MAISHA YA MAOMBI KWA MKRISTO (PART 5)

KUTAZAMA VIDEO YAKE BONYEZA
HAPA CHINI▼▼


PICHA ZAKE ZOTE AKIWA MTUPU BONYEZA
HAPA CHINI▼▼


MAISHA YA MAOMBI KWA MKRISTO (PART 5)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu tunapokuwa katika maombi.
(1) hatupaswi kuwa na mashaka yoyote!
Maandiko yanasema katika yakobo 1:5-7,
“…ila naombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari la bahari lililochukuliwa na upepo,na kuleperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa bwana.”

Hayo ndiyo maandiko! Hata kama tunaomba masaa 100 mfululizo, hata kama tunaomba kwa viwango vya vinavyoonekana vya juu sanaa kibinadamu, lazima maombi yetu yawe ndani ya kanuni, lazima tuombe pasipokuwa na mashaka tena mashaka yoyote! Hayo ndio maandiko hakuna njia ya mkato; kama tunamuomba mungu lakini tuna mashaka moyoni au vinywani hilo ni tatizo linalopelekea kutopokea majibu yetu ya maombi! Kwa nini nasema mtu anaweza akawa na mashaka moyoni. Mtu mwingine anaweza akaonekana ana imani katika mazungumzo yake, hasa pale anapokutana na watu , lakini ndani ya moyo wake kumejaa mashaka, na mashaka hayo mungu huyaona pale mtu anapokuwa peke yake katika fikra au pale mambo yanapokwenda kinyume na alivyotarajia kutokana na maombi yake! Akizungumza na watu ni kama amejaa imani! Lakini moyoni kumejaa mashaka makubwa! Mashaka ni ile hali ya wasiwasi ya kutokuamini. “hivi kweli mungu inawezekana kweli? Itakuwa kweli? Mungu ananisikia kweli?” N.k.

Hayo yote ni mashaka na kwa mashaka hayo kamwe hatutaweza kupokea majibu yetu ya maombi! Kamwe! Tukiruhusu mashaka hata kama ni kidogo tunaambiwa waziwazi, “maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kutoka kwa bwana.” Yaani, hata ile kudhani, kutegemea, kufikiri, isiwepo. Mashaka ni adui mkubwa sana anayeshindana na majibu ya maombi yetu yasitufikie.
Wakati mwingine mashaka yanakuwepo baada ya kuomba kitu muda mrefu na kutoona majibu ya maombi! Wakati mwingine inatokana na kuona mambo yanakuwa mabaya zaidi kuliko mwanzo! Au uzito wa jambo pia linaweza kuchangia kukaribisha mashaka na hata shetani pia anahusika lakini anapitia maeneo hayo hayo!

Ili tuone majibu ya maombi yetu yakiwa dhahiri, hatupaswi kuruhusu mashaka yoyote hata kidogo! Tukishaomba tu! Mawazo yetu yanapaswa kufikiri sawasawa na majibu ya maombi yetu, kusema kwetu kuendana na majibu yetu ya maombi kwa imani, inaweza kuwa sio rahisi kuishi hivyo haiwezi kuwa rahisi hata kidogo! Na hakuna mbadala wake lazima mashaka yasiwepo ili tupokee majibu yetu ya maombi! Tunamuomba mungu kwa sababu sisi hatuwezi, tumeshindwa ndio maana tunaomba! Kama mtu unawashwa mgongoni utamwomba mungu “niwezeshe kujikuna?” La! Tutajikuna kwa sababu jambo hilo liko ndani ya uwezo wetu!

Tunapomuomba mungu maana yake sisi hatuwezi, tumeshindwa! Rahisi kufikiri nguvu za mungu hazipo; rahisi kufikiri ukimwomba mungu basi majibu yanachukua muda mrefu! Hatupaswi kuyaruhusu mawazo hayo kufanya kazi ndani yetu kamwe! Sisi tunachotakiwa kuamini mungu yupo na anajibu maombi na hakuna gumu la kumshinda! Mashaka yanapokuwa yanakuja kwa njia zozote zile, iwe kupitia watu kwa maneno yao; n.k. Hatupaswi kuyaruhusu kwa sababu, tukiruhusu mashaka maandiko yanasema tusitarajie kupokea kitu kutoka kwa bwana!

Kuna wakati yesu alikuwa anatembea juu ya bahari! Na petro akaomba atembee au apewe uwezo na yesu wa kutembea juu ya bahari! Yesu akayajibu maombi yake na akamwambia petro atembee…lakini petro aliporuhusu mashaka baada ya kuuona upepo, akazama mbele ya yesu! Yesu akamuokoa kwa kumshika mkono sio kwa kumuombea bali alimshika mkono na akamwambia! (mathayo 14:26-31.31):

“mara yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, ‘ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?’”
Unaona hapa! Petro anazama mbele ya yesu kwa sababu aliruhusu mashaka, na sisi sio kama tukimuomba mungu kitu fulani basi kinakuwa mtelemko! Inaweza ikatokea upepo mkali kwenye biashara zetu kwa viwango vya kuporomosha kabisa mitaji yetu! N.k. hatutakiwi kuwa na mashaka katika hali yoyote! Tusimamie matokeo tusiangalie mazingira tuliyonayo kwa sasa, tukiwa na mashaka tutazama tu hata kama yesu yupo ndani mwetu!

Wakati wote tunapomuomba mungu, tuombe bila mashaka yoyote yale! Mungu yupo na nguvu zake zipo vilevile! Hata mimi nikikufanyia maombi na ukaanza kuona matokeo, yaani, unatembea juu ya bahari kama petro! Lolote likitokea kama upepo likiwa na lengo la kubadilisha hilo, hupaswi kuwa na mashaka unapaswa kuendelea kuamini! La sivyo utazama kama petro na kuupoteza muujiza wako! Kama petro alizama mbele ya yesu kwa sababu ya kuruhusu mashaka! Sembuse mwanadamu anayeitwa….. .
Yakobo 1:5-6,
“…ila naombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari la bahari lililochukuliwa na upepo, na kuleperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa bwana.”

Tumwombe mungu atuongezee imani atupilie mbali mashaka yaliyomo ndani mwetu na atupe kuyashinda kila yanapoinuka. Hata kama maombi yetu yatachukua muda mrefu bila kuona majibu yake, bado hatupaswi kuruhusu mashaka, tena mashaka yoyote yale.

 MAISHA YA MAOMBI KWA MKRISTO ( 6)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu, tunapokuwa katika maombi.
(2) kuomba vibaya ili tuvitumie kwa tamaa zetu!
Tunaweza tukawa kweli tunaomba, tunaomba ili tupate kazi fulani, tunaomba mungu atutumie tukiombea watu wapone na mungu akutane na haja zao! Mwingine anaomba apate nyumba nzuri, mwingine gari, honda, n.k. Yote haya ni mema, lakini kama mtu anaomba moyoni kumejaa nia nyingine (kama uchoyo au kiburi), moyoni anasema au anawaza kwamba, “nikipata gari ninalolitaka, watu watanikoma.” “nikipata pesa hee! Watanitambua”, n.k.

Mwingine ni kipofu tangu kuzaliwa anamuomba mungu lakini moyoni anawaza au anasema, “sijawahi kuona mwanamke tangu kuzaliwa kwangu, nikiona sijui itakuwaje watanikoma, maana naishia kusikia tu na kuhisi” unaona! Mtu anaomba lakini moyoni mwake anawaza nikikipata nitakutumia hivi au vile, matumzi yenyewe ni nje ya mpango wa mungu. Ndugu yangu hapo tutaomba na kuombewa lakini kamwe hatuwezi kupokea majibu ya maombi! Tunataka mtoto lakini hatujaoa/hatujaolewa wala hatutaki kusikia habari za kuoa au kuolewa!

Mwingine anataka mungu amtumie lakini moyoni mwake kumejaa mashindano ya dhahiri, anawaza kumzidi yule, mwingine anataka sifa tu! Mwingine anawaza utajiri kwamba nitakuwa napata sadaka nyingi za watu n.k. Maandiko yanasema katika yakobo 4:3,
“hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.”
Unaona maandiko hayo? Kama tunamuomba mungu tukiwa na hali hiyo! Kamwe hatuwezi kupokea majibu ya maombi. Ni kupoteza muda tu! Na mwisho wa siku tunaona kama mungu hayupo; mungu yupo na anajibu maombi! Tatizo lipo kwetu tu! Tunaomba ili tukipata tuvitumie vibaya! Kama tunataka kumuona mungu lazima tuzingatie tunaomba ili tuvitumiaje? Nje ya mpango wa mungu! Tuko watu wengi tunaomba na kufikia wakati tunafunga! Lakini tunaomba ili tuvitumiaje hivyo tunavyovitaka kwa njia ipi?

“hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.” Yakobo 4:3.
Kuomba tunaomba kweli! Lakini hatupati kwa sababu tunaomba vibaya ili tuvitumie kwa tamaa zetu! Tangu wakati huu tuhakikishe nia zetu zinakuwa safi mbele za mungu ili tuyaone majibu yetu ya maombi na nguvu ya maombi! Maombi yana kanuni zake na ikiwa mtu anataka kumuomba mungu na kumuona mungu dhahiri akijidhihirisha kwake binafsi hatuna budi kuzingatia yote tunayopaswa kuyazingatia.

Lolote tunaloliomba lazima tangu moyoni huko ambako mungu anaanza nako kwa kumuangalia mtu anataka hili ili iwe nini? Mwingine anatumia pesa kunyanyasa watu, mungu huwa hamuinui mtu ambaye ana visasi, yaani mungu akinipa hivi fulani atanikoma! Kila anachofanya mungu ni kwa utukufu wake tu sio kwa utukufu wa mtu yeyote.

MAISHA YA MAOMBI KWA MKRISTO (7)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu, tunapokuwa katika maombi.
(3) hatupaswi kukata tamaa na kuachia maombi njiani baada ya kuona tunaomba muda mrefu bila kuyaona majibu yetu ya maombi kwa dhahiri!

Hakuna sehemu ngumu inayotushinda watu wengi kama hii! Watu wengi tunataka tukishaomba tu; basi tupokee majibu yetu ya maombi muda huo huo! Mungu hafanyi kazi hivyo ndugu yangu! Mungu ni wa utaratibu sana! Tunapomuomba mungu tunatakiwa kuamini kwamba imekuwa. (matha 7:7).
Hilo ndilo la kuliamini na kulishikilia wakati wote, haijalishi majibu yetu ya maombi tutayaona lini, sisi tuamini kwamba mungu ametenda huku tunaendele kumwomba mungu mpaka liwe dhahiri lile tunaloliomba. Mungu aliumba mbingu na nchi kwa muda wa siku 6, (mwa 1:1). Unafikiri kwa uwezo wa mungu! Kwa nini hakutumia siku moja tu kufanya kila kitu? Je! Hakuwa na uwezo huo? Uwezo upo mkubwa tena sana – mungu ni wa utaratibu sana, ana nguvu ana uwezo lakini ni wa utaratibu mno! Mnoooo! Mbona basi wewe na mimi tunakata tamaa mapema hivyo na kuacha kuendelea kuomba! Tunaona mungu hatusikii ni kama anawasikia wengine! Ni kama ana watu wake maalumu na sio sisi? Hatupaswi kuwaza hivyo hata kidogo, na tusiyape nafasi mawazo hayo! Tunapaswa kuendelea kung’ang’ania mbele za bwana mpaka tuone majibu yetu ya maombi yawe dhahiri. Maandiko yanasema katika luka 18:1,

“akaawambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba mungu sikuzote, wala wasikate tamaa”.
Hayo ni maandiko! Mungu anatambua kwamba! Mtu anaweza akaomba jambo na likachukua muda mrefu na mpaka mtu anafikia mahali kukata tamaa na kuacha kuomba, ndio maana inatajwa hapo “wala wasikate tamaa”.

Uwezekano wa kuchelewa kuyaona majibu yetu ya maombi unawekwa wazi na bwana mwenyewe, lakini hatupaswi kukata tamaa! Marufuku kukata tamaa, usikate tamaa! Endelea kuomba, usiachie njiani hata kidogo! Usiwaze “ooh! Labda kuna makosa nimeyafanya, labda nimefanya dhambi.” Kwani ukifanya dhambi hujui? Maandiko yanasema! 1 petro 5:6, “basi nyenyekeeni chini ya mkono wa mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake”. Kumbe kuna wakati wa mungu! Wakati wa mungu ni mzuri ndugu kuliko wakati wetu sisi! Mungu ndio anajua wakati mzuri wa kukupa jibu lako la maombi! Usione unakawia, wakati wako ndio unakawia, lakini wakati wa mungu ni bora saaana! Mungu anajua wakati gani ukipata kazi utakuwa mzuri kuliko wakati fulani; mungu ndio anajua wakati gani ukipata mtoto utakuwa mzuri zaidi! Wewe unataka mtoto sasa lakini mungu akiangalia anona sasa sio salama! Unataka mungu akutumie kwenye hili au lile n.k. Sisi tuendelee kumlilia bwana! Kupokea ni lazima! Kukata tamaa ni marufuku! Hatupaswi kukata tamaa kamwe! Tuyashinde mawazo ya kutukatisha tamaa! Mungu yupo na anajibu maombi.

 MAISHA YA MAOMBI KWA MAOMBI KWA MKRISTO (PART 8)
Mambo ya kuzingatia tunapokuwa tunamuomba mungu,tunapokuwa katika maombi.
(4) Tunapaswa kuwa na imani kwamba mungu yupo na anatusikia na anajibu maombi!
Ndugu yangu, hata kama tutaomba na kujigalagaza na kulia kwa uchungu mpaka kutoka makamasi! Lakini kama hatuna imani ni buuure, bure!
IMANI NI NINI? Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana na mambo yasiyoonekana, waebrania 11:11. Hiyo ndio imani! Tunaomba tunatarajia kupokea, sasa imani ni kuwa na uhakika kwamba! Hiki ninachikiomba kinakwenda kuwa sawasawa na nilivyoomba! Imani huwa haingalii mtu wala huwa haijilinganishi na mtu yeyote! Imani inaangalia uwezo wa mungu tu na neno lake basi! Imani haingalii mazingira n.k. Imani inaweza kukufanya wewe kuwa wa kwanza kukipata hicho unachokiomba! Maandiko yanasema,

“lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (waebrania 11:6).
Tunatakiwa kuwa hivyo tunapokuwa tunamuomba mungu, tusiombe ili mradi tu, tusiombe ili kutimiza wajibu tu, tusiombe kwa desturi na mazoea! Kwa kufanya hivyo tutadangayika kwamba hakuna nguvu yeyote katika maombi, kumbe ni uongo wa ibilisi tu. Tunapaswa kumuamini mungu tunapokuwa tunaomba! Na imani pasipo matendo imekufa! Baada ya maombi lazima uonyeshe matendo na sio unalala tu na kupigapiga soga na watu! Lazima ufanye matendo kama ni kazi tafuta kazi n.k.

Kutokuwa na imani ni dhambi vilevile! Ndugu yangu inawezekana umekuwa una muomba mungu kwa muda mrefu lakini huna imani! Yesu alikutana na vipofu,angalia hapa! “yesu alipokuwa akipita kutoka huko,vipofu wawili wakimfuata wakipaza sauti. Yesu akawaambia, ‘mnaamini kwamba naweza kufanya hili?’ wakamwambia, ‘naam bwana.’ ndipo alipowagusa macho yao yakafumbuka.” Mathayo 9:27-30.

Unaona hapo? Baada ya kusema wanaamini ndipo yesu alipowajibu majibu yao kwa kuwafumbua macho yao! Na hakuwafumbua macho kabla ya kujibu kwamba anaweza! Kabla ya kuionyesha imani yao! Na sisi mungu anatuuliza kila tunapomuomba! Je! Tunaamini kwamba anaweza kufanya hilo au hayo tunayomuomba? Kila tunapoomba swali linakuja katika ulimwengu wa roho kwako binafsi, “je! Unaamnini naweza kufanya hili?”

Imani ni lazima tunapokuwa katika maombi!
KWA NAFASI ZA KAZI POPOTE TANZANIA, BONYEZA
HAPA CHINI▼▼

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
[3.00 MB]VIDEO YA ALIKIBA AKIBANDUANA NA JOKATE, BONYEZA
HAPA CHINI▼▼



0 coment�rios: