SURA YA TATU: MAMBO YA MSINGI YA KUYAZINGATIA
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Tunapokwenda
kumalizia kijitabu hiki naona ni muhimu nikikukumbusha kwa ufupi maswala matatu
ya kuyazingatia unapomuongoza mtu kumpokea Roho Mtakatifu
1. Ni muhimu kuwa na ujuzi wa kile Biblia
inachokisema kuhusu somo hili
Ni muhimu
kufahamu kuwa kama mtu anapenda kusaidia wengine kwa kusudi la kumpokea Roho
Mtakatifu anapaswa kufahamu na kutafuta kujua kwa undani kuhusu somo la Roho
Mtakatifu na hivyo atapaswa kusoma neno la Mungu hususani kitabu cha Matendo ya
mitume ili kuona somo hili kivitendo na pia anaweza kusoma Vitabu vingine
vizuri vinavyozungumzia kwa undani kuhusu Roho Mtakatifu kwa kadiri mtu
anavyomjua Roho Mtakatifu na kazi zake
na utendaji wake katika maisha ya waamini na umuhimu wake ndivyo anavyokuwa msaada
mkubwa na Baraka katika swala hili.
2. Usikubali uvivu wa kiroho ukuharibie
wajibu wako
Kama
unasaidia watu kumpokea Roho Mtakatifu ni lazima uhakikishe kuwa unaacha uvivu
wa Kiroho kwa sababu sio kazi rahisi kuombea wengine kumpokea Roho Mtakatifu na
ndio maana wengine wanaona aibu kufundisha somo hili na kutokujishuhulisha
kuwafanya wengine wapokee Roho Mtakatifu na kama una tabia hii unapaswa kutubu,
tubia uvivu wa Kiroho ulionao na jitoe kwa ukamilifu katika huduma na Mungu
atakutumia
3. Laizima ufikie ngazi ya kujihusisha
sana.
Mwisho
msomaji wangu ni muhimukufahamu kuwa kuombea wengine kumpokea Roho Mtakatifu
kunaambatana na kufikia ngazi ya kujihusisha
sana na kutaka wengine wajazwe hili ni swala linalohitaji kujituma na
kumaanisha na kuhurumia na kutia moyo wengine kupokea Roho wa Mungu uwe na
Bidii katika kuomba na hapo utakuwa na mafanikio, sasa tunafikia mwisho wa somo letu la jinsi
ya kumuongoza mtu kupokea Roho Mtakatifu Ni matumaini yangu kuwa sasa utajiweka
wakfu katika kazi hii muhimu kama nini na hii ndio kiu kubwa tuliyonayo
kuwasaidia watu wajazwe na kuishi katika uwepo na nguvu za Roho wake siku zote
za maisha yao Mungu akubariki ni matumaini yangu somo hili litakuwa Baraka na
kuwa utalitendea kazi na kulifanya halisi katika maisha yako ya huduma na kuwa
tangu sasa utakuwa ukiwafanyia watu maombezi ya kumpokea Roho Mtakatifu bila
woga ubarikiwe na Bwana Neema yake iwe juu yako Amen!.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: