Jinsi Ya Kumpokea Roho Mtakatifu
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDR7POsdR4YQsemk6h1BRJoRodpReXytbLo-TqBuZB06BXsKzAweUB1Ix9NpzhFFmQ1T1YozD_ftvjW1YCiG12X4qHO7k5iFY6p-O3v5kwf1vADnKQSNkep-1HIVpP-4VAyZWONYlYldw/s400/Holy+spirit.gif)
Kabla ya
kujadili kuhusu hatua za kumuongoza mtu anayetaka kubatizwa katika Roho
Mtakatifu kwa mara ya kwanza ni muhimu kwetu kuzingatia maswala muhimu
yafuatayo. Kwanza ni nani anaweza kujazwa na Roho Mtakatifu, Pili ni nani
anaweza kuomba na wengine kumpokea Roho Mtakatifu na Tatu Mambo yanayoambatana
na kumpokea Roho Mtakatifu.
Kwanza Ni
nani anaweza kujazwa Na Roho Mtakatifu
Roho
Mtakatifu ni ahadi ya Mungu Baba na inaweza kupokewa na mtu yeyote aliyezaliwa
mara ya pili yaani aliyeokoka, hili ni jambo la msingi. Kwa msingi huo kupokea
Roho Mtakatifu sio swala la wakristo waliofikia ngazi Fulani ya kiroho au
waliookoka muda mrefu a kufikia ukomavu Fulani wa kiroho wala sio kwa daraja la
watu Fulani muhimu katika dhehebu Fulani ni ahadi ya Mungu kwa wakristo wote
wamjiao Bwana kwa kila kizazi Matendo ya Mitume 2;17-18,38-39.
Pili Ni nani
anaweza kuomba Na wengine kumpokea Roho Mtakatifu
Kumbuka kuwa
swala la kuombea wengine kumpokea Roho Mtakatifu pia sio la watu Fulani maalumu
hili ni la kila mtu ambaye amekwisha jazwa nguvu na kumpokea Roho Mtakatifu na
sharti la kutaka kuwaombea wengine ujazo wa Roho Mtakatifu ni kutamani kuona
wengine wakipokea ahadi hii yenye Baraka na kufurahia kuona wengine
wakibarikiwa na kutumiwa na Mungu Matendo 8;14-17.
Mambo
yanayoambatana na kumpokea Roho Mtakatifu.
Ni muhimu
kwa kila mtenda kazi kuwa na ufahamu kwamba kuna maswala matano muhimu
yanayohusika kama ishara ya mtu kumpokea Roho Mtakatifu maswala hayo ni shauku
au hamu, Imani, maombi, utii, na kujiachilia katika neema ya Mungu.
1. Shauku au Hamu.
Biblia
inakazia umuhimu wa kuwa na kiu au shaku au hamu Biblia inasema “Heri wenye
njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa” Mathayo 5;6, mtu mwenye njaa na
kiu humtafuta Mungu kwa Bidii na kila unapomtafuta Mungu kwa bidii hupatikana
Yeremia 29;13,”Nanyi mtanitafuta na kuniona
mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” Tafuteni nanyi mtaona Luka 11:9 Mtu
awaye yote mwenye kiu na hamu na shauku na kuvumilia katika kutamani kuendelea
kujazwa na nguvu za Roho Mtakatifu atapewa, kwa hiyo kiu na hamu au shauku ni
ya Muhimu sana.
2. Imani.
Imani ni
nguzo ya msingi na muhimu katika kupokea nguvu za Roho Mtakatifu au kiu
chochote kutoka kwa Mungu, Paulo anawakumbusha wakristo wa Galatia kuwa
walimpokea Roho Mtakatifu kwa imani na sio kwa kutokana na matendo ya sheria ni
kwa kuamini Wagalatia 3;2 Yesu alisema yeyote Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena mito ya maji
yaliyo hai (yaani Roho Mtakatifu) atatiririka ndani yake Yohana 7;38 kwa msingi
huo ni wajibu wa kila mtu anayetaka kuwaombea wengine ujazo wa Roho Mtakatifu
kuwapandisha wapokeaji wake imani
3. Maombi.
Roho
Mtakatifu hutolewa kama jibu la maombi yanayoambatana na imani, Yesu alisema
ombeni nanyi mtapewa Luka 11;9, sehemu nyingine alifundisha akisema kila
muombalo aminini ya kuwa limekuwa lenu Marko 11;24-25, Kumbuka kuwa wakati Yesu
alipokuwa anaomba ndipo Roho alipompaka mafuta Luka 3;21-22, ni jambo kama hilo
liliwatokea wanafunzi siku ya Pentekoste walikuwa wamejifungia wakiomba Matendo
1;14, Kabla Paulo mtume hajajazwa Roho alikuwa na Muda wa kuomba Matendo 9;11
kwa msingi huo kila mtu anayetaka kujazwa na nguvu za Roho Mtakatifu anapaswa
kuomba kwa bidii na kwa sauti kubwa.
4. Utii.
Moyo wa utii
ni wa muhimu sana katika kumpokea Roho Mtakatifu, Petro alisema Mungu anampa
Roho Mtakatifu kwa wote wamtiio Matendo 5; 32, alikuwa akizungumza kuhusu wale
watakaomtii Mungu na kuiamini injili yake Mstari 29-32 na kusudi la msingi la
kumpokea Roho Mtakatifu pia ni kwaajili ya kushuhudia Matendo 1;8 na Mungu Yuko
tayari kumpa nguvu kila mtu ambaye yuko tayari kwaajili ya kazi yake na kutii
agizo kuu.
5. Kujiachilia katika neema ya Mungu.
Kujiachilia
kwa Mungu au kujinyenyekeza ni moja ya hatua nyingine muhimu katika kumpokea
Roho Mtakatifu, Kama ilivyo kwa mtu anayebatizwa katika maji anapaswa
kujinyenyekeza kwa Mchungaji anyembatiza, Kujazwa kwa Roho Mtakatifu nako
kwahitajiwa kwa mtu kujiachilia katika neema ya Mungu ni lazima ukubali kufuata
maelekezo ya Bwana huku ni kujiachia Mwili nafsi na roho Warumi 6:13, 12:1 ni
kwa kupitia kujitoa na kujinyenyekeza katika neema yake ndipo Roho wa Mungu
anachukua nafasi na hatimaye kukuwezesha kuzungumza kwa lugha.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: