HATUA ZA NAMNA YA KUMUOMBEA MTU ILI AMPOKEE ROHO MTAKATIFU
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Hapa naweza
kupendekeza hatua tatu za kichungaji za kuweza kumuombea mtu akampokea Roho
Mtakatifu aina hizi za maombi ni pamoja na mahojiano, kuingia katika maombezi,
na Muongozo kabla ya maombi
1. Hatua za mahojiano.
Endapo
utatumia njia hii ya majojiano latika kutaka kumuombea mtu ujazo wa Roho
Mtakatifu unapaswa kuzingatia maswala muhimu manne kwanza ikiwa ni pamoja na
kustawisha uhusiano mwema na muhitaji yaani kutafuta kujenga mahusiano naye
kisha utatakiwa kumshawishi na kuikuza imani ya muhitaji na tatu unatakiwa
kuelewa au kugundua hali halisi ya muhitaji kuwa ana kiu kiasi gani na mwisho
utamfundisha muhitaji kipi anatakiwa akifanye ili apokee Roho Mtakatifu.
Kustawisha uhusiano hili ni kusudi la kwanza
kabisa katika kifikia hatua ya kumpokea Roho unapaswa kuwa umemfahamu vema na
kama yeye hakufahamu ni vema na yeye akakufahamu unaweza kuzungumza jambo
ambalo litamfanya yeye kujisikia vema na salama, kisha mpe nafasi ya kujieleza
kila anachokihitaji msikilize vema kila anachokieleza na wakati wote tumia jina
lake kila unapowasiliana naye.
Chochea na kukuza imani yeke ni muhimu sana
kjaribu kuinua imani ya muhitaji na kuichochea unaweza kumueleza jinsi
unavyofurahishwa na jinsi alivyoitikia swala la kuja kumpokea Roho Mtakatifu,
umefanya uamuzi ulio sahii sana unaweza pia kumuhakikishia kuwa hii itakuwa
siku ya kihistoria katika maisha yake na kuwa Mungu ana kitu maalumu sana
kwaajili yake na inawezekana kuwa muhitaji
anaweza asiwe na ujuzi kuhusu hilo lakini kwa ujumla linamuandaa katika
kufungua moyo wake kumpokea Roho Mtakatifu.
Mafundisho wakati huu sasa mtenda kazi wa
Bwana utatakiwa kufanya maswala ya msingi mawili moja likiwa ni kuchochea imani
ya muhitaji katika moyo wake na kumleta sasa katika uelewa halisi wa nini
anatakiwa kukifanya na nini kitatokea
wakati tendo la kujazwa Roho linapotokea kuichochea imani ya muhitaji ni pamoja
na kumuhakikishia kuwa hii ni ahadi ya Mungu na kuwa Mungu yuko tayari na kuwa
kama amezaliwa mara ya pili Mungu atamjaza kwa Roho wake mkumbushe swala la
kuomba Luka 11;9-10 na kuwa anapaswa kuamini na kutegemea kuwa atapokea na
atanena kwa lugha nyingine kama matokeo ya kuwa Roho anamuwezesha.Mkumbushe
kujiandaa na kuwa anapaswa kutambua kuwa kujazwa Roho sio swala gumu na kuwa ni
jambo la kawaida kwa wakristo na kuwa hatapokea roho nyingine bali Roho halisi
wa Mungu Ukimuomba Munu baba mkate hawezi kukupa jiwe na kuwa kujazwa Roho ni
rahisi tu ni kama kupuliziwa pumzi Yohana 20;22. Mkumbushe pia kuwa Roho huyo
hayuko mbali kwani alishakaa ndani yake tangu siku aliyookoka kisha muhitaji
anapaswa kujua kuwa nini kitatokea hivyo mwambie kuwa tutaomba pamoja kisha
nitakuongoza katika maombi yatakayokusaidia kubatizwa katika Roho Mtakatifu
tunachotakiwa ni kumuomba Mungu aje na kutubatiza kwa Roho wake Mtakatifu na
Mungu ni lazima atatusikia kwa sababu tunaomba sawa na mapenzi yake 1Yohana
5;14 na wakati huu ni muhimu sana kuwa na usikivu mkubwa kwa Roho Mtakatifu na
utahisi ujio wake. Na kisha baada ya hilo itakupasa kuchukua hatua ya imani ya
kumpokea Roho na kisha nitakuombea na utapokea Marko 11;24 na mara utakapopokea
utasema kwa lugha mpya linapotokea hilo usiogope endelea kujiachilia katika
neema yake. Muulize kama ana swali lolote na kama hakuna ingieni katika maombi.
2. Hatua ya Maombezi.
Katika hatua
ya maombezi utapaswa kuzingatia maswala muhimu mawili utamuongoza muhitaji
kuingia katika maombi ya kumuomba Mungu amjaze kwa Roho Mtakatifu na pia
utainua imani yake kwa kumuongoza kumpokea Roho Mtakatifu.
Muongoze muhitaji katika kuomba kama
unavyomuongoza mtu kumpokea Yesu sasa unaweza kumuongoza muhitaji katika
kumuomba Roho Mtakatifu Bwana mwema nimekuja mbele zako sasa na mbele za Roho
wako sasa sina ninalohitaji katika maisha yangu sasa zaidi ya ahadi yako
nategemea utanihurumia utanipa kibali na utanijaza kwa Roho wako niwezeshe
nijaze kwa Roho wako mwambie Bwana nijaze kwa Roho wako jiachilie kwake paaza
sauti omba tarajia uwepo wake sasa.
Muongoze muhitaji katika hatua ya imani
anaweza kuinua mokono yake juu na kuomba kwa imani nawe waombee wapokee Roho sasa na unapoiona
imani yao iko juu amuru wapokee sasa atahisi uwepo wa Mungu kwa ndani sana na ataanza kunena kwa lugha bila kutumia
akili kunena huko hakutakuwa kwa kulazimisha kunakuja tu kama matokeo ya Roho
wa Mungu kuja ju yake na inapotokea watie moyo kuwa wasiogope bali waendelee
kujiachia katika uwepo wa Mungu mwili nafsi na roho na anaponena kwa lugha tia
moyo ili waendelee waache kwa muda waendelee kunena kwa lugha ni raha iliyoje kwani
wakti huu sasa unajua kuwa Mungu amemuhudumia muhitaji.
3. Muongozo kabla ya maombi.
Ni muhimu
sana kufanya au kutoa ushauri kabla ya maombi kwa muhitaji kama amekwisha
kujazwa na Roho Mtakatifu utampa aina ya ushauri na kama hajajazwa pia atahitaji
aina moja ya ushauri
Kama amepokea Ujazo wa Roho Mtakatifu na
kunena kwa lugha ushauri ufuatao utamfaa sana Mweleze kuwa kumpokea Roho
hakujaishia hapo kwani jukumu kubwa la kumpokea Roho Mtakatifu ni kwa kusudil a
kumtumikia kwa hivyo huu sio mwisho bali ndio mwanzo Mungu sasa ataanza
kukutumia kwa nguu sana unaposhuhudia unapoomba na kuombea wengine kwa msingi
huo una wajibu wa kushuhudia wengine na kuendelea kuomba katika Roho haya
yatakupa nguvu kubwa kila siku katika
maisha yako pia usisahau kuendelea kujisomea Neno la Mungu.
Kama muhitaji ahajapokea unapashwa kumpa ushauri huu kwamba usikate
tamaa kwa sababu hukumpokea Roho wakati huu kumbuka kuwa ahadi ya Yesu Kristo
ni dhahiri na ni kwa kila mtu aliyempokea Luka 11;10 kwa hivyo endelea komba na
kutafuta na utapokea kama Mungu apendavyo hata ukiwa popote Luka 11;9
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: