MAMBO MHIMI AU KUPIGANA VITA YA KIROHO KWA MAOMBI YA VITA.
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
ANGALIA KWANZA MAMBO HAYA
1. Kuomba
kwa imani na utakatifu
Waebrania
11:6 '' Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale
wamtafutao.''
Hautakiwi
kuomba kwa imani tu bali omba kwa imani ukiwa msafi kwa MUNGU.
Mathayo 5:8 '' Heri wenye moyo safi; Maana hao
watamwona MUNGU. ''
Wenye moyo
safi ni watakatifu waliosafishwa kwa damu ya YESUY KRISTO, hao ndio wakiomba
kwa imani wanaweza kumwona MUNGU vyema katika maisha yao.
Waebrania 12:14 '' ....... na huo utakatifu,
ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; ''
Yaani pasipo
imani huwezi kumwona MUNGU akikutendea muujiza.Yaani pasipo imani huwezi
kupokea muujiza wako kutoka kwa MUNGU.
Jambo la
pili hapo hapo ni kwamba pasipo utakatifu huwezi kumwona MUNGU maana yake
huwezi kuingia uzima wa milele na maana ya pili pasipo utakatifu huwezi kumwona
MUNGU akikutendea muujiza.
Hivyo wewe
Muombaji shika kanuni hiyo ya kiroho kwamba ''Pasipo imani siwezi kumpendeza
MUNGU na pasipo utakatifu siwezi kumwona MUNGU''
Kumbuka
Biblia inasema katika Yohana 1:18 '' Hakuna mtu aliyemwona MUNGU wakati wo
wote; MUNGU Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba(MUNGU), huyu ndiye
aliyemfunua.''
Kumbe Hakuna
mwanadamu awezaye kumwona MUNGU kwa sura lakini Mathayo 5:8 inasema wenye moyo
safi yaani watakatifu watamuona MUNGU, Yaani watakatifu wataingia uzima wa
milele na kumwona MUNGU lakini pia watakatifu watasikiwa na MUNGU na kutendewa
muujiza.
Ndio maana leo unaweza ukasikia mtu nasema
kwamba ''Hakika nimemuona MUNGU'' Je amemuonaje?
Jibu ni
kwamba ametendewa muujiza na MUNGU yaani amemuona MUNGU kupitia alichokifanya
MUNGU kwenye maisha yake.
2. Kuomba
katika jina la YESU KRISTO.
Kuomba
katika jina la YESU KRISTO inajumuisha mambo mawili.
A. Kuomba
ukilitaja na kulitegemea jina la YESU ili ushinde.
Yohana 14:13
''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu(YESU KRISTO), hilo nitalifanya, ili
Baba(MUNGU) atukuzwe ndani ya Mwana. ''
B. Kumtii
YESU KRISTO na Neno lake.
Kumtii YESU
KRISTO ni kibali cha kupokea hitaji lako.
Yohana 15:16
''Si ninyi mlionichagua mimi(YESU), bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami
nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo
lote mmwombalo Baba(MUNGU0 kwa jina langu awapeni. ''
Ndio maana
Biblia inasema kila alitajaye jina la YESU KRISTO na auache uovu.
2 Timotheo
2:19 ''Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana
awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana(YESU) na auache
uovu.''
3. Kuomba
katika ROHO MTAKATIFU.
Kuomba
katika ROHO MTAKATIFU inajumuisha mambo mawili.
1. Kunena
kwa lugha katika ROHO MTAKATIFU.
Marko 16:16-17 "Aaminiye na kubatizwa
ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;
kwa jina langu watatoa pepo; WATASEMA KWA LUGHA MPYA;"
2. Kuomba
kwa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU au kujulishwa na ROHO MTAKATIFU.
Yuda 1:20 "Bali ninyi, wapenzi,
mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO
MTAKATIFU,"
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: