JAMBO LA PILI MTAKWENDA NA KUNIOMBA.
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
JAMBO LA
PILI MTAKWENDA NA KUNIOMBA.
Sasa baada
ya kuwa umemuita mungu kinachofuata ni kwenda na kumuomba mungu. Anaposema
mtakweda na kuniomba ana maana mtaanza kuomba sawasawa na vile nilivyowaonyesha
au nilivyowafunulia wakati mliponiita katika haja zenu.hivi ulishawahi
kujiuliza ni mambo gani makubwa na magumu ambayo mungu atakuonyesha_pindi
utakapomuita?. Kumbuka tulikotoka tumeona kumuita mungu ni kumfanya mungu
akufunulie mambo usiyoyajua kuhusu hitaji lako ili ujipange vizuri kuyaombea.
Sasa kwenda
na kuomba maana yake ni kuomba sawasawa na vile mungu alivyojifunua kwako
kuhusu hitaji ulilonalo.utakapoomba namna hii ndiko kunaitwa kuomba sawasawa na
mapenzi ya mungu maana yake unaombea mambo ambayo mungu anataka uyaombee kwa
wakati huo. Kwa lugha nyepesi jifunze kuomba mambo ambayo mungu anakuongoza
kuyaombea. Labda nitoe mifano michache ndio somo litaeleweka vema.
Mfano wa
kanza huenda mnaombea mgonjwa au mtu aliyefungwa na mapepo. Ni kweli biblia
imesema mtaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya.sasa si kila mgonjwa
ni wa kuweka mikono na kuanza kukemea ugonjwa au mapepo, kuna magonjwa mengine
yanasababishwa na mawazo yaani tatizo ni mtu mwenyewe, mwingine huenda ni kwa
sababu ya kujeruhiwa nafsi yake na mwingine huenda ni kwa sababu ya dhambi, na
mwingine huenda mikataba aliyoingia mwenyewe na mapepo na huenda mengine ni
mungu mwenyewe ameruhusu shetani aguse afya ya huyo mtu kama alivyomruhusu
shetani kwa ayubu nk..
Saa nafikiri
mpaka hapa umeshaona si wagonjwa wote utakawawekea mikono watapona. Hivyo ni
vema umuite mungu akufunulie nini cha kufanya, mwingine atakuambia huyu
anahitaji ushauri tu wala si maombi,mwingine anaweza kukuambia huyu ametenda
dhambi hii na hii akizitubia nitamponya, na mwingine atakuambia huyu hicho ni
kipimo chake mpe tu neno la uvumilivu na ushindi,mwingine atakuambia huyu ndugu
mwenyewe au wazazi wake waliingia mkataba na mapepo hivyo vunja kwanza mktaba
huo nk.
Mfano wa
pili,huenda mnaombea kanisa lenu. Ni rahisi kusema tumuombe mchungaji ndani ya
kanisa,mara tuombee kamati ya ujenzi tuombe mungu kuhusu ujenzi nk.kweli ni
maombi mazuri lakini una uhakika mungu kwa wakati huo anataka muombee hayo
mambo.huenda kuna roho ya mpinga kristo ina vamia washirika au kuna maajenti
wanajiingiza kwa siri makanisani na kuwapofusha macho ninyi mnakazana kuombea
ujenzi. Maana yangu ni hii ikiwa wewe ni mchungaji au kiongozi wa maombi katika
kundi lolote lile ni vema kila wakati kumuita mungu akupe mambo ya kuombea kwa
wakati huo. Mungu atakufunulia nini unachotakiwa kuombea kwa wakati huo.
Nina ujasiri
na ninachokisema kwa sababu siku moja tukiwa katika kambi la vijana.nilikuwa
kwenye timu ya maombi ya hilo kambi.ndani ya hiyo timu tulikuwa na wajumbe wa
shetani kutoka kuzimu yaani maajenti (vibaraka wa shetani).hawa jamaa walikuwa
wakiomba na kufimga kuzidi masaa yale tuliyokuwa tukifunga sisi.na wakati wa
kuomba walikuwa wanapendekeza tuombee na kukemea roho ambazo hazifanyi kazi
katika lile eneo tulilokuwepo.na walikuwa wanajita watumishi wa mungu.nina
uhakika wa habari hii kwani mungu alinifungua macho tukaomba na nguvu za mungu
ziliposhuka mmoja wo akasema “sisi ni wajumbe wa shetani kutoka
kuzimu,tulitumwa kuleta uharibifu lakini katika yale tuliyotumwa tumeshindwa
kuyatekeleza”.
Nakuambia
tangia siku hiyo ndipo nilipofunguka macho yangu ya ndani na kuanza kuhitaji
uongozi wa mungu katika yale tunayoomba kila siku.hujawahi kuona kiongozi wa
maombi anasema jamani hee tutaombea hili na hili na hili,lakini mnapoanza
kuomba unakuta mungu anakuongza kuombea vitu vingine kabisa ?.
Kumbuka siku
zote katika kila unaloliomba ,mwambie mungu nifunulie zaidi kuhusu mambo ya
kuomba kuhusu hili jambo.lwe ndoa,kanisa,mkutano au semina,watoto,elimu nk sasa
nimalizie kwa kusema kuomba kwa namna hii ndiko kibiblia kunaitwa kumtafuta
bwana.sikiliza huwezi kumtafuta mtu mahali asikopatikana.unapomtafuta bwana ni
lazima umtafute kwenye maeneo yake yaani kule anakopatikana.sasa kunaitwa
kumtafuta bwana kwa sababu umeomba kulingana na ufunuo wake
Ni imani
yangu kuwa baada ya kuwa umesoma ujumbe huu basi naamini umeshapata maarifa ya
kukusaidia katika kumtafuta bwana na hivyo kwa jambo lolote utakalotaka kuomba
siku zote utaomba kwanza ufunuo wa mungu juu ya hili jambo.
IMANI YAKO
ITAKUPONYA, MWAMINI BWANA YESU LEO
Kila mwaka
tarehe 1 / 12 ni siku ya kuadhimisha janga la ukimwi kwa kuwa na ujumbe
mbalimbali jinsi ya kutokomeza na kuelemisha watu jinsi ya kujikinga na kuzuia
maambukizo mapya ya virusi vya ukimwi na vile vile kuishi kwa matumaini
kuhusiana na ugonjwa huu. Japo kuna baadhi ya maeneo elimu bado sijui niseme ni
changa au haijawafikia walengwa vizuri, na
la kushangaza yakiwemo baadhi ya maeneo ya mijini yakiongoza kwa
asilimia kubwa ya kuwa na maongezeko mapya ya mambukizi ya virusi vya ukimwi.
Swali la kujiuliza ni kuwa watu hawataki kuelewa au ni elimu imezoeleka kiasi
kwamba watu wanaona hakuna jipya au maisha ndio yanawalazimisha kutokuzingatia
yanayosemwa. Au je waelemishaji nao pia hawana elimu ya kutosha ya kuwaelimisha
watu / watoaji elimu ni wachache kuliko walengwa / walioathirika? Au wamekosa
imani na asasi / ngo zinazotoa huduma hii? Ukiangalia kwa mtazamo wa kawaida tu
kuna asasi/ngo mbalimbali zimeazishwa kwa ajili ya kusaidia na kuelimisha
waathirika wa ukimwi / na ambao bado hawajapata maambukizi pamoja na watoto
yatima na wajane.
Je wanatoa elimu sahihi na yakutosha? Kama ndio kwa nini kuna
ongezeko kubwa la watoto yatima na maabukizi mapya yanaibuka siku hadi siku? Au
waanzilishi wa hizi asasi / ngo
wanatafuta maslahi yao wenyewe kwa kupitia mgongo wa walioathirika badala ya
kutoa elimu ya sahihi na ya kutosha? Japo kwenye takwimu zinaonyesha kuwa
tanzania imeshuka kwenye kiwango cha maambukizi ya ukimwi ukilinganisha na nchi
nyingine za africa. Je hili nalo ni kweli yanaweza kuwa ongezeko la maambukizi
mapya limepungua wakati bado tunashuhudia watoto yatima wakiongezeka kutokana
na hili janga? (tutafakari hili) mimi sina jibu ila haya yote ni mtazamo wa
kibinadamu tu. Hebu tungalie biblia inatuambia nini kwa habari ya magonjwa? Je
kuna ambalo linashindikana kwa bwana? Kama yeye alitufinyanga kwa mikono yake si
anajua kila sehemu ya viungo vyetu hivyo ni rahisi yeye kuturekebisha pale
penye madhaifu na kupatia uzima. Hebu tuone biblia inasema nini basi kwa habari
ya uponyaji....
Ukisoma
kwenye biblia zetu utaona kwamba ukoma ndio uliokuwa ugonjwa mbaya sana na ulikuwa
unatishia watu enzi hizo za kale pia ulikuwa ni ugonjwa usioponyeka lakini
watumishi wa mungu walikuwa wanauwezo wa kuwaponya watu kutokana na ugonjwa huu
kilichokuwa kinahitajika ni imani na kutii tu, kwa mfano naaman aliyekuwa
unaukoma lakini alipokea uponyaji. Soma 2wafalme 5: 8-19 na pia soma mathayo
8:1-4 yesu anaponya ukoma.
Japo kwa
jambo la kushangaza na la kuhuzunisha ni kuwa huu ugonjwa hadi sasa upo toka
enzi za akina musa hadi leo lakini je ni kwamba dawa za kuuponya huu ugonjwa
haijapatikana? Imepatikana na ipo sema watu hawatilii maanani. Wako wapakwa
mafuta wa bwana ambao wamepewa karama ya kuponya wanaponyesha huu ugonjwa,
kadhalika na ukiwmi pia wako watumishi wapakwa mafuta wa bwana waliopewe karama
ya uponyaji wako kukusaidia leo. Kama huu ukoma ambao ulikuepo toka enzi hizo
za akina musa unawezekana kuponyeka kwanini watu wasiamini kuwa hata ukimwi
waweza kupona? Ukimwamini mungu na kuyashika maagizo yake na kutii hakika
utapona.
Mfano wa
mwanamke aliyetoka damu kwa miaka kumi na miwili biblia inatuambia kuwa yule
mwanamke aliazimia kuwa akiweza kushika tu upindo wa vazi aliyovaa yesu hakika
atapona na kweli alivyofanya hivyo kwa imani yake kuu aliyokuwa nayo alipokea
uponyaji muda ule ule soma mathayo 9 : 20 - 22; pia kwenye marko 5: 25-34; sasa
je wewe wawezaje kukata tamaa na kushindwa kumwammini yesu kuwa kwa jina lake
tu magonjwa yanatoweka hayatakuwa na nafasi tena ndani ya maisha yako utapona
na utakuwa na nguvu na mwenye afya tele.
Kama bado
haujaambukizwa acha njia zako mbaya mtafute yesu shika maagizo yake na
kuyatenda hakika atakuponya na hili janga wewe na familia yako na watu wa
nyumbani mwako. Ingawa unaweza kuwa mwaminifu, waweza kuwa unatenda yaliyo mema
kwa mtazamo wa kibinadamu lakini bado ukaupata huu ugonjwa kwa njia nyingine
kwa mfano katika ajali kama ya gari, pikipiki au njia yoyote ile nk. (unajua
kuwa maambukizi waweza pata kwa njia nyingi si kwa kuzini tu japo kuzini ndio
njia kubwa ya maambukizi haya ya virusi vya ukimwi). Lakini ukimtegemea mungu
na kukubali kuwa yesu alikufa msalabani kwa ajili yako na kuyatenda yote aliyokuamuru, hali hii
haitakupata wewe na familia yako kwa ujumla na hata hutaacha wanao yatima bali
utaishi hadi miaka mia na ishirini na utakufa ungali ukiwa na nguvu zako.
Yesu
alifanya miujiza mingi ya uponyaji na hata sasa bado anafanya kwani anawatumia
watumishi mbalimbali kufanya kazi aliyoianzisha kinachoturudisha nyuma ni
kutokutilia maanani na imani kuwa haba kama nilivosema hapo juu. Watu tumekuwa
na kiburi tukidhani kuwa wanayofanya watumishi wa mungu ni ya uongo lakini mimi
nakusihi leo hebu mwamini yesu halafu utaona matunda yake na hakika hautajuta.
Soma mistarii hii ikusaidie kwa habari ya imani katika uponyaji mathayo 8 : 5-13;
mathayo 8 : 14-17;
Mathayo 9 :
27 - 31 n.k.
Mwamini yeye
leo mtumainie bwana peleka haja zako kwake naye atatenda, atakushindia na pia
atakuponya, usikate tamaa usihangaike ikuze imani yako kwa kusikiliza na kusoma
neno la mungu mara kwa mara kwani biblia inasema hivi "imani chanzo chake
ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo"
Warumi 10 :
17 kisha mweleze shida yako peleka haja zako kwake naye atafanya. Pia yesu
anasema hivi, hata ukiwa na imani kiasi cha punje ya haradali ukisema mlima huu
ung'oke mahali hapa uende kule, nao utang'oka. Hivyo basi na uponyaji wako
unahitaji imani yako kidogo tu kama punje ya haradali kwa yesu kuwa anaweza
kukuponya nawe utapokea uponyaji. Tumwamini yeye tuuone mkono wa bwana ukitenda
ndani ya maisha yetu.
MAOMBI, UPONYAJI NA UREJESHAJI
(yakobo
5:13-20)
Somo limekaa
kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza
kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya
barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye
>>nguvuyamungublog.blogspot.com>>kwa lugha ya kiswahili na kwa
lugha ya kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile kifaransa, kijerumani.
Omba kwa ajili ya uongozi wa roho mtakatifu unapojifunza.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼

0 coment�rios: