USHIRIKA NA MUNGU

KUTAZAMA VIDEO YAKE BONYEZA
HAPA CHINI▼▼


PICHA ZAKE ZOTE AKIWA MTUPU BONYEZA
HAPA CHINI▼▼


UTANGULIZI: JE, umewahi kuwasikia watu wakisema kuwa wanaabudu kwa namna zao wenyewe? Wamechoshwa na “kanisa” na kwamba kukutanikia jangwani ni bora zaidi kwa sababu jangwa haliwaambii maneno yasiyo mazuri. Ingawa ni ukweli kwamba ni muhimu kutenga muda binafsi wa kuwa na mungu, katika somo letu juma hili yakobo anaelezea manufaa ya kushirikiana [kuchangamana] kiibada na wakristo wenzetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la biblia ili tujifunze zaidi!


USHIRIKA NA MUNGU
A. SOMA YAKOBO 5:13. Maelezo ya fungu hili yanatuhusu watu wengi. Uwezekano mkubwa ni kwamba aidha tuna matatizo au hatuna furaha. Tunatakiwa kuitikiaje uzoefu huu wenye tofauti kubwa? (kwa kumgeukia mungu. Ama tunatakiwa kuomba kwa ajili ya kupata msaada au tunatakiwa kumsifu mungu kwa njia ya nyimbo.)
1.  Mwitikio wako kimaadili ni upi unapojikuta kwenye matatizo? (siku za nyuma, papo hapo nilifanya kile nilichoweza ili kutatua tatizo. Sasa nimejifunza kwamba hatua ya kwanza lazima iwe ni kumgeukia mungu.)
2.  Je, huwa unakasirika unapokabiliana na matatizo? (asili ya mwanadamu huwa ni kuwalaumu watu wengine, na kisha kukasirika kutokana na kile walichotutendea. Ikiwa, kwa uwezo wa roho mtakatifu, tutamgeukia mungu kwanza, itatuepusha kusema au kutenda jambo baya papo hapo kwa sababu ya hasira. Hii itaepusha kufanya tatizo kuwa gumu zaidi.)

B. Mtazamo wa namna gani unaakisiwa kwenye ushauri wa yakobo kwa ajili yetu kuomba au kusifu? (mungu ndiye anayeyashikilia maisha yetu. Yeye ndiye chanzo cha mibaraka yote. Tunamgeukia ili kupata msaada na tunamshukuru kwa kumpa sifa.)

   USHIRIKA NA WAUMINI
A.  Soma yakobo 5:14-15. Kuugua ni mfano mahsusi wa tatizo. Kwa nini usijiombee tu wewe mwenyewe – kama anavyobainisha yakobo katika mstari wa 13? Kwa nini kuwahusisha wazee katika jambo hili? (mungu hahitaji wazee kumshawishi ili afanye uponyaji, lakini wazo la kushirikiana na waumini wenzako linaelezewa hapa.)

1. Kuna nyakati kadhaa nilikuwa sehemu ya kundi la wazee waliomwombea na kumpaka mafuta mgonjwa. Nchini marekani, watengenezaji wa dawa wanaeleza bayana athari za dawa zao wakati ule ule wanapotangaza jinsi dawa zao zinavyoweza kutibu. Mke wangu alikuwa akiniambia kwamba nilitakiwa kubainisha jambo hili nilipokuwa sehemu ya wanaofanya maombi na kupaka mafuta katika kipindi cha nyuma ambapo wagonjwa hawakupona. Mke wangu alikuwa akitania, lakini hadi siku za hivi karibuni, jambo hilo lilibakia kuwa ukweli mtupu. Je, yakobo anatoa ahadi za uongo kuhusu uponyaji?
A.  Je, mimi ndiye niliyekuwa tatizo? Yakobo anapoandika “na kule kuomba kwa imani,” je, alikuwa akiandika kuhusu imani ya wazee? Kama sivyo, anaelezea imani ya watu gani, je, ni imani ya mgonjwa?
B. Soma marko 2:1-5. Je, hapa yesu anazungumzia imani ya nani? (haiko wazi. Yesu anaonekana kuzungumzia imani yao wote.)


C.  Soma mathayo 18:19. Vipi kama mgonjwa alikuwa na imani na mzee mmoja pekee ndiye alikuwa mwenye haki, je, imani hiyo ingetosha kuleta uponyaji? (utagundua kwamba yesu haonyeshi kiwango cha imani au haki inayotakiwa, anabainisha tu idadi ya waumini waliokubaliana. Wawili wanatosha.)

D. Hebu tuangalie tena yakobo 5:15. Je, yakobo anatoa muda wa kuinua na kuponya? (hapana. Nina uhakika kila mtu aliyekuwa kwenye huduma ya kupaka mafuta ambapo mimi pia nilihusika alikuwa mdhambi – kuanzia mgonjwa hadi kwa wazee wote. Yakobo hasemi kwamba hatutakiwi kuwa na dhambi, anasema kwamba tunatakiwa kuwa na imani. Kwa kuongezea, hatoi muda kwa ajili ya uponyaji. Ninaamini mungu atawafufua katika uzima wa milele wote waliolala wakimtumaini yeye.)

E.   Kipindi cha hivi karibuni kabisa ambapo nilikuwa sehemu ya kundi la wazee waliokwenda kufanya maombi, mgonjwa aliponywa. Mungu anatenda miujiza maishani mwangu, na kwenye maisha ya wale ninaowaombea, na ninaamini hili linahusiana zaidi na mapenzi ya mungu mwenye enzi, badala ya haki yangu. Je, wewe unadhanije?

UPONYAJI, IMANI NA DHAMBI
A. Angalia tena sehemu ya mwisho ya yakobo 5:15 na marko 2:5. Yesu anamwambia mwenye kupooza kwamba dhambi zake zimesamehewa. Yakobo anasema, dhambi zinaweza kusamehewa. Je, kuna uhusiano gani kati ya uponyaji na dhambi?
B.  Soma yohana 9:1-3. Kwa nini wanafunzi waliuliza kuhusu dhambi na upofu? (uelewa wa kipindi hicho ulikuwa ni kwamba dhambi ilisababisha magonjwa. Nadhani bado kuna ukweli mwingi kwenye uelewa wao.)

1.  Je, yesu alisema kuwa sababu ya upofu ni ipi? (ili mungu aweze kutukuzwa. Haikuwa suala la dhambi.)
2.  Dhambi inapoungamwa na kusamehewa, je, mungu anatukuzwa? (ndiyo! Angalao kauli za yakobo na yesu kuhusu ugonjwa na dhambi zina maelezo ya aina mbili. Kwanza, ni uelewa wa watu wa kipindi hicho. Lakini, jambo la muhimu zaidi ni kwamba, mungu anataka kutuponya dhambi. Lengo lake kuu kwetu ni kuwa na maisha yasiyo na dhambi na ugonjwa – na lengo hilo litatimia mbinguni.)
C. Siku chache zilizopita nilikuwa mapumzikoni kwa muda wa siku kadhaa eneo la “disney world,” ambapo watu wanene wanakusanyika na kuendesha vijigari. Kiukweli, watu wengi waliokuwepo mahali pale pia walikuwa wanene. (katika kuzungumzia suala la unene, niliweza kuongezeka uzito wa kilogramu 1.8 nilipokuwa likizo!) Wakati huo huo, sikumwona mtu hata mmoja akivuta sigara. Inaonekana kwamba hatari ya kiafya inayotokana na uvutaji wa sigara imebadilishwa na hatari ya kiafya inayosababishwa na unene mkubwa kupita kiasi. Swali gumu ni hili: je, dhambi inaweza kuingiliana na uponyaji?
1.  Kama utasita kumwombea mvuta sigara ili aweze kuponywa, vipi kuhusu mtu mnene kupita kiasi?
2.   Je, kiasili baadhi ya watu si ni wanene tu? Je, hilo linajalisha?
3.  Nimesoma sana kuhusu ubongo, na ninashawishika kwamba mazoezi ni tiba ya watu wote kwa magonjwa ya aina yote, yakiwemo masuala ya kiakili. Je, kushindwa kufanya mazoezi ni dhambi inayotuzuia tusiponywe?
4.  Je, nimemtukana takribani kila mtu? Ninachokimaanisha ni kwamba tunawaangalia wavuta sigara wanaougua saratani ya mapafu, na wasenge wanaougua ukimwi, na hatuwahurumii sana kutokana na matendo yao.

KUTUBU [KUUNGAMA] DHAMBI
A.   Soma tena yakobo 5:15. Muda wa msamaha ni upi? (baada ya mtu kuponywa. Hii inaashiria kwamba uponyaji upo kwa ajili ya watu wote.)
B.  Soma yakobo 5:16. Hebu subiri kidogo! Baada ya mjadala wetu juu ya dhambi, je, yakobo anasema kuwa tunatakiwa kutubu dhambi zetu ili tuweze kuponywa? Au, je, kuombeana sisi kwa sisi ndio kigezo pekee kinachohusiana na uponyaji?
C. Angalia tena yakobo 5:16. Unafikiria nini kuhusu kutubu dhambi kwa waumini wenzetu?
D. Soma zaburu 51:4, zaburi 32:5 na 1 yohana 1:9. Je, mafungu haya yanapendekeza kwamba tutubu dhambi zetu kwa nani? (tunatenda dhambi dhidi ya mungu, na mungu ndiye ana uwezo wa kusamehe dhambi. Hivyo, inaleta mantiki kutubu dhambi zetu kwa mungu.)
E.  Unapotafakari kuhusu jambo hili, je, kuna aina mbalimbali za kutubu? (ninadhani hivyo. Kwanza, kuna kutubu na msamaha wa dhambi, jambo ambalo ni suala kati yako na mungu. Pili, mathayo 18:15, luka 17:4 na mambo ya walawi 6:1-5, mafungu yote hayo yanaashiria kwamba kuna dhambi ambazo tunatakiwa kuombana msamaha sisi kwa sisi. Tatu, ni kile ninachodhani yakobo anakizungumzia; mantiki ya jumla kwamba tunatenda kazi na waumini wenzetu ili kuelekea kwenye haki. Tunaombeana sisi kwa sisi, tunajadiliana dhambi zetu sisi kwa sisi, tunajadiliana masuala ya kiroho sisi kwa sisi.)

NGUVU YA MAOMBI
A. Soma yakobo 5:17-18 kisha usome sehemu ya mwisho ya yakobo 5:16. Tumekuwa tukijadili juu ya dhambi, lakini nadhani yakobo amejikita kwenye maombi. Kwa nini yakobo anamtaja eliya kama mfano? (anasema alikuwa “mwanadamu mwenye tabia moja na sisi.” Sote tuna uwezekano wa kuwa na maombi yenye nguvu na ufanisi mkubwa.)
1. Soma 1 wafalme 19:3-4. Kwenye mjadala wetu hadi tulipofikia, nimelinganisha [nimehusianisha] masuala ya kiafya na dhambi. Katika mathayo 15:16-18 yesu anapendekeza kwamba mlingayo huu si sahihi. Kwa upande mwingine, kutokumtumaini mungu ni dhambi (ufunuo 21:8). Yakobo anapotuelekeza kwa eliya, je, anasema nini? (imani na udhati katika maombi ndio ufunguo wa uponyaji, sio kutokuwepo kwa dhambi.)
B. Soma yakobo 5:19-20. Haya yanaonekana kama madai ya mwisho ya “matendo” – ikiwa tutawaongoa upya “waliorudi nyuma” dhambi nyingi zitasamehewa. Je, muktadha huu unaashiria kuwa uelewa sahihi wa jambo hili ni upi? (unazungumzia juu ya uelewa wetu wa dhambi, badala ya asili ya wokovu. Sura hii ilikuwa inazungumzia juu ya kufanya ushirika [kuchangamana]. Ikiwa mtazamo wako ni kuwaunga mkono na kuwaokoa washiriki wenzako wa kanisa, basi kitendo hicho, badala ya kupoteza muda, ndicho kilicho cha muhimu machoni mwa mungu.)
C.Rafiki, je, wewe ni sehemu ya watu wanaofanya ushirika wa mara kwa mara? Kama wewe si sehemu ya kundi hilo, basi unakosa kipengele cha muhimu sana cha kuwa mkristo. Kwa nini usitubu juu ya jambo hili na kuungana na kundi linaloshikilia imani na utii?


MAOMBI YA KUSAMBARATISHA UCHAWI NA NGUVU ZA GIZA
 Baba katika jina la yesu. Laana zote nilizo tupiwa na wabaya wangu zimeshindwa kwa jina la yesu na nazivunja na kuzisambaratisha kwa damu ya yesu. Mshindwe wote mnao tuma laana kwangu katika jina la la yesu.

Nawavunja na kuwaharibu na kuwakatakata wachawi wote kwa damu ya yesu.

Nasambaratisha kila neno la uovu lililosemwa juu yangu na famila yangu katika jina la yesu.

Naharibu na kuisambaratisha madhabahu yenu mliyo fanyia kafara kwa damu ya yesu.

Navunjavunja na kubomoa kila uovu na uchawi mnaonifanyia katika jina la yesu.

Nairudisha misukule yote na majini yote yawarudie nyie na kuwalipa dhambi zote mnazo fanya katika jina la yesu.

Naharibu kila uchawi, kila urogi, kila ndumba kila aina ya uovu ambao mnaufanya ili uniumize mimi na familia yangu katika jina la yesu.

nawateketeza kupitia damu ya yesu wachawi wote walio tumiwa kunitumia uchawi katika jina la yesu.

Nawateketeza na kuwaharibu majini yote yaliyo tumwa kuja kufanya kazi hiyo waliyo tumwa na wachawi katika jina la yesu.

Nawateketeza na kuwauwa makuhani wote ambao walienda kunishitaki kwa wachawi ili waniharibie maisha, nawateketeza kupitia damu ya yesu. Nawachoma kwa moto wa roho mtakatifu katika jina la yesu.

Nateketeza aina zote za vyombo vya kichawi vilivyo tumiwa kuja kunichunguza katika jina la yesu.

Naharibu fikra zao zote ambazo wanazitumia kufanya kazi zao za kichawi katika jina la yesu.

Nafuta kumbukumbu zoote zangu ambazo wamewapa mashetani, majini, roho chafu, nafuta hizo kumbukumbu kwa kutumia damu ya yesu, katika jina la yesu aliye hai.

Nawateketeza waweka kumbukumbu wa kimashetani kupitia damu ya yesu aliye hai. Naharaibu na kuchoma kupitia moto wa roho mtakatifu makabrasha yote yenye kumbukumbu zangu katika jina la yesu.

Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuharibu maisha yangu na ubomoa kupitia damu ya yesu.

Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuniua nauvunja na kuuteketeza kupitia damu ya yesu.

Kila uchawi ulio fanywa ili kuja kuiba mali zangu, nauvunja na kuubomoa na kuuharibu kupitia damu ya yesu.

Kila uchawi ulio fanya kuja kuniharibia familia yangu, nausambaratisha na kuuvunja na kuubomoa katika jina la yesu.

Kila neno la kichawi lililo tumwa ili kuja kuniharibia, kunidhihaki, kunitendea mabaya nalirudisha kwa aliye lituma katika jina la yesu.

Kila uovu, uchawi, wanga, ndumba, ramli, yaliyo tumwa kuja kwangu navunja yote hayo kupitia damu ya yesu na katika jina la yesu.

Nyota yangu ambayo wanaita nairudisha kupitia damu ya yesu. Nyota yangu ya baraka nailinda na kuzungushia na kuizingira na damu ya mwana kondoo katika jina la yesu.

Namteketeza yule mtu aliye kuja kuiba nyota yangu katika jina la yesu.

Nateketeza mbinu zote wanazo tumia ili kuja kuiba nyota yangu katika jina la yesu.

Nateketeza wivu wao, chuki yao, laana zao, maovu yao na kila aina ya uchafu ambao wanao kwa ajili yangu katika jina la yesu.

Naizungushia na kuizingira nyumba yangu na damu ya yesu.

Naishungushia na kuizingira familia yangu na damu ya yesu.

Nashungushia na kuzingira maisha yangu yote na damu ya yesu.

Navunja laana zote zilizo semwa na mabau zangu katika jina la yesu.

Navunja laana zato ambazo zilisemwa bila ya mimi kufahamu, nazivunja na kuziharibu kupitia damu ya yesu na katika jina la yesu.

Narudisha kila mali walizo ziiba kutoka kwangu katika jina la yesu.

Narudisha kila baraka walizo ziiba kwangu katika jina la yesu.

Narudisha amani na upendo katika familia yangu.

Damu ya yesu ipo juu ya maisha yangu na inasafisha kila uovu, kila uchawi unaaribiwa na damu ya yesu katika jina la yesu.

Leo hii mtaiona nguvu iliyopo katika damu ya yesu.

Katika jina la yesu aliye hai ninaomba.

Amen


MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUPATA KITABU NINAMANI KITAKUSAIDIA / KIMEKUSAIDIA KATIKA KAISHA YAKO YOTE.

HII NI SEHEMU YA KWANZA YA KITABU JUU YA SOMO LA MAOMBI.


KIMEANDALIWA NA MWINJILIST LAURENT E. MPOMA.

KANISA LA PENTECOSTAL CHRISTIAN CENTER – MISUNA SINGIDA

KUJIPATIA VITABU VINGINE AU UNAHITAJI MAOMBI FIKA KANISANI PENTECOSTAL CHRISTIAN CENTER – MISUNA –SINGIDA

AU PIGA SIMU:+255763652896, 714890889.

MUNGU AKUBARIKI SANA>>>>>>AMINA.


KWA NAFASI ZA KAZI POPOTE TANZANIA, BONYEZA
HAPA CHINI▼▼

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
[3.00 MB]VIDEO YA ALIKIBA AKIBANDUANA NA JOKATE, BONYEZA
HAPA CHINI▼▼



0 coment�rios: