KITABU CHA USHINDI WA MAOMBI , SOMA HAPA
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
1. Maombi ni nini?
Maombi ni mawasiliano kati ya mungu aliye hai na mmwanadamu,
kupitia; sala,shukrani, maombezi, dua na maombi. 1tim 2:1
kwa ajili hii ni lazima pawepo na njia mbili, yaani: kuomba,
na kujibiwa. Kwahiyo ukiomba ni lazima ujibiwe.
2. AINA ZA MAOMBI
i. Maombi ya kufunga.
Ii. Maombi ya rufaa.
Iii. Maombi ya utetezi.
Iv. Maombi ya mapatano.
V. Maombi ya shukrani.
Vi. Maombi ya kuteka mateka.
Vii. Maombi ya vita.
Viii. Maombi ya kubariki.
Ix. Maombi ya kulaani.
X. Maombi ya kunuiza.
Xi. Maombi ya ulinzi.
Mt 4:1-3, yosh 1:1-3, zab 35:1-9, hes 6:22-24, 1tim 2:1-4,
uf 8:1-5, zab 34:7-9.
MAANDALIZI YA MAOMBI; KUT 19:7-20
Kabla haujaingia katika maombi ya muda mrefu au siku kadhaa,
zingatia yafuatayo;
i. Andaa chumba utakachofanyia maombi.
Ii. Fanya usafi katika chumba hicho utakachofanyia maombi.
Iii. Na wewe binafsi uwe msafi, yaani uoge vizuri.
Iv. Vaa nguo safi kila asubuhi, baada ya kuoga.
V. Uwe na biblia , daftari na kalamu.
Vi. Unapoingia ili kuanza maombi, jitakase kwanza kwa damu
ya yesu kristo wa nazareth.
Vii. Takasa chumba unamofanyia maombi.
Viii. Imba nyimbo kadha.
Ix. Fungua mbingu.
X. Mwangushe mfalme wa giza wa anga.
Xi. Karibisha malaika wa maombi, ulinzi, nguvu, vita na wa
enzi ya mungu baba.
Xii. Mtukuze mungu baba, mwana na roho mtakatifu.
Xiii. Panga mahitaji ya kuombea kwa kuzingatia sheria za
ufalme wa mbinguni, na ulimwengu wa roho.
Xiv. Hakikisha simu yako uwe umeizima siku zote za maombi.
Xv. Baada ya kupeleka mahitaji yako, tenga muda wa
kutafakari neno kwa kujisomea biblia.
Xvi. Tenga muda tena wa kutulia ili usubirie majibu ya
maombi yako.
4. NJIA ANAZOTUMIA MUNGU KUKUJIBU MAOMBI
i. Njozi. Dan2:27.
Ii. Ndoto. Mwa 37:1-9.
Iii. Maono. Ezek 8:1-3.
Iv. Ufunuo. Uf 1:1-11.
V. Dhamiri safi au njema, mdo 23:1.
5. NAMNA YA KUHAKIKI MAJIBU YA MAOMBI
amuz 6:14-17
ili uwe na uhakika na sauti inayo sema na wewe kutoka
ulimwengu wa roho, uliza hivi: “ni nani wewe unayesema nami katika jina la
yesu?” Rudia swali hili mara 3, wakati unahoji juu ya sauti au kiumbe hai
kinachosema na wewe wakati huo kutoka ulimwengu wa roho….. Kama ni ni malaika
kutoka mbinguni, atajitambulisha kwako. Kama ni pepo au shetani atakimbia.
6. AINA ZA MAJIBU YA MAOMBI
i. Niko pamoja na wewe- ayubu.
Ii. Nitakusaidia- yesu kristo.
Iii. Nitakupigania- mfalme daudi. (hili ndilo jibu zuri).
Isa 41:8-13, zab 35:1-9.
7. BAADA YA KUMALIZA MAOMBI
Umalizapo maombi, tenga muda wa kutulia nyumbani kwako.
Epuka haya yafuatayo;
i. Epuka kwenda kukaa kijiweni.
Ii. Epuka maongezi ya kipuuzi yasiyokuwa na maana.
Iii. Epuka kuongea kwa makelele sana, bali uwe mtulivu.
Iv. Epuka vijiwe vya umbea na masengenyo, maana yanapunguza;
utukufu na nguvu.
V. Epuka kuangali vipindi vya runinga kama filamu au
tamthilia zenye matukio ya kuhuzunisha, au kusikitisha au ya aibu.
Vi. Epuka kukaa maeneo yenye makelele.
Vii. Kama wewe ni mchungaji, askofu au kiongozi wa huduma
fulani; tulia nyumbani kwako siku3, siku ya jumapili usihubiri wewe, bali
mwachie mwingine ahubiri madhabahuni. Maana baada ya maombi malaika wataendelea
kukuhudumia, huku wakikujenga utu wa ndani, wakikukarabati utu wa ndani kama
watakavyokuwa wameelekezwa na mungu, hii ni pamoja na kukuvika silaha za
mbinguni, vipawa na karama na kukuumba utu wa ndani. (mt 4:1-11).
Viii. Aidha jitenge na marafiki wapagani na wasiomcha mungu,
mapema tu baada ya kumaliza maombi. Bali ambatana na wale walio jaa nguvu za
mungu na wanao maanisha katika utumishi na maombi. Luka 9:28-32.
8. FAIDA ZA KIROHO ZA MAOMBI
i. Maombi ni silaha.
Ii. Maombi ni nguvu.
Iii. Maombi ni ulinzi.
Iv. Maombi ni dawa.
V. Maombi ni afya.
9. UPENYO WA MAOMBI KATIKA KUVUNJA LAANA NA ASILI
ZINAZOWATESA WATU.
Zifuatazo ni aina 8 za asili zinazo watesa wanadamu katika
sura ya laana, ambazo, kwa njia ya maombi ya ukombozi, na kwa msaada wa uongozi
wa roho mtakatifu, 1kor 2:10-14, tunafanikiwa kuponyeka na kuwekwa huru kwa
jina la yesu kristo wa nazareth.
Kama kiongozi wako wa; taifa, mkoa, wilaya, kanisa, msikiti,
kampuni, shirika, kabila au ukoo anasumbuliwa na asili hizi mbaya, atawasumbua
sana. Na nivigumu kutoboza au kustawi kiuchumi, kijamii kiroho na kiutumishi.
Tafakari mafundisho haya ili upate maarifa, halafu uyafanyie kazi kuanzia leo
kwa faida yako wewe , familia yako na yenu, jamii nzima na kanisa unalolichunga
na kulisimamia.
Ukichunguza kwa makini, utagundua, asili hizi mbaya, ndio
chanzo cha ufisadi, wizi na rushwa , hapa tanzania na duniani mwote.
ASILI HIZI ZINASUMBUA TAKRIBANI DUNIA NZIMA NA WALE WAKAAO
KATIKA USO WA NCHI KUPITIA MAAENEO HAYA YAFUATAYO;
i. Asili na laana ya utaifa.
Ii. Asili na laana ya ukabila.
Iii. Asili inayotokana na namna ulivyo zaliwa.
Iv. Asili na laana inayotokana na siku au tarehe
uliyozaliwa.
V. Asili inayotokana na madhabahu za kishetani za ukoo.
Vi. Asili na laana inayotokana na tabia sugu na mbaya ya
kifamilia.
Vii. Asili inayotokana na maneno uliyotamkiwa ukiwa tumboni.
Viii. Asili inayotokana na mapito uliyopitia.
I. ASILI INAYOTOKANA NA UTAIFA
ezekiel 16:3 “useme bwana mungu auambia yeerusalemu
hivi;asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya mkanaani, mwamori
alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa mhiti”
kama nchi imefanya uovu fulani, laana inaingia hadi ardhini.
Ukizaliwa hapo laana inakutafuna. Ezekiel 22:3-4, “ nawe utasema bwana mungu
asema mji umwagao damu ndani yake, ili wakati wake upate kuja, mji ufanyao
vinyago juu ya nafsi yake ili ujitie unajisi, umekuwa na hatia ktk damu yako
uliyoimwaga, nawe umekuwa unajisi kwa vinyago vyako ulivyovifanyanawe
umezileeta karibu siku zako, nawe umefika karibu na miaka yako, basi kwa sababu
ya hayo nimekufanya kuwa lawama, kwa mataifa na kuwa dhihaka ktk nchi zote”
kila taifa hapa duniani lina wakilishwa na alama ya mnyama.
Mfano; tanzania alama ya mnyama wake ni twiga. Mnyama huyu anashingo ndefu
anaona mbali na kutazama wakati mwingine, wenzake wakiliwa na chui, na yeye
hachukui hatua yoyote. Hii ni hali ya kuzubaa, hofu na kutojitambua. Nchi ta
tanzania imekuwa ikiibiwa rasilimali zake kama; madini, lakini watu walikuwa
wakitazama na kusema bila ya kuchukua hatua. Lakini ashukuriwe mungu, tanzania
imempata rais; magufuli, aliyeliona hili na kuwarudishia wa-tanzania haki ya
kufaidi keki ya taifa.
Alama ya mnyama ya kenya ni jogoo. Hii ni alama iletayo
ufuska na ukahaba. Na hili ndilo tatizo la nchi ya kenya kiroho. Alama ya
mnyama ya marekani ni ndege aitwaye; tai. Maana ya tai ni ufalme uliotukuka. Ndio
maana marekani inatawala dunia; kiuchumi, kisayansi na kijeshi.
II. ASILI INAYOTOKANA NA KABILA ULILOTOKA
ezekiel 16:3 “useme bwana mungu auambia yeerusalemu
hivi;asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya mkanaani, mwamori
alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa mhiti”
kila kabila hapa duniani linasumbuliwa na asili fulani chafu
ambayo si njema na inawavunjia heshima na kuwaletea aibu. Mfano: wahehe
wanatatizo la kujinyonga, wachaga wanatatizo la roho ya wizi, wapare ni ubaili,
wasambaa ni umbea, wasukuma wanasumbuliwa na roho ya uchawi, wakurya ni ukatili
na kuua , wangoni uchawi na mizimu, wamakonde wanasumbuliwa na roho za ujinga
na ushirikina. Shida hii imelitatiza sana taifa hili, taasisi zake, jamii na
makanisa.
III. ASILI INAYOTOKANA NA JINSI ULIVYOZALIWA
zaburi 51:5 “ tazama mimi naliumbwa ktk hali ya uovu, mama
yangu alinichukuwa mimba hatiani”
zaburi 58:3 “wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao,
tangu tumboni wamepotea wakisema uongo”
ni muhimu kujua haya kuwa; mimba yako ilitungwaje?, kulikuwa
na tukio gani siku hiyo? Waamuzi 11:1-3. Kama mama yako yuko hai muulize ili
ujue namna utakavyo omba ili ujinusuru. Hii ni kwakuwa; yale yaliyotoke siku
unazaliwa, yanahusiana na hatma ya maisha yako, nay ale yanayokupata hivi sasa.
IV. ASILI INAYOTOKANA NA TAREHE AU SIKU ULIYOZALIWA
ayubu 3:1-7
tarehe uliyozaliwa imebeba hatma ya maisha yako. Baadhi ya
mambo yanayokupata yanahusiana na tarehe au siku uliyozaliwa. Jiulize maswali
haya; siku uliyozaliwa ni siku iliyo barikiwa ulimwengu wa roho au la?. Nyota
gani ilionekana angani? Mathayo 2:1-2. Nyota yako ina mvuto kiasi gani?,
mathayo2:9-11. Siku hiyo mwezi ulikuwa na umbile gani?......
Nani walikuwepo
V. ASILI INAYOTOKANA NA MADHABAHU ZA KISHETANI NA ZA UKOO
isaya 60:2, “ maana tazama giza litafunika dunia, na giza
kuu litafunika kabila za watu……………………….”
Ezekiel 20:30-34.
Giza kuu linalifunika makabila ni mambiko, maagano ya
kishetani ktk makabila na ukoo. Vilevile giza kuu ni kuabudu mizimu na
kushiriki mambo ya waganga na wachawi. Mambo haya yote yanaleta madhara makubwa
ya kiroho na ya kimwili ktk uso wa nchi.
Maombolezo 5:7 “baba zetu walitenda dhami hata hawako, na
sisi tumeyachukuwa maovu yao”
adhabu itakayo shambulia kabila au ukoo ulioshiriki matendo
haya ya giza ni: laana, magonjwa, vita, ufukara, kutokufanikiwa ktk utumishi,
na kudumaa kwa kihuduma.
VI. ASILI INAYOTOKANA NA TABIA MBAYA
1kor 2:14” mwanadamu ya tabia ya asili hayapokei mambo ya
roho wa mungu…….”
Baadhi ya watumishi au waumini wanasumbuliwa na tabia mbaya
mbaya kutoakana na asili mbaya ya kishetani iliyo ndani yao. Mfano; tabia ya
jeuri, tabia ya ukorofi, kuwa mkali sana, hasira kali sana, na ubishi uliovuka
mpaka au kawaida.
VII. ASILI INAYOTOKANA NA MANENO ULIYOTAMKIWA UKIWA TUMBONI.
ezekieli 16:5 “ hapana jicho lililokuhurumia ili kukutendea
lolote la mambo hayo kwa kukuhurumia, lakini ulitupwa nje uwandani, kwakuwa
nafsi yako ilichukiwa ktk siku ile uliyozaliwa”
maneno uliyotamkiwa siku ile uliyozaliwa, yanahusiana na
hatma yako au yale yanayotokea hivi sasa maishani mwako.
Jiulize maswali haya;
a) siku uliyozaliwa wajomba zako walitamka maneno gani?
B) au wakwe zake mama yako walisema nini siku uulizokuwa
tumboni?
C) iliposemekana kuwa umezaliwa, watu walifurahi au
walichukia?
D) mawifi zake mama yako walikutamkia maneno gani?
Majibu ya maswali haya waweza kuyapata kwa njia ya ufunuo wa
roho mtakatifu,fu 1kor 2:10…….. Au fanya utafiti uliize kwa wazazi wako au
wakubwa zako walokuwepo siku hizo.
VIII. ASILI INAYOTOKANA NA MAPITO ULIYOPITIA
waamuzi 11:1-4
mapito uliyopitia yanaweza kujenga usugu fulani, na kuamsha
asili fulani ya kishetani ndani yako na kuleta maadhara fulani. Mfano:
i. Mateso: yanaathiri mfumo wa akili na saikolojia.
Ii. Kuvuta bangi: akili inaharibika.
Iii. Ulevi: unaleta ufukara na upumbavu.
Isaya 55:6 “mtafuteni bwana maadam anapatikana, mwiteni
maadam yu karibu”….
Sasa , kumtafuta mungu aliye hai, inamaana yuko umbali
fulani, ulimwengu wa roho. Ni lazima ujue kanuni na maarifa ya kuutafuta uso wa
bwana…
anaposema “mwiteni bwana”, maana yake ni kusema; yuko sehemu
au mahali fulani, mahali mbapo ukimlilia na kuliitia jina lake, atakusikia… hii
nayo yataka ufahamu wa ki-mungu wa kukusaidia kujua namna ya kumwita mungu
aliye hai
Math 7:7 "ombeni,nanyi mtapewa,tafuteni nanyi
mtaona,bisheni nanyi mtafunguliwa"
1.maombi ni kutafuta,kubisha hodi kwa mungu.luka 18:1
"akawaambia mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba mungu sikuzote wala
wasikatetamaa"
2.maombi ni kumwendea mungu
ebr 11:6b "kwa maana mtu amwendeaye mungu lazima aamini
kwamba yeye yuko,na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao"
3.maombi ni kuzungumza na mungu isaya 1:18 "haya njoni
tusemezane,asema bwana wa majeshi,
4.maombi ni kuweka wazi haja/mahitaji yetu mbele za mungu
,filip 4:6 "msijisumbue kwa neno lolote,bali katika kila neno kwa kusali
na kuomba,pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na mungu"
5.maombi ni ibada mbele za mungu..mdo 13:2 "basi hawa
walipokuwa wakimfanyia bwana ibada na kufunga,roho mtakatifu akasema,
6.maombi ni kupigana vita vya kiroho,efeso 6:18 "kwa
sala zote na maombi mkisali kila wakati katika roho,mkikesha kwa jambo hilo na
kudumu katika kuwaombea watakatifu"
7.maombi ni kutulia na mungu isaya 30:15 "kwa maana
bwana mungu asema hivi,kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa,nguvu zenu zitakuwa
katika kutulia na kumtumaini lakini hamkukubali"
KWANINI YATUPASA KUOMBA?? MATH 7.7
1..tunaomba ili tupewe haja zetu, "ombeni nanyi
mtapewa",tena neno la mungu linasema wala hamna kitu kwa kuwa
hamwombi,yakobo 4:2 "mwatamani wala hamna kitu,mwaua na kuona wivu,wala
hamwezi kupata,mwafanya vita na kupigana,wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi"
2.ni agizo kutoka kwa yesu..luka 18:1 "akawaambia
mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba mungu siku zote,wala wasikate tamaa"
1thes 5:17 "ombeni bila kukoma"
3.kwa sababu kuomba ni huduma..huponya taifa,familia,kanisa
na watu wanaponywa magonjwa na shida zao na kazi yake jehova hufanikiwa
2nyak 7:14 "ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina
langu,watajinyenyekesha,na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya
basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi
yao"
4. Isaya 59:16 "akaona ya kuwa hapana mtu,akastaajabu
kwa kuwa hapana mwombezi basi mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu na
haki yake ndiyo iliyomsaidia"
yak 5:14-16 "mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite
wazee wa kanisa nao wamwombee na kumpaka mafuta kwa jina la bwana na kule
kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule na bwana
Atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa ungameni
dhambi zenu ninyi kwa ninyi,na kuombeana mpate kuponywa,kuomba kwake mwenye
haki kwafaa sana akiomba kwa bidii"
5..kwa sababu ya kujenga mahusiano yetu karibu na mungu
yak 4:8 "mkaribieni mungu naye atawakaribia
ninyi,itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu,enye
wenye nia mbili"
6..kwa kuwa mungu ni baba na sisi ni watoto wake,yatupasa
kumwomba haki zetu tukiwa kama watoto..
Math 6:9 "basi ninyi salini hivi,baba yetu uliye
mbinguni,jina lako litukuzwe,ufalme wako uje"
MAISHA YA MAOMBI KWA MKRISTO (1)
Wako wakristo ambao tunashindwa kuwa na maisha ya maombi kwa
sababu zifuatazo.
(1) kukosa muda wa kuomba kwa sababu ya majukumu ya muhimu
ya hapa na pale.
(2) mazingira ya mtu anapoishi.
(3) mwingine hajui faida za maombi wala umuhimu wake.
(4) mwingine anasema huwa anaishiwa maneno kwa haraka
anapokuwa kwenye maombi.
(5) mwingine hapendi maombi tu!
(6) shetani.
(7) mwili.
KATIKA MAOMBI KUNA VIKWAZO VINGI, KWA SABABU MAOMBI YANA
NGUVU!
(a) maombi yanaongeza uhusiano wa mtu na mungu!
Maombi ni mawasiliano baina ya mwanadamu na mungu au ni njia
ambayo tunaweza kuwasiliana na mungu. Tunafanya mawasiliano na mungu kwa njia
ya maombi, na kama tunavyojua kwamba! Mawasiliano yanaongeza uhusiano wa mtu na
mtu, hata wewe ni shahidi katika hili! Unaweza ukawa na ndugu wengi sana au
marafiki wengi sana n.k. Lakini yule ambaye atawasiliana na wewe mara kwa mara
huyo ndiye anayeukuza ukaribu kupita wengine. Na pia uhusiano wa mtu
unaanzishwa kwa mawasiliano na vilevile unaweza ukafa au kupungua kwa kukosa
mawasiliano ya mara kwa mara na kuelekezwa kule kwenye mawasiliano ya mara kwa
mara! Mawasiliano yamewafanya watu wengi kuwa karibu, kupitia mitandao yetu.
Mtu alipoanza mawasilano na wewe kwa njia ya kukutumia ujumbe wa maandishi au
wa picha ulipojibu! Mawasilano yakakua mwisho wake ukaribu ukaongezeka kati
yako na huyo….
Tunapokuwa tunaomba mara kwa mara uhusiano wetu na mungu
unakuwa kwa kasi sana kuzidi yule asiyeomba, au yule anayeomba mara moja moja
au yule anayeomba kwa viwango vya juu zaidi! Na kama tujuavyo, kadiri uhusiano
wa mtu na mtu unavyokuwa na kuongekezeka ndivyo wanavyoweza kushirikishana
mambo mengi saaaana!
Ndivyo inavyokuwa kwa mungu kwetu! Kwa sababu mahusiano yetu
yanakuwa na kuongezeka! Mungu hataacha kutushirikisha mambo mengi yanayoendelea
ili kuyaombea au kuzuia yasitokee au kuwashauri watu n.k. Mungu atatuonyesha
hata hatari iliyopo mbele yetu, kwamba! Kuna ajali mbaya itatokea na
kusababisha hiki na hiki na jinsi ya kuikwepa n.k. Yakiambatana na maelekezo
yake jinsi ya kufanya ambayo yatakuwa na lengo la kujenga na si kubomoa!
Utakuwa na furaha na amani wakati woote hata kwenye dhiki za namna gani! Sijui
nitumie lugha gani nieleweke jamani: ili uelewe hili na kulishika kwamba!
Maombi yanaongeza uhusiano wa mtu na mungu!
Tuanze maisha ya maombi kuanzia sasa ili uhusiano wetu na
mungu ukue, anzisha mahusiano yako na mungu kwa kuwasiliana naye mara kwa mara
kwa njia ya maombi. Hata kama zamani tulikuwa na bidii ya kuwasiliana na mungu
kwa njia ya maombi halafu tukayakata mawasilano hayo! Bado tunaweza kuyaanzisha
upya na kuyakuza! Pia usiache kuwasiliana na mungu mara kwa mara kwa njia ya
maombi kwa sababu kwa kutofanya hivyo utauvunja au utaupunguza uhusianao wako
na mungu!
MAISHA YA MAOMBI KWA
MKRISTO (PART 2)
Kwa nini tunazuiwa kuomba? Pamoja na sababu nyingine
zinaonekana kama ni za msingi! Angalia hii!
(b) maombi yanaweza kubadili maamuzi ya mungu aliyoyapanga
kwa taifa au kwa mtu n.k.
Hii tunaipata kwa nabii isaya! Tusome maandiko haya kwa
makini saaana! Isaya 38:1 “siku hizo hezekia aliugua, akawa katika hatari ya
kufa; na isaya nabii, mwana wa amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, ‘bwana
asema hivi, tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa,wala hutapona’.”
Ni ujumbe kutoka kwa nabii! Mungu mwenyewe hapo anasema kwamba
“utakufa”, hebu jaribu kufikiri! Ingekuwa wewe mungu anakwambia hivyo
ungefanyaje? Lakini mfalme huyu alijua hata kama mungu amesema, bado ninaweza
kubadili maamuzi yake kwa sasa kwa njia ya maombi! Alichokifanya mfalme ni
hiki! Isaya 38:2 “basi hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani,
akamwomba bwana..hezekia akalia sana sana.” Hezekia alijua na aliamini kwamba
maombi yanaweza kubadili maamuzi ya mungu kabisa! Baada ya maombi hayo angalia
kilichotokea. Isaya 38:4, “ikawa, neno la bwana likamjia isaya, kusema, enenda
ukamwambie hezekia, ‘mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako;
tazama nitaziongeza siku zako…”. Hapo kuna vitu viwili mungu aliviangalia
wakati hezekia anaomba,
(1) kuomba kwa imani. “ikawa, neno la bwana likamjia isaya,
kusema, ‘enenda ukamwambie hezekia, mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona
machozi yako.” (isaya 38:4).
(2) machozi yaliyoambata na kuomba, japokuwa wako watu huwa
wanasema walokole wanalialia, tunalia ili mungu ayapokee maombi yetu, sisi
hatulii kama hao waliliao mapenzi usiku na mchana!
Maombi hapa yaligeuza maamuzi ya mungu, nafikiri sasa
unaweza kuelewa kwa nini tunazuiwa kuomba. Ndugu kama unaomba; hata kama ni
nani alitamka kitu gani kwako, au katika ukoo wako kwa kulaani laana zozote
zile, unakuta familia nyingine hakuna maendeleo yoyote yale pamoja na bidii
zote za kufanya kazi na kusoma! Hakuna kuoa wala kuolewa n.k. Maombi yana uwezo
wa kubadilisha laana na kuwa baraka na kufumua fumua kila vitu vibaya
vinavyohusika kutukandamiza na kutudidimiza katika maeneo fulani fulani. Hata
kama bosi alisema nitakusimamisha kazi, maombi yanaweza kubadili maamuzi ya
bosi! Kama maombi yaliweza kugeuza maamuzi ya mungu sembuse bosi ? Sembuse rais
wa nchi?
Twende kwenye mfano wa pili uone maombi ambavyo yanakitu cha
kipekee.
Hapa sasa tunaona ibrahimu ambavyo alikuwa anawashawishi
malaika waliotumwa na mungu kwa ajili ya kuiangamiza sodoma na gomora.
Mwanzo18:32. “je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye
haki hamsini katika mji, utaharibu wala hutaacha mji.hasha usifanye
hivyo,…bwana akasema, nikiona katika sodoma wenye haki hamsini mjini,
nitapaacha kwa ajili yao.”
Ibrahimu aliendelea kusema na wale malaika mpaka akafikia
hesabu ya watu 10! Na ibrahimu akaishia hapo, kama ibrahimu angeendelea kusihi
bila shaka maangamizo yasingetokea. (mwa 18:30-32). Zaidi sana walichokifanya
malaika ni kumuondoa lutu na mkewe na wanawe ambao inaonyesha hawakufika 10
kama wangekuwa 10 wasingetolewa ili mji uangamizwe kwa sababu ibra alifanya
maombi na yakajibiwa kwamba kwa idadi ya watu 10 tu na kama hao 10 wangekuwepo
sodoma na gomora isingeangamizwa, wangeachwa na mungu angetumia njia nyingine!
Maana alisema kama wamgekuwa 10 asingeuangamiza mji.
Maombi ni ni kumshawishi mungu kufanya yale ambayo wewe
unataka ambayo yatakuwa ndani ya mpango wake. Kama maombi yanaweza kubadilisha
maamuzi ya mungu; sembuse kubadilisha maaumuzi ya mtu? Ndio maana sijatoka
kuzungumzia mifano ya maamuzi ya wanadamu yalivyobadilishwa baada ya maombi,
nimezungumzia upande wa mungu ili uone maombi ambavyo yana nguvu! Kuna kitu
gani umetamkiwa? Kuna kitu gani unakitaka? Muombe mungu kwa imani!
MAISHA YA MAOMBI KWA
MKRISTO (PART 3)
(c) kuwaacha watu na kwenda kuomba!
Hili ni tendo la ajabu sana ambalo yesu alilifanya! Lilikuwa
ni fundisho kwetu! Hebu jaribu kufikiri; kwa jinsi yesu ambavyo ana kila kitu,
lakini pamoja na yesu na kuwa na kila kitu, lakini alijua pasipo maombi yote
aliyokuwa nayo haiwezekani! Yesu mwenyewe alikuwa anajua hapa bila maombi hamna
kitu! Alifikia mahali anawaacha makutano halafu anakwenda kuomba. Luka 5:12-16.
Hebu tusome mstari wa 16.
“lakini yeye alikuwa akijiepua,akaenda mahali pasipokuwa na
watu,akaomba.”
Hapo yesu anawakimbia makutano na kuelekea zake kwenye
maombi, japokuwa ni ngumu sana kwa baadhi ya watu kuwaacha watu na kwenda kwa
kuomba katika mazingira kama haya ya yesu, kwao ni utukufu. Ikiwa yesu alifanya
hivyo, sisi tunapaswa kufanya hivyo na kuzidi kulingana na maisha yetu na dunia
ya leo, lakini leo mtu anasema hana muda wa kuomba, eti kazi zinambana, na kwa
sababu nyingine zinazofanana na hizo, lakini bado mtu huyohuyo ambaye anasema
hana muda wa kuomba huyo huyo unaweza kumuona katika makundi ya watu au
marafiki akiongea muda mrefu, lakini hao hao wanaosema hawana muda wa kuomba ni
watu hodari sana kwa kuchat, hana muda wa kuomba lakini ana muda wa kuchat na
watu kwa njia ya whatsapp, muda wote anafanya kazi huku yuko whats app! Hana muda
wa kuomba lakini ana muda wa kuongea na watu kwenye simu masaa na masaa, hana
mua wa kuomba lakini anaangalia movie masaa na masaa; hana muda wa kuomba
lakini ana muda wa kuangalia mpira …ninaweza kusema huyu hana muda wa kuongea
na mungu lakini ana muda wa kuongea na watu! Kwa sababu maombi ndiyo kuongea na
mungu.
Kuongea na watu si vibaya; si vibaya kuchat na watu kwa njia
mbalimbali za mitandao, lakini ni mbaya kama tuna muda wa kufanya hivyo lakini
hatuna muda wa kuomba! Ni mbaya sana! Sana ! Inatakiwa ifikie mahali tunaongea
na watu lakini ukifika muda fulani tunajiepua na kwenda mahali kusikokuwa na
watu au mahali ambapo tutaweza kuomba bila buguza! Hapa yesu hakwenda kanisani!
Maombi tunaomba popote pale kama mazingira hayaturuhusu kwenda kanisani, tukipata
nafasi tu kidogo tu; tunaomba hata kimoyomoyo! Kuomba sio lazima iwe kanisani.
Bila maombi tutajikuta tunaishi maisha ya unafiki! Maisha ya
uhitaji wa kupitiliza na kujikuta kwenye madeni wakati wote, ukiondoa maombi
hata unahubiri kila siku lazima iko siku utaanguka tu! Lazima! Tuache mambo ya
kukaa kaa na watu na kuongeaongea muda mwingi tunaumalizia kwa watu. Tena
wakati mwingine mambo mengine hayana hata maana, tunaopoteza kuongea na watu
ambao hata tukienda kulala hata hawajui yanayotusibu katika usingizi wetu.
Hawana sifa ya kuongea na sisi kabla ya kuongea na mungu wetu! Kama yesu
aliomba mwenye huduma kubwa kuliko huduma yako wewe ambaye unalewa na sifa za
watu lakini kuomba hutaki! Sisi tutapona? Shetani alikuwa hana kitu kwa yesu
lakini bado yesu alikuwa anaomba. Tusidanganywe na sifa zinazotoka vinywani mwa
watu.
Tuweke ratiba kwamba! Kuanzia muda fulani ni muda wa maombi.
Hapo hata simu ipigwe hakuna kupokea, tunakwenda mahali pasipokuwa na watu
kifikra! Yesu alikwenda sehemu halisi! Lakini kama mazingira yetu hayaturuhusu
kufanya hivyo, tunapaswa kwenda mbali na watu kifikra! Wakati wa kuomba
ikiwezekana zima simu yako au weka silent kama simu yako ndio kila kitu! Nikiwa
na maana kuna bible n.k.
Yesu naye tungesema hana muda, kwa sababu pale alikuwa
kazini! Lakini alijua umuhimu wa maombi! Kama wewe huna muda usile chakula
basi! Kinachokufanya ule nini wakati huna muda?
Nb: maombi ni kwa faida yetu wenyewe
MAISHA YA MAOMBIKWA
MKRISTO (PART 4)
(d) maombi yanatupa nguvu ya kutoingia majaribuni!
Yesu aliwawaambia wanafunzi wake maneno haya kwa uzito sana
baada ya kuona wanafunzi hawana maisha ya maombi! Walikuwa wanafikiri jukumu la
kuomba ni la yesu tu! Kama sisi tunavyofikiri sasa, kwamba jukumu la kuomba ni
la watu fulani tu, na si la kwetu! Kila mahali ambapo yesu alikuwa anaomba
wanafunzi wake ambao leo tunawatambua kama mitume! Walikuwa hawana maisha ya
maombi. Angalia hapa luka 9:28-32,
“baada ya maneno hayo yapata saa nane, akawatwaa petro na
yohana na yakobo, akapanda mlimani ili kuomba (hilo ndio lilikuwa lengo lakini
angalia matokeo yake).ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka….”.
(hapa yesu anaomba peke yake wale aliopanda nao walishamwacha walikuwa na
usingizi). Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na
usingizi:lakini walipokwisha amka…”
Inaonyesha wazi walikuwa wamelala wakati yesu anaomba!
Walikuwa wanaona shida kuomba kama sisi tunavyoona shida! Lakini tatizo
lilikuwa linajirudia tena na tena kwa wanafunzi mpaka ikabidi yesu awaambie
madhara ya kutokuwa na maisha ya maombi! Hapa lilikuwa tukio jingine sio lile
la mlimani! Mathayo 26:40-41,
“akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia
petro, je! Hamkuweza kukesha nami hata saa moja?.kesheni, mwombe, msije
mkaingia majaribuni.”
Sio toeni sadaka ili msiingie majaribuni, sio hubirini sana
ili msiingie majaribuni, hapa yanatajwa maombi pekee. Kinyume chake hatutaweza
kukabiliana na majaribu, tutashindwa bila shaka. Maombi ndio yananifanya mimi
na wewe kutoingia majaribuni, majaribu yamejaa kila kona katika dunia ya leo,
lakini tutawezaje kuyashinda kama hatuna maisha ya maombi? Hatutaweza kamwe!
Kamwe! Yesu akishasema amesema! Mtu yeyote ambaye hana maisha ya maombi ana
maisha ya kuingia majaribuni! Mtu ambaye kuomba anaona shida; mtu huyo haina
haja ya kupeleleza maisha yake. Jibu lake linajulikana ni mtu wa kuingia
majaribuni na matokeo yake anajikuta anaishi maisha ya unafiki! Anaonekana anahubiri
na kufundisha, anaoneka anapost vitu vya kutia moyo, anaonekana anaombea watu,
lakini maisha yake ni ya kujilaumu wakati wote hana uwezo wa kushinda majaribu.
Ndugu yangu hata kama sisi tunajiita mtume nabii hata kama! Hata kama
tunajulikana vipi kiuimbaji na kukubalika katika nyimbo za injili, sifa na
kuabudu, kama hatuna maisha ya maombi majaribu yakija lazima tutaingia
majaribuni! Hatutaweza kushinda hata siku moja! Leo tunaweza tukajipiga piga
vifua kama petro,na kusema, “mimi nimuache yesu”. Ukisalimiwa “mambo”, unajibu
“mambo kwa yesu”. Misimamo hiyo kama huna maisha ya maombi lazima siku moja
utaingia majaribuni tu! Misimamo bila maombi! Hakuna matokeo ya ushindi.
Namkumbuka binti mmoja ambaye alikuwa ameokoka! Binti huyu
tulikuwa tunaishi naye jirani! Binti alikuwa na misimamo ya hatari sana!
Ilikuwa tukimsalimia “mambo?”. Aanajibu “mambo kwa yesu.” Alikuwa hajibu kwa
mizaha! Alikuwa hataki mchezo mchezo ukizingatia pia kwao pesa zipo na wakati
huo yupo kidato cha tatu! Mimi wakati huo nilikuwa mbali na ufalme wa mungu!
Misimamo ya binti huyu haikudumu kwa sababu hakuwa na maisha ya maombi!
Akaangukia kwa muuza mitumba na uwokovu akauacha! Akakataa shule wakati huo
tayari ameshaanguka tayari; wakati hilo halijaisha vizuri mimba ikaingia
akamwacha yesu! Misimamo bila maisha ya maombi ninakuambia waziwazi wewe binti
ambaye unajulikana shuleni kwako unaposoma, chuoni kwako au kazini kwako, bila
maisha ya maombi unaweza kujikuta unaanguka mahali usipoptarajia.
Yesu alimwambia petro waziwazi katika mathayo 26:34-35,
“…yesu akamwambia, ‘amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo,
utanikana mara tatu. Petro akamwambia, ‘ijaponipasa kufa nawe, sitakukana
kamwe.’”
Petro anajigamba wakati hana maisha ya maombi; muda wa
maombi yeye anasinzia, na ndivyo ilivyokuwa, alimkana yesu kwa kiapo na alisema
mathayo 26:69-74, “ndipo alipoanza kulaani na kuapa na kusema, simjui mtu
huyu.” Unaona, anasema “mtu huyu.”
Wakati petro alikuwa ananyenyekea kwa bwana! Alikuwa anamuita yesu
bwana! Lakini hapa anasema “mtu huyu “. Ndivyo ilivyowatokea wengine ambao
walipuuza maombi, leo ukiwaona utashangaa! Unajiuliza huyu si alikuwa moto wa
kuhubiri, kuomba, kutoa, kuimba n.k.! Peleleza maisha yake kabla, utakuja
gundua alikuwa hana maisha ya maombi! Na ndivyo itakavyotokea kwetu kama
hatutakuwa na maisha ya maombi, ninakuambia wazi kabisa utashindwa tu!
Ndugu yangu omba! Omba! Omba! Ndani ya maombi ndio kuna
nguvu ya kutuwezesha kushinda ushawishi huu uliotanda kila kona katika dunia,
kila siku inafunguliwa mitandao mipya ya kuturahisishia kufanya mambo mema na
hapohapo ya kuturahishia kuingia majaribuni! Tutawezaje kushinda vishawishi
kama hatuna maisha ya maombi? Tutajikuta tunaishi maisha ya unafiki na mwisho
ya siku tutamwita yesu “mtu ” badala ya “bwana” kama ilivyotokea kwa petro!
Tusipoomba kuingia majaribuni sio jambo la kutafuta! Mtu yeyote ambaye hana
maisha ya maombi, mtu huyo hawezi kujizuia katika majaribu, kama sivyo yesu
tunamfanya yesu kuwa ni muongo, na kamwe yesu hawezi kuwa muongo!
Nb: maombi ni kwa faida yetu wenyewe, tukiacha kuomba kwa
sababu zozote kumkana yesu kuko karibu! Omba! Omba! Omba!
MAISHA YA MAOMBI KWA
MKRISTO (PART 5)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu tunapokuwa
katika maombi.
(1) hatupaswi kuwa na mashaka yoyote!
Maandiko yanasema katika yakobo 1:5-7,
“…ila naombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye
mashaka ni kama wimbi la bahari la bahari lililochukuliwa na upepo,na
kuleperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu
kwa bwana.”
Hayo ndiyo maandiko! Hata kama tunaomba masaa 100 mfululizo,
hata kama tunaomba kwa viwango vya vinavyoonekana vya juu sanaa kibinadamu,
lazima maombi yetu yawe ndani ya kanuni, lazima tuombe pasipokuwa na mashaka
tena mashaka yoyote! Hayo ndio maandiko hakuna njia ya mkato; kama tunamuomba
mungu lakini tuna mashaka moyoni au vinywani hilo ni tatizo linalopelekea
kutopokea majibu yetu ya maombi! Kwa nini nasema mtu anaweza akawa na mashaka
moyoni. Mtu mwingine anaweza akaonekana ana imani katika mazungumzo yake, hasa
pale anapokutana na watu , lakini ndani ya moyo wake kumejaa mashaka, na
mashaka hayo mungu huyaona pale mtu anapokuwa peke yake katika fikra au pale
mambo yanapokwenda kinyume na alivyotarajia kutokana na maombi yake!
Akizungumza na watu ni kama amejaa imani! Lakini moyoni kumejaa mashaka
makubwa! Mashaka ni ile hali ya wasiwasi ya kutokuamini. “hivi kweli mungu
inawezekana kweli? Itakuwa kweli? Mungu ananisikia kweli?” N.k.
Hayo yote ni mashaka na kwa mashaka hayo kamwe hatutaweza
kupokea majibu yetu ya maombi! Kamwe! Tukiruhusu mashaka hata kama ni kidogo
tunaambiwa waziwazi, “maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kutoka
kwa bwana.” Yaani, hata ile kudhani, kutegemea, kufikiri, isiwepo. Mashaka ni
adui mkubwa sana anayeshindana na majibu ya maombi yetu yasitufikie.
Wakati mwingine mashaka yanakuwepo baada ya kuomba kitu muda
mrefu na kutoona majibu ya maombi! Wakati mwingine inatokana na kuona mambo
yanakuwa mabaya zaidi kuliko mwanzo! Au uzito wa jambo pia linaweza kuchangia
kukaribisha mashaka na hata shetani pia anahusika lakini anapitia maeneo hayo
hayo!
Ili tuone majibu ya maombi yetu yakiwa dhahiri, hatupaswi
kuruhusu mashaka yoyote hata kidogo! Tukishaomba tu! Mawazo yetu yanapaswa
kufikiri sawasawa na majibu ya maombi yetu, kusema kwetu kuendana na majibu
yetu ya maombi kwa imani, inaweza kuwa sio rahisi kuishi hivyo haiwezi kuwa
rahisi hata kidogo! Na hakuna mbadala wake lazima mashaka yasiwepo ili tupokee
majibu yetu ya maombi! Tunamuomba mungu kwa sababu sisi hatuwezi, tumeshindwa ndio
maana tunaomba! Kama mtu unawashwa mgongoni utamwomba mungu “niwezeshe
kujikuna?” La! Tutajikuna kwa sababu jambo hilo liko ndani ya uwezo wetu!
Tunapomuomba mungu maana yake sisi hatuwezi, tumeshindwa!
Rahisi kufikiri nguvu za mungu hazipo; rahisi kufikiri ukimwomba mungu basi
majibu yanachukua muda mrefu! Hatupaswi kuyaruhusu mawazo hayo kufanya kazi
ndani yetu kamwe! Sisi tunachotakiwa kuamini mungu yupo na anajibu maombi na
hakuna gumu la kumshinda! Mashaka yanapokuwa yanakuja kwa njia zozote zile, iwe
kupitia watu kwa maneno yao; n.k. Hatupaswi kuyaruhusu kwa sababu, tukiruhusu
mashaka maandiko yanasema tusitarajie kupokea kitu kutoka kwa bwana!
Kuna wakati yesu alikuwa anatembea juu ya bahari! Na petro
akaomba atembee au apewe uwezo na yesu wa kutembea juu ya bahari! Yesu
akayajibu maombi yake na akamwambia petro atembee…lakini petro aliporuhusu
mashaka baada ya kuuona upepo, akazama mbele ya yesu! Yesu akamuokoa kwa
kumshika mkono sio kwa kumuombea bali alimshika mkono na akamwambia! (mathayo
14:26-31.31):
“mara yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, ‘ewe
mwenye imani haba, mbona uliona shaka?’”
Unaona hapa! Petro anazama mbele ya yesu kwa sababu
aliruhusu mashaka, na sisi sio kama tukimuomba mungu kitu fulani basi kinakuwa
mtelemko! Inaweza ikatokea upepo mkali kwenye biashara zetu kwa viwango vya
kuporomosha kabisa mitaji yetu! N.k. hatutakiwi kuwa na mashaka katika hali
yoyote! Tusimamie matokeo tusiangalie mazingira tuliyonayo kwa sasa, tukiwa na
mashaka tutazama tu hata kama yesu yupo ndani mwetu!
Wakati wote tunapomuomba mungu, tuombe bila mashaka yoyote
yale! Mungu yupo na nguvu zake zipo vilevile! Hata mimi nikikufanyia maombi na
ukaanza kuona matokeo, yaani, unatembea juu ya bahari kama petro! Lolote
likitokea kama upepo likiwa na lengo la kubadilisha hilo, hupaswi kuwa na
mashaka unapaswa kuendelea kuamini! La sivyo utazama kama petro na kuupoteza
muujiza wako! Kama petro alizama mbele ya yesu kwa sababu ya kuruhusu mashaka!
Sembuse mwanadamu anayeitwa….. .
Yakobo 1:5-6,
“…ila naombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye
mashaka ni kama wimbi la bahari la bahari lililochukuliwa na upepo, na
kuleperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu
kwa bwana.”
Tumwombe mungu atuongezee imani atupilie mbali mashaka
yaliyomo ndani mwetu na atupe kuyashinda kila yanapoinuka. Hata kama maombi
yetu yatachukua muda mrefu bila kuona majibu yake, bado hatupaswi kuruhusu
mashaka, tena mashaka yoyote yale.
MAISHA YA MAOMBI KWA
MKRISTO ( 6)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu, tunapokuwa
katika maombi.
(2) kuomba vibaya ili tuvitumie kwa tamaa zetu!
Tunaweza tukawa kweli tunaomba, tunaomba ili tupate kazi
fulani, tunaomba mungu atutumie tukiombea watu wapone na mungu akutane na haja
zao! Mwingine anaomba apate nyumba nzuri, mwingine gari, honda, n.k. Yote haya
ni mema, lakini kama mtu anaomba moyoni kumejaa nia nyingine (kama uchoyo au
kiburi), moyoni anasema au anawaza kwamba, “nikipata gari ninalolitaka, watu
watanikoma.” “nikipata pesa hee! Watanitambua”, n.k.
Mwingine ni kipofu tangu kuzaliwa anamuomba mungu lakini
moyoni anawaza au anasema, “sijawahi kuona mwanamke tangu kuzaliwa kwangu,
nikiona sijui itakuwaje watanikoma, maana naishia kusikia tu na kuhisi” unaona!
Mtu anaomba lakini moyoni mwake anawaza nikikipata nitakutumia hivi au vile,
matumzi yenyewe ni nje ya mpango wa mungu. Ndugu yangu hapo tutaomba na
kuombewa lakini kamwe hatuwezi kupokea majibu ya maombi! Tunataka mtoto lakini
hatujaoa/hatujaolewa wala hatutaki kusikia habari za kuoa au kuolewa!
Mwingine anataka mungu amtumie lakini moyoni mwake kumejaa
mashindano ya dhahiri, anawaza kumzidi yule, mwingine anataka sifa tu! Mwingine
anawaza utajiri kwamba nitakuwa napata sadaka nyingi za watu n.k. Maandiko
yanasema katika yakobo 4:3,
“hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili
mvitumie kwa tamaa zenu.”
Unaona maandiko hayo? Kama tunamuomba mungu tukiwa na hali
hiyo! Kamwe hatuwezi kupokea majibu ya maombi. Ni kupoteza muda tu! Na mwisho
wa siku tunaona kama mungu hayupo; mungu yupo na anajibu maombi! Tatizo lipo
kwetu tu! Tunaomba ili tukipata tuvitumie vibaya! Kama tunataka kumuona mungu
lazima tuzingatie tunaomba ili tuvitumiaje? Nje ya mpango wa mungu! Tuko watu
wengi tunaomba na kufikia wakati tunafunga! Lakini tunaomba ili tuvitumiaje
hivyo tunavyovitaka kwa njia ipi?
“hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili
mvitumie kwa tamaa zenu.” Yakobo 4:3.
Kuomba tunaomba kweli! Lakini hatupati kwa sababu tunaomba
vibaya ili tuvitumie kwa tamaa zetu! Tangu wakati huu tuhakikishe nia zetu
zinakuwa safi mbele za mungu ili tuyaone majibu yetu ya maombi na nguvu ya maombi!
Maombi yana kanuni zake na ikiwa mtu anataka kumuomba mungu na kumuona mungu
dhahiri akijidhihirisha kwake binafsi hatuna budi kuzingatia yote tunayopaswa
kuyazingatia.
Lolote tunaloliomba lazima tangu moyoni huko ambako mungu
anaanza nako kwa kumuangalia mtu anataka hili ili iwe nini? Mwingine anatumia
pesa kunyanyasa watu, mungu huwa hamuinui mtu ambaye ana visasi, yaani mungu
akinipa hivi fulani atanikoma! Kila anachofanya mungu ni kwa utukufu wake tu
sio kwa utukufu wa mtu yeyote.
MAISHA YA MAOMBI KWA MKRISTO (7)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu, tunapokuwa
katika maombi.
(3) hatupaswi kukata tamaa na kuachia maombi njiani baada ya
kuona tunaomba muda mrefu bila kuyaona majibu yetu ya maombi kwa dhahiri!
Hakuna sehemu ngumu inayotushinda watu wengi kama hii! Watu
wengi tunataka tukishaomba tu; basi tupokee majibu yetu ya maombi muda huo huo!
Mungu hafanyi kazi hivyo ndugu yangu! Mungu ni wa utaratibu sana! Tunapomuomba
mungu tunatakiwa kuamini kwamba imekuwa. (matha 7:7).
Hilo ndilo la kuliamini na kulishikilia wakati wote,
haijalishi majibu yetu ya maombi tutayaona lini, sisi tuamini kwamba mungu
ametenda huku tunaendele kumwomba mungu mpaka liwe dhahiri lile tunaloliomba.
Mungu aliumba mbingu na nchi kwa muda wa siku 6, (mwa 1:1). Unafikiri kwa uwezo
wa mungu! Kwa nini hakutumia siku moja tu kufanya kila kitu? Je! Hakuwa na
uwezo huo? Uwezo upo mkubwa tena sana – mungu ni wa utaratibu sana, ana nguvu
ana uwezo lakini ni wa utaratibu mno! Mnoooo! Mbona basi wewe na mimi tunakata
tamaa mapema hivyo na kuacha kuendelea kuomba! Tunaona mungu hatusikii ni kama
anawasikia wengine! Ni kama ana watu wake maalumu na sio sisi? Hatupaswi kuwaza
hivyo hata kidogo, na tusiyape nafasi mawazo hayo! Tunapaswa kuendelea
kung’ang’ania mbele za bwana mpaka tuone majibu yetu ya maombi yawe dhahiri.
Maandiko yanasema katika luka 18:1,
“akaawambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba mungu
sikuzote, wala wasikate tamaa”.
Hayo ni maandiko! Mungu anatambua kwamba! Mtu anaweza
akaomba jambo na likachukua muda mrefu na mpaka mtu anafikia mahali kukata
tamaa na kuacha kuomba, ndio maana inatajwa hapo “wala wasikate tamaa”.
Uwezekano wa kuchelewa kuyaona majibu yetu ya maombi
unawekwa wazi na bwana mwenyewe, lakini hatupaswi kukata tamaa! Marufuku kukata
tamaa, usikate tamaa! Endelea kuomba, usiachie njiani hata kidogo! Usiwaze
“ooh! Labda kuna makosa nimeyafanya, labda nimefanya dhambi.” Kwani ukifanya
dhambi hujui? Maandiko yanasema! 1 petro 5:6, “basi nyenyekeeni chini ya mkono
wa mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake”. Kumbe kuna wakati wa
mungu! Wakati wa mungu ni mzuri ndugu kuliko wakati wetu sisi! Mungu ndio
anajua wakati mzuri wa kukupa jibu lako la maombi! Usione unakawia, wakati wako
ndio unakawia, lakini wakati wa mungu ni bora saaana! Mungu anajua wakati gani
ukipata kazi utakuwa mzuri kuliko wakati fulani; mungu ndio anajua wakati gani
ukipata mtoto utakuwa mzuri zaidi! Wewe unataka mtoto sasa lakini mungu
akiangalia anona sasa sio salama! Unataka mungu akutumie kwenye hili au lile
n.k. Sisi tuendelee kumlilia bwana! Kupokea ni lazima! Kukata tamaa ni
marufuku! Hatupaswi kukata tamaa kamwe! Tuyashinde mawazo ya kutukatisha tamaa!
Mungu yupo na anajibu maombi.
MAISHA YA MAOMBI KWA
MAOMBI KWA MKRISTO (PART 8)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu,tunapokuwa
katika maombi.
(4) Tunapaswa kuwa na imani kwamba mungu yupo na anatusikia
na anajibu maombi!
Ndugu yangu, hata kama tutaomba na kujigalagaza na kulia kwa
uchungu mpaka kutoka makamasi! Lakini kama hatuna imani ni buuure, bure!
IMANI NI NINI? Imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni bayana na mambo yasiyoonekana, waebrania 11:11. Hiyo ndio
imani! Tunaomba tunatarajia kupokea, sasa imani ni kuwa na uhakika kwamba! Hiki
ninachikiomba kinakwenda kuwa sawasawa na nilivyoomba! Imani huwa haingalii mtu
wala huwa haijilinganishi na mtu yeyote! Imani inaangalia uwezo wa mungu tu na
neno lake basi! Imani haingalii mazingira n.k. Imani inaweza kukufanya wewe
kuwa wa kwanza kukipata hicho unachokiomba! Maandiko yanasema,
“lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu
amwendeaye mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale
wamtafutao.” (waebrania 11:6).
Tunatakiwa kuwa hivyo tunapokuwa tunamuomba mungu, tusiombe
ili mradi tu, tusiombe ili kutimiza wajibu tu, tusiombe kwa desturi na mazoea!
Kwa kufanya hivyo tutadangayika kwamba hakuna nguvu yeyote katika maombi, kumbe
ni uongo wa ibilisi tu. Tunapaswa kumuamini mungu tunapokuwa tunaomba! Na imani
pasipo matendo imekufa! Baada ya maombi lazima uonyeshe matendo na sio unalala
tu na kupigapiga soga na watu! Lazima ufanye matendo kama ni kazi tafuta kazi
n.k.
Kutokuwa na imani ni dhambi vilevile! Ndugu yangu
inawezekana umekuwa una muomba mungu kwa muda mrefu lakini huna imani! Yesu
alikutana na vipofu,angalia hapa! “yesu alipokuwa akipita kutoka huko,vipofu
wawili wakimfuata wakipaza sauti. Yesu akawaambia, ‘mnaamini kwamba naweza
kufanya hili?’ wakamwambia, ‘naam bwana.’ ndipo alipowagusa macho yao
yakafumbuka.” Mathayo 9:27-30.
Unaona hapo? Baada ya kusema wanaamini ndipo yesu
alipowajibu majibu yao kwa kuwafumbua macho yao! Na hakuwafumbua macho kabla ya
kujibu kwamba anaweza! Kabla ya kuionyesha imani yao! Na sisi mungu anatuuliza
kila tunapomuomba! Je! Tunaamini kwamba anaweza kufanya hilo au hayo tunayomuomba?
Kila tunapoomba swali linakuja katika ulimwengu wa roho kwako binafsi, “je!
Unaamnini naweza kufanya hili?”
Imani ni lazima tunapokuwa katika maombi!
MAISHA YA MAOMBI KWA MKRISTO (PART 9)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu, tunapokuwa
katika maombi.
Sehemu ya 9 na mwisho kwa somo hili!
(5) DHAMBI
Maandiko yanasema katika kitabu cha isaya,
“tazama, mkono wa bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa
wala sikio lake si nzito,hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu
yamewafirikisha ninyi na mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone
hata hataki kusikia.” (isaya 59:1-2).
Kama tunafanya dhambi, mungu kamwe! Hawezi kutusikiliza.
Kamwe! Lazima maisha yetu yampendeze yeye tunayemuomba ili atupe kile
tunachomuomba! Tunapaswa kuhakikisha dhambi kwetu ni mwiko kabisa kuzifanya
wala kuziwaza! Tukiwa hivyo tunauhakika wa wazi wa kupokea majibu yetu ya
maombi! Na hivi ndivyo ninavyohitimisha somo la maisha ya maombii! Maandiko
yanasema katika isaya 53:1,
Kwa nini tuombe?
Kwa mkristo, maombi ni kama kupumua. Ni rahisi kufanya
kuliko kutofanya. Tunaomba kwa ajili ya sababu mbalimbali. Kwa sababu moja
maombi ni njia ya kumtumikia mungu (luka 2:36-38) na kumtii. Tunaomba kwa
sababu mungu anatuamuru kuomba (wafilipi 4:6-7). Maombi yamedhihirishwa kwetu
na yesu pamoja na kanisa la kwanza (mariko 1:35; matendo ya mitume 1: 14; 3:1;
4: 23-31; 6:4; 13:1-3). Kama yesu aliehesabu kuwa maombi ni kitu cha maana, pia
nasi lazima. Kama aliitajika kuomba ili asalie katika mapenzi ya baba yake, je
tunahitajika kuomba kiazi gani?
Sababu nyingine ya kuomba ni kuwa mungu anataka maombi yawe
njia kupata suluhisho lake kwa hali zetu. Tunaomba tukijiandaa kufanya maamuzi
muimu (luka 6:12-13); ilitushinde vizuizi vya shetani (mathayo 17:14-21);
kukusanya wafanyi kazi kwa sababu ya mavuno ya kiroho (luka 10: 2); kupata
nguvu ili tuyashinde majaribu (mathayo 26:41); na kupata njia ya kuwatia
wengine nguvu kiroho (waefeso 6:18-19).
Tunakuja kwa mungu katika mahitaji yetu kamili, na tuko na
ahadi ya mungu kwamba maombi yetu si ya bure, hata kama hatupati chenye
tunauliza (mathayo 6:6; warumi 8:26-27). Ameahidi kuwa tunapouliza vitu ambavyo
viko katika mapenzi yake, atatupa chochote tuitizacho (1 yohana 5: 14-15).
Wakati mwingine anakawisha majibu yake kulingana na hekima yake kwa manufaa
yetu. Katika hali hii tunastahili kuwa makini na kudumu katika maombi (mathayo
7:7; luka 18:1-8). Maombi yasionekane kama njia zetu za kumfanya mungu kutenda
mapenzi yetu duniani, bali iwe ni njia ya mungu kutenda mapenzi yake duniani.
Hekima ya mungu inapita hekima yetu.
Kwa hali ambazo hatuwezi jua mapenzi ya mungu kamili, maombi
ni njia ya kutambua mapenzi yake. Ikiwa mwanamke myunani aliyekuwa na binti
aliyepagagwa na mapepo angeponywa (mariko 7:26-30). Ikiwa kibofu nche ya yeriko
angemwita kristo kwa sauti, angebaki kibofu (luka 18: 35-43). Mungu amesema
kuwa kila mara tunaenda bila kwa sababu hatuulizi (yakobo 4:2). Kwa njia
nyingine maombi ni kama kushiriki injili na watu. Hatujui ni nani ataitikia
ujumbe wa injili hadi pale tunapoishiriki. Kwa njia hiyo hiyo, hatuwezi kuyaona
matunda ya maombi yakijibiwa hadi tuombe.
Ukusefu wa maombi yaonyesha ukosefu wa imani na ukosefu wa
imani katika neno la mungu. Tunaomba ili tuonyeshe imani yetu kwa mungu, kuwa
atatenda vile ameahidi katika neno lake na kubariki maisha yetu utele zaidi ya
vile tumeuliza na kutumainia (waefeso 3:20). Maombi ni njia ya kuona kazi ya
mungu katika maisha ya wengine. Kwa sababu ni njia yetu ya “kujitupa ndani” ya
nguvu za mungu, ni njia yetu ya kumshinda shetani na jeshi lake ambalo hatuna
nguvu za kulishinda sisi wenyewe. Kwa hivyo mungu anatupata kila mara mbele ya
kiti chake cha enzi, kwa vile tuko nakuani mkuu mbinguni anayeweza jua yote
amboyo tunayapitia (waebrania 4:15-16). Tuko na ahadi yake kuwa maombi ya
mwenye haki yatatenda mengi (yakobo 5:16-18). Na mungu atukuze jina lake katika
maisha yetu tunapomwamini na kukuja kwake kila mara katika maombi.
AINA ZA MAOMBI YA KUFUNGA
Tunapofunga na kuomba tunayatafuta mapenzi ya mungu katika
jambo fulani. Bwana yesu alitufundisha kuomba na akasema tuombapo tuombe ya
kwamba “mapenzi ya mungu yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” #mathayo
6:10. Kwa hyo kusudi la kufunga na kuomba ni kuyatimiza mapenzi ya mungu hapa
duniani kama huko mbinguni! Kuyatimiza mapenzi katika hayo tunayoutafuta uso wa
mungu.
Kufunga na kuomba hakumfanyi mungu ayabadilishe mapenzi
yake. Hatufungi kuwaonyesha wanadamu ya kwamba sisi ni wa kiroho sana. Kwamba
labda twamjua mungu sana. Hapana. Tunayatafuta mapenzi ya mungu maishani mwetu.
Haijalishi umeokoka miaka mingi ilopita au hivi karibuni.
Tukumbuke maneno ambayo mungu aliyasema ktk 2nyak 7:14
“ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na
kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na
kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao”
kwa kufunga na kuomba tunamruhusu roho mtakatifu azihuishe
nafsi zetu na kutufanya tuweze kusikia sauti ya mungu na kumtii katika maisha
yetu.
KWA UJUMLA TUNAFUNGA ILI:
• kuna watu wanafunga kwa sababu za kimwili kabisa. Kwamba
miili yao imefika wakati inawapa shida. Matamanio ya mwili yameshindwa kuwasiliana
vizuri na roho. Kuna nyakati tamaa za mwili zinakuwa kubwa na hivyo kwa kufunga
na kuomba waweza kuutiisha mwili huu. Kwa vijana hasa, vyakula na vinywaji
tunavyokula vinaleta shida wakati mwingine ndani ya mwili. Kwa kufunga
unautiisha mwili na kuzinyamazisha tamaa hizo. Wengine wanafunga kwa ajili ya
kuyatiisha mawazo. Bwana yesu akasema mawazo ndiyo yamtiayo mtu unajisi. Kabla
mtu hajafanya uasi fulani huanza kujichafua katika mawazo yake. Ndani ya mawazo
yake ataua, atamtukana mtu, atazini, ataiba yani atafanya kila lililo baya
kabla hajalifanya katika ulimwengu wa kimwili. Rafiki yangu mmoja akasema ikiwa
mwanadamu anaweza kupangilia mipango mbali mbali miovu hadi akaitimiza kwa nn
asiweze kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya mungu? Kwa hyo wakati mwingine mtu
anafunga kuyatiisha mawazo machafu ndani yake. Mawazo machafu hututia unajisi!
Ndo maana mtume paulo akasema “basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo,
na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza
utakatifu katika kumcha mungu” 2kor 7:1
• lakini kiroho tunafunga ili kuweka mahusiano yetu na mungu
vizuri rohoni. Ezra 8:21-23
“ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto ahava, ili tupate
kujinyenyekeza mbele za mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu
sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
AINA YA MIFUNGO:
1. MFUNGO KAMILI
katika mfungo huu hakuna kula kabisa chakula kigumu bali
waweza kunywa maji au kimiminika chochote cha kukusupport.
Siku ngapi waweza kufunga mfungo wa aina hii unategemea na
neema na malengo yako katika mfungo huo. Wengine huenda siku moja, mbili, tatu,
wiki, n.k n.k
2. MFUNGO NUSU
mfungo nusu huanzia saa 12 asbh hadi saa 9 mchana au kuanzia
jua linapoibuka hadi linapozama. Mfungo ambao madhehebu mengine wamewazoeza
waumini wao kuufanya. Wengine wameweza kuufanya kila ijumaa. Madhehebu ambayo
yamewazoesha watu wao kufunga angalau kila wiki mara moja wameweza kuwa na
mafanikio makubwa sana katika kuzifungua nira na vifungo mbali mbali
3. MFUNGO WA DANIEL
daniel alifunga mifungo miwili ya aina yake;
• katika sura ya i daniel alifunga alikula mboga mboga tu
(yaweza kuwa alikula mboga mboga na juisi fulani fulani)
• katika sura ya 10 daniel alifunga kwa siku 21 kwa kutokula
chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwake”
MAOMBI KWAAJILI YA WAGONJWA.
Bwana yesu ninakushukuru kwaajili ya majira na muda huu
ambao umenipa kibali kwaajili ya kuombea wagonjwa. Nakushukuru sana mungu wetu
kwani wewe ni mwuumbaji wetu. Mungu ulituumba kwa mfano wako na kwa sura yako.
Nakushukuru mungu. Asante kwa mamlaka ambayo umetupati wanao kwa damu yako
takatifu iliyomwagika msalabani. Asante kwani ulisema tutaweka mikono juu ya
wagonjwa nao watapata afya. Asante mungu kwani wewe si mwanadamu hata useme
uongo.nakuja kwako muda huu kwa unyenyekevu mkuu nikiomba toba kwaajili ya
wagonjwa wote. Natubu kwaajili yao bila kujali kuwa magonjwa waliyonayo ni
matokeo ya dhambi ipi. Haijalishi iwe ni matokeo ya zinaa,kukiuka kanuni za uumbaji,uchafu,uchawi,uganga
au ushirikina natubu mungu wangu. Najua wewe ni mungu wa rehema naam
utatusamehe. Natubu kwakutokuamini kwetu naomba utusamehe mungu wetu. Umesema
nami ktk neno lako la zaburi 103:3 kuwa akusamehe maovu yako yote,akuponye
magonjwa yako yote.ndivyo hivyo mungu leo tenda kwa wagonjwa wote. Haijalishi
ni ugonjwa gani mtumishi wako anasumbuliw,haijalishi taarifa ya daktari
inasemaje juu ya ugonjwa wake,haijalishi wauguzi wake wamemtishaje na wala
haisumbui kuwa dawa zake hazipo duniani kote lakini ninachojua kuwa upo wewe
yesu usiyeshindwa jambo. Ktk jina la yesu kristo naachilia uponyaji wa mama
yule,baba yule,kijana yule,mtoto yule na wana wa kike kwa wa kiume.pokea
uponyaji ktk jina la yesu kristo. Naharibu makao yote ya shetani ndani yako ktk
jina la yesu. Nang'oa kila pando lisilotokana na mungu ndani yako sasa ktk jina
la yesu kristo. Nafuta maneno yote machafu yaliyosemwa kinyume nawe naam
napanda maneno ya kristo ndani yako sasa. Sikia hii ripor ya daktari imesema
una ukimwi nami kwa mamlaka ya yesu kristo naifuta riport hiyo naninatangaza
riport ya yesu kuwa huna ukimwi tena ktk jina la yesu kristo. Daktari
kakuandikia kuwa poor prognosis yaani unakufa nami leo nakuandikia ktk jina la
yesu kuwa huta kufa bali utaishi na utasimulia ukuu wa mungu. Ktk jina la yesu
natangaza uponyaji kwa kila mgonjwa au ndugu wa mgonjwa aliyesoma sala hii kwa
imani. Umekuwa mzima ktk jina la yesu kristo mwana wa mungu. Amina..
Kama una mgonjwa hajiwezi au yupo mbali nawe basi soma sala
hii kwa imani kisha ukimaliza mpigie mwambie anywe au anyweshwe maji kidogo
kwenye glass na mara atapokea uponyaji ktk jina la yesu. Na wale wenye virusi
vya ukimwi baada ya sala hii wakae siku saba alafu wakapime virusi naam wataona
mungu atakavyo washangaza. Mrudishie mungu sifa na utukufu kwani yeye ndiye
afanyaye
NAMNA YA KUMWITA,KWENDA NA KUMUOMBA MUNGU ILI AKUSIKILIZE.
.yeremia 29:12 “nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami
nitawasikiliza”.
Watu wengi wamekuwa wakitamani maombi wanayoyapeleka mbele
za mungu kusikilizwa.watu wanaomba kila aina ya maombi inayowezakana maadam
mungu asikie na kuwaokoa kutoka kwenye shida waliyonayo au kuwapa haja za mioyo
sawasawa na uhitaji wao.
Wapo wanaoomba na wanaona majibu yao yanajibiwa lakini pia
lipo kundi jingine kubwa ambalo wanaona kama vile mungu
amenyamaza,amewaacha,hawasikii, au wanajiona kama vile mungu amewakataa na
kuziona ahadi za mungu kwamba si za kweli na mbaya zaidi wengine wamefika
mahali pa kumwacha mungu kwa sababu ya kushindwa kuvumilia majibu kutoka kwa
mungu na hivyo kutafuta njia mbadala za kutatua matatizo yao.wapo walioomba
kuhusu watoto,ndoa zao,afya zao,ajira,biashara,elimu zao nk. Walipoona katika
fahamu zao mungu hajibu basi wakaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji,wachawi na
kwa miungu mingine kutafuta msaada huko.
Sasa ili mungu aweze kusikiliza au kujibu maombi yako huenda
kuna mambo mengi ya msingi ambayo mwombaji anapaswa kuyajua na kuyatendea
kazi.sasa baada ya kuona maombi mengi ninayoomba na pia ambayo wana wa mungu
pia wanaomba hayajibiwi ili nilazimu nimuombe mungu anifundishe vizuri kuhusu
hili neno.
Hivyo hayo ninayoenda kukushirikisha ni sehemu ya yale
ambayo mungu amekua akifundisha naamini na wewe yatakusaidia maana nimeona
yakinisaidia binafsi pamoja na wale ambao mungu amenipa kuwafundisha kwa njia
nyingine.
Lengo la ujumbe huu ni kukupa maarifa yatakayokusaidia
kuomba maombi ambayo wewe mwenyewe.pindi unapoomba utakua na uhakika mungu
anakusikiliza kwa wakati huo.zaidi
ujumbe huu umekusudia kukufundisha namna unavyoweza ukapeleka maombi mbele za
mungu.
Siku moja nikiwa chuoni mwaka wa kwanza majira ya tisa
jioni,nilikua nikipandisha ngazi kuelekea chumbani kwangu ambacho kilikua
ghorofa ya tatu juu kabisa.wakati naanza kupandisha zile ngazi nikasikia mtu
ananiuliza ndani yangu je hivi mungu huwa
anaitwaje?anaendwaje?anatafutajwe?anakaribiwaje? Nilipofika chumbani nikaanza
kutafakari haya maswali na baadae ndipo nikapata hii mistari katika yeremia
29:12-13 inayosema “nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza.
nanyi mtanifuata na kuniona,mtakaponifuata kwa moyo wenu wote.”Baada ya kuisoma
vizuri ndio nikagundua karibu maswali yale yote yalitoka hapa.
Mungu anasema nanyi mtaniita, sasa na mimi nikuulize swali,
hivi umeshawahi kujiuliza mungu tunamwitajemwitaje? Tunamwendeaje? Na
tunamtafutaje. Usiishie kusema mungu ameseam nikaribieni nami nitawakaribia,
umneshawahi kujiuliza anaposema tumkaribie yeye yuko wapi? Na pia tunamkaribia
kwa namna gani? Sasa hayo ndio maswali yaliokuwa yakinijia.
Picha ambayo mungu alitaka niipate kwenye zile ngazi ni hii,
nifikirie kwamba kile chumba kule juu ndiko aliko yeye yaani mbinguni. Sasa
baada ya kufikiria hivyo ndio niwaze na nijiulize amesema nimuite nimwendee
nimtafute n.k sasa hivi ndio ninamwitaje, ninamwendeaje na ninamtafutaje?
Nilipozidi kutafakari hiyo mistari roho mtakatifu akanifundisha yafuatayo:
Kwanza alinionyesha makosa matatu ambayo watoto wake mara
nyingi tumekuwa tukiyafanya wakati wa maombi. Na ningependa na wewe uyajue kwa
maana itakusaidia ili bado unayafanya basi usiyafanye tena.
KOSA LA KWANZA, KUOMBA KINYUME AU NJE YA MAPENZI YA MUNGU.
1 yohana 5:14 inasema na huu ndio ujasiri tulionao kwake ,ya
kuwa,tukiomba kitu sawa na mapenzi yake atusikia” moja ya tafsiri za kiingereza
inasema “we are certain that god will hear our prayers when we ask for what
pleases him” kosa kubwa ambalo tumekuwa tukilifanya mara nyingi ni kuomba vitu
au mambo ambayo ni kinyume na mapenzi ya mungu.
Anaposema sawasawa na mapenzi ya mungu maana yake ni lazima
ujue kwanza nini ni mtazamo au mawazo ya mungu juu ya hilo unalotaka
kuliombea.maombi ni kuzungumza au kusemezana na mungu kwa kumwambia yale ambayo
amesema kwenye neno lake kuhusu haja zako wewe.
Kwa lugha nyingine usiombe kitu ambacho hujui nini mawazo ya
mungu juu ya hicho kitu. Mawazo ya mungu juu ya kila haja ujyonayo yako ndani
ya neno lake .hivyo ni lazima neno la mungu likae kwa wingi ndani yako ili
unapoomba uombe kulingana na ahadi zake na pia sawa na kile alichokisema.
Zaidi pia wengi wanapotaka kuomba huenda kuhusu
ndoa,kanisa,ajira,watoto ,biashara nk huwa wanomba kimazaoea. Maana yake ni hii
wengi wamezoea ninpoombea ndoa nitaombea amani,upendo ,furaha nk sasa sina
maana hayo maombi hayafai ila ninachotaka ukipate ni hiki hoja unazozipeleka
mbinguni hakikisha umefunuliwa na mungu mwenyewe.maana yake mungu ndiye akupe
mambo ya kuombea kuhusu nchi ,ndoa,biashara yako nk.
KOSA LA PILI:, KUKOSA UTULIVU NA USKIVU WA ROHONI WAKATI WA
MAOMBI NA BAADA YA MAOMBI.
Sikiliza mungu anayo mambo mengi ya kukuambia wewe kuliko
yaje wewe uliyonayo wewe kumweleza yeye. Chungu hakiwezi kumwambia mfinyanzi
kwamba ulinumba kwa kazi hii tu, bali mfmyazi ndiye mwenye mengi kuhusu kile
chungu.
Ndio maana yesu anasema si ninyi mlionichagua mimi bali ni
mimi niliyewachagua njnyi (yohana 15:16),sasa watu wengi sana wana bidii nzuri
ya maombi wanaweza wakakaa hata masaa matatu mfululizo na hata zaidi wanamuomba
mungu tu.
Katika mda huu wote wao ndio wanaojieleza na mara
wanapomaliza ni kusema ameni na kuondoka.hii ni picha ya mtoto anayekuja kwako
kama mzazi anasema baba/mama naomba hela ya daftari, nauli na ya kula shuleni,
pia naomba uninunulie suruali nk. Sasa kabla wewe hujamjibu yeye ameshafungua
mlango na kuondoka.sasa kibiblia ndiko kunaitwa kukosa utulivu na usikivu wa
rohoni mbele za mungu.
Mara zote unapoomba jifunze kuwa na wakati wa kutulia
kusikiliza mungu naye anasema nini.kwenye utulivu ndiko mungu anakosema sio
kwenye kelele maana anjua hamwezi kusikilizana.soma isamwel 3:1-10 utaelewa
ninachokisema hapa.mungu alisema na samweli alipotulia.
KOSA LA TATU, KUMUOMBA MUNGU WAKATI TAYARI
UMESHAJITAFUTIAJIBU LA SHIDA ULIYO NAYO.
Hili ni kosa jingine kubwa ambalo wana wa mungu wamekuwa
wakilifanya. Wengi wana mahitaji mbalimbali.wapo watu wengi ambao kweli
wanaomba kwa kumaanisha mbele za mungu na wengine hata kufunga kwa masaa mengi
lakini tatizo lao katika fahamu zao wameshafanya uamuzi wa nini watafanya baada
ya maombi yao.sasa hata mungu akikushirikisha mawazo yake si rahisi ukamwelewa
kwa sababu tayari kwenye nafsi na ufahamu wako kuna jibu na biblia inasema
aonavyo mtu katika nafsi yake ndivyo alivyo.
Sambamba na hilo, kosa linalofanana na hili ni wale watu
wanaomwomba mungu afanye kama vile wao waonavyo kataka nafsi zao. Yaani
wanamtaka mungu akubaliane na mawazo yao na njia zao juu ya shida au haja
walizo nazo wao wenyewe.
Na jambo hili tunalielewa vizuri tunaposoma katika kitabu
cha luka 9:12 -17 .habari za wanafunzi wa yesu pindi njaa ilipokuwa ikiwauma
watu wakati yesu anaendelea na mkutano. Wao walimwambia bwana waage watu
wakajijinunulie chakula vijijini na mashambani, wao walidhani hili ndilo jibu
la njaa ya watu. Hawakufikiri kwamba sio wote wenye pesa za kununua chakula,
kuwaaga watu kungemaanisha yesu aache kufundisha nk. Sasa jibu la njaa ya wale
watu halikuwa kama wanafunzi walivyowaza na walivyotaka bali jibu lilikuwa kwa
yesu kufanya muujiza wa kubariki mikate mitano na samaki wawili vitosheleze
watu wote 5000.
Sasa baada ya kuwa tumeona hayo makosa makubwa matatu
tuangalie mungu anaposema nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami
nitawasikiliza ana maana gani?.
Katika mstari huu kuna mambo makubwa matatu yamezungumziwa.
MOJA NI MTANIITA,MBIII MTAKWENDA NA KUNIOMBA, TATU NI NAMI
NITAWASIKILIZA.
JAMBO LA KWANZA NI ,MTANIITA.
Ukisoma kitabu cha yeremia 33:3 anasema “niite,nami
nitakuitikia ,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua. Mungu ansema
utakapomwita yeye atafanya mambo mawili.moja atakuitikia na mbili atakuoyesha
mambo makubwa,magumu usiyoyajua.
Maana yake ni hii, kukuonyesha mambo makubwa,magumu
usiyoyajua ni kukufunulia mambo ambayo ulikuwa huyajui katika lile
ulilomuita.hivyo basi kumuita mungu ni kumuomba au kumtaka mungu akufunulie
mambo makubwa na magumu usiyoyajua kuhusu shida au hitaji au haja uliyonayo mbele
zake.mfano unamuita mungu akufunulie ndoa yako jinsi ilivyo, nini kinaendelea
usichokijua, nini ukiombee, nini hakijakaa sawasawa kwenye hiyo ndoa k.
hivyo basi unapotaka
kuomba juu ya jambo lolote lile ni vizuri kwanza ukamuita mungu juu ya hilo
jambo.maana yake muombe mungu akupe picha kamili ya hilo unalotaka
kuliombea,akufunulie jinsi lilivyo ili ujue uanzie wapi kuomba.,kama ni
ndoa,nchi,mke au mme mtarajiwa,huduma yako nk.
JAMBO LA PILI MTAKWENDA NA KUNIOMBA.
Sasa baada ya kuwa umemuita mungu kinachofuata ni kwenda na
kumuomba mungu. Anaposema mtakweda na kuniomba ana maana mtaanza kuomba
sawasawa na vile nilivyowaonyesha au nilivyowafunulia wakati mliponiita katika
haja zenu.hivi ulishawahi kujiuliza ni mambo gani makubwa na magumu ambayo
mungu atakuonyesha_pindi utakapomuita?. Kumbuka tulikotoka tumeona kumuita
mungu ni kumfanya mungu akufunulie mambo usiyoyajua kuhusu hitaji lako ili
ujipange vizuri kuyaombea.
Sasa kwenda na kuomba maana yake ni kuomba sawasawa na vile
mungu alivyojifunua kwako kuhusu hitaji ulilonalo.utakapoomba namna hii ndiko
kunaitwa kuomba sawasawa na mapenzi ya mungu maana yake unaombea mambo ambayo
mungu anataka uyaombee kwa wakati huo. Kwa lugha nyepesi jifunze kuomba mambo
ambayo mungu anakuongoza kuyaombea. Labda nitoe mifano michache ndio somo
litaeleweka vema.
Mfano wa kanza huenda mnaombea mgonjwa au mtu aliyefungwa na
mapepo. Ni kweli biblia imesema mtaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata
afya.sasa si kila mgonjwa ni wa kuweka mikono na kuanza kukemea ugonjwa au mapepo,
kuna magonjwa mengine yanasababishwa na mawazo yaani tatizo ni mtu mwenyewe,
mwingine huenda ni kwa sababu ya kujeruhiwa nafsi yake na mwingine huenda ni
kwa sababu ya dhambi, na mwingine huenda mikataba aliyoingia mwenyewe na mapepo
na huenda mengine ni mungu mwenyewe ameruhusu shetani aguse afya ya huyo mtu
kama alivyomruhusu shetani kwa ayubu nk..
Saa nafikiri mpaka hapa umeshaona si wagonjwa wote
utakawawekea mikono watapona. Hivyo ni vema umuite mungu akufunulie nini cha
kufanya, mwingine atakuambia huyu anahitaji ushauri tu wala si maombi,mwingine
anaweza kukuambia huyu ametenda dhambi hii na hii akizitubia nitamponya, na
mwingine atakuambia huyu hicho ni kipimo chake mpe tu neno la uvumilivu na
ushindi,mwingine atakuambia huyu ndugu mwenyewe au wazazi wake waliingia
mkataba na mapepo hivyo vunja kwanza mktaba huo nk.
Mfano wa pili,huenda mnaombea kanisa lenu. Ni rahisi kusema
tumuombe mchungaji ndani ya kanisa,mara tuombee kamati ya ujenzi tuombe mungu
kuhusu ujenzi nk.kweli ni maombi mazuri lakini una uhakika mungu kwa wakati huo
anataka muombee hayo mambo.huenda kuna roho ya mpinga kristo ina vamia
washirika au kuna maajenti wanajiingiza kwa siri makanisani na kuwapofusha
macho ninyi mnakazana kuombea ujenzi. Maana yangu ni hii ikiwa wewe ni mchungaji
au kiongozi wa maombi katika kundi lolote lile ni vema kila wakati kumuita
mungu akupe mambo ya kuombea kwa wakati huo. Mungu atakufunulia nini
unachotakiwa kuombea kwa wakati huo.
Nina ujasiri na ninachokisema kwa sababu siku moja tukiwa
katika kambi la vijana.nilikuwa kwenye timu ya maombi ya hilo kambi.ndani ya
hiyo timu tulikuwa na wajumbe wa shetani kutoka kuzimu yaani maajenti (vibaraka
wa shetani).hawa jamaa walikuwa wakiomba na kufimga kuzidi masaa yale
tuliyokuwa tukifunga sisi.na wakati wa kuomba walikuwa wanapendekeza tuombee na
kukemea roho ambazo hazifanyi kazi katika lile eneo tulilokuwepo.na walikuwa
wanajita watumishi wa mungu.nina uhakika wa habari hii kwani mungu alinifungua
macho tukaomba na nguvu za mungu ziliposhuka mmoja wo akasema “sisi ni wajumbe
wa shetani kutoka kuzimu,tulitumwa kuleta uharibifu lakini katika yale
tuliyotumwa tumeshindwa kuyatekeleza”.
Nakuambia tangia siku hiyo ndipo nilipofunguka macho yangu
ya ndani na kuanza kuhitaji uongozi wa mungu katika yale tunayoomba kila
siku.hujawahi kuona kiongozi wa maombi anasema jamani hee tutaombea hili na
hili na hili,lakini mnapoanza kuomba unakuta mungu anakuongza kuombea vitu
vingine kabisa ?.
Kumbuka siku zote katika kila unaloliomba ,mwambie mungu
nifunulie zaidi kuhusu mambo ya kuomba kuhusu hili jambo.lwe
ndoa,kanisa,mkutano au semina,watoto,elimu nk sasa nimalizie kwa kusema kuomba
kwa namna hii ndiko kibiblia kunaitwa kumtafuta bwana.sikiliza huwezi kumtafuta
mtu mahali asikopatikana.unapomtafuta bwana ni lazima umtafute kwenye maeneo
yake yaani kule anakopatikana.sasa kunaitwa kumtafuta bwana kwa sababu umeomba
kulingana na ufunuo wake
Ni imani yangu kuwa baada ya kuwa umesoma ujumbe huu basi
naamini umeshapata maarifa ya kukusaidia katika kumtafuta bwana na hivyo kwa
jambo lolote utakalotaka kuomba siku zote utaomba kwanza ufunuo wa mungu juu ya
hili jambo.
IMANI YAKO ITAKUPONYA, MWAMINI BWANA YESU LEO
Kila mwaka tarehe 1 / 12 ni siku ya kuadhimisha janga la
ukimwi kwa kuwa na ujumbe mbalimbali jinsi ya kutokomeza na kuelemisha watu
jinsi ya kujikinga na kuzuia maambukizo mapya ya virusi vya ukimwi na vile vile
kuishi kwa matumaini kuhusiana na ugonjwa huu. Japo kuna baadhi ya maeneo elimu
bado sijui niseme ni changa au haijawafikia walengwa vizuri, na la kushangaza yakiwemo baadhi ya maeneo ya
mijini yakiongoza kwa asilimia kubwa ya kuwa na maongezeko mapya ya mambukizi
ya virusi vya ukimwi. Swali la kujiuliza ni kuwa watu hawataki kuelewa au ni
elimu imezoeleka kiasi kwamba watu wanaona hakuna jipya au maisha ndio
yanawalazimisha kutokuzingatia yanayosemwa. Au je waelemishaji nao pia hawana
elimu ya kutosha ya kuwaelimisha watu / watoaji elimu ni wachache kuliko
walengwa / walioathirika? Au wamekosa imani na asasi / ngo zinazotoa huduma
hii? Ukiangalia kwa mtazamo wa kawaida tu kuna asasi/ngo mbalimbali zimeazishwa
kwa ajili ya kusaidia na kuelimisha waathirika wa ukimwi / na ambao bado
hawajapata maambukizi pamoja na watoto yatima na wajane. Je wanatoa elimu
sahihi na yakutosha? Kama ndio kwa nini kuna ongezeko kubwa la watoto yatima na
maabukizi mapya yanaibuka siku hadi siku? Au waanzilishi wa hizi asasi / ngo wanatafuta maslahi yao
wenyewe kwa kupitia mgongo wa walioathirika badala ya kutoa elimu ya sahihi na
ya kutosha? Japo kwenye takwimu zinaonyesha kuwa tanzania imeshuka kwenye
kiwango cha maambukizi ya ukimwi ukilinganisha na nchi nyingine za africa. Je
hili nalo ni kweli yanaweza kuwa ongezeko la maambukizi mapya limepungua wakati
bado tunashuhudia watoto yatima wakiongezeka kutokana na hili janga?
(tutafakari hili) mimi sina jibu ila haya yote ni mtazamo wa kibinadamu tu.
Hebu tungalie biblia inatuambia nini kwa habari ya magonjwa? Je kuna ambalo
linashindikana kwa bwana? Kama yeye alitufinyanga kwa mikono yake si anajua
kila sehemu ya viungo vyetu hivyo ni rahisi yeye kuturekebisha pale penye
madhaifu na kupatia uzima. Hebu tuone biblia inasema nini basi kwa habari ya
uponyaji....
Ukisoma kwenye biblia zetu utaona kwamba ukoma ndio uliokuwa
ugonjwa mbaya sana na ulikuwa unatishia watu enzi hizo za kale pia ulikuwa ni
ugonjwa usioponyeka lakini watumishi wa mungu walikuwa wanauwezo wa kuwaponya
watu kutokana na ugonjwa huu kilichokuwa kinahitajika ni imani na kutii tu, kwa
mfano naaman aliyekuwa unaukoma lakini alipokea uponyaji. Soma 2wafalme 5: 8-19
na pia soma mathayo 8:1-4 yesu anaponya ukoma.
Japo kwa jambo la kushangaza na la kuhuzunisha ni kuwa huu
ugonjwa hadi sasa upo toka enzi za akina musa hadi leo lakini je ni kwamba dawa
za kuuponya huu ugonjwa haijapatikana? Imepatikana na ipo sema watu hawatilii
maanani. Wako wapakwa mafuta wa bwana ambao wamepewa karama ya kuponya
wanaponyesha huu ugonjwa, kadhalika na ukiwmi pia wako watumishi wapakwa mafuta
wa bwana waliopewe karama ya uponyaji wako kukusaidia leo. Kama huu ukoma ambao
ulikuepo toka enzi hizo za akina musa unawezekana kuponyeka kwanini watu
wasiamini kuwa hata ukimwi waweza kupona? Ukimwamini mungu na kuyashika maagizo
yake na kutii hakika utapona.
Mfano wa mwanamke aliyetoka damu kwa miaka kumi na miwili
biblia inatuambia kuwa yule mwanamke aliazimia kuwa akiweza kushika tu upindo
wa vazi aliyovaa yesu hakika atapona na kweli alivyofanya hivyo kwa imani yake
kuu aliyokuwa nayo alipokea uponyaji muda ule ule soma mathayo 9 : 20 - 22; pia
kwenye marko 5: 25-34; sasa je wewe wawezaje kukata tamaa na kushindwa
kumwammini yesu kuwa kwa jina lake tu magonjwa yanatoweka hayatakuwa na nafasi
tena ndani ya maisha yako utapona na utakuwa na nguvu na mwenye afya tele.
Kama bado haujaambukizwa acha njia zako mbaya mtafute yesu
shika maagizo yake na kuyatenda hakika atakuponya na hili janga wewe na familia
yako na watu wa nyumbani mwako. Ingawa unaweza kuwa mwaminifu, waweza kuwa
unatenda yaliyo mema kwa mtazamo wa kibinadamu lakini bado ukaupata huu ugonjwa
kwa njia nyingine kwa mfano katika ajali kama ya gari, pikipiki au njia yoyote
ile nk. (unajua kuwa maambukizi waweza pata kwa njia nyingi si kwa kuzini tu
japo kuzini ndio njia kubwa ya maambukizi haya ya virusi vya ukimwi). Lakini
ukimtegemea mungu na kukubali kuwa yesu alikufa msalabani kwa ajili yako na kuyatenda yote aliyokuamuru, hali hii
haitakupata wewe na familia yako kwa ujumla na hata hutaacha wanao yatima bali
utaishi hadi miaka mia na ishirini na utakufa ungali ukiwa na nguvu zako.
Yesu alifanya miujiza mingi ya uponyaji na hata sasa bado
anafanya kwani anawatumia watumishi mbalimbali kufanya kazi aliyoianzisha
kinachoturudisha nyuma ni kutokutilia maanani na imani kuwa haba kama
nilivosema hapo juu. Watu tumekuwa na kiburi tukidhani kuwa wanayofanya
watumishi wa mungu ni ya uongo lakini mimi nakusihi leo hebu mwamini yesu
halafu utaona matunda yake na hakika hautajuta. Soma mistarii hii ikusaidie kwa
habari ya imani katika uponyaji mathayo 8 : 5-13; mathayo 8 : 14-17;
Mathayo 9 : 27 - 31 n.k.
Mwamini yeye leo mtumainie bwana peleka haja zako kwake naye
atatenda, atakushindia na pia atakuponya, usikate tamaa usihangaike ikuze imani
yako kwa kusikiliza na kusoma neno la mungu mara kwa mara kwani biblia inasema
hivi "imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la
kristo"
Warumi 10 : 17 kisha mweleze shida yako peleka haja zako
kwake naye atafanya. Pia yesu anasema hivi, hata ukiwa na imani kiasi cha punje
ya haradali ukisema mlima huu ung'oke mahali hapa uende kule, nao utang'oka.
Hivyo basi na uponyaji wako unahitaji imani yako kidogo tu kama punje ya
haradali kwa yesu kuwa anaweza kukuponya nawe utapokea uponyaji. Tumwamini yeye
tuuone mkono wa bwana ukitenda ndani ya maisha yetu.
MAOMBI, UPONYAJI NA
UREJESHAJI
(yakobo 5:13-20)
Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au
sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una
kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma
moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye
>>pentecostalchurch2.blogspot.com>>kwa lugha ya kiswahili na kwa
lugha ya kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile kifaransa, kijerumani.
Omba kwa ajili ya uongozi wa roho mtakatifu unapojifunza.
UTANGULIZI: JE, umewahi kuwasikia watu wakisema kuwa
wanaabudu kwa namna zao wenyewe? Wamechoshwa na “kanisa” na kwamba kukutanikia
jangwani ni bora zaidi kwa sababu jangwa haliwaambii maneno yasiyo mazuri.
Ingawa ni ukweli kwamba ni muhimu kutenga muda binafsi wa kuwa na mungu, katika
somo letu juma hili yakobo anaelezea manufaa ya kushirikiana [kuchangamana]
kiibada na wakristo wenzetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la biblia ili
tujifunze zaidi!
USHIRIKA NA MUNGU
A. SOMA YAKOBO 5:13. Maelezo ya fungu hili yanatuhusu watu
wengi. Uwezekano mkubwa ni kwamba aidha tuna matatizo au hatuna furaha.
Tunatakiwa kuitikiaje uzoefu huu wenye tofauti kubwa? (kwa kumgeukia mungu. Ama
tunatakiwa kuomba kwa ajili ya kupata msaada au tunatakiwa kumsifu mungu kwa njia
ya nyimbo.)
1. Mwitikio wako
kimaadili ni upi unapojikuta kwenye matatizo? (siku za nyuma, papo hapo
nilifanya kile nilichoweza ili kutatua tatizo. Sasa nimejifunza kwamba hatua ya
kwanza lazima iwe ni kumgeukia mungu.)
2. Je, huwa
unakasirika unapokabiliana na matatizo? (asili ya mwanadamu huwa ni kuwalaumu
watu wengine, na kisha kukasirika kutokana na kile walichotutendea. Ikiwa, kwa
uwezo wa roho mtakatifu, tutamgeukia mungu kwanza, itatuepusha kusema au
kutenda jambo baya papo hapo kwa sababu ya hasira. Hii itaepusha kufanya tatizo
kuwa gumu zaidi.)
B. Mtazamo wa namna gani unaakisiwa kwenye ushauri wa yakobo
kwa ajili yetu kuomba au kusifu? (mungu ndiye anayeyashikilia maisha yetu. Yeye
ndiye chanzo cha mibaraka yote. Tunamgeukia ili kupata msaada na tunamshukuru
kwa kumpa sifa.)
USHIRIKA NA WAUMINI
A. Soma yakobo
5:14-15. Kuugua ni mfano mahsusi wa tatizo. Kwa nini usijiombee tu wewe
mwenyewe – kama anavyobainisha yakobo katika mstari wa 13? Kwa nini kuwahusisha
wazee katika jambo hili? (mungu hahitaji wazee kumshawishi ili afanye uponyaji,
lakini wazo la kushirikiana na waumini wenzako linaelezewa hapa.)
1. Kuna nyakati kadhaa nilikuwa sehemu ya kundi la wazee
waliomwombea na kumpaka mafuta mgonjwa. Nchini marekani, watengenezaji wa dawa
wanaeleza bayana athari za dawa zao wakati ule ule wanapotangaza jinsi dawa zao
zinavyoweza kutibu. Mke wangu alikuwa akiniambia kwamba nilitakiwa kubainisha
jambo hili nilipokuwa sehemu ya wanaofanya maombi na kupaka mafuta katika
kipindi cha nyuma ambapo wagonjwa hawakupona. Mke wangu alikuwa akitania,
lakini hadi siku za hivi karibuni, jambo hilo lilibakia kuwa ukweli mtupu. Je,
yakobo anatoa ahadi za uongo kuhusu uponyaji?
A. Je, mimi ndiye
niliyekuwa tatizo? Yakobo anapoandika “na kule kuomba kwa imani,” je, alikuwa
akiandika kuhusu imani ya wazee? Kama sivyo, anaelezea imani ya watu gani, je,
ni imani ya mgonjwa?
B. Soma marko 2:1-5. Je, hapa yesu anazungumzia imani ya
nani? (haiko wazi. Yesu anaonekana kuzungumzia imani yao wote.)
C. Soma mathayo
18:19. Vipi kama mgonjwa alikuwa na imani na mzee mmoja pekee ndiye alikuwa
mwenye haki, je, imani hiyo ingetosha kuleta uponyaji? (utagundua kwamba yesu
haonyeshi kiwango cha imani au haki inayotakiwa, anabainisha tu idadi ya
waumini waliokubaliana. Wawili wanatosha.)
D. Hebu tuangalie tena yakobo 5:15. Je, yakobo anatoa muda
wa kuinua na kuponya? (hapana. Nina uhakika kila mtu aliyekuwa kwenye huduma ya
kupaka mafuta ambapo mimi pia nilihusika alikuwa mdhambi – kuanzia mgonjwa hadi
kwa wazee wote. Yakobo hasemi kwamba hatutakiwi kuwa na dhambi, anasema kwamba
tunatakiwa kuwa na imani. Kwa kuongezea, hatoi muda kwa ajili ya uponyaji.
Ninaamini mungu atawafufua katika uzima wa milele wote waliolala wakimtumaini
yeye.)
E. Kipindi cha hivi
karibuni kabisa ambapo nilikuwa sehemu ya kundi la wazee waliokwenda kufanya
maombi, mgonjwa aliponywa. Mungu anatenda miujiza maishani mwangu, na kwenye
maisha ya wale ninaowaombea, na ninaamini hili linahusiana zaidi na mapenzi ya
mungu mwenye enzi, badala ya haki yangu. Je, wewe unadhanije?
UPONYAJI, IMANI NA DHAMBI
A. Angalia tena sehemu ya mwisho ya yakobo 5:15 na marko
2:5. Yesu anamwambia mwenye kupooza kwamba dhambi zake zimesamehewa. Yakobo
anasema, dhambi zinaweza kusamehewa. Je, kuna uhusiano gani kati ya uponyaji na
dhambi?
B. Soma yohana 9:1-3.
Kwa nini wanafunzi waliuliza kuhusu dhambi na upofu? (uelewa wa kipindi hicho
ulikuwa ni kwamba dhambi ilisababisha magonjwa. Nadhani bado kuna ukweli mwingi
kwenye uelewa wao.)
1. Je, yesu alisema
kuwa sababu ya upofu ni ipi? (ili mungu aweze kutukuzwa. Haikuwa suala la
dhambi.)
2. Dhambi
inapoungamwa na kusamehewa, je, mungu anatukuzwa? (ndiyo! Angalao kauli za
yakobo na yesu kuhusu ugonjwa na dhambi zina maelezo ya aina mbili. Kwanza, ni
uelewa wa watu wa kipindi hicho. Lakini, jambo la muhimu zaidi ni kwamba, mungu
anataka kutuponya dhambi. Lengo lake kuu kwetu ni kuwa na maisha yasiyo na
dhambi na ugonjwa – na lengo hilo litatimia mbinguni.)
C. Siku chache zilizopita nilikuwa mapumzikoni kwa muda wa
siku kadhaa eneo la “disney world,” ambapo watu wanene wanakusanyika na kuendesha
vijigari. Kiukweli, watu wengi waliokuwepo mahali pale pia walikuwa wanene.
(katika kuzungumzia suala la unene, niliweza kuongezeka uzito wa kilogramu 1.8
nilipokuwa likizo!) Wakati huo huo, sikumwona mtu hata mmoja akivuta sigara.
Inaonekana kwamba hatari ya kiafya inayotokana na uvutaji wa sigara
imebadilishwa na hatari ya kiafya inayosababishwa na unene mkubwa kupita kiasi.
Swali gumu ni hili: je, dhambi inaweza kuingiliana na uponyaji?
1. Kama utasita
kumwombea mvuta sigara ili aweze kuponywa, vipi kuhusu mtu mnene kupita kiasi?
2. Je, kiasili
baadhi ya watu si ni wanene tu? Je, hilo linajalisha?
3. Nimesoma sana
kuhusu ubongo, na ninashawishika kwamba mazoezi ni tiba ya watu wote kwa
magonjwa ya aina yote, yakiwemo masuala ya kiakili. Je, kushindwa kufanya
mazoezi ni dhambi inayotuzuia tusiponywe?
4. Je, nimemtukana
takribani kila mtu? Ninachokimaanisha ni kwamba tunawaangalia wavuta sigara
wanaougua saratani ya mapafu, na wasenge wanaougua ukimwi, na hatuwahurumii
sana kutokana na matendo yao.
KUTUBU [KUUNGAMA] DHAMBI
A. Soma tena yakobo
5:15. Muda wa msamaha ni upi? (baada ya mtu kuponywa. Hii inaashiria kwamba
uponyaji upo kwa ajili ya watu wote.)
B. Soma yakobo 5:16.
Hebu subiri kidogo! Baada ya mjadala wetu juu ya dhambi, je, yakobo anasema
kuwa tunatakiwa kutubu dhambi zetu ili tuweze kuponywa? Au, je, kuombeana sisi
kwa sisi ndio kigezo pekee kinachohusiana na uponyaji?
C. Angalia tena yakobo 5:16. Unafikiria nini kuhusu kutubu
dhambi kwa waumini wenzetu?
D. Soma zaburu 51:4, zaburi 32:5 na 1 yohana 1:9. Je,
mafungu haya yanapendekeza kwamba tutubu dhambi zetu kwa nani? (tunatenda
dhambi dhidi ya mungu, na mungu ndiye ana uwezo wa kusamehe dhambi. Hivyo,
inaleta mantiki kutubu dhambi zetu kwa mungu.)
E. Unapotafakari
kuhusu jambo hili, je, kuna aina mbalimbali za kutubu? (ninadhani hivyo.
Kwanza, kuna kutubu na msamaha wa dhambi, jambo ambalo ni suala kati yako na
mungu. Pili, mathayo 18:15, luka 17:4 na mambo ya walawi 6:1-5, mafungu yote
hayo yanaashiria kwamba kuna dhambi ambazo tunatakiwa kuombana msamaha sisi kwa
sisi. Tatu, ni kile ninachodhani yakobo anakizungumzia; mantiki ya jumla kwamba
tunatenda kazi na waumini wenzetu ili kuelekea kwenye haki. Tunaombeana sisi
kwa sisi, tunajadiliana dhambi zetu sisi kwa sisi, tunajadiliana masuala ya
kiroho sisi kwa sisi.)
NGUVU YA MAOMBI
A. Soma yakobo 5:17-18 kisha usome sehemu ya mwisho ya
yakobo 5:16. Tumekuwa tukijadili juu ya dhambi, lakini nadhani yakobo amejikita
kwenye maombi. Kwa nini yakobo anamtaja eliya kama mfano? (anasema alikuwa
“mwanadamu mwenye tabia moja na sisi.” Sote tuna uwezekano wa kuwa na maombi
yenye nguvu na ufanisi mkubwa.)
1. Soma 1 wafalme 19:3-4. Kwenye mjadala wetu hadi
tulipofikia, nimelinganisha [nimehusianisha] masuala ya kiafya na dhambi.
Katika mathayo 15:16-18 yesu anapendekeza kwamba mlingayo huu si sahihi. Kwa
upande mwingine, kutokumtumaini mungu ni dhambi (ufunuo 21:8). Yakobo
anapotuelekeza kwa eliya, je, anasema nini? (imani na udhati katika maombi ndio
ufunguo wa uponyaji, sio kutokuwepo kwa dhambi.)
B. Soma yakobo 5:19-20. Haya yanaonekana kama madai ya
mwisho ya “matendo” – ikiwa tutawaongoa upya “waliorudi nyuma” dhambi nyingi
zitasamehewa. Je, muktadha huu unaashiria kuwa uelewa sahihi wa jambo hili ni
upi? (unazungumzia juu ya uelewa wetu wa dhambi, badala ya asili ya wokovu.
Sura hii ilikuwa inazungumzia juu ya kufanya ushirika [kuchangamana]. Ikiwa mtazamo
wako ni kuwaunga mkono na kuwaokoa washiriki wenzako wa kanisa, basi kitendo
hicho, badala ya kupoteza muda, ndicho kilicho cha muhimu machoni mwa mungu.)
C.Rafiki, je, wewe ni sehemu ya watu wanaofanya ushirika wa
mara kwa mara? Kama wewe si sehemu ya kundi hilo, basi unakosa kipengele cha
muhimu sana cha kuwa mkristo. Kwa nini usitubu juu ya jambo hili na kuungana na
kundi linaloshikilia imani na utii?
MAOMBI YA KUSAMBARATISHA UCHAWI NA NGUVU ZA GIZA
Baba katika jina la yesu. Laana zote nilizo tupiwa na wabaya
wangu zimeshindwa kwa jina la yesu na nazivunja na kuzisambaratisha kwa damu ya
yesu. Mshindwe wote mnao tuma laana kwangu katika jina la la yesu.
Nawavunja na kuwaharibu na kuwakatakata wachawi wote kwa
damu ya yesu.
Nasambaratisha kila neno la uovu lililosemwa juu yangu na
famila yangu katika jina la yesu.
Naharibu na kuisambaratisha madhabahu yenu mliyo fanyia
kafara kwa damu ya yesu.
Navunjavunja na kubomoa kila uovu na uchawi mnaonifanyia
katika jina la yesu.
Nairudisha misukule yote na majini yote yawarudie nyie na
kuwalipa dhambi zote mnazo fanya katika jina la yesu.
Naharibu kila uchawi, kila urogi, kila ndumba kila aina ya
uovu ambao mnaufanya ili uniumize mimi na familia yangu katika jina la yesu.
nawateketeza kupitia damu ya yesu wachawi wote walio tumiwa
kunitumia uchawi katika jina la yesu.
Nawateketeza na kuwaharibu majini yote yaliyo tumwa kuja
kufanya kazi hiyo waliyo tumwa na wachawi katika jina la yesu.
Nawateketeza na kuwauwa makuhani wote ambao walienda
kunishitaki kwa wachawi ili waniharibie maisha, nawateketeza kupitia damu ya
yesu. Nawachoma kwa moto wa roho mtakatifu katika jina la yesu.
Nateketeza aina zote za vyombo vya kichawi vilivyo tumiwa
kuja kunichunguza katika jina la yesu.
Naharibu fikra zao zote ambazo wanazitumia kufanya kazi zao
za kichawi katika jina la yesu.
Nafuta kumbukumbu zoote zangu ambazo wamewapa mashetani,
majini, roho chafu, nafuta hizo kumbukumbu kwa kutumia damu ya yesu, katika
jina la yesu aliye hai.
Nawateketeza waweka kumbukumbu wa kimashetani kupitia damu
ya yesu aliye hai. Naharaibu na kuchoma kupitia moto wa roho mtakatifu
makabrasha yote yenye kumbukumbu zangu katika jina la yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuharibu maisha yangu na
ubomoa kupitia damu ya yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuniua nauvunja na
kuuteketeza kupitia damu ya yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili kuja kuiba mali zangu, nauvunja
na kuubomoa na kuuharibu kupitia damu ya yesu.
Kila uchawi ulio fanya kuja kuniharibia familia yangu,
nausambaratisha na kuuvunja na kuubomoa katika jina la yesu.
Kila neno la kichawi lililo tumwa ili kuja kuniharibia,
kunidhihaki, kunitendea mabaya nalirudisha kwa aliye lituma katika jina la
yesu.
Kila uovu, uchawi, wanga, ndumba, ramli, yaliyo tumwa kuja
kwangu navunja yote hayo kupitia damu ya yesu na katika jina la yesu.
Nyota yangu ambayo wanaita nairudisha kupitia damu ya yesu.
Nyota yangu ya baraka nailinda na kuzungushia na kuizingira na damu ya mwana
kondoo katika jina la yesu.
Namteketeza yule mtu aliye kuja kuiba nyota yangu katika
jina la yesu.
Nateketeza mbinu zote wanazo tumia ili kuja kuiba nyota
yangu katika jina la yesu.
Nateketeza wivu wao, chuki yao, laana zao, maovu yao na kila
aina ya uchafu ambao wanao kwa ajili yangu katika jina la yesu.
Naizungushia na kuizingira nyumba yangu na damu ya yesu.
Naishungushia na kuizingira familia yangu na damu ya yesu.
Nashungushia na kuzingira maisha yangu yote na damu ya yesu.
Navunja laana zote zilizo semwa na mabau zangu katika jina
la yesu.
Navunja laana zato ambazo zilisemwa bila ya mimi kufahamu,
nazivunja na kuziharibu kupitia damu ya yesu na katika jina la yesu.
Narudisha kila mali walizo ziiba kutoka kwangu katika jina
la yesu.
Narudisha kila baraka walizo ziiba kwangu katika jina la
yesu.
Narudisha amani na upendo katika familia yangu.
Damu ya yesu ipo juu ya maisha yangu na inasafisha kila
uovu, kila uchawi unaaribiwa na damu ya yesu katika jina la yesu.
Leo hii mtaiona nguvu iliyopo katika damu ya yesu.
Katika jina la yesu aliye hai ninaomba.
Amen
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUPATA KITABU NINAMANI KITAKUSAIDIA
/ KIMEKUSAIDIA KATIKA KAISHA YAKO YOTE.
HII NI SEHEMU YA KWANZA YA KITABU JUU YA SOMO LA MAOMBI.
KIMEANDALIWA NA MWINJILIST LAURENT E. MPOMA.
KANISA LA PENTECOSTAL CHRISTIAN CENTER – MISUNA SINGIDA
KUJIPATIA VITABU VINGINE AU UNAHITAJI MAOMBI FIKA KANISANI
PENTECOSTAL CHRISTIAN CENTER – MISUNA –SINGIDA
AU PIGA SIMU:+255763652896, 714890889.
MUNGU AKUBARIKI SANA>>>>>>AMINA.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: