AINA YA MIFUNGO:
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
AINA YA MIFUNGO:
1. Mfungo kamili
Katika mfungo huu
hakuna kula kabisa chakula kigumu bali waweza kunywa maji au kimiminika
chochote cha kukusupport.
Siku ngapi waweza
kufunga mfungo wa aina hii unategemea na neema na malengo yako katika mfungo
huo. Wengine huenda siku moja, mbili, tatu, wiki, n.k n.k
2. Mfungo nusu
Mfungo nusu huanzia saa
12 asbh hadi saa 9 mchana au kuanzia jua linapoibuka hadi linapozama. Mfungo
ambao madhehebu mengine wamewazoeza waumini wao kuufanya. Wengine wameweza
kuufanya kila ijumaa. Madhehebu ambayo yamewazoesha watu wao kufunga angalau
kila wiki mara moja wameweza kuwa na mafanikio makubwa sana katika kuzifungua
nira na vifungo mbali mbali
3. Mfungo wa Daniel
Daniel alifunga mifungo
miwili ya aina yake;
• Katika Sura ya I
Daniel alifunga alikula mboga mboga tu (Yaweza kuwa alikula mboga mboga na
juisi Fulani Fulani)
• Katika sura ya 10
Daniel alifunga kwa siku 21 kwa kutokula chakula kitamu, wala nyama wala divai
haikuingia kinywani mwake”
Ngoja nikomee hapa kwa
leo hadi wakati mwingine na Mungu akubariki sana na kama umependezwa na ujumbe
huu hebu share na mwingine ili naye abarikiwe.
Nakushukuru sana wewe
ambaye umekuwa ukibarikiwa na neno la Mungu ambalo tumekuwa tukijifunza pamoja
kwenye huduma hii na umeona ni vema kuungana nasi kuwafikishia pia wengine
injili (hasa walioko vijijini) kwa njia ya vipeperushi. Nawashukuru wote
mnaoendelea kujitoa kwa ajili ya hili. Lengo letu ni kutengeneza vipeperushi
angalau 5,000 kwa mwezi. Kipeperushi 1 ni tshs 250 tu. Kama unabarikiwa na neno
ambalo tumekuwa tukishirikishana naamini utapenda pia watu walioko mazingira
yasiyokuwa na Internet wafikiwe na injili hii kwa njia ya vipeperushi.
Ungana nasi kwenye
huduma hii kwa kadri ya kufanikiwa kwako na Mungu akubariki. ‘Apandaye haba
atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama
alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu
humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema
kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi
sana katika kila tendo jema” #2KOR. 9:6-8. Hebu fanya kazi nasi kwa njia hii
kwa kupenda. Ukichangia hata vipeperushi 2 (tshs 500 tu) kwa wiki au kwa mwezi
waweza kuwafikishia injili watu zaidi ya 10. Utakuwa umeshiriki utume mkuu
pamoja nasi. Basi changia kwa kadri ya kufanikiwa kwako.
YASIYOWEZEKANA KWA
WANADAMU, KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
0 coment�rios: