NJIA SABA(7) ZA KUPIGANA VITA YA KIROHO KWA MAOMBI
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
mwinjilisti: LAURENT ELIAS MPOMA
2. Kufunga na kufungua.
Mathayo 16:19 ''Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na
lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.''
Hii ni njia yenye vipengele viwili tofauti lakini kila
kipengele kinamhitaji mteule wa KRISTO.
Kufunga maana yake kukataa jambo lisitokee.
Kufunga ni kuzuia jambo la kishetani ambalo lilipangwa
likupate, lakini kwa maombi yako ya kulizuia hakika jambo hilo halitakupata.
Unaweza ukazuia ajali kwa maombi yako, unaweza ukazuia
ugonjwa, unaweza ukazuia kuonewa, unaweza ukazuia kuteswa na wachawi, unaweza
ukazuia kutokuzaa, unaweza ukazuia kila kazi ya shetani katika maisha yako. Ni
Mamlaka hiyo MUNGU amekupa kama Mteule wake ili ukizuia vitu katika ulimwengu
wa roho hakika vinazuiliwa.
Mathayo 18:18 '' Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga
duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani
yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.''
Kipengele cha pili ni kufungua.
Hiyo maana yake unaruhusu kilicho cha MUNGU kitokee.
Unaruhusu kilicho haki yako ambacho kilizuiliwa kipepo sasa
kitokee kupitia maombi yako ya kufunga kazi za shetani na kufungulia baraka
zako.
Katika njia hii ya kufunga na kufungua ni muhimu sana kuwa
mtu unayeongozwa na ROHO MTAKATIFU ndipo utashinda kwa urahisi.
Kumbuka sio vitu vyote unaweza kufunga na sio kila kitu
unaweza kufungua. Maombi ni somo pana sana na maombi sahihi ni yale ambayo ROHO
MTAKATIFU anakuongoza tu.
Kazi ya ROHO MTAKATIFU ni kutuongoza katika kweli ya MUNGU
hivyo hata katika maombi yako ya kufunga kazi za shetani na kufungulia baraka
zako zilizokuwa zimeshikiliwa kipepo na mawakala wa shetani hakika unamuhitaji
sana ROHO MTAKATIFU ili akujulishe ni nini cha Kufunga kwa maombi na ni nini
cha Kufungua kwa maombi.
Ukikataa ushauri na maongozo ya ROHO MTAKATIFU huwezi kuwa
sahihi hata siku moja.
Zaburi 32:8 '' Nitakufundisha na kukuonyesha njia
utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.''
Mteule wa MUNGU una mamlaka kuu sana MUNGU amekupa kwa sababu
umekubali kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako, lakini mamlaka ya kimaombi ya
kufunga mambo ya giza na kufungua mambo ya baraka unahitaji sana sana ROHO
MTAKATIFU akufundishe na kukujulisha.
Ndugu unayo mamlaka kubwa sana ambayo wasio na YESU hawana,
wasio na ROHO MTAKATIFU hawana lakini unahitaji sana kumwambia ROHO MTAKATIFU
akusaidie na kukujulisha ni vitu gani vya kufunga na ni vipi vya kufungua.
3. Kuziondoa nguvu za giza.
Marko 16:17-18 '' Na ishara hizi zitafuatana na hao
waaminio; kwa jina langu WATATOA PEPO; watasema kwa lugha mpya; watashika
nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono
yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.''
Maandiko haya yana vitu vingi lakini kwenye somo langu
nahusika na kanuni/Njia za kiroho za kupigana vita ya kiroho.
Njia hii inaitwa kutoa nje nguvu za giza ndio maana Biblia
inasema ''Watatoa mapepo''
Mapepo ni nguvu za giza ambazo zinaweza zikawekwa na
mawakala wa shetani popote.
Wengi sana wanateswa na majini ambayo ndiyo hayo hayo
mapepo.
Unaweza ukateswa na ugonjwa mbaya sana na ambayo huwa
unaondoka na kurudi kumbe ulirushiwa jini likajigeuza ugonjwa usiopona na
ugongwa huo unakutesa.
Kuna ambao hadi walikufa kwa kuteswa na magonjwa ya ajabu
huku hawajui kama ni majini walirushiwa yakajigeuza ugonjwa ndani ya miili yao
na magonjwa hayo yanawatesa na wengine magonjwa mengine hata wakienda
hospitalini vipimo havionyeshi kama wanaumwa, lakini wao wanaumwa sana sana.
Hata biashara yako inaweza ikarushiwa majini na wachawi
wanaokusakama.
Ufahamu wako unaweza ukatupiwa mapepo kiasi kwamba huwa
unalitumikia kusudi la shetani na sio la MUNGU.
Mapepo kama nguvu za giza zinaweza zikatesa ndoa, ukoo,
familia au mwili wako.
Neema ya MUNGU ni ya ajabu sana sana maana kwa waliookoka
haswa MUNGU ametupa Mamlaka na uwezo wa kuwatoa nje majini wote na kila nguvu
za giza ili watoke katika miili yetu na maisha yetu.
Bwana YESU alisema kwamba moja ya kazi za wateule wake ni
kuzitupa nje kazi za shetani ziitwazo mapepo/majini.
Ni kazi ya mteule wa KRISTO kuyatoa nje ya mwili au familia
au ukoo au biashara mapepo yote yaliyotumwa.
4. Kushindana.
Waefeso 6:11-13 ''Vaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza
kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya
majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha
zote za MUNGU, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza
yote, kusimama.''
Tunashindana kimaombi na tunashinda.
Tunashindana na viumbe wasioonekana lakini tunawashinda na
kuwangamiza.
Ni Mamlaka tumepewa na ni ushindi kwetu ni lazima.
Ni muhimu sana kuomba maombi ya kushindana na adui ili
umshinde.
Kumbuka adui hakuogopi wewe ila anamuongopa YESU KRISTO
Mwokozi wako.
Adui anamuogopa ROHO MTAKATIFU aliye ndani yako.
Unahitaji kuwa muombaji sana ili uwashinde maadui zako
kiroho.
Kiufunuo unaweza kujikuta hata unaomba maombi ya kufunga ili
kuwashinda maadui zako.
Mawakala hao wa shetani wanajua kabisa kwamba wewe ukikaa
katika nafasi yako ya maombi hakika unawashinda na kuwadhuru sana, ndio maana
moja ya kazi ambazo shetani anazifanya kwako ili akufunge zaidi basi ni
kuhakikisha hujifunzi Neno la MUNGU la kukusaidia na huombi.
Lakini kwa wanaojitambua hakika uko ushindi mkuu kutoka kwa
MUNGU kwa wewe kuomba maombi ya kuwapiga adui zako ili wakimbie.
Shetani na watoto wake hawana jinsi wakisikia jina la YESU
KRISTO, Ni lazima wakimbie hakika. Ndugu hakikisha unaitumia mamlaka ya KRISTO
iliyo ndani yako kuwashinda maadui zako.
Biblia inasema ''Kushindana kwetu sio juu ya damu na nyama''
maana yake kumbe tunapaswa kushindana na mawakala wa shetani.
Usiposhindana nao watakuonea sana maana hawatakutana na vita
wakikuvamia.
Ndugu itumie kanuni hii ya kushindana nao ili uwashinde.
Huwezi ukawa na jina la YESU KRISTO, Damu ya YESU KRISTO,
Nguvu za ROHO MTAKATIFU na Neno la MUNGU harafu adui ashindwe kukukimbia,
haiwezekani.
Unahitaji kuomba maombi ya kuwashindana maadui zako, hiyo ni
kanuni ya kimaombi na njia ya kimaombi inayokuhitaji wewe muombaji.
Msaada wa MUNGU huwa ni mkubwa sana kwa mtu anayejua
kupigana vita vya kiroho vya kushindana na mawakala wa shetani.
Yeremia 1;19 '' Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda;
maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe. ''
5. Kupinga.
Yakobo 4:7 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye
atawakimbia. ''
Hii kanuni muhimu sana yaani kimaombi unapinga kila kazi ya
shetani na hakika haitafanikiwa kazi hiyo ya giza.
Kumtii MUNGU ndio kumpinga shetani.
Tunahitaji kumpinga shetani katika mambo yake yote, ni
kanuni ya wateule wa MUNGU.
Kipengele hiki kina maana ya kumwingilia shetani katika kazi
zake na kumzuia kuendelea kufanya kazi hizo, hiyo ni mamlaka ya mteule wa
MUNGU.
Tunampingaje Shetani?
1.Tunampinga shetani kwa maombi ya kumpinga.
2. Tunampinga kwa kukataa kufuata kazi zake na matendo yake.
3. Tunampinga shetani kwa sisi kulitii Neno la MUNGU.
4. Tunampinga shetani kwa sisi kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.
5. Tunampinga shetani kwa Neno la MUNGU.
1 Petro 5:8-9 ''Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki
wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale
yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. ''
Ndugu, ni kazi yako na jukumu lako kumpinga shetani.
Kumpinga shetani ni kanuni ya kimaombi iliyo muhimu sana.
Kumpinga shetani ni kumzuia kuendelea kukunyanyasa na
kukuonea.
Kumpinga shetani ni kumkataza kuingilia ndoa yako, uchumi
wako, uchumba wako, au akili yako.
Kwa maombi hakika unaweza kuwapinga ,mawakala wa shetani na
wakakimbia hakika maana wanajua kwamba yeye shetani hana nguvu hata moja kwa
aliyeko ndani yetu yaani ROHO wa MUNGU wetu.
1 Yohana 4:4 ''Ninyi, watoto wadogo(Wateule wa KRISTO),
mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda(Mawakala wa shetani), kwa sababu yeye
aliye ndani yenu(ROHO MTAKATIFU) ni mkuu kuliko yeye(Shetani) aliye katika
dunia.''
6. Angusha.
2 Kor 10:3-5 '' Maana ingawa tunaenenda katika mwili,
hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili,
bali zina uwezo katika MUNGU hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila
kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU; na tukiteka nyara kila
fikira ipate kumtii KRISTO; ''
Kanuni nyingi muhimu ya kimaombi ni kuteka fikra ili zipate
kumtii YESU KRISTO.
Ni kanuni ambayo kanisa la MUNGU linaagizwa liitumie katika
maombi.
Unaweza ukawa na mawazo ndani yako ya kufanya kitu fulani
kumbe ni mawazo ambayo hayatokani na MUNGU, Usipojua kuyaangusha mawazo na
fikra mbaya ambazo ziko kinyume na Neno la MUNGU hakika unaweza kujikuta wewe
ni mtu wa kufanyia kazi wazo la shetani kila siku na mwisho wake hakuna baraka
za MUNGU katika wazo lililotokana na shetani.
Hakikisha unaangusha kila fikra iliyo kinyume na Bwana YESU
ndipo utapata fikra ya MUNGU.
Tiisha mawazo yako ili yawe mawazo yanayokubaliana na Neno
la MUNGU.
Kuna mawazo ya kipepo mengi tu yanaweza kukukumba na
hakikisha unaangusha mawazo hayo na fikra hizo zilizo kinyume na Neno la MUNGU.
Moja ya fikra ambazo inawezekana unazo na hizo fikra ni
potofu sana na za kipepo ni hizi hapa.
1. Mawazo ya dhambi.
2. Mawazo ya kujilaumu.
3. Mawazo ya kujiona hufai hata kama umeshatubu na kuokoka.
4. Mwazao ya kujihukumu bila kosa
5. Mwazao ya kujidhania huwezi bila watu fulani n.k
Ni aina nyingi sana za mawazo ya kipepo ambayo mtu wa MUNGU
unaweza kujikuta unafanyia kazi na kwa njia hiyo unapishana na kusudi la MUNGU.
Unahitaji sana kuitumia kanuni hii ya kimaombi ya kuangusha
kila mawazo na fikrra ili zipate kumtii KRISTO na Neno lake.
Mawazo ya shetani siku zote yako kinyume na Neno la MUNGU.
Hakikisha unaangusha kila fikra na mawazo ili yapate kumtii
KRISTO.
Tumia kanuni hiyo ya kimaombi ya kuangusha fikra na mawazo
mabaya yote ili yasifanye kazi katika maisha yako.
7. Kung'oa, Kubomoa, Kuharibu na kuangamiza
Yeremia 1:10 ''angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu
ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na
kupanda. ''
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: