SOMO: KUTEMBEA NA MUNGU
HAPA CHINI▼▼
HAPA CHINI▼▼
VITU VYA KUZINGATIA UNAPOAMUA KUTEMBEA NA MUNGU
Mwanzo
5:21-24
1.
Mwisho wa maisha yako ni wa muhimu sana kuliko mwanzo wako.
"Mwanzo
wako ni kiashiria cha mwisho wako lakini mwisho wako hutuonesha/hudhihirisha
hatima yako"
Biblia
inatoa hesabu ya idadi ya siku zote alizoishi Henoko kuwa ni miaka mia tatu na
sitini na mitano (365), lakini inasema katika miaka hiyo Henoko alitembea na
Mungu miaka mia tatu (300). Maana yake miaka sitini na mitano (65) Henoko
alikuwa akitembea kwenye njia yake mwenyewe. Biblia inaweka wazi kabisa kuwa
Henoko alianza kutembea na Mungu baada ya kumzaa Methusela na utakumbuka kuwa
Methusela alizaliwa Henoko akiwa na miaka sitini na mitano (65).
”Enock
alipomzaa Methusela akiwa na umri wa miaka 65 aliamua kutembea na Mungu kwa
imani katika muda wa miaka 300. Hii ikiwa na maana kuwa maisha ya Enoko kabla
ya kufanya uamuzi wa kukubaliana na Mungu kutembea pamoja katika kila hatua ya
maisha yake, alitembea katika njia zake mwenyewe au katika mwelekeo aliodhania
mwenyewe kuwa ulimfaa, ni mpaka pale alipoamua kwenda na Mungu katika mwelekeo
anaotaka Mungu.
2.kutembea
na Mungu kunahusisha uamuzi na utayari.
Mungu
hawezi kutembea na mtu ikiwa mtu huyo hayupo tayari kutembea na Mungu. Ni kwa
yule ambaye anatafuta kwa bidii kutembea na Mungu ndiye atakaye weza kutembea
na Mungu. Kwa lugha rahisi naweza kusema ni mpaka utakapogundua umuhimu na
uhitaji wa kutembea na Mungu kwenye maisha yako na kuchukua hatua ya kutafuta
ndipo ufahamu huo utakusukuma kwenye hatua ya kuanza kutafuta kutembea na
Mungu. Waebrania 11:6 Waebrania 11:6 inasema "6 Na pasipo imani
haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu anayemjia ni lazima aamini kuwa
yupo na kwamba yeye huwapa tuzo wale wanaomtafuta kwa bidii.
Wakristo
wengi wanaona kuwa wanaweza kwenda mwendo wa maisha yao bila uwepo wa Mungu
kwenye kila kitu ambacho kinazunguka maisha yao. Kutokujua au kuona umuhimu wa
jambo hilo, kumesababisha wengi kwenda uelekeo wowote wanaoutaka kwenye maisha
yao kwasababu kukosekana kwa Mungu kwenye hatua za maisha ya mwanadamu humfanya
mtu kuwa huru kwenda uelekeo wowote lakini kuwepo kwa Mungu katika matembezi
yako hukupa nidhamu inayokusaidia kwenda kwa uelekeo ambao Mungu anataka uende
nae. Hii ni kwasababu "Kujua unapokwenda hukusaidia kutokwenda katika
mwelekeo usiotakiwa kwenda"
3.
kutembea na Mungu kunahusisha kuishi tofauti na tamaduni zilizokinyume na
maadili ya ufalme wa Mungu
Kutembea
na Mungu kwenye maisha yetu kunahusisha kuishi katika mila, desturi na tamaduni
za ufalme wa Mungu uliekubali kutembea pamoja nae ili ikusaidie kwenda pamoja
nae.Kwa lugha rahisi naweza kusema "kutembea na Mungu kunahusisha kuishi
kinyume na tamaduni zilizokinyume na maadili ya ufalme wa
Mungu"uliekubaliana nae kwenda pamoja katika safari yenu.
Enoko
kutembea na Mungu katika wakati wake kulihitaji uamuzi mgumu na utayari wa moyo
kwasababu wakati alioishi, jamii iliyomzunguka, maadili ya watu katika jamii
yake yalikuwa yameharibika sana. Aliamua kuishi kwa mujibu wa kanuni na mila za
ufalme wa Mbinguni ambazo zilitofautiana sana na kupingana na tamaduni za jamii
aliyokuwa akiishi wakati huo.
Mungu
alipoumba ulimwengu huu alikuwa amekusudia ulimwengu huu utawaliwe kwa kanuni,
Mila na desturi za mbinguni. Hii ni kwasababu dunia ni ulikuwa ni mwendelezo wa
kiutawala wa serikali ya mbinguni. Ni muhimu kufahamu wakati wa ukoloni kuwa ni
serikali za kifalme tu ndio zilikuwa zinamiliki makoloni ambapo koloni
lilihesabiwa kuwa ni mwendeleo wa eneo lakini ambalo liko mbali na serikali
inayotawala koloni hilo.
4.Kutembea
na Mungu kunahusisha kwenda na Mungu katika kila hatua unayopiga katika maisha
yako.
Kutembea
na Mungu kunahusisha makubalino katika uhusiano wako na Mungu. Amos 3:3 inasema
" Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja wasipokuwa wamepatana? "
Kutembea
uhusisha hatua moja kwenda nyingine na uhusisha kwenda katika uelekeo mmoja,
hatua kwa hatua. Biblia haisemi kuwa Enoko na Mungu walitembea kwa miaka 30
kisha Enoko akatembea mwenyewe kisha alipofikisha miaka 80 akaanza tena
kutembea na Mungu, Hapana! Mwendo wao ulikuwa ni wa kila siku kwa miaka 300.
Kutembea
kwa Enoko na Mungu kulikuwa na maana hii ni kumfanya Mungu kuwa ni sehemu ya
maamuzi yako, sehemu ya mawazo yako, ni sehemu ya kalenda (ratiba yako), ni
sehemu ya muda wako, ni sehemu ya mahusiano yako. Kila hatua unayochukua kila
siku kwenye maisha yako, Mungu anakuwa sehemu muhimu, hakuna unachokifanya bila
yeye kuhusika
5.Kutembea
na Mungu kunahusisha Imani.
Enock
aliweza kutembea na Mungu kwa njia ya Imani sio kwa kuona. Inawezekana labda
alipata nafasi ya kusikia habari kuhusu Mungu na akaamua kuamini kuhusu Mungu
huyo. Miaka 300 aliweza kuwa na uhakika na Mungu ambaye hajawahi kumuona kwa
macho lakini akaamini kuhusu Mungu huyo. Katika wakati alioishi Enoko hapakuwa
na Bliblia kama ilivyo kwetu leo, hata amri sheria alizotoa Mungu kupitia Musa
zilikuwa bado hazijatolewa, hapakuwa na mashujaa wa imani kama akina Ibrahimu,
Daniel na wengine wengi ambao tunasoma habari zao leo na zinatusaidia kuinua
viwango vya imani mioyo mwetu kuhusu Mungu.
Waebrania
11:6 inasema"
Wakati
alizoishi Enoko inawezekana kutembea kwake na Mungu kwa maana ya kumshirikisha
Mungu katika kila eneo la maisha yake ilionekana ni kama kupoteza muda au kuwa
mshamba, lakini mwisho wa matembezi yao Mungu alimpa thawabu ya uaminifu wake
katika matembezi yao ya miaka 300 kwakua haikuwa jambo rahisi.
6.Kutembea
na Mungu kunahusisha mazungumzo kati yako na Mungu.
Watu
wawili wanapokuwa wanatembea ni lazima mazungumzo yanajitokeza katikati yao,
kila mmoja anazungumza na mwenzake na kushirikiana mawazo au mipango
waliyonayo. Ndio maana Biblia inasema 1Wathesalonike5:16 inasema"Ombeni
bila kukoma"
Haiwezekani
kutenganisha Neno la Mungu,maombi na mtu alieamua kutembea na Mungu. Maombi na
kusoma Neno la Mungu ni njia pekee ambayo hudumisha/uhimarisha mazungumzo kati
yetu na Mungu. Kwa maombi unapata nafasi ya kumueleza Mungu na kwa Neno lake
Mungu anazungumza na wewe. Ikiwa watu wawili wanatembea safari ndefu bila
mazungumzo(conversation), huona safari yao kuwa ni ndefu, ngumu na yenye
kuchosha sana, lakini wanapozungumza hujikuta safari yao imekuwa fupi Licha ya
kuwa ilikuwa na uchovu mwingi, ni tofauti na mtu anaetembea Peke yake.
Hiki
ndicho kitu kinachotokea mtu anapokuwa anazungumza na Mungu kwa njia ya maombi
na kumsikiliza Mungu katika Neno lake katika safari ya maisha tunayoishi, kwa
kadiri tatizo alilonalo mtu anavyoliona kubwa, kila wakati anapozungumza na
Mungu kwa njia ya maombi, hujikuta anaona tatizo alilonalo sio zito au kubwa
kama alivyokuwa akifikiri.
7 .
kutembea na Mungu kunahitaji kuwa na picha kamili ya wapi unapoelekea.
"Kujua
unapokwenda hukusaidia kutokwenda katika mwelekeo usiotakiwa kwenda "
Neno
la Mungu hutusaidia kufahamu zaidi kuhusu njia tunayoiendea, ni muhimu kwa mtu
anaetembea na Mungu kufahamu na kuliishi neno la Mungu. Kulifahamu Neno ni
jambo jingine na kuliishi neno ni hatua nyingine. Wakristo wengine wana fahamu
Neno ila wameshindwa kuliishi Neno kama linavyoelekeza, hivyo inapoteza ile
maana ya Kulifahamu Neno, ni sawa na mwanafunzi aliyepelekwa shule kuelimika
halafu tunamleta kwenye elimu ya vitendo anashindwa ku apply ujuzi, maarifa na
ufahamu alionao maana kunakuwa hakuna tofauti na ambaye hakwenda shule
kujifunza ulichojifunza.
Yuda
1:14-15 inasema " Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu (mwandishi
hakutaka wasomaji wachanganyikiwe maana kulikuwa na Henoko wawili katika
familia ya mzee Adamu Mwanzo 4:17, hivyo mwandishi alitaka wasomaji waelewe
kuwa alikuwa hazungumzi Henoko huyo mtoto wa Kaini bali nazungumzia Henoko baba
yake Methusela kwasababu watu wanaweza kuwa na majina yanayofanana lakini wasiwe
na tabia zinazoendana au kufanana.tofauti yao ilikuwa hivi; Henoko mtoto wa
Kaini alifahamika na watu kwasababu baba yake alijenga mji na kuuita Henoko
lakini Henoko huyu baba yake Methusela hakufahamika sana na watu lakini
alifahamika sana na Mungu mbinguni. Swali ni unataka nani kulijua jina lako?),
mwandishi wa kitabu cha Yuda anaendelea kusema Henoko huyo baba wa
Methusela...alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja
na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote, na
kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu
walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao
wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake."
8.Namna
unavyoishi inaamua namna unavyoondoka (How you live will determine how you
leave).
Paulo
katika 2Timotheo 4:6-8 inasema “6Kwa maana mimi sasa namiminwa, na wakati wa
kufariki kwangu umefika. 7Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza,
imani nimeilinda
mungu akubariki
ukihitaji maombi
piga 0763652896, 0782859946, 0714890889
HAPA CHINI▼▼
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
HAPA CHINI▼▼
Mungu akubariki sana Mtumishi wa Mungu kwa somo zuri.
ReplyDeleteBinafsi Nimeongeza ufahamu kupitia somo hili hasa kwa habari ya Henoko