Katika maombi ni muhimu sana kujua mambo yafuatayo.
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
1. Kuomba kwa
imani na utakatifu
Waebrania
11:6 '' Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale
wamtafutao.''
Hautakiwi
kuomba kwa imani tu bali omba kwa imani ukiwa msafi kwa MUNGU.
Mathayo 5:8 '' Heri wenye moyo safi; Maana hao
watamwona MUNGU. ''
Wenye moyo
safi ni watakatifu waliosafishwa kwa damu ya YESUY KRISTO, hao ndio wakiomba
kwa imani wanaweza kumwona MUNGU vyema katika maisha yao.
Waebrania 12:14 '' ....... na huo utakatifu,
ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; ''
Yaani pasipo
imani huwezi kumwona MUNGU akikutendea muujiza.Yaani pasipo imani huwezi
kupokea muujiza wako kutoka kwa MUNGU.
Jambo la
pili hapo hapo ni kwamba pasipo utakatifu huwezi kumwona MUNGU maana yake
huwezi kuingia uzima wa milele na maana ya pili pasipo utakatifu huwezi kumwona
MUNGU akikutendea muujiza.
Hivyo wewe
Muombaji shika kanuni hiyo ya kiroho kwamba ''Pasipo imani siwezi kumpendeza
MUNGU na pasipo utakatifu siwezi kumwona MUNGU''
Kumbuka
Biblia inasema katika Yohana 1:18 '' Hakuna mtu aliyemwona MUNGU wakati wo
wote; MUNGU Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba(MUNGU), huyu ndiye
aliyemfunua.''
Kumbe Hakuna
mwanadamu awezaye kumwona MUNGU kwa sura lakini Mathayo 5:8 inasema wenye moyo
safi yaani watakatifu watamuona MUNGU, Yaani watakatifu wataingia uzima wa
milele na kumwona MUNGU lakini pia watakatifu watasikiwa na MUNGU na kutendewa
muujiza.
Ndio maana leo unaweza ukasikia mtu nasema
kwamba ''Hakika nimemuona MUNGU'' Je amemuonaje?
Jibu ni
kwamba ametendewa muujiza na MUNGU yaani amemuona MUNGU kupitia alichokifanya
MUNGU kwenye maisha yake.
2. Kuomba
katika jina la YESU KRISTO.
Kuomba
katika jina la YESU KRISTO inajumuisha mambo mawili.
A. Kuomba
ukilitaja na kulitegemea jina la YESU ili ushinde.
Yohana 14:13
''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu(YESU KRISTO), hilo nitalifanya, ili
Baba(MUNGU) atukuzwe ndani ya Mwana. ''
B. Kumtii
YESU KRISTO na Neno lake.
Kumtii YESU
KRISTO ni kibali cha kupokea hitaji lako.
Yohana 15:16
''Si ninyi mlionichagua mimi(YESU), bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami
nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo
lote mmwombalo Baba(MUNGU0 kwa jina langu awapeni. ''
Ndio maana
Biblia inasema kila alitajaye jina la YESU KRISTO na auache uovu.
2 Timotheo
2:19 ''Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana
awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana(YESU) na auache
uovu.''
3. Kuomba
katika ROHO MTAKATIFU.
Kuomba
katika ROHO MTAKATIFU inajumuisha mambo mawili.
A. Kunena
kwa lugha katika ROHO MTAKATIFU.
Marko 16:16-17 "Aaminiye na kubatizwa
ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;
kwa jina langu watatoa pepo; WATASEMA KWA LUGHA MPYA;"
2. Kuomba
kwa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU au kujulishwa na ROHO MTAKATIFU.
Yuda 1:20 "Bali ninyi, wapenzi,
mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO
MTAKATIFU,"
Hayo Mambo
matatu niliyokufundisha hufanya kazi pamoja na ni kitu kimoja cha kuleta majibu
sahihi ya maombi ya Mtu.
Mimi Binafsi
kwa kupitia kuomba mara kwa mara na kumsikiliza ROHO MTAKATIFU nimegundua
mifumo kadhaa ya maombi ambayo mteule wa KRISTO
anaweza akaomba kutokana na ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.
Mifumo
miwili katika mingi ni hii;
1. Kuhusika na
MUNGU tu.
Hapa unaomba
kwa MUNGU bila kukemea wala kuamuru mamlaka za giza ziachane na wewe. Humtaji
mtu wala humfukuzi adui wewe unamwita tu MUNGU ili aje akusaidie.
Kwa maombi
hayo kama ni katika ROHO MTAKATIFU hakika MUNGU atawapiga maadui zako na
kuwafukuza hata kama hujawataja.
Hapa MUNGU
atakuletea msaada kwa sababu umemhitaji yeye.
Hapa MUNGU
anaweza kutuma malaika au watu kukusaidia japokuwa hukuita watu wakusaidie ila
umemwita MUNGU ili akusaidie.
2 Samweli
22:1-7 ''Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA
alipomwokoa mikononi mwa adui zake zote, na mkononi mwa Sauli; akasema, BWANA ndiye jabali langu, na ngome
yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu;
MUNGU wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu
wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa; Hivyo
nitaokoka na adui zangu. Maana mawimbi
ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu
zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA,
Naam, nikamlalamikia MUNGU wangu; ''
2.Kutumia
mamlaka ya KRISTO YESU iliyoko ndani yako.
Maombi haya
ni maombi ya vita.
Wafilipi
2:13 ''Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda
kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.''
Ni maombi ya
kumwamuru shetani akuachie hata kama hataki.
Kwa maombi
haya MUNGU atatuma Malaika au Neno na maadui zako watakimbia.
Tofauti ya
maombi haya ya maombi ya kuhusika na MUNGU tu ni kwamba hapa unawataja wabaya
wako na kuwaelekeza wafanyeje, kama wakimbie hakika watakimbia na kama kazi zao
zife hakika hizo kazi zao cha kichawi zitakufa.
Yeremia 1:10
''angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na
kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda. ''
Yaani maombi
ya kwanza ni maombi ya kumsihi MUNGU na maombi ya pili ni maombi ya wewe
kutumia mamlaka ya YESU KRISTO iliyoko ndani yako.
Katika
maombi haya wewe ndio unaamuru iweje.
Katika
maombi haya unaweza kulisemesha tatizo lako ili lisikie na kuondoka na hakika
linaondoka.
Unaweza
kuusemesha ugonjwa ili ukuachie na hakika ugonjwa huo ukakuachia.
Maombi haya
mhusika ni wewe maana unatumia mamlaka ya MUNGU wako iliyo katika KRISTO YESU.
Waefeso
6:10-13 '' Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana(YESU) na katika uweza wa
nguvu zake. Vaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme
na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza
kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.''
Maombi haya
hutuonyesha kwamba tuna mamlaka ndani yetu ambayo MUNGU wetu aliyetuokoa
ametupa.
Baada ya
hayo sasa naingia katika kiini cha ujumbe wangu wa leo.
Sasa ndio
tunaingia sasa katika kanuni au njia za kupigana vita ya kiroho kwa maombi.
Kuna njia
kadhaa Biblia inazitaja kama njia za
kupigana vita ya kiroho kwa maombi. Husika nazo itakusaidia.
1.
Kukanyaga.
Luka 10:19
'' Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui,
wala hakuna kitu kitakachowadhuru.''
Mhusika hapa
sio MUNGU kukanyaga nguvu za giza ili zisifanye kazi bali mhusika ni wewe
kwamba ukanyage hizo nguvu za giza.
Bwana YESU
amekupa mamlaka ya kukanyaga hivyo itumie mamlaka yako hiyo kukanyaga nguvu za
giza.
Maana yake
ni kwamba usiwaruhusu mawakala wa shetani kukushambulia, hivyo kabla hawajainua
silaha zao wewe muombaji unayejitambua unakuwa umeziharibu silaha zao na hata
wao wenyewe.
Kwenye ndoto
au maono wakati mwingine huwa
unajulishwa mipango ya kipepo kukuhusu ili unyamazishe mipango hivyo ya shetani
iliyokusudiwa juu yako.
Mfano unaota
nyoka anakufukuza. Tukio hilo linakuwa wakati mwingine halijatokea yaani
linakuwa ndio liko katika kutekelezwa. MUNGU kwa upendo wake na neema yake
amekufunulia ili umkanyage huyo nyoka na kunyamazisha kilichokusudiwa kibaya
ili kikupate. Ziada kuhusu mfano huo ni kwamba Nyoka anaweza akawakilisha
majini, uchawi, mizimu, shetani mwenyewe, uganga wa kienyeji, kutumia mapepo na
nyoka ni roho ya uongo. Hivyo unaweza ukapambana na hayo niliyokutajia ambayo
wewe kwenye ulimwengu wa roho umemuona nyoka.
Ili ukanyage kazi za shetani timia katika haya
itakusaidia.
A. Kwanza unatakiwa uwe unaishi maisha
matakatifu katika KRISTO YESU.
1 Petro 1:15
'' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika
mwenendo wenu wote; ''
B.
Unatakiwa kumwamini MUNGU kwamba katika yeye yote yanawezekana.
2 Nyakati
20:20 '' ............... mwaminini
BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo
mtakavyofanikiwa. ''
C, Uombe kwa imani katika jina la YESU KRISTO.
Yakobo 1:6-8
'' Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama
wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana
mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa BWANA. Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake
zote. ''
Pia ujue
kutumia mamlaka za kiroho za MUNGU za kukushindia.
Mamlaka hizo
ni;
1. Jina la
YESU KRISTO.
Yohana 14:14 ''Mkiniomba neno lo lote kwa jina
langu, nitalifanya.''
2. Damu ya
YESU KRISTO.
Ufunuo 12:11
'' Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda
wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. ''
3. Neno la
MUNGU
Zaburi
107:20 ''Hulituma neno lake, huwaponya,
Huwatoa katika maangamizo yao.''
4. Nguvu za
ROHO MTAKATIFU.
1 Yohana 4:4
'' Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda(shetani), kwa
sababu yeye aliye ndani yenu(ROHO MTAKATIFU) ni mkuu kuliko yeye aliye katika
dunia(Shetani). ''
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: