoka mahali
fulani, inaingia katika roho yangu, na mwili wangu wote. Je! hicho ni kitu
gani? Je, naweza kuipata wapi hiyo nguvu inifanyayo mimi kuwa mtu mpya na
kuniokoa mimi, niliye mzee duni sana, niliyechoka na maisha, ambayo itaniinua
juu ya dunia hii? Inatoka nje yangu - wala hakuna nguvu yo yote ulimwenguni
humu ambyo ingeweza kuipinga."
Katika
mwongozo huu tunaona jinsi maombi yanavyotusaidia kujenga uhusiano wenye nguvu
zaidi pamoja na maisha ya Kikristo yenye nguvu.
1.
Kuzungumza Na Mungu
Je,
tunawezaje kuwa na uhakika kwamba Mungu anatusikia tunapoomba?
"Ndipo
mtaniita mimi na kwenda KUNIOMBA, nami NITA SIKILIZA. Nanyi mtanitafuta na
kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote." - Yeremia 29:12,13.
Je, ni
uthibitisho gani aliotoa Yesu kuonyesha kwamba atasikia na kujibu maombi yetu?
"Basi
nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, na mlango
utafunguliwa kwenu." - Luka 11:9.
Maombi ni
maongezi ya pande mbili. Hii ndiyo maana Yesu anaahidi anasema:
"Tazama
nasimama mlangoni, nabisha. Mtu ye yote akiisikia sauti yangu, na kuufungua
malngo, nitaingia na kula pamoja naye, na yeye pamoja nami." - Ufunuo
3:20.
Kwa jinsi
gani inawezekana kwetu kuketi na kuwa na maongezi mazuri wakati wa chakula cha
jioni pamoja na Kristo? Kwanza, kwa kumwambia kila kitu tulicho nacho moyoni
mwetu kwa njia ya maombi. Pili, kwa kusikiliza kwa makini. Tunapotafakari
wakati wa maombi, Mungu anaweza kuongea nasi moja kwa moja. Na tunapolisoma
Neno la Mungu kwa roho ya ibada, Mungu ataweza kuongea nasi kupitia katika
kurasa zake.
Maombi
yanaweza kuwa njia ya maisha kwa Mkristo.
"OMBENI
BILA KUKOMA; shukuruni kwa kila jambo, maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu
katika Kristo Yesu." - 1 Wathesalonike 5:16-18.
Je! sisi
tunawezaje "kuomba bila kukoma?" Je, yatupasa kupiga magoti wakati
wote au kurudia-rudia kusema maneno ya kumsifu au kutoa dua? La, hasha. Lakini
tunapaswa kuishi karibu sana na Yesu kiasi cha kujisikia huru kusema naye
wakati wo wote, na mahali po pote.
"Tukiwa
katika makundi ya watu mitaani, katika shughuli ya kibiashara, tunaweza kutoa
dua yetu kwa Mungu na kumsihi atupe uongozi wake… Daima tungeacha wazi mlango
wa moyo wetu na kuuacha mwaliko wetu ukipanda juu ili Yesu aweze kuja moyoni
mwetu na kukaa humo kama mgeni wetu wa mbinguni." - Steps to Christ, uk.
99.
Mojawapo ya
njia bora sana ili kujenga uhusiano huo wa karibu sana ni kujifunza kutafakari
wakati tunapoomba.
"Kutafakari
kwangu na kumpendeze yeye, mimi ninapomfurahia BWANA." -Zaburi 104:34.
Unapoomba
usiharakishe tu kupitia orodha ya mambo unayotaka. Ngojea. Sikiliza. Kutafakari
kidogo ukiwa katika maombi kunaweza kuuboresha sana uhusiano wako na Mungu.
"Mkaribieni
Mungu, naye atawakaribia ninyi." - Yakobo 4:8.
Kadri sisi
tunavyozidi kumkaribia sana Yesu ndivyo kadri tunavyoweza kuonja kuwako kwake.
Basi wewe unapaswa kuwa katika umbali wa kuweza kuongea na Yesu, wala usiwe na
wasi wasi juu ya kusema maneno yaliyo sahihi. Ongea tu naye kwa unyofu wa moyo
na bila kuficha kitu. Ongea juu ya kila kitu. Yeye amepitia maumivu makali sana
ya kifo kile chenyewe ili apate kuwa Msiri wako.
2. Jinsi Ya
Kuomba
Tunapoingia
katika maombi, tunaweza kupenda kufuata muhtasari wa sala ya Bwana, sala ya
mfano ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuitikia ombi lao hili:
Tufundishe
sisi kuomba.
"Baba
yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako
yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni
zetu, kama sisi nasi tulivyowasamehe wadeni wetu. Wala usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu,
hata milele. Amina" - (Mathayo 6:9-13).
Kulingana na
mfano huo ambao Yesu aliutoa katika sala yake, sisi tunatakiwa kumwendea Mungu
kama Baba yetu aliye mbinguni. Tumwombe kwamba mapenzi yake yatawale mioyo yetu
kama vile mapenzi yake yanavyotawala katika mbingu yote. Tunamtafuta ili
atupatie mahitaji yetu ya kimwili, msamaha wake, kwa ajili ya kuwa na roho ya
kuwasamehe wengine.
Kumbukeni ya
kwamba uwezo wetu wa kuipinga dhambi unatoka kwa Mungu. Sala ya Kristo
inahitimisha kwa maneno ya sifa kwake.
Safari
nyingine Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kumwomba Baba "kwa jina
langu" (Yohana 16:23) - yaani, kuomba kulingana na kanuni zake Yesu. Hii
ndiyo maana Wakristo kwa kawaida hufunga sala zao kwa maneno haya: "Katika
jina la Yesu, Amina." Amen (amina) ni neno la Kiebrania limaanishalo
"Na iwe hivyo".
Japokuwa
sala ya Bwana inatoa mwongozo juu ya mambo tunayotakiwa kuyaomba na jinsi ya
kutunga sala, mawasiliano yetu na Mungu yanakuwa bora sana kama yanatoka moyoni
mwetu kwa hiari.
Tunaweza
kuomba juu ya kila kitu. Mungu anataka tumwombe msamaha kwa dhambi zetu
(1Yohana 1:9), tumwombe atuongezee imani (Marko 9:24), tumwombe uponyaji wa
maumivu na magonjwa yetu (Yakobo 5:15), na kumwagiwa kwa Roho (Zakaria 10:1).
Yesu anatuthibitishia kwamba tunaweza kumpelekea yeye mahitaji yetu yote,
pamoja na mashaka yetu; mno kuweza kumwomba.
("Mwekeeni
matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni") - 1 Petro 5:7.
Mwokozi wetu
anapendezwa na mambo yo yote madogo yahusuyo maisha yetu. Moyo wake huchangamka
wakati inapomwendea mioyo yetu kwa upendo na imani.
3. Maombi Ya
Faragha
Wengi wetu
tunayo mambo fulani ambayo tunasita kuwaambia hata marafiki zetu wa karibu
sana. Kwa hiyo, Mungu anatualika sisi kuutua mzigo huo katika maombi yetu ya
faragha: tukiwa kila mmoja peke yake na yeye. Si kwamba yeye anahitaji maelezo
yote. Mwenyezi anajua vizuri sana kuliko sisi tunavyojua, makusudi yetu
yaliyojificha moyoni mwetu, na chuki zetu zilizojificha ndani. Lakini
tunahitaji kuifunua mioyo yetu kwake yeye atujuaye mpaka ndani kabisa, na
atupendaye milele. Uponyaji unaweza kuanza Yesu anapoweza kuyagusa majeraha
yetu.
Tuombapo,
Yesu, Kuhani wetu Mkuu, yu karibu nasi kutusaidia:
"Tunaye
mmoja ALIYEJARIBIWA KWA KILA NJIA, KAMA SISI TUNAVYOJARIBIWA -lakini alikuwa
hana dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupate kupokea
rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" - (Waebrania
4:15,16).
Je, una wasi
wasi, mfadhaiko, hatia? Weka hayo mbele zake Bwana. Ndipo yeye anaweza kukidhi
kila hitaji tulilo nalo.
Je, ni
lazima tuwe na mahali maalumu pa maombi hayo ya faragha?
"wewe
unaposali, ingia katika chumba chako, funga mlango na kumwomba Baba yako,
ambaye.. atakujazi." - Mathayo 6:6.
Zaidi ya
kuomba wakati wa kutembea mitaani, kufanya kazi, au kufurahia mkutano fulani,
kila Mkristo angekuwa na muda fulani uliotengwa kila siku kwa maombi yake yeye
peke yake pamoja na kujifunza Biblia. Tunza miadi yako ya kila siku na Mungu
wako wakati unapokuwa mchangamfu sana na wakati unapokuwa makini sana.
4. Maombi Ya
Hadhara
Kujiunga
pamoja na wengine katika maombi huwaunganisha watu kwa kifungo maalum na
kukaribisha uweza wa Mungu kwa njia ya pekee.
"Kwa
kuwa wawili au watatu wanapokusanyika pamoja katika jina langu, nipo pamoja nao
pale." - Mathayo 18:20.
Mojawapo ya
mambo makuu kuliko yote tuwezayo kufanya sisi kama familia ni kukuza maisha ya
maombi ya pamoja. Waonyesheni watoto kwamba tunaweza kupeleka mahitaji yetu
kwake moja kwa moja. Watakuwa na msisimko juu ya Mungu watakapoona anajibu
maombi yanayohusu mambo halisi ya maisha yao. Ifanyeni ibada ya familia kuwa
wakati wa furaha na kubadilishana uzoefu wa maisha katika hali ya uhuru.
5. Siri Saba
Za Maombi Yanayojibiwa
Musa
alipoomba, Bahari ya Shamu iligawanyika. Eliya alipoomba, moto ulishuka kutoka
mbinguni. Danieli alipoomba, malaika aliyafumba makanwa ya simba wale wenye
njaa kali. Biblia inatueleza visa vingi vya kusisimua vya maombi yaliyojibiwa.
Tena inapendekeza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza kwetu maombi kama
njia ya kupata ule uweza mkuu wa Mungu. Yesu anaahidi hivi:
"Mkiniomba
neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya" - (Yohana 14:14).
Lakini
maombi mengine bado yanaonekana kana kwamba hayasikilizwi. Kwa nini? Hapa chini
zipo kanuni saba zitakazokusaidia wewe kuomba kwa ufanisi zaidi:
(1) Uwe
karibu sana na Kristo.
"NINYI
MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote
nanyi mtapewa." - Yohana 15:7.
Tunapoupa
kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na kuwa karibu naye, tutakuwa tunasikiliza na
kutazamia kupata majibu kwa maombi yetu ambayo, vinginevyo, tusingeyatambua.
(2) Endelea
Kumtumaini Mungu.
"MKIAMINI,
mtapokea yote myaombayo katika sala zenu" - (Mathayo 21:22).
Kuamini au
kuwa na imani, maana yake ni kwamba tunamtazamia Baba yetu aliye mbinguni
kwamba kweli atatupa hayo mahitaji yetu. Kama wewe una wasiwasi kwamba huna
imani, basi, kumbuka kwamba Mwokozi alitenda mwujiza kwa mtu yule aliyemsihi
sana akiwa amekata tamaa, aliyesema:"
"Naamini,
nisaidie kutokuamini kwangu!" - (Marko 9:24).
Wewe kazana
tu kuitumia imani ULIYO nayo; usiwe na waiswasi juu ya imani ile usiyo nayo.
(3)
Jisalimishe kimya kimya chini ya mapenzi ya Mungu.
"Huu
ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA
MAPENZI YAKE, anatusikia" - (1 Yohana 5:14).
Kumbuka
kwamba Mungu anataka kutufundisha sisi, pamoja na kutupa sisi vitu, kwa njia ya
maombi. Kwa hiyo, wakati mwingine anatuelekeza upande mwingine. Maombi ni njia
ya kutusogeza sisi zaidi na zaidi karibu na mapenzi ya Mungu. Hisia zetu zinatakiwa
ziwe kali kutambua majibu ya Mungu na kujifunza kitu kutokana nayo.
Kuyafuatilia kwa karibu maombi yetu fulani fulani ya pekee pamoja na kile
kinachotokea kuhusiana nayo ni msaada mkubwa kwetu.
Roho
Mtakatifu atakusaidia kulenga shabaha yenyewe: "Roho anawaombea watakatifu
kulingana na mapenzi ya Mungu" (Warumi 8:27. Kumbuka kwamba mapenzi yetu
yangeweza kulandana siku zote na mapenzi ya Mungu endapo sisi tungeweza kuona
kama yeye anavyoona.
(4) Mngojee
Mungu kwa Saburi.
"NALIMNGOJA
BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kilio changu" - (Zaburi 40:1).
Jambo kubwa
hapo ni kukaza mawazo yako yote kwa Mungu, kukaza mawazo yako yote juu ya
suluhisho lake. Wala usithubutu kumwomba Mungu akusaidie kwa dakika moja, na
halafu kujaribu kuzizamisha shida zako kwa kujifurahisha katika anasa dakika
inayofuata. Umngoje Bwana kwa saburi; tunahitaji kuwa na nidhamu hiyo vibaya
sana.
(5)
Usiing'ang'anie Dhambi iwayo yote.
("Kama
ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza")- Zaburi
66:18.
Dhambi ijulikanayo
hukata mara moja uweza wa Mungu katika maisha yetu; inatutenga mbali na Mungu
(Isaya 59:1-2). Huwezi kuishika na kuing'ang'ania dhambi kwa mkono mmoja na
kunyosha mkono mwingine kupokea msaada wa Mungu. Ungamo la dhambi litokalo
moyoni hasa pamoja na toba ya kweli ndilo suluhisho la tatizo hilo.
Kama sisi
hatutaki kumruhusu Mungu kutuweka huru mbali na mawazo, maneno na matendo yetu
mabaya, basi, maombi yetu hayawezi kutuletea jibu lo lote.
"Hata
mwaomba, wala hampati, kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa
zenu" - (Yakobo 4:3).
Mungu
hatajibu "ndiyo" kwa maombi ya uchoyo. Acha wazi masikio yako yapate
kuisikia sheria ya Mungu [Amri Kumi], yaani, mapenzi yake, naye ataacha masikio
yake wazi kuzisikia dua zako.
"Yeye
aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria [Amri Kumi], hata sala yake ni
chukizo" - (Mithali 28:9).
(6) Tambua
Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu
huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha yao.
"Heri
wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa." - Mathayo 5:6.
(7)
Kuendelea Kuomba Tu.
Yesu alitoa
kielelezo cha kuwapo kwa haja ya kuendelea tu kutoa dua zetu kwa kusimulia kisa
kile cha mjane aliyekuwa anaendelea tu kuomba na kuendelea kuja kwa hakimu
akiwa na ombi lake lile, lile. Mwishowe yule hakimu alisema, huku akiwa
ameudhika vibaya sana, "Kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitahakikisha
kwamba nampatia haki yake." Kisha Yesu alitoa hitimisho lake hili:
"Je! Mungu hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je!
atazidi kuahirisha kuwapatia haki yao?" (Luka 18:5-7).
Zungumza na
Mungu juu ya mahitaji yako yote, matumaini yako yote, na ndoto zako zote. Omba
mibaraka ya pekee, omba msaada unapokuwa na shida. Endelea kutafuta, tena
endelea tu kusikiliza, mpaka ujifunze kitu fulani kutokana na jibu lake Mungu.
6. Malaika
Wanayahudumia Mahitaji Ya Waombao
Mtunga
Zaburi alishangilia kwamba kwa njia ya huduma ya malaika wa Bwana maombi yake
yalijibiwa:
"Nalimtafuta
BWANA akanijibu; akaniponya na hofu zangu zote... malaika wa BWANA hufanya
kituo kuwazunguka wale wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:4-7).
Tunapoomba,
Mungu anawatuma malaika zake kujibu maombi yetu (Waebrania 1:14). Kila Mkristo
anaye malaika wake mlinzi anayetembea pamoja naye:
"Angalieni
msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO
mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni." - Mathayo
18:10.
Kwa sababu
ya maombi yetu tunayotoa:
"Bwana
yu karibu. Msiwe na wasiwasi na jambo lo lote, lakini katika kila jambo kwa
maombi na dua zetu pamoja na kushukuru, wekeni mambo yenu myatakayo mbele zake
Mungu. Ndipo amani ya Mungu, ipitayo ufahamu wote, itawahifadhi mioyo yenu na
nia zenu katika Kristo Yesu." - Wafilipi 4:5-7.
7. Mtindo Wa
Maisha Ya Kikristo
Biblia
inaeleza wazi juu ya mtindo wa maisha ya Kikristo. Kulingana na Waefeso 4:
22-24, Mkristo anatakiwa ku"vua" mtindo wake wa maisha ya zamani
uliotokana na "tamaa zenye kudanganya", na ku"vaa" mtindo
mpya wa maisha ambao ume"umbwa kwa mfano wa Mungu." Katika maandiko
hayo na mwongozo tuligundua kwamba wakati ule wa kuzaliwa upya sisi
tuna"umbwa upya" kuwa watu tofauti ndani ya Kristo.
Mwongozo huu
na miongozo sita inayofuata hutangaza upya mtindo wa maisha ya Mkristo;
huifunua siri ya maisha ya Kikristo yenye furaha. Itakusaidia wewe kujenga
uhusiano wenye nguvu zaidi na Kristo, ambao matokeo yake yatakuwa mtindo wa
maisha ya Kikristo ulio tofauti. Kwa hiyo kaza macho yako kwa Yesu leo hii,
nawe unaweza kuwa na sehemu katika sherehe ile ya mwisho ya ushindi wakati
amani yake Kristo itakapotawala bila kupingwa.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼

0 coment�rios: