HUDUMA YA UKOMBOZI WA FAMILIA NA MIJI
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
Lengo la
maelezo haya tunayokupa ni kukuandaa kimaombi,maombi ya mwendelezo wa huduma ya Madhabahu
tuliyoijenga hapo nyumbani kwako.
Ninaamini kwamba mwisho wa maombi haya na yatakayoendelea kulingana na
ufunuo tuliopewa na Bwana kupiti (matayo1:23b.Nao watamwita jina lake
Imanuel;Yaani Mungu pamoja nasi).Tunahitaji hilo neno litimie kwako la Mungu
kuwa pamoja na mji,familia na mazingira yako.
Safari ya
somo letu la ujenzi wa madhabahu umeanzia mbali sana toka katika Ukombozi wa
ardhi ambo chazo chake ni katika mwanzo (3:14 – 19) baada ya Anguko la Adamu.
Tunaona ardhi ikilaaniwa maana yake ni uzima/uwepo wa Mungu ukiondoka katika
ardhi/makazi na mauti ikitawala.
Kutokana na
Anguko hili ambalo halikuwa katika mpango wa Mungu, kwa nyakati mbalimbali
Mungu alionekana akijidhihirisha kupitia watu tofauti tofauti kwa nyakati
mbalimbali kama vile Nuhu, Ibrahimu, Taifa la Israeli na mwishowe kupitia
Kristo Yesu Bwana.
Kupita Nuhu
na familia yake tunamwona Mungu akifunua ule mpango aliokuwa ameuweka Maishani
mwa Adamu ya kumiliki na kutawala viumbe vyote (mwanzo 1:26-28), Pia tunaona
Mungu akibatilisha laana na kurejesha majira na nyakati katika Nchi (ardhi)
(Mwanzo 8:21– 22,).
Agano ambalo
Mungu aliliweka kupitia Nuhu, halikuishia kwa Nuhu na watoto wake ila pia uzao
utakao kuja baada yao (mwanzo 9:8-12), wanyama, ndege, pamoja na Nchi (ardhi).
Kwa upande
wa Ibrahimu, yeye pia tunajifunza mambo kadha wa kadha, jambo la muhimu
tutakalo lichukuwa kwake ni lile la ujenzi wa madhahabu katika kila eneo ambalo
aliweka hema/makazi /Nyumba yake Mwanzo 12:7-8).
Wapendwa,
naomba niwakumbushe maana ya Madhahabu.Madhabahu ni mahali
(Kutoka25:8)/eneo/nafasi/makazi /msakani/nyumba
(mwanzo28:17)ambayo Mungu anakaa.
Kwa maana
nyingine, Madhabahu inawakilisha uwepo wa Mungu/Miungu fulani katika eneo
walilotengewa.
Hivyo
madhabahu zinawakilisha uwepo wa Mungu hapa duniani anayeishi/kaa katika
Ulimwengu wa Roho
Madhabahu ni
Nyumba /Nyumba/kiti
(ufunuo2:13)/makazi/eneo/anapoishi Mungu.
Sasa kwa
kuwa madhabahu ni Nyumba /makazi/ eneo/ maskani ya Mungu, inapojengwa nyumbani
Mwako/ kwenye makazi yako/mji wako kinachotokea ni kwamba Mungu aliyejengewa
hiyo madhabahu anatoka katika ulimwengu wa Roho na kuja kuweka/ Kuishi na wewe
katika mji wako/nyumba/familia yako.
Hivyo hiyo Madhabahu inakuwa ni ishara ya
uwepo wa Mungu katika mji wako na Mungu anajifunua kupitia hiyo madhabahu.
Baada ya kupata maana halisi ya madhabahu
basi utafahamu kwamba Ibrahimu alitambua umuhimu wa Mungu wake kuishi naye katika kila mahali alipokwenda lengo ni
kwamba alitambua umuhimu wa uwepo wa Mungu katika maisha yake ya kila siku,
lakini pia alijua siri ya yeye kufanikiwa katiki ulimwengu huu wa mwili na
nyama unaaza katika ulimwengu wa Roho hivyo ni lazima auvute ulimwengu wa Roho
ambao umekamilika kwa kila kitu uje uishi hapa duniani ambapo pana mapungufu ya
kila namna.
Naomba nikufahamishe kwamba hakuna namna
tutakavyoweza kuishi hapa duniani kwa mafanikio na maisha yenye ushuhuda tena
ya ushindi kama hatutakuwa na mfungamano na ulimwengu wa Roho wa Mungu aliye
hai.
Njia itakayokuunganisha wewe uliyeko
katika Ulimwengu wa mwili (dunia) na
ulimwengu wa roho (mbingu) ni madhabahu.
Mahusiano
kati ya mtu aliyeko hapa duniani na Mungu aliyeko Mbinguni yanajengwa kwa
kupitia Madhabahu.
Katika
kitabu cha kutoka 25:1 –8, ili Mungu apate kuishi katikati ya wana wa Israel
aliwaagiza wamfanyie patakatifu. Maana yake wamtengee mahali/wamjengee
nyumba/wamtengenezee kiti cha yeye kuketi/kutawala juu ya Israel wote.
Alichokuwa
anakitaka ni Madhabahu ili aje akae nao na kuishi nao katika maisha ya kila siku.
Tumekwisha
kuwatazama Makundi ya watu wa aina tatu. Makundi mawili yanatabia zinazofanana
ambayo ni Nuhu na familia yake na Ibarahimu na uzao wake.
Tumekwisha
kuwatazama makundi ya watu wa aina tatu.Makundi mawili yanatabia
zinazofanana. Ambayo ni Nuhu na familia
yake pamoja na Ibrahimu na nyumba yake na kundi la pili ni Taifa la Israel.
Katika kundi la kwanza madhabahu zote
walizozifanya ziligusa familia/ndoa na watu, pamoja na maendeleo yao ya kila
siku.
Hawakujenga
kwa nia ya huduma au kisiasa bali ni kwa ajili ya miji na maisha yao ya kifamilia.Makundi haya mawili ndio
yatakayokuwa msingi wa maombi yetu kwani madhahabu zile tulizozijenga,
tulizijenga katika mji/makazi/nyumba/zetu, lengo likiwa ni kwamba Mungu aliye
mbinguni aje aweke makazi katika familia na miji yetu.
Kwamba
tulijifunza aina tatu za Madhahabu wakati wa ujenzi. Tulisema kuna madhahabu ya
udongo kutoka 20:24, Madhahabu ya mawe kutoka 24:4 na Madhahabu ya mti ambayo
tunaipata katika kitabu cha kutoka 27: 1 – 8.
Madhahabu
tuliyoichukuwa ni ile ya mti inayotasfirika katika Agano jipya kama Msalaba wa
Kalvari (Yesu).
Hii
Madhahabu ndiyo tunayotembea nayo na ndiyo msingi wa maombi yetu tuliyoyafanya
kwako.
Kumbuka pia
kwamba katika Msalaba wa Yesu tuliona mambo manne ambayo yalitolewa/yalipelekwa
hapo kama dhabibu na Yesu mwenyewe. Mambo hayo ni:
1. Mwili wake ambao kwetu uliwakilishwa na
Biblia/Neno takatifu (Yohana 1:14)
2. Damu yake
ambayo sisi iliwakilishwa na uzao wa Mzabibu (Luka 22:14 – 20) (Yohana
19:34)
3. Maji ambayo kwetu tuliwakilishwa na chupa
12 za maji (Yohana 19:34) (Yohana 4:10 –14) Wafalme18:33 – 35.
4. Roho wake – ambao sisi tuliwakilishwa na
chupa saba za mafuta (Isaya 11:2 – 3)
Rejea katika
zaburi 50:5 ambao wanasema “Nikusanyieni wacha Mungu wangu waliofanya
Agano/(walionijenga Madhabahu) kwa njia ya sadaka/dhabibu.
Hapa ningetaka ujue kwamba kila
kinachotolewa madhabahuni ni sadaka/na pia sadaka hizo hugeuka kuwa Agano kati
ya aliyetoa na aliyepokea.
Kwa tafsiri hii tutakubalia kwamba Bwana
Yesu alipeleka pale Msalabani (katika Madhabahu yake aliyomjengea Mungu
(madhabahu 27:1-8) dhabibu za aina nne ambazo zote kwa pamoja zinanenwa kuwa
toleo moja lidumulo hata milele (Hebania 10:12 – 13. Lakini huyu alipokwisha
kutoa dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;).
Kama matolea/sadaka /dhabibu hugeuka na
kuwa Agano, basi ndani ya hizi sadaka nne ambazo ni maji, damu, mwili na roho
tutapata agano la maji, Agano la Damu, Agano katika mwili wake na Agano katika
roho wake.
Hivyo Agano
jipya limejengwa na maagano madogo madogo manne ambayo ni:
· Agano katika damu yake Luka 22:14 – 20
· Agano katika Mwili wake Luka 22:14 –
20, Yohana 6:49 – 59
· Agano katika maji yaliyotoka mwilini
mwake Yohana 19:34, Yohana 4:10 – 14.
· Agano katika roho wake Isaya 11:2 – 3.
Isaya 59:21.
Haya ni maagano manne yahayotengeneza
Agano jipya ambalo Yesu Kristo alilifanya pale Kalvari kwa ajili ya ulimwengu
wote.
Ninaamini kwamba umenielewa kwa mafafanuzi
hayo hapo juu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Agano la Maji ya uzima.
Yohana 4:10 – 14 Baadaya mwanamke msamaria
kukutana na Bwana Yesu, tunamwona Bwana yesu akimwambia ''Kama ungejua karama
ya Mungu naye ni nani akuambiaye Nipe maji ninywe,ungelimwomba naye angalikupa maji yaliyo hai.Kama kuna maji ambayo hayakuwepo ulimwenguni ni yale
ambayo Yesu/Mungu aliyatoa katika mwili wake. Baada ya kifo chake pale
msalabani tuna mwona Askari mmoja akienda na kumchoma mkuki ubavuni. ''Lakini
askari mmoja wapo alimchoma ubavu kwa mkuki na mara ikatoka damu na maji''
(Yohana 19: 34).
Haya ndio yale maji ambayo Yesu alikuwa
ameyabeba yaliyo kuwa yamebeba uzima.
Uzima ni zaidi ya uhai , mtu anaweza kuwa
hai lakini asiwe na uzima katika eneo fulani la mwili wake.
Hivyo uzima
ni ile hali ya ustawi/ufanisi/kufanikiwa/afya bora/kuongezeka (Yeremia 17:5 –
10). Vifungu hivi vinaelezea jinsi makundi ya watu wawili wanavyoonekana
kimaisha.
Kundi la
kwanza ni la mtu aliyeko katika laana na matokeo ya maisha yake ambayo ni:
· Ufukara
· Maisha ya ukame
· Ukiwa /mahama
· Uduni /udhaifu n.k
Haya maisha ni maisha ya mtu aliye kata
tamaa kabisa, ni miji iliyosambaratika kabisa. Miji iliyokufa imebaki kuwa
magofu, watu wameicha, hapafai kuishi, maana yake kila kinachofanyika hapa
badala ya kuongezeka vinapukutika na baadaye kufa. Kama ni wanyama wa kufugwa
wanakufa, au hawazai,au wanazaa na watoto wanakufa, ndoa zinavurugika,watu
hawapati mimba,ukiweka mradi unakufa au unakupelekea hasara,magonjwa ya mara
kwa mara na hali kama hizo.
Kundi la pili ni kundi la watu
waliobarikiwa. Kundi hili limefananishwa na mti ambao umepandwa kando ya maji.
Kutokana na uwepo wa maji maisha ya ule mti yalikuwa ni mazuri yenye kupendeza,
ulizaa matunda mazuri na ukawa kama eneo la kusitiri watu kwa kivuli chake
wasipigwe na jua.
Hivyo tumeona maji yanavyoweza kubadilisha
hali ya mmea na kuupelekea katika maisha mengine kabisa.
Kitendo cha Yesu kutuletea maji pale
msalabani alikuwa hatuletei tu maji bali uzima utakao badilisha maisha yetu.
Ndiyo maana aliyatoa yale maji ubavuni ili
yakabatilishe yale maisha ya laana ambayo ilikuwa ikitembea juu ya ardhi na
katika maisha yetu.
Agano hili la maji ya uzima/ Baraka
linapotembea katika maisha yetu,linageuza
hali ya maisha yetu kutoka katika
kundi la yule mtu aliyekuwa amefungwa kwenye kifungo gereza la laana na
kutuingiza katika maisha ya uzima ambapo ni mahali pale ambapo Adamu wa kwanza
alikuwa anaishi, mazingira yale yaliyokuwa yanaonekana katika ile bustani ya
edeni kabla ya anguko.
Bustani ya edeni likuwa ni mazingira
mazuri ya kupendeza ambapo Mungu alimwekea Adamu kuwa makazi yake ya kuishi.
Tukiangalia bustani ya Edeni tunaiona
ikiwa na mto ambao ulikuwa umegawanyika vipande vinne kila kimoja kikielekea
upande fulani na hivyo kutengeneza pande nne za dunia ambapo ni Kaskazini,
Kusini,Mashariki na Magharibi.( Mwanzo 2:10 – 15)
Tena
ukiangalia mji wa Yesulemu ule mpya ambapo ndipo tunapokwenda kuweka makazi
yetu ya umilele, umezungukwa pande nne za dunia na malango kumi na mbili ambayo
Kaskazini kuna mlango matatu, Kusini matatu, Mashariki matatu na Magharibi pia
matatu.
Huu ni mji mpya ambao sisi tuliookoka
tutakwenda kuishi. Ni mahali pazuri penye nuru inayo angaza maasa yote na
hakuna usiku mahali hapo. Tunaweza kusema ni eneo lililojawa na uzima/uwepo wa
Mungu.
Tuliposimama na maji chupa 12,
tulimaanisha kwamba kila moja inawakilisha toleo la maji ya uzima. Agano la
uzima linasimama kwa kila kabila moja.
Maana nyingine ni kwamba kila chupa
iliwakilisha toleo dhidi ya kila kabila/mlango ambayo yanatengeneza Taifa la Israel na ambayo jumla yake ni 12.
Tunachotaka kitokee ni malango 12 ambayo
ni makabila 12, kupitisha uzima kuja katika mji wetu.
Mji wako unasimama badala ya mji wa Yerusalemu (mpya) (ufunuo 21:
1-8)na yale malango yake ni yale mawe 12 ambayo tuliyatumia katika kujenga
madhabahu, na hizo chupa 12 za maji ni Agano la uzima dhidi ya kila
mlango/kabila.
Hatutaki tena mauti/laana kuingia na
kutawala juu ya mji/nyumba/familia
yako,tunataka uanze kuishi maisha
ya umilele/Yerusalemu mpya hapa duniani kwa muda huu ambao Mungu
amekupa.
Tunaivuta Yerusalemu mpya katika maisha
yako kuja kaika wakati wa sasa kwa
imani(waebrania 11:1) na unaanza kufaidi mambo ya baadae wakati ,huku ukisubiri
wakati wa kwenda katika ule mji halisi
wa Yerusalemu.
Naomba nikurudishe nyuma kidogo idadi ya
chupa kumi na mbili tunaipata katika Agano la kale katika 1waflme18:33-34)
ambapo Nabii Elia alimjengea Mungu Madhabahu na baada ya matoleo yale matatu
ambayo ni mwli,damu na roho ya yule ng'ombe, aliagiza toleo lingine la nne ambalo lilikuwa ni la maji mapipa 12 (kumi na
mbili) juu ya madhabahu. Hapa ndipo palipotupa namba 12 ya maji ambayo
tunatembea nayo katika ufunuo huu.
Mahusiano kati ya Mungu na maji na Ibilisi
na maji
Katika Kitabu cha Mwanzo 1:2 – 3 tunamwona
Roho wa Mungu akiwa juu ya vilindi vya maji maana ya neno juu kiroho
linamaanisha utawala dhidi ya kitu kingine.
Hivyo Roho wa Mungu alikuwa
ameketi/anatawala juu ya vilindi vya maji. Ufunuo 17:1 -5 hapa tunamwona
Yezebeli ambaye katika ufunuo 13:1-10 amenenwa kama mnyama aliyetoka katika
maji. Tena inamwelezea uwezo wake mkubwa aliokuwa nao na jinsi alivyotenda
mambo ya ajabu.
Mwanamke huyo aitwaye Yezebeli (Ufunuo 17:
1 – 6) anaonekana akiwa na vichwa saba ambavyo kwa upande wa Kristo tuna
wakilishwa na Roho saba za Mungu.
Pia ameonekana na pembe 10, Ufunuo 13:1 – 10, ufunuo 17:3,
ambazo ziko juu yake na pembe nyingine mbili zilikuwa juu ya yule mnyama aliye
toka katika nchi (ardhi) ufunuo 13:11 – 18.
Ukichukuwa pembe 10 za yule mwanamke na
mbili za yule mnyama aliyetoka katika ardhi/nchi zinatupa namba 12, idadi ya
makabila/malango 12 ya Taifa la Israel.
Hizo
pembe ni
mamlaka/falme/nguvu/uwezo/malango 12 ambazo ibilisi anayatumia
katika ufalme wake kama vile Yesu alivyo na Makabila 12
yayopisha na kusimamisha ufalme wake wa
Mbingini.
Mnyama aliyetoka katika nchi/ardhi alikuwa
na pambe mbili ambazo zinawakilsha falme/mamlaka/roho/uwezo/ mbili zinazotawala
juu ya ardhi.Kuna nguvu/falme mbili za kuzimu zinazotawala juu ya ardhi.
Pembe kumi zilizokuwa juu ya Yule mwanamke
ni mamlaka/falme/idara 10 za kuzimu zilizoko chini ya Yezebeli zinzotawala juu
ya maji/watu.
Kumbuka huyo anavyo vichwa saba (falme 7)
pia anazo pembe 10 zote hizi ni Mamlaka na uwezo wa kipepo unaotenda kazi ndani
ya roho ya Yezebeli.
Maji Kibiblia yana maanisha watu wengi,
hivyo kuna mapepo/ roho saba ambazo zinaishi au tawala ndani au juu ya
mtu/maisha yake, ambzo ni nguvu ya kiyezebeli na pia zipo nyingine kumi Idara
ambazo kazi yake ni kuhakikisha unaishi katika utumwa wa Ibilisi hata kama wewe
hupendi.
Katika ardhi zipo pembe mbili (2) ambazo
ni mapepo/nguvu/falme mbili ambazo zinatawala ardhi na kuendesha utawala wa
kuzimu katika mazingira tunayoishi. Hivyo Ibilisi ameweka utawala wake juu ya
watu (maji) na juu ya nchi ambayo ni ardhi/mazingira yanayotuzunguka.
Huyu mwanamkw alipewa uwezo mwingi sana
13:5 – 6 na uwezowa kinywa chake kunena
makufuru.
Neno kufuru ni kitendo cha kufanya jambo
lililo katika uwezo wa Mungu. (marko 2:1-6)''Katika kifungu hichi Yesu
aliposema kwamba umesamehewa dhambi zako mafarisayo walisema huyu anakufuru kwa
sababu hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kusamehe dhambi ila Mungu pekee''
Yeye alipoonekana kana kwamba ni mtu wa
kawaida, watu wote walikuwa wanamwona kama mwanadamu ila yeye hakuwa tu
mwanadamu lakini pia Mungu kamili.(yohana 1:1).............naye neno alikuwa
Mungu''
Sasa aliposimama kama Mungu, wale
waliokuwa wanamtambua kama mwanadamu, hawakumwelewa ndio maana wakawa wanaona
kwamba Yesu Kristo anajifananisha na Mungu kitendo ambacho kwake yeye hakikuwa
kujifananisha bali alikuwa Mungu kweli.
Marko3:22-23
Hapa tunaona kitendo cha Yesu akitoa pepo. Jambo hili la kumtoa mtu pepo
lilileta mtafaruku kwa watu. ….Nao waandishi walioshuka kutoka yerusalem
wakasema,Ana Beelzbuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.Hivyo tunaona
wakimfananisha/wakifananisha kazi ya utendaji wa Mungu aliye hai na (Mkuu wa pepo)
Baada ya maneno yao, Bwana Yesu akaanza
kuwaeleza kwamba hayo maneno yenu ni makufuru kwa Mungu kwani kitendo cha
kumfananisha Mungu/Yesu/Roho mtakatifu na mapepo au ibilisi au mojawapo ya
idara yake ni kukufuru.
Hivyo kukufuru ni kujifanya wewe kuwa ni
Mungu au ni kunena kinyume cha Yesu/Roho mtakatifu au kufanya jambo lolote
linaloibeza kazi ya Mungu.
Kama kukufuru ni kufanya yale ambayo ni
Mungu pekee anayoyatenda ili wewe uonekane kuwa ni Mungu au uabudiwe ni dhahri
kwamba vile vichwa saba ni ambavyo viko juu ya Yezebeli ni roho saba chafu za
kuzimu zinazosimama mbadala wa Roho saba za Mungu.
Kumbuka tuna Roho Saba za Mungu (Isaya
11:2 – 3) ambazo ni:
1. Roho wa BWANA
2. Roho wa Hekima
3. Roho wa ufahamu
4. Roho wa uweza
5. Roho wa shauri
6. Roho wa maarifa
7. Roho wa kumcha Bwana
Hizi zipo katika upande wa Mungu aliye
hai. Na hizo Roho saba ndizo zinazotengeneza
namba saba ambayo ni ukamilifu wa BWANA/Mungu.
Sasa kama ibilisi ameweka makufuru,
inamaana badala ya Roho wa bwana yeye amegeuza na kumweka belzebuli ambaye ndiye
mkuu wa mapepo
· Hekima -ameweka hekima ya
dunia/kipepo.
· Maarifa -ameweka pepo la ufahamu wa
giza/dunia.
· Uwezo
-Pepo la uwezo / upako/mamlaka ya kishetani/dunia.
· Shauri - pepo la mashauri ambayo hayatokani na
Mungu yenye lengo la kupotosha watu waende nje ya mpango wa mungu.
· Kumcha Bwana-hapa shetani amesimamisha
pepo ambalo kazi yake ni kuhakikisha watu wanamtii/Mwabudu shetani/joka.
Namba kumi
na mbili katika Kanisa inawakilishwa na majina kumi na mbili ya kabila la
Israeli ambyo ni:
1. Rubeni – Macho ya Mungu (mwanzo 29:32)
2. Yuda – Ufalme/Utawala
3. Lawi – Ibaada/ukuhani (mwanzo 29:34)
4. Yusufu – Mamlaka juu ya ardhi
5. Dani – Haki/hukumu (mwanzo 30:6)
6. Benjamini – Nguvu za Kijeshi
7.
Asheri-Chakula/tunu/watoto/kibali/heri/baraka.(
Mwanzo30::13,mwanzo49.20,kumbukumbu 33:24)
8. Naftaili-Ushindi/utele/fadhili(mwanzo
30:8,kumbukumbu 33:23)
9. Gadi -Mtoa sheria(kumbukumbu 33:21-22)
10.Isachari
– Kazi/mapato/mshahara(mwanzo 30:14-18)
11.Zabloni -Furaha/makazi/mahari(Mwanzo30:20,Kumbukumb
33:18
12.Simeoni –
Kusikia/ masikio ya Bwana (mwanzo 29:33)
Kila kabila
linapitisha maana Fulani katika Taifa la Israel. Hivyo kila kabila ni
Idara/Pembe/mamlaka inayoratibisha maisha ya watu katika Taifa la Israel.
Sasa katika
ufalme wa giza yapo malango mawili
ambayo yanayotenda kazi kwa ajili ya
kuthibitisha ufalme wa giza juu ya ardhi.
Hivyo
mengine yote yapo chini ya Yezebeli ambapo uratibu wake ni juu ya watu.
Baada ya
mafafanuzi haya yote tunataka tuingie katika maombi.Tutakuwa na siku saba za
kung'oa na kuharibu vile vichwa saba (mapepo saba) baadaye tutakuwa na siku
nyingine saba za kupanda Roho saba za Mungu.Maombi haya
1. Wiki ya kwanza siku saba(Yeremia 1:10 )
(Matayo 15:13)
Maombi yake
ni kama ifuatavyo
Toba kwa
familia:
Baba katika
jina la Yesu ninakuja mbele zako kwa damu ya mwanao Yesu Kristo. Ninatambua
maovu yangu yote ambayo nimekutenda wewe kwa kujua na kutokujua. Ninatubu kwa
ajili ya mji wangu, Baba yangu, mama yangu, watoto wangu (taja wote kwa majina)
mke wangu, mume wangu, mashangazi, wajomba, mama wadogo, mama wakubwa,
mabinamu, wajukuu, na uzao wangu wote na watu wote wanonihusu kutoka upande wa
baba na kutoka upande wa mama.
Toba kwa
ajili ukoo:
Ninatubu pia
kwa upande wa ukoo wangu maovu yao yote na yote waliokutenda yaliyokuchukiza
mbele zako kwa sababu nimejua ya kuwa Yezebeli alipewa watu wa kila ukoo.Ninatubu
kwa ajili ya waasisi wa ukoo wangu,viongozi wate waliopita na waliopo katika
ukoo wangu,maovu yao,dhambi na machukizo waliyokutendea,maagano na makafara
yote waliyofanya juu ya ukoo wetu na vizazi vyake.Naomba rehema zako na msamaha
kwa ajili ya mambo yote tuliyoyatenda kama ukoo,kwa upande wa babu mzaa
baba,bibi mzaa baba,babu mzaa mama na bibi mzaa mama yagu na koo zote
tuliyofungamana kwa namna mbalimbali.
Toba kwa
ajili kabila
Ninasimama
pia na damu ya Yesu kwa ajili ya kabila langu. Ninawaleta wote kwako nakuomba
Bwana utusamehe maovu na dhambi ambazo
waasisi na wahenga wa kale waliyoyatenda,ikiwa ni pamoja na maagano yote
yaliyofanyika ,yaliyotuunganisha na ulimwaengu wa giza kwa njia mbalimbali ikiwemo
mila na desturi na kila uchafu tulioufanya kupitia machifu na viongozi
mbalimbali,ambazo katika hayo sisi kama familia tumejikuta tukiunganishwa na kupalizwa japo sisi hatukutenda hayo sawa
na kutoka 20:1-5
Toba kwa
ajili ya Taifa.
Ninakuomba
unisamehe na ulisamehe Taifa langu na watu wote
wa Tanzania katika damu
yako.Tumetenda dhambi sisi kama watanzani,wahenga wetu,waasisi wetu,viongozi
mbalimbali na maagano yote yaliyotuunganisha na Yezebeli pamoja na kuzimu kwa
ngazi ya kitaifa.
Ninajifunika
mimi na damu yako, nafunika mji wangu na wote walioko ndani yake kwa damu ya
yesu kabila langu na taifa langu lote pia ninalifunika kwa damu ya Yesu Kristo.
Ninasimama na Agano la maji ya uzima sawa
na Yohana 4:10 kung’oa, kuharibu na kuangamiza kabisa roho ya Yezebel na vichwa
vyake saba ndani na juu ya maisha yangu. Ninasimama kinyume cha Yule mnyama
aliye toka katika maji na vichwa vyake saba pamoja na matokeo ya utendaji wake
na athari zake ndani yangu. Ninapeleka makombora ya maji ya uzima katika jina
la yesu kristo,Ninampiga huyo mnyama napiga na kuharibu vichwa vyake vyote vile
vilivyosimama mbadala wa Roho saba za Mungu katika maisha yangu zinazotembea
katika mwili wangu, zinazotembea katika damu na mfumo wa maji ulioko katika
miili yetu ambayo tumeridhi kutoka kwa baba na mama zetu sawa na 1 petro 1:18 –
24 na Ezekiel 16: 1 – 6.katika jina la Yesu Kristo tunaziangamiza kabisa hizo
silka ambazo ni kutoka kwa baba zetu, leo tunaziangusha, tunabomoa,
tunaziteketeza kabisa katika jina la Yesu ili tuweze kuishi na kutembea katika
uhuru na maisha yale mapya uliyotupa kupitia msalaba wa Yesu. Ili sisi wanao,
miji yetu, Nyumba zetu na familia zetu ziwe na ule uzima ulioutoa tena tuwe nao
tele.
Katika jina la Yesu Kristo ninaendelea
kuharibu mfungamano wa hizo roho/mapepo/vichwa saba vya Yule Yezebeli pamoja na
Yezebeli Mwenyewe, unaotokana na ukoo wangu/ zetu, kabila langu/letu, na Taifa
letu kwa ujumla maana yule mnyama aliyetoka baharini alipewa watu wa kila
kabila, koo/jamaa na Taifa (ufunuo 13:7) Hivyo ninasimama kinyume cha huyo
mnyama katika ngazi ya ukoo, kabila na Kitaifa kwa mamlaka ya jina la Yesu
Kupitia Agano hili la maji ya uzima. Ninaharibu maagano yote yanayotushikilia
na tabia/silka/vichwa vyote saba vya ukoo, kabila,na kitaifa vinavyofuatilia
maisha yetu na vinavyotawala,vile vichwa saba katika ngazi ya familia,vichwa
saba katika ngazi ya ukoo,vichwa saba katika ngazi ya jamaa,vichwa saba katika
ngazi ya kabila na vichwa saba katika ngazi ya taifa. Tunavipiga na
kuviangamiza, tunaharibu na kuviteketeza kabisa katika jina la Yesu.
Tunakuharibu belzebel mkuu wa mapepo,
hekima za kipepo, maarifa ya kishetani, ufahamu wa kuzimu, mashauri na roho
zote za kishauri za kipepo, uweza wa giza na roho zote zinazotupelekea kumcha
shetani/ Yule joka (ibilisi) kwa mamlaka ya jina la Yesu kristo Wanazareti,
wewe bwana ndiwe uliyesema na kanisa na kutuambia tuje tuone hukumu ya yule
babel mama wa makahaba na machukizo ya nchi (ufunuo 17 :1 – 3, tena wewe ndiwe
uliyewaanganiza wamisri, Farao na jeshi lake kwa maji ya bahari ya shamu wakati
walipokuwa wanawafuatilia watu wako Israel baada ya kuwatoa katika utumwa kule
misri.(kutoka 14:26-31)
Hawa wamisri waliokuwa wanawafuatilia
watu wako wanawakilisha utawala wa kichawi katika ulimwengu wa roho uliokuwa
unatawala kule Misri na uliokuwa unawakandamiza watu wako Israel.
Leo hii ninatangaza kwamba kwa mamlaka
ya jina la Yesu kama vile wewe baba ulivyotenda kwa lile Kanisa la kwanza ni
wakati wako sasa kutenda katika maisha, nyumba, familia, miji na uzao
wetu.Katika jina la Yesu ninatangaza kwamba Yezebeli na vichwa vyako kwamba
umeanguka vichwa vyako vimeanguka, falme zako, mamlaka zote, majina yote,
usulutani wako wote na majeshi yako yote yameanguka (Isaya 21:9b)) kwa pigo la
maji ya uzima yaliyotoka ubavuni mwa Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai.
Kuanzia leo Yezebeli hauna mamlaka
tena juu yangu, mji wangu, familia yangu, uzao wangu na wote wanaofungamana na
maisha yangu, kazi zangu, na eneo lolote linalonihusu katika jina la yesu
Kristo.Tena ninatangaza minyororo na kamba zote zilizokuwa zimenifunga, kamba
za kifamilia,kiukoo,kikabila,kijamii na kitaifa kukatika na kuniachia mimi, mji
wangu, familia yangu na uzao wangu kuanzia sasa kwa mamlaka ya jina la Yesu.
Ninakiri na kutangaza ushindi juu yangu,
familia yangu, mji wangu na uzao wangu tangu sasa katika jina la Yesu
Kristo.Ninatangaza uzima juu yangu, waliokuwa hawajaolewa kuolewa na kuwa na
ndoa bora yenye furaha, watoto wangu wa kiume/kike ambao walikuwa wamefungwa
kuoa/kuolewa, sasa waoe/waolewe na kuwa na familia njema yenye ushindi, ustawi
wa kiuchumi, afya bora katika miili yao, maendeleo katika kazi zetu za mashamba,
mifugo, miradi, na kila tunachokifanya kifanyike Baraka katika jina la Yesu
Kristo.
Wiki ya pili
Hii itakuwa ni mfululizo wa siku nyingine
saba za kupanda na kujenga Yeremia 1:9 – 10,Mwanzo 1:3-27).''Tazama nimekuweka
juu ya falme na mamlaka ili kung'oa kubomoa na kuharibu kuangamiza ili kupanda
na kujenga.'' wiki iliyopitailikuwa ni kung’oa kubomoa, kuharibu na kuangamiza.
Wiki hii ni
ya kujenga, kumbuka Bwana Yesu alisema pepo amtokapo mtu, huenda akitafuta
mahali pasipo na maji akikosa husema nitarudi katika nyumba niliyotoka. Tena
hutafuta mapepo mengine Saba yaliyomabaya kuliko yeye na hali ya mtu Yule huwa
mbaya kuliko ilivyokuwa mwanzo (luka11:24-26).Tunataka tukapande Roho saba za
Mungu ndani na juu ya maisha yetu. Hizo Roho Saba za Mungu ndizo zitakazo
chukua nafasi ya vile vichwa saba vilivyokuwa vikitawla juu nya maisha yetu vya
yule mwanamke babeli.
Maombi yake yatakuwa
ni haya:
Baba katika
jina la Yesu ninakuja mbele zako umesema na tukikaribia kiti chako cha rehema
kwa ujasiri. Nami sasa ninakikaribia kiti chako cha rehema nakuomba toba kwa
ajili yangu mahali popote ambapo nimekutenda dhambi kwa kufahamu na pasipo
kufahamu. Unirehemu sawa sawa na fadhila zako kiasi cha wingi wa rehema zako
nakuomba ufute maovu, makosa, dhambi na machukizo yangu. Nioshe katika damu ya
mwana kondoo Yesu Kristo, nitakase Bwana katika jina la Yesu nafsi yangu, Mwili
na roho yangu.
Ninajipatanisha
sasa na wewe kupitia damu yako katika jina la yesu Kristo. Ninasimama na damu
yako katika ukuhani kwa ajili ya familia yangu, jamaa zangu, rafiki zangu,
watoto wangu, mke/mume wangu, baba na mama yangu, wajomba na mashangazi, mama
wakubwa/wadogo katika jina la yesu, ninaita utakaso wa damu ya yesu juu ya
nafsi zao, roho na miili yao, maisha na kazi zao katika jina la
Yesu.Ninawapatanisha na wewe kupitia msalaba/damu ya mwanao nafsi/roho na miili
yao katika jina la Yesu Kristo.
Ninasimama
kwa ajili ya jmaa,ukoo, kabila langu na taifa langu. Ni kweli yapo maovu
yaliyotendeka kwa ngazi ya kikabila, Ukoo na taifa. Ninaleta maovu haya yote
katika msalaba wako, ninakiri uovu wote mbele zako kama kuhani wako katika damu
yako. Naomba usamehe na rehema zako uzielekeze kwetu. Tunajipatanisha na damu
yako na kufanya amani na wewe Mungu wetu (efeso1:13-17), tunakukaribisha sasa
uje na umiliki na kutawala juu yetu katika jina yesu Kristo “Ameni”
siku ya kwanza
Kupanda na kujenga mithali 9:1,mwanzo1:3-5
Baba katika jina la Yesu wewe ndiwe
uliyesema kwamba hekima ameijenga nyumba yake amesimamisha nguzo saba. katika
jina la Yesu Kristo ninasimama sasa na agano hili la maji ya uzima kwa ajili ya
kupanda na kujenga uzima juu na ndani ya maisha yangu.Ninapanda na kujenga yule
Roho wa Bwana katika mji wangu, familia yangu, ndoa yangu, uzao wangu, ndani ya
damu yangu, Mwilini mwangu, maishani mwangu, katika jina la Yesu Kristo,
atawale na kumiliki.
Ninabatilisha
uwepo wa Belzebel ndani yangu, juu yangu kwa watoto wangu, mke wangu, nyumba
yetu, ukoo wangu kabila langu na taifa langu katika jina la yesu kiristo.Nafasi
aliyokuwa belzebuli ninakusimamisha na kukupanda wewe Roho wa BWANA katika jina
la Yesu. Ninaachilia maji ya uzima juu yako ee Roho wa Bwana yakuneemesha na
kukustawisha ili uwe wa mizizi ndani yangu sawa na Yeremia 17:9 – 10.Amen.
Siku ya pili
mwanzo 1:6-8
Ninapanda Roho wa hekima ya Mungu aliye hai
maishani mwangu, ndani ya damu na mfumo wa maji mwilini mwangu, juu ya mji wetu, familia, nyumba na uzao wangu,
katika ukoo wangu, kabila langu na Taifa langu kwa mamlaka ya jina la Yesu,
kupitia agano la maji ya uzima yaliyotoka ubavuni mwako, nabatilisha uwepo wa
hekima ya kidunia na kipepo katika maisha yangu ndani yangu, damu na mfumo wa maji
mwilini mwangu, familia yetu, mji wetu, ukoo wetu, kabila letu, jamaa zangu,
Taifa letu na eneo lolote linalonihusu.Ninakiri uwepo wa hekima yako maishani
mwangu, familia yangu, mji, ukoo, taifa na nyumba yangu.Ninaachilia maji haya
ya uzima juu yangu, familia yangu, kabila, ukoo na taifa langu kwa ajili ya
kustawisha na kuneemesha pando la Roho wa hekima ya Mungu alie hai, kama
ulivyosema utaleta manyunyu kwa wakati wake, manyunyu ya Baraka (Ezekiel
34:26). Sasa yaachilie hayo maji ya ubavuni mwako kama manyunyu kustawisha na
kuneemesha Roho huyU wa hekima katika maisha yangu,mji
wangu,familia,ukoo,jamaa,kabila na taifa langu katika jina la Yesu kristo.
Siku ya tatu
mwanzo 1:9-13
Ninapanda
Roho wa ufahamu katika mji, ndoa yangu, kazi yangu, ukoo wangu, kabila langu,
taifa langu, katika maisha yangu, ndani ya damu na mfumo wa maji mwilini
mwangu.Ninabatilisha uwepo wa ufahamu wa kipepo unaotembea ndani na juu yetu
tuliouridhi kwa mababa na mama zetu, familia tulizotoka, miji, ukoo, kabila na
taifa kwa ujumla.Tunasimamisha na kupanda ufahamu wa Mungu aliye hai ndani na
juu ya maisha yetu kupitia agano la maji ya uzima yaliyotoka ubavuni mwako na
katika miji, familia,ukoo, kabila na taifa letu.Ninakiri uwepo wa ufahamu wako
ee Yesu Kristo ndani na juu ya maisha yangu mji, famila, uzao, kabila, ukoo,
Taifa langu lote.Ninatangaza ya kwamba Roho wa ufahamu wa Yesu Kristo tangu leo
yuko ndani na juu ya maisha yangu, familia, mji, uzao wangu, kabila, ukoo na
taifa akiachilia ufahamu wa Mungu kwetu unaotuongoza katika njia ya haki
kweli.Katika jina la Yesu ninaona ufahamu wako Yesu Kristo ukibadilisha kabisa
maisha na hatima ya maisha yangu, mji wangu, ukoo, kabila, uzao wangu na
taifa.Ninaendelea kuachilia maji yako ya uhai juu yangu, mji wangu, familia,
uzao wangu, kabila,ukoo na taifa langu yaendelea kuchilia mvua ya Baraka kwa
ajili ya kustawisha ufahamu wako ee Yesu Kristo Bwana wangu siku zote na katika
kila eneo la maisha Yetu.
Siku ya nne:mwanzo 1:14-18
Ninapanda Roho wa shauri katika maisha
yangu, mji wangu, familia, ukoo, kabila, ndoa yangu, kazi, huduma na eneo
lolote la maisha yetu.Wewe ndiwe uliyesema kwamba utanifundisha na kunionyesha
njia utakayoiendea utanishauri jicho lako litanitazama (zab 32:8) sasa Bwana,
katika jina la Yesu nahitaji huyo Roho wa ushauri apandwe ndani na juu ya
maisha yetu ili kupitia Roho wako wa shauri atupe mashauri ya njia sahihi
tutakayoiendea ili tusije tukapotea au kuenenda nje ya mapango wako.Kwa mamlaka
ya jina la Yesu tunabatilisha uwepo wa yule Roho wa ushauri wa ibilisi
aliyekuwa anatembea ndani na juu ya maisha yetu ambaye alikuwa anatupa mashauri
yaliyo nje na makusudi yako ee Bwana Yesu.Ninakiri kuanzia sasa Roho wako wa
ushauri atatuongoza katika shauri lako (zab 74:24), miji ,familia, kabila, koo
na taifa letu kwa ujumla.Katika jina la Yesu Kristo kama vile mtumishi wako
Daudi (2 Samweli 2:1) alivyokuwa akipata mashauri kwako katika mipango
mbalimbali kwako, na jinsi ulivyokuwa ukimshauri katika njia ya mafanikio ndiyo
na Roho wako wa shauri anavyotenda kazi ndani na juu ya maisha yetu kuanzia
siku ya leo na hata milele na milele
.Amen.
Siku ya tano mwanzo 1:20-23
Ninapanda Roho wa uweza katika maisha yangu,
mji wangu, familia, kabila, ukoo na taifa langu, kazi, ndoa na eneo lolote
linalofungamana na maisha yangu katika jina la Yesu.
“Hili ndilo
neno la Bwana kwa zerubabel, kusema sio kwa uwezo wala si kwa nguvu bali ni kwa
Roho yangu asema Bwana wa majeshi (zacharia 4:6).Sawa sawa na neno lako
ninamkiri huyo Roho wa uwezo ndani na juu ya maisha yangu, familia, mji, uzao,
ndoa, mashamba, kazi, mifugo, uchumi wangu, kabila, ukoo, taifa, huduma yangu
na eneo lolote la maisha yetu, ili aachilie uweza wake katika kutuwezesha
kutenda mambo na kuyakamilisha.Kama Roho wa uweza alivyoonekana katika maisha ya
Zerubabel ya kumpatia uwezo wa kujenga hekalu la Mungu, nasi tunamhitaji kwa
ajili ya kuachilia uweza wake ndani yetu utakaotuwezesha kuwa watendaji katika
jina la Yesu Kristo.Ninatangaza kubatilika kwa Roho wa uweza wa kipepo uliokuwa
ukitembea ndani na juu ya maisha yetu kutoka kwa mababa na mama zangu upande wa
baba na upande wa mama yangu.Kupitia agano hili la maji ya uzima yaliyotoka
ubavuni mwako ninaona uweza wako ukidhihirika ndani na juu ya maisha yangu,
familia yetu, mji wetu, uzao wangu, kabila langu, ukoo wangu, taifa langu, kazi
yangu na eneo lolote linalohusu maisha yangu.Ninatangaza uwepo wa madhihiriko
katika kila eneo la maisha yangu, mahuisho ya mji wangu, familia, uzao wangu,
afya yangu mwili wangu, katika damu na mfumo wa maji yaliyoko ndani yangu, kazi
zangu, uchumi wangu, ndoa yangu, maisha yangu katika jina la Yesu
Kristo.Ninatangaza juu yangu na familia, mji, uzao wangu, uwezo wa kielimu,
kiuchumi, kiroho, afya ya mwili na roho, maisha ya kila siku, kuoa na kuolewa
kwa watoto wangu na kuwa na familia zao bora, kumiliki na kutawala katika
ardhi.
Siku ya sita mwanzo 1:24-31
Ninapanda Roho wa maarifa katika maisha
yangu, mji wangu, familia, kabila, ukoo na taifa langu, kazi, ndoa na eneo
lolote linalofungamana na maisha yangu katika jina la Yesu.
Sawa sawa na
neno lako katika mithali24:4''Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa'' ninamkiri
huyo Roho wako wa maarifa ndani na juu ya maisha yangu, familia, mji, uzao,
ndoa, mashamba, kazi, mifugo, uchumi wangu, kabila, ukoo, taifa, huduma yangu
na eneo lolote la maisha yetu, ili aachilie ujazo wa kila jambo jema katika
jina la yesu.Kama Roho wa Maarifa alivyomwezesha yesu kristo kuwafanya wengi kuwa wenye haki nasi
leo tunamhitaji katika jina la yesu kristo.Ninatangaza kubatilika kwa Roho wa
maarifa ya kipepo aliyekuwa akitembea
ndani na juu ya maisha yetu kutoka kwa mababa na mama zangu upande wa baba na
upande wa mama yangu.Kupitia agano hili la maji ya uzima yaliyotoka ubavuni
mwako ninaona maarifa yako yakidhihirika
ndani na juu ya maisha yangu, familia yetu, mji wetu, uzao wangu, kabila langu,
ukoo wangu, taifa langu, kazi yangu na eneo lolote linalohusu maisha
yangu.Ninatangaza uwepo wa madhihiriko
ya maarifa ya Mungu katika kila eneo la maisha yangu, mahuisho ya mji
wangu, familia, uzao wangu, afya yangu mwili wangu, katika damu na mfumo wa
maji yaliyoko ndani yangu, kazi zangu, uchumi wangu, ndoa yangu, maisha yangu
katika jina la Yesu Kristo.Ninatangaza juu yangu na familia, mji, uzao wangu,
maarifa katika elimu,uchumi, kiroho, afya ya mwili na roho, maisha ya kila
siku, kwa watoto wangu na familia zao,
maarifa yatuongezee uwezo (mithali24:5b) wa kumiliki na kutawala katika katika
ardhi,kutunza familia zetu,fedha, kumiliki mashamba, kuwekeza, kutenda mambo
yote mema ya kimaendeleo katika jina la Yesu Kristo.Tena umesema (Isaya
53:11a).Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye
haki'' nami ninatangaza maarifa yako katika mji wangu,
nyumba,familia,ukoo,taifa,kabila na
jamaa zangu ili wote yatuvushe katika
maeneo mbalimbali ya maisha yetu.Amen
Siku ya saba: mwanzo 2:1-4
Ninapanda Roho wa kumcha Bwana katika maisha
yangu, mji wangu, familia, kabila, ukoo na taifa langu, kazi, ndoa na eneo
lolote linalofungamana na maisha yangu katika jina la Yesu.
''Kumcha Bwana
ni chanzo cha maarifa''(mithali 1:7a).Sawa sawa na neno lako ninamkiri
huyo Roho wa kumcha Bwana ndani na juu ya maisha yangu, familia, mji, uzao,
ndoa, mashamba, kazi, mifugo, uchumi wangu, kabila, ukoo, taifa, huduma yangu
na eneo lolote la maisha yetu, ili aachilie uweza roho wake kwetu katika
kukutii wewe na kukuabudu.Ninatangaza kubatilika kwa Roho wa kumcha na kumtii
shetani uliokuwa ukitembea ndani na juu ya maisha yetu kutoka kwa mababa na
mama zangu upande wa baba na upande wa mama yangu.Kupitia agano hili la maji ya
uzima yaliyotoka ubavuni mwako ninaona Roho wako wa kukucha akidhihirika ndani
na juu ya maisha yangu, familia yetu, mji wetu, uzao wangu, kabila langu, ukoo
wangu, taifa langu, kazi yangu na eneo lolote linalohusu maisha
yangu.Ninatangaza madhihiriko ya kumcha Bwana
katika kila eneo la maisha yangu,mji wangu, familia, uzao wangu, afya
yangu mwili wangu, katika damu na mfumo wa maji yaliyoko ndani yangu, kazi
zangu, uchumi wangu, ndoa yangu, maisha yangu katika jina la Yesu
Kristo.Ninatangaza juu yangu na familia, mji, uzao wangu uweza ule uliomwezesha
Ibrahimu na Bwana yesu kristo kumtii Mungu
hadi mauti(wafilipi2:8). ...Tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu ,alijinyenyekeza akawa mtii
hata mauti,naam mauti ya msalaba.Bwana umesema basi nyenyekeeni chini ya
mkono wako ulihodari ili utukweze kwa wakati wako,sasa ninaachulia Roho
wako wa
kumcha Bwana ili aendelee unyenyekevu
ndani na juu ya maisha yangu, familia, mji, uzao, ndoa, mashamba, kazi,
mifugo, uchumi wangu, kabila, ukoo, taifa, huduma yangu na eneo lolote la
maisha yetu.Ninatangaza utii wako katika mji wangu,
nyumba,familia,ukoo,taifa,kabila na
jamaa zangu. .Ninatangaza juu yangu na familia, mji, uzao wangu, watu wote
wamtii na kumwabudu Yesu kristo tena watetemeke mbele zake sawa na
wafilipi2:9-10 katika jina la Yesu Kristo Amen.
KWA MAELEZO
ZAIDI YA MAOMBI YA KUFUNGULIWA NA UKOMBOZI KATIKA
FAMILIA WASILIANA NA MWINJILIST: LAURENT MPOMA KWA SIMU : 0763652896, 0782859946
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: